MWENYEKITI WA CCM NA RAIS MSTAAFU DKT. KIKWETE AHITIMISHA KAMPENI ZA UCHAGUZI KATIKA MAJIMBO MATANO YA ZANZIBAR

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, leo amehit...

Latest Post

RAIS DKT. SAMIA AMPONGEZA MWANARIADHA SIMBU

Written By CCMdijitali on Saturday, September 27, 2025 | September 27, 2025



  • Amkabidhi Nyumba jijini Dodoma

  • Mheshimiwa Majaliwa asema Simbu ameliheshimisha Taifa

  • Atoa zawadi kwa Timu zilizofanya vizuri kimataifa

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amempongeza Mwanariadha Alphonse Simbu kwa kuwa Bingwa wa Dunia wa mbio za marathon za Tokyo na kwamba ataendelea kutoa kipaumbele katika sekta ya michezo ili itoe mchango zaidi katika kukuza uchumi wa nchi na kuongeza wigo wa upatikanaji ajira kwa vijana  

Pongezi hizo zimetolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Jumamosi (Septemba 27, 2025) alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye hafla kuwapongeza wanamichezo na timu zilizofanya vizuri kwenye medani za kimataifa, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa mikutano wa hotel jijini Dar es Salaam.

Katika tukio hilo Mheshimiwa Majaliwa alitangaza kuwa, Mheshimiwa Rais. Dkt. Samia amempatia Mwanariadha Simbu zawadi ya nyumba jijini Dodoma, sambamba na kikabidhiwa kitita cha shilingi milioni 20 ikiwa ni ishara ya kutambua ushindi huo ambao umeliletea Taifa heshima kwenye jukwaa la kimataifa"

"Mheshimiwa Rais Dkt. Samia ameandaa nyumba iliyopo mkoani Dodoma, ambayo itakabidhiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na zoezi hilo lisichukue muda mrefu kuanzia leo, tusiwe tunatamka ahadi za viongozi halafu zinakaa muda ambao mtu anajiuliza"

Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Mwanariadha Simbu ameandika ukurasa wa upekee kwa kuwa mtanzania wa Kwanza kutwaa tuzo ya dhahabu katika marathoni ya Dunia ya mwaka 2025 "Haya ni Mashindano makubwa zaidi ya riadha duniani baada ya Michezo ya Olympic, yakihusisha wanariadha Bora kutoka Mataifa yote duniani"

Amesema kuwa Serikali mara zote umekuwa ikiweka jitihada za kutosha za kuhakikisha sekta ya Michezo inakuwa na mchango kwa Taifa "Matokeo tunayoyashuhudia hivi sasa ni matokeo ya uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali ikiwemo ukarabati WA viwanja na kuongezwa kwa bajeti kutoka shilingi bilioni 38 mwaka 2022 Hadi bilioni 326 mwaka 2025/2026"

Katika hatua nyingine Mheshimiwa Majaliwa ametoa wito kwa wanamichezo nchini kuweka jitihada binafsi katika kushiriki katika michezo kwani ushindi unaweza kupatikana kwa kuweka nia "Wekeni mikakati ya ushindi ili muweze kuipeperusha bendera ya Taifa letu kimataifa".

Naye RAIS wa Shirikisho la Riadha Tanzania (SRT) Rogath Stephen ameishukuru Serikali kwa namna inavyotoa mchango kubwa kwa vyama na namna anavyoendeleza Michezo. "Hatujawahi kufanyiwa mambo ambayo kwasasa yanafanyika, kupitia Serikali tumekuwa tunahudumiwa kwa namna ya kipekee"

Kwa Upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Gerson Msigwa amesema kuwa Medali ya dhahabu ya Alphose Simbu imefanikiwa kupata tiba ya kiu ya Watanzania ya kupata Medali za dhabau katika michezo ya kimataifa. "Hii imewezekana kutokana na na maamuzi ya viongozi wetu kuwa na maono ya kurudisha heshima kwa Taifa baada ya kufanya uwekezaji mkubwa mchezoni"

Ameongeza kuwa Kiu kubwa iliyobaki ni kuhakikisha watanzania wanapata medali kwenye Michezo ya Olympic pamoja na michezo ya jumuiya ya madola "Sisi kama Serikali tumejipanga kuhakikisha tunafanikiwa kuleta medali hizi hapa nyumbani, tunaweka mikakati imara ya usimamizi, kwa sasa kuwa wasindikizaji imetosha, Tunaamini mwakani tunaweza kupata media kwenye Michezo ya jumuiya ya madola na 2028 tutapata medali kwenye olympic"

Timu nyingine zilizopongezwa na kupewa zawadi ya shilingi milioni kumi ni Timu ya Taifa ya Futsal ya Wanawake ambayo imefuzu kushiriki kombe la dunia (Philippines 2025), Timu ya JKT Queens ambao ni mabingwa wa Mashindano ya CAF Woman's Championship League Cecafa Qualifiers 2025.

