MAJALIWA AAGIZA USIMAMIAJI NA UDHIBITI WA UBORA WA ELIMU
▪️Asema lengo ni kuendelea kutoa wahitimu wenye uwezo wa kukidhi vigezo vya kimataifa ▪️Rais Dkt. Samia atoa milioni 100 kuchangia maendel...

WAZIRI KOMBO AFANYA MAZUNGUMZO NA UONGOZI WA KAMPUNI YA VIETTEL
Written By CCMdijitali on Monday, April 28, 2025 | April 28, 2025
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo, amefanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Viettel, ambayo ni kampuni tanzu ya Kampuni ya Mawasiliano ya Haotel Tanzania Kanali Dao Xuan Vu, katika makao makuu ya kampuni hiyo jijini Hanoi, Vietnam.
Mazungumzo hayo yalilenga kujadili kuhuhusu fursa mpya za uwekezaji zilizopo nchini na kuimarisha ushirikiano katika sekta za biashara na uwekezaji.
Waziri Kombo yuko nchini Vietnam kwa ziara ya kikazi, akiwa ameambatana na Balozi wa Tanzania nchini humo mwenye Makazi yake Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Khamis Omar, Mkurugenzi wa Idara ya Diplomasia ya Uchumi na Biashara ya Kimataifa Balozi John Ulanga, Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia Bi. Felista Rugambwa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania Bw. Gilead Teri na Viongozi wa Sekta Binafsi na Wafanyabiashara.
Mkurugenzi wa Idara ya Diplomasia ya Uchumi na Biashara ya Kimataifa Balozi John Ulanga akichangia jambo wakati wa mazungumzo na Kampuni Viettel ya Vietnam Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania Bw. Gilead Teri akifafanua jambo wakati wa mazungumzo na Kampuni Viettel ya Vietnam Mkurugenzi Mtendaji wa Nakiete Pharmacy na Rais wa Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) Bw. Vicent Bruno Minja akichangia jambo wakati wa mazungumzo na Kampuni Viettel ya Vietnam PICHA YA PAMOJA Balozi wa Tanzania nchini Vietnam mwenye Makazi yake Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Khamis Omar,akichangia jambo wakati wa mazungumzo na Kampuni Viettel ya Vietnam Balozi wa Tanzania nchini Vietnam mwenye Makazi yake Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Khamis Omar,akichangia jambo wakati wa mazungumzo na Kampuni Viettel ya Vietnam
WAZIRI KOMBO AWASILI NCHINI VIETNAM KWA ZIARA YA KIKAZI
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) amewasili jijini Hanoi, Vietnam kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kuanzia Aprili 27 hadi 30, 2025.
Akiwasili nchini humo Aprili 27, 2025, kupitia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Noi Bai, Waziri Kombo amepokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Vietnam mwenye Makazi yake Jamhuri ya Watu wa China Mhe.Khamis Omar na Viongozi Waandamizi wa Serikali ya Vietnam.
Waziri Kombo akiwa nchini humo anatarajiwa kuongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mazungumzo baina ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Viongozi wa Ngazi za Juu wa Serikali ya Vietnam kujadili masuala mbalimbali kwa lengo la kuibua maeneo mapya ya ushirikiano, kukuza na kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia na kiuchumi.
Aidha, mazungumzo hayo yanatarajiwa kufungua na kuongeza fursa mpya za uchumi na biashara kwa manufaa ya pande zote mbili, ikiwemo upatikanaji wa soko la bidhaa za mazao ya kilimo na uvuvi yanayozalishwa nchini,uwekezaji, teknolojia na viwanda.
