Home » » NAIBU KATIBU AFUNGA MAFUNZO YA WAONGOZAJI WATALII MARUHUBI

NAIBU KATIBU AFUNGA MAFUNZO YA WAONGOZAJI WATALII MARUHUBI

Written By CCMdijitali on Friday, March 7, 2025 | March 07, 2025

 Na Ali Issa Maelezo 7/3/2025

 

Naibu katibu Mkuu Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar  Amina Ameir Issa amewataka wahitimu wamafunzo ya kutembeza watalii nchini (tour Guider) kufuata Sheria na taratibu zilizopo ili kulinda mila na desturi za Mzazibari.

 

Ameyasema hayo katika Chuo cha Maendeleo ya Hoteli na Utalii Maruhubi wakati akifunga mafunzo ya kuwajengea uwezo waongozaji watalii kukuza utamadni na kuwa na maadili mema katika kazi zao.

 

Amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekuwa ikitoa mafunzo mfulululizo kwa waongozaji watalii ili kuona wafanyakazi wa sekta hiyo wanafanyakazi  kwa uweledi na ustadi kwa kufuata Sheria na taratibu kwa lengo la kuleta matumaini na maeendeleo nchini.

 

"Nimeambiwa Mafunzo haya mmefuzwa heshima,mmerekebishwa tabia, na maadili yetu hivyo na amiini mtakua vijana waledi kulinda maslahi ya Nchi na tamaduni zetu" alisema Naibu Katibu Mkuu.

 

Alifahamisha kuwa Serikali ilifanya ukaguzi katika maeneo mbali mbali ya kiutalii na kubaini kuwepo  kwa baadhi ya watembeza watalii  hawana maadili wala tabia njema katika utendaji wa kazi zao na kuamua kuwapatia elimu vijana  hao ili kuwajenga katika maadili, silka na utamaduni  za Mzazibari.

 

Aidha aliwataka kuwa mabalozi kwa wengine pamoja na kusambaza elimu hiyo ambapo matumaini yao kuona utalii unaendeshwa na watu waledi na kuipa sifa nchii na kukuza uchumi wa nchi.

 

Mapema Mkurugenzi Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Dkt. Abdalla Muhamed alisema Mafunzo kama hayo wameshawahi kutoa katika maeneo mbalimbali ya utalii nchini ikiwemo Paje, Matemwe, Jambiani na Maruhubi ambapo mafunzo  kama hayo wanatarajia kuyatoa katika Kisiwa cha Pemba wiki ijayo.

 

Nae mshiriki wa mafunzo hayo Ahlam Abdalla Ali kutoka Magogoni aliishukuru Serikali ya awamu ya nane na Benki ya NMB Foundation kwa kuwapatia Mafunzo hayo na kuahidi kuifanyia kazi elimu waliyoipata na kutokwenda kinyume na sharia na taratibu ziliwekwa        ili kuipa hadhi na heshima nchi kupitia Sekta ya utalii.

 

Mafunzo hayo ya siku tatu (3) yamewashirikisha vijana150 wakiwemo watembeza watalii  ambapo mada mbalimbali zilitolewa ikiwemo historia ya Zanzibar na watawala waliowahi kuingia zanzibar.

 


Naibu katibu Mkuu Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar  Amina Ameir Issa


Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link