Timu nyingine ni timu ya Taifa ya Cricket U-19 ambayo itashiriki mashindano ya Dunia 2026 nchini Zimbabwe na timu ya wenye ulemavu (Tembo Worriers) ambao wamekuwa mshindi wa Pili wa Michezo ya Afrika Mashariki na Kati.
Published from Blogger Prime Android App
Published from Blogger Prime Android App
Published from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android App

WANANCHI MAGU WAISHUKURU SERIKALI KUWAPATIA HATI ZA HAKIMILKI ZA KIMILA



Na Munir Shemweta, WANMM MAGU 

 

Wananchi wa vijiji vitatu vya Chandulu, Salama, Mwabulenga vilivyopo kata ya Ng'haya wilaya ya Magu mkoa wa Mwanza wameishukuru serikali kwa uamuzi wake wa kuwapimia na kuwamilikisha maeneo yao kwa kuwapatia Hati za Hakimilki za Kimila.

 

Zoezi hilo la kuwapatia Hati za Hakimilki za Kimila limefanyika baada ya kufanyika mipango wa matumizi ya ardhi pamoja na upimaji ardhi katika vijiji hivyo vitatu.

 

Mipango ya Matumizi ya Ardhi huwekwa katika maeneo mbalimbali kwa lengo la kuboresha usalama wa umiliki wa ardhi, kukuza matumizi endelevu ya ardhi pamoja na kupunguza migogoro ya ardhi.

 

Wananchi wa vijiji hivyo wametoa kauli hiyo tarehe 26 Septemba 2025 katika kijiji cha Chandulu wilayani Magu wakati wa zoezi la kutoa hakimilki za kimila kwa wananchi waliomilikishwa maeneo yao.

 

Jumla ya Hati za Hakimilki za Kimila 1,415 zimeandaliwa huku takriban hatimilki 5000 ukamilishaji wake ukiendelea ambapo Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhandisi Anthony Sanga alikabidhi Hati za Hakimilki za kimila 50 kwa niaba ya wannachi wote waliomilikishwa.

 

Wananchi hao wamesema, wanajisikia furaha kubwa kumilikishwa maeneo yao waliyoyaelezea kuwa sasa umilikishaji wake umeongeza thamani ya maeneo hayo.

 

"Najisikia vizuri sana kwa sababu ardhi yangu nimemilikishwa kwa hati na sitokuwa tena na uharaka wa kuiuza, niipongeze sana serikali kwa uamuzi wake huu wa kutumilikisha" amesema mkazi wa Chadulu Bw. Mashiku Machunge.

 

Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhandisi Anthony Sanga amewataka wananchi waliokabidhiwa Hati za Hakimilki za kimila kuhakikisha wanazitunza na kuacha tabia ya kuuza ardhi hovyo ili ziweze kusaidia vizazi vijavyo.

 

"Ndugu wananchi hati hizi inatakiwa mzitunze kwa sababu huu ni urithi wenu, ardhi hii ni ya kwenu mzitunze na pili tusiwe na tabia ya kuuza ardhi, ardhi tuitunze itusiadie sisi, watoto wetu, wajukuu zetu na watakaotufutia katika vizazi vyetu" amesema.

 

Ametaka hati milki walizokabidhiwa wananchi zilete mabadiliko ya kimaisha kwa kuwa mbali na kuwatambulisha kisheria lakini zinasaidia kupata mikopo na kueleza matarajio ya serikali ni kwamba pawepo matokeo chanya ya kimaendeleo na kusisitiza kuwa hati hizo zisiwe sehemu ya migogoro ya kudhulumiana.

 

Kwa upande wake Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Mwanza Bw. Wilson Luge ameeleza msingi mkubwa wa ofisi yake ni kuhakikisha wanawamilikisha wananchi maeneo yao kwa kuwapatia hati milki kwa kuwa ardhi ni rasimali itakayowawezesha kiuchumi.