Ujumbe wa Tanzania katika mazungumzo hayo utajumuisha Watendaji na Viongozi mbalimbali wa Serikali na Sekta binafsi akiwemo Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania Bw. Gilead Teri, Mkurugenzi wa Idara ya Diplomasia ya Uchumi na Biashara ya Kimataifa Balozi John Ulanga na, Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia Bi. Felista Rugambwa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Tanzania na Vietnam zimekukwa na uhisiano mzuri wa kihistoria ambao umechangia kustawi kwa biashara baina ya mataifa hayo mawili. Madhalani, kiwango cha mauzo ya bidhaa kutoka Tanzania kwenda Vietnam yaliongezeka kutoka USD milioni 226.6 mwaka 2020 hadi USD milion 314.2 mwaka 2024, sawa na ongezeko la asilimia 38 ndani ya miaka mitano. Vilevile, uagizaji wa bidhaa kutoka nchini Vietnam kuja nchini uliongezeka kutoka USD milioni 20.4 mwaka 2020 hadi USD milioni 60 mwaka 2023.
Kadhali, kwa upande wa uwekezaji Vietnam imewekeza katika sekta mbalimbali hapa nchini ikiwemo ujenzi, fedha, uzalishaji viwandani, na mawasiliano, ukiwa na jumla ya thamani ya USD bilioni 2.362, ambayo imezalisha ajira kwa takribani Watanzania 226,642.
Vietnam ilifungua Ubalozi wake hapa nchini kwa mara ya kwanza Februari 14, 1964.
DKT.DIMWA : ATOA MAAGIZO KWA WIZARA YA AFYA NA WIZARA YA MAJI ZANZIBAR ZITATUE CHANGAMOTO PEMBA.
NA IS-HAKA
OMAR,PEMBA.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Mohamed Said Dimwa,ameziagiza Wizara ya Afya Zanzibar pamoja na Wizara ya Maji,Nishati na Madini Zanzibar kumaliza changamoto za malalamiko ya Wananchi juu ya urasimu wa kuungiwa huduma ya umeme pamoja na huduma duni za Afya katika Hospitali ya Wilaya ya Micheweni.
Ametoa wiki moja
kuletewa ripoti ya utekelezaji wa maagizo hayo kwa Wizara husika ili wananchi
wa Wilaya hiyo na maeneo mengine kisiwani Pemba waendelee kupata huduma bora na
zenye viwango kama ilivyokusudiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Amesema CCM ipo kwa ajili ya kusimamia Serikali itoe huduma bora kwa wananchi bila ubaguzi wa duni,rangi,kabila na itikadi za kisiasa na kwamba Chama hicho hakitovumilia viongozi na watendaji wasiotekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Hayo ameyasema
katika mwendelezo wa ziara yake ya Sekretarieti ya Kamati maalum ya NEC,CCM
Taifa Zanzibar ya kuimarisha uhai wa Chama wakati akizungumza na wajumbe wa
Kamati za siasa ngazi za matawi,wadi,majimbo na Wilaya ya Micheweni
kichama katika ukumbi wa mikutano uliopo micheweni kisiwani Pemba.
Amesema wapo
baadhi ya watendaji na viongozi Serikalini wamekuwa wakifanya urasimu wa
kuchelewesha au kuwakosesha huduma muhimu wa wananchi kwa kusudi
ili ionekane Serikali haitekelezi ahadi zake kwa wakati.
Dkt Dimwa,ameweka
wazi kuwa kila ikikaribia wakati wa uchaguzi kuna baadhi ya watendaji wasiokuwa
waadilifu wamekuwa hawafanyi kazi kwa ufanisi na kusababisha malalamiko yasiyo
ya lazima.
"Kuna malalamiko mengi Pemba ya baadhi ya maeneo kukatika umeme mara kwa mara na wengine wakitaka kuungiwa umeme kuna urasimu pia zipo Hospitali zina vifaa tiba vya kisasa,zina madaktari wa kutosha dawa zote lakini bado wananchi hawapati huduma bora za Afya kwa wakati, naelekeza niletewe ripoti ndani ya wiki moja changamoto hizo ziwe zimemaliza.
CCM ndio tunaosimamia Serikali kuhakikisha inatekeleza Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020/2025 kwa ufanisi,,,,hatucheki na mtu ukiona wewe ni mtendaji huwezi kufanya kazi serikalini acha kazi waajiriwe wengine". alisema Dkt Dimwa.
Katika maelezo
yake Dkt.Dimwa,amesema lengo la ziara hiyo ni kuimarisha uhai wa Chama na
kuwakumbusha viongozi hao umuhimu wa kujiandaa na uchaguzi mkuu wa dola wa
mwaka 2025.
Amewataka
viongozi hao kuwahamasisha wanachama mbalimbali wenye nia ya kugombea kujitokeza
kwa wingi kuchukua fomu katika uchaguzi wa ndani wa kura za maoni ili wapate
haki ya kidemokrasia ya kuchagua na kuchaguliwa.
Alisema CCM
itatenda haki na haitomuonea mtu yeyote hivyo kila mtu atapata haki yake
kulingana na vigezo vya uteuzi vilivyowekwa na vikao vya juu.
Alitumia ziara
hiyo kukemea vitendo vya rushwa,fitna na kuchagua na kisiasa na kwamba uchaguzi
huo wa kura za maoni usiwagawe na kutengeneza migogoro ndani ya Chama badala
yake uwaunganishe wanachama wote na kuunda umoja wenye nguvu za kupatikana
ushindi katika uchaguzi wa dola wa Octoba 2025.
Akitoa ufafanuzi
wa baadhi ya hoja Mjumbe wa Kamati ya siasa ya CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba
ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa huo Salama Mbarouk Khatib,alisema alieleza kuwa
baadhi ya wananchi wamekuwa hawataki kitibiwa katika vituo vya afya na badala
yake wanaenda katika Hospitali ya Wilaya ambayo ina utaratibu maalum wa kupokea
wagonjwa na wakati mwingine wagonjwa wanakuwa ni wengi kuliko uwezo wa
Hospitali hali inayopelekea malalamiko hayo.
Salama,akizungumza
changamoto ya baadhi ya wananchi kuchelewa kuungiwa umeme alieleza kuwa shirika
la umeme Zanzibar (ZECO) limekuwa likifanya juhudi za kuimarisha huduma zao na
kwa sasa wanaendelea na mchakato wa kutatua changamoto hizo za ucheleweshwaji
wa kuungiwa umeme ili kumaliza malalamiko ya ukosefu wa huduma hizo.
"Tumepokea maelekezo ya Sekretarieti tutayafanyia kazi kwa wakati,,,pia wananchi wenyewe nao wanatakiwa kubadilika tunavyo vituo vya afya mbalimbali katika wilaya ya Micheweni lakini hawaendi naamini Hospitali ya Wilaya ndio yenye uwezo wa kutoa huduma bora wakati huduma hizo hizo zinapatikana hata katika vituo vya afya.
Naye Katibu wa
Kamati Maalum ya NEC,Idara ya itikadi,uenezi na mafunzo CCM Zanzibar Khamis
Mbeto Khamis amewataka wananchi wa Pemba kupuuza kauli za viongozi wa
ACT-wazalendo kupotosha kuwa Serikali haijafanya mambo ya maendeleo kisiwani
humo na badala yake wapime maendeleo yaliyotekelezwa na Serikali chini ya
Uongozi wa Rais wa Zanzibar Dk.Hussein Mwinyi na wafanye maamuzi ya kuipigia
kura CCM na kuhakikisha inashi nda uchaguzi mkuu wa 2025.
Amesema viongozi
wa ACT-Wazalendo wamekuwa wakipotosha na kuendelea siasa za ubaguzi dhidi ya
Serikali ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila kujali maisha ya
wananchi ambao ustawi wa maisha yao unategemea amani,utulivu na maendeleo
endelevu ya kiuchumi na kijamii.
Amesema viongozi
wa ACT-Wazalendo wameishiwa na hoja badala yake wamekuwa wakifanya siasa
za ulaghai na fitna zisisokuwa na nafasi katika ulimwengu wa siasa za kisayansi
zinazozingatia utafti,tathimini na hoja zinazotafsiriwa kwa maendeleo ya
vitendo sio ahadi hewa.
"Wanachama na wananchi wote wa kisiwa cha Pemba hakuna cha kumdai Rais Dk.Mwinyi,ameendelea kuifungua Pemba kiuchumi katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayogusa maisha ya watu wa rika zote bila ya ubaguzi.
Tunasikia maneno
eti Serikali haijafanya kitu ebu watwambie hizo barabara,shule za
ghorofa,bandari za kisasa,matengenezo ya uwanja wa ndege,miundombinu ya
maji,uwekezaji katika utalii,boti za kisasa za uvuvi,kupanda kwa bei ya mwani
na karafuu na huduma bora za afya na mengine mengi je yamefanywa na Serikali
ipi wao watwambie wamefanya nini mpaka hivi Sasa",alihiji Mbeto.
Naye Katibu wa
Kamati Maalum ya NEC,Idara ya mambo ya siasa na uhusiano wa kimataifa Khadija
Salum Ali,amewasihi viongozi hao kuhakikisha CCM inashinda pia wajitokeze
kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Chama hicho kwani kila
mwanachama ana haki ya kugombea nafasi yoyote anayotaka.
Akizungumza
Katibu wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya organazesheni CCM Zanzibar Ibrahim Omar
Kilupi,amewaonya baadhi ya wanachama na viongozi mbalimbali walioanza kutoa
kauli za vitisho kwa wenzao wanapotaka kugombea na kwamba hakuna mwenye hati
miliki ya kuwa kiongozi wa kudumu ndani ya CCM kila mtu anqpata nafasi kwa
wakati wake.
Kilupi,amesema
tayari CCM ishatangaza ratiba ya uchukuaji na urejeshaji wa fomu kupitia Wilaya
na mikoa ya CCM hivyo wanachama wote wanaopiga kura ya maoni wahakikishe
wanachagua viongozi wachapakazi,waadilifu na wenye uzalendo wa kusimamia na
kutetea maslahi ya wengi na sio maslahi binafsi.
Mwenyekiti wa CCM
Wilaya ya Micheweni Ali Masoud Kombo,amesema kila mwanachama ana wajibu wa
kuhakikisha Chama hicho kinapata ushindi mkubwa katika uchaguzi Mkuu ujao.
#sisitunatekeleza #NeemaZaAwamuYaNane
#Vitendovinasauti
#kazinaututunasongambele
#Miaka4YaSamia #Miaka4YaMageuzi
“KAZI NA UTU, TUNASONGA MBELE”
TAASISI YA JAKAYA MRISHO KIKWETE FOUNDATION NA NEXLAW WAUNGANA KUINUA WAJASIRIAMALI VIJANA TANZANIA
Taasi ya Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) na kampuni ya wanasheria NEXLAW Advocates ya Dar es salaam wamesaini rasmi makubaliano ya ushirikiano (MoU) yenye lengo la kuimarisha na kukuza ujasiriamali wa vijana nchini Tanzania kupitia Mpango wa JMKF wa Kuharakisha Wavumbuzi wa Kijamii wa Kijana Leo (Kijana Leo Social Innovator Accelerator).
Hafla ya kusaini makubaliano hayo imefanyika leo Aprili 28, 2025, katika ofisi za makao makuu ya JMKF zilizopo Masaki, Dar es Salaam, ikishuhudiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa JMKF, Bi. Vanessa Anyoti, na Mshirika Mwandamizi wa NEXLAW, Profesa Saudin Mwakaje.
Ushirikiano huu wa kihistoria unalenga kuwawezesha vijana wajasiriamali wa kijamii kwa kuwapatia maarifa muhimu kuhusu masuala ya kisheria, rasilimali za kufanikisha uzingatiaji wa sheria na zana za uongozi — ambazo ni msingi muhimu kwa ujenzi wa biashara endelevu na zinazovutia wawekezaji.
“Hili ni tukio kubwa sana,” alisema Prof. Mwakaje. “Tuna furaha kubwa kusaini rasmi makubaliano haya na JMKF. Vijana wengi wana mawazo bora na yenye nguvu ya mabadiliko — lakini mara nyingi hukosa mwongozo wa namna ya kulinda, kurasimisha au kupanua mawazo yao kwa njia ya kisheria. Ushirikiano huu utaleta suluhisho.”
Kupitia makubaliano haya, wataalam wa NEXLAW Advocates waliobobea katika elimu ya kisheria na uzingatiaji wa sheria kwa sekta ya kuanzisha biashara na SME, wataendesha moduli muhimu ndani ya Accelerator iitwayo Sheria, Uzingatiaji, Elimu ya Fedha na Ushirikiano na Mamlaka za Udhibiti.
Moduli hii itawapatia vijana msaada wa kitaalam wa masuala ya kisheria, msaada wa usajili wa hati miliki, na mbinu bora za kupita katika mifumo ya udhibiti.
Kwa mujibu wa Bi. Anyoti, mpango huu umejikita moja kwa moja katika utekelezaji wa Mpango Mkakati wa JMKF wa 2023–2030, ambao umebaini changamoto kubwa kwa vijana kupata huduma za kisheria na maandalizi ya kupokea uwekezaji.
“Ushirikiano huu wa kwanza wa aina yake tunaamini utazaa matunda,” alisema Bi. Anyoti. “Huduma za ulinzi na ushauri wa kisheria zinazotolewa na NEXLAW zitakamilisha juhudi zetu za kuwawezesha vijana na SMEs Tanzania. Tunataka vijana wetu wasiwe tu waotaji, bali wachukua hatua — wenye nguvu ya kufanikisha ndoto zao.”
Programu ya Kijana Leo ilianzishwa mwaka 2021 kwa ushirikiano na Ofisi ya Waziri Mkuu – Idara ya Maendeleo ya Vijana (PMO-LYED) na inarushwa kupitia AZAM TV kwa lugha ya Kiswahili.
Tangu kuanzishwa kwake, programu hii imekuwa nembo ya kitaifa ya ujenzi wa uwezo kwa vijana, ikigusa sekta kama vile kilimo kinachozingatia mabadiliko ya tabianchi, elimu na uvumbuzi wa kidijitali.
Kijana Leo imepata mafanikio makubwa kitaifa kwa wastani wa watazamaji zaidi ya milioni 4 kwa kila kipindi na kushinda Tuzo mbili za Umahiri katika Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT).
Kuanzisha na kudumisha biashara changa ni safari ngumu. Kupitia makubaliano haya mapya, JMKF na NEXLAW wamejipanga kuhakikisha kuwa biashara za vijana zinakuwa na uimara wa kisheria, udhibiti na fedha tangu hatua za awali — jambo ambalo litasaidia kuimarisha mfumo wa ujasiriamali Tanzania na kuufanya kuvutia zaidi kwa uwekezaji.
Mbali na malengo ya ndani ya nchi, washirika hawa wawili pia wana ndoto ya kupanua wigo wao kikanda, wakilenga kuendeleza modeli ya Kijana Leo Accelerator kote Afrika Mashariki, huku wakijenga mfumo mpana wa maendeleo ya vijana unaojumuisha uwezeshaji wa kisheria.
“Nina shauku kubwa ya kuona mustakabali ambapo vijana wavumbuzi hawatatiwa moyo tu kuanza safari zao, bali pia kupewa vifaa sahihi vya kuvumilia na kustawi,” alisisitiza Bi. Anyoti. “Mustakabali huo unaanza leo — kwa kutumia vifaa sahihi, ushirikiano sahihi, na maono sahihi.”
JMKF na NEXLAW walitoa shukrani za dhati kwa washirika wote, wadau na wafuasi wanaoendelea kuunga mkono dhamira ya kuwawezesha vijana, wakieleza kuwa makubaliano haya ni zaidi ya hati tu — ni ahadi ya kulinda, kukuza na kusimama bega kwa bega na waanzilishi wapya wa Tanzania katika safari yao ya mafanikio.
MWISHO
(ENGLISH VERSION)
Jakaya Mrisho Kikwete Foundation and NEXLAW Join Forces to Empower Young Entrepreneurs in Tanzania
The Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) and Dar es slaam based NEXLAW Advocates have officially signed a Memorandum of Understanding (MoU) to formalize a transformative partnership aimed at boosting youth entrepreneurship in Tanzania through the former’s Kijana Leo Social Innovator Accelerator.
The signing ceremony took place today April 28, 2025, at JMKF’s headquarters in Masaki, Dar es Salaam, officiated by JMKF Chief Executive Officer Ms. Vanessa Anyoti and NEXLAW Senior Partner Prof. Saudin Mwakaje.
This landmark collaboration marks a shared commitment to equip young Tanzanian social entrepreneurs with critical legal knowledge, compliance resources, and governance tools—essential pillars for building sustainable, investment-ready enterprises.
“This is a huge milestone,” said Prof. Mwakaje. “We’re thrilled to formalize this partnership with JMKF. Many young people have compelling, transformative ideas—but often lack a guidebook for how to protect, formalize, or scale those ideas legally. This partnership changes that.”
Under the new agreement, domain experts from NEXLAW Advocates—specialists in legal literacy and corporate compliance for startups and SMEs—will deliver a core training module within the Accelerator titled Legal, Compliance, Financial Literacy & Regulatory Engagement. Participants will benefit from expert legal advisory services, patent registration assistance, and practical navigation of regulatory frameworks, empowering them to build ventures that are both resilient and scalable.
According to Ms. Anyoti, the initiative aligns closely with JMKF’s 2023–2030 Strategic Plan, which identified gaps in legal support and investor readiness among youth enterprises.
“This is the first of what we hope will be many fruitful partnerships,” said Ms. Anyoti. “The legal protection and advisory services offered by NEXLAW complement our broader mission to empower youth and SMEs in Tanzania. It’s about transforming budding entrepreneurs from dreamers into doers—equipping them to go the distance.”
Launched in 2021 in collaboration with the Prime Minister’s Office – Youth Development Division (PMO-LYED), the Kijana Leo Program started as a Swahili-language television show airing on AZAM TV.
It quickly evolved into a national flagship for youth capacity building, impacting sectors such as climate-smart agriculture, education, and digital innovation. The program enjoys a national reach of more than 4 million viewers per episode and has twice been recognized with Excellence in Journalism Awards Tanzania (EJAT).
Forming and sustaining an early-stage company remains a daunting task. Through this MoU, JMKF and NEXLAW aim to embed legal, regulatory, and financial resilience into the DNA of Tanzania’s next generation of startups—strengthening the country’s entrepreneurial ecosystem and positioning it for greater investment appeal.
Beyond Tanzania, the partners are also setting their sights on regional expansion, positioning the Kijana Leo Accelerator model as a catalyst for youth empowerment across East Africa.
“I am passionate about building a future where young innovators are not just inspired to start, but equipped to endure,” Ms. Anyoti emphasized. “That future starts today—with the right tools, partnerships, and foresight.”
Both JMKF and NEXLAW expressed heartfelt gratitude to all partners, stakeholders, and supporters of the youth empowerment mission.
They emphasized that the MoU is more than a document—it’s a pact: to safeguard, nurture, and walk hand-in-hand with Tanzania’s newest pioneers on their journey toward sustainable success.
ENDS