 

"Ndani ya mkoa wa Mwanza katika halmashauri zote sita tutashirikiana na kampuni za upimaji kuhakikisha ardhi za wananchi wetu zinapimwa na kuwapatia hati zikiwemo hizi Hati za Hakimilki za kimila bila kuwacheleweshea" amesema Luge.

 

Zoezi la upimaji maeneo katika wilaya ya Magu limefanywa kwa ushirikiano na kampuni za upimaji za GMS Geo tech Consultancy Co.Ltd, GNT Property Ltd na CAIWAY Company Ltd ambazo zinatekeleza mazoezi katika vijiji 16 kati ya vijiji 82 vilivyoko ndani ya Wilaya ya Magu.

Published from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android App

Tanzania yalaani kuibuka upya kwa ukiukwaji wa sheria za kimataifa

Written By CCMdijitali on Friday, September 26, 2025 | September 26, 2025

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amesema Tanzania inalaani kuibuka upya kwa ukiukwaji wa sheria za kimataifa na kupelekea matumizi ya nguvu kama njia ya kutatua migogoro hali inayopelekea ukatili uliokithiri kwa binadamu hususani watoto, wanawake, wazee pamoja na wagonjwa katika maeneo ya migogoro.
 
Makamu wa Rais amesema hayo wakati akihutubia Kikao cha 80 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kinachofanyika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa Jijini New York nchini Marekani. Amesema uwepo wa mitazamo ya kibeberu, ikiwa ni pamoja na ile ya kuichukulia Afrika kuwa sehemu ya uchukuaji rasilimali na uporaji wa ardhi, pamoja na uwepo wa makampuni ya kimataifa kuendelea kufanikiwa kutokana na unyonyaji wa mali asili za Afrika, huku wakisababisha au kuunga mkono migogoro inapaswa kumalizika sasa.
 
Makamu wa Rais amesema Tanzania inauchukulia msimamo wa upande mmoja na matumizi mabaya ya nguvu za kijeshi, pamoja na kushindwa kwa jumuiya ya kimataifa na mataifa yenye nguvu duniani katika kukomesha umwagaji damu na vita vya hatari vinavyoendelea katika maeneo mengi duniani, kuwa ni jambo lisilokubalika.
 
Pia ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kutambua kuwa ongezeko la matumizi ya fedha katika masuala ya kijeshi ikiwemo utafiti na utengenezaji wa silaha ni jambo la kusikitisha na ni kinyume cha maadili. Amesema hali hiyo inazuia jitihada za kutafuta amani duniani, na inachukua kiasi kikubwa cha rasilimali ambazo zingeweza kutumika kuendeleza maendeleo endelevu na ustawi kwa wanadamu wote.
 
Makamu wa Rais amesema dunia inapaswa kuendelea kutafuta amani bila kuchoka kwani ndio sharti la maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Amepongeza juhudi za Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, viongozi wa dunia, na mashirika ambayo yanashiriki kikamilifu katika upatanishi na utatuzi wa migogoro katika nchi na maeneo kama vile Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Sudan, Urusi, Ukraine, na Mashariki ya Kati. Ametoa wito wa ushirikishwaji kamili wa wanawake katika kutafuta amani hususani katika kipindi hiki inaposherehekewa miaka 30 tangu azimio la Beijing na maendeleo yaliyopatikana katika kukuza usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake.
 
Amesema Rais wa kwanza mwanamke wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan ameonyesha njia katika kueleza sera na vitendo vinavyoimarisha nafasi ya mwanamke katika sekta zote za jamii. Amesema kikanda na kimataifa, amekuwa mtetezi wa amani, haki, usalama na matumizi ya nishati safi.
 
Amesema Tanzania kama mwanachama wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika, pia nafasi iliyotumikia kama Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa Ulinzi na Usalama Jumuiya ya SADC ilichangia kikamilifu katika mipango ya amani na kuunga mkono hatua za kuzuia na kutatua migogoro.
 
Tanzania imetangaza kugombea kiti kisicho cha kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa muhula wa 2029-2030, ili kuthibitisha dhamira iliyonayo ya amani na usalama duniani.
Halikadhalika, Makamu wa Rais amesema, Tanzania inasisitiza msimamo wa Afrika wa kurekebisha uwakilishi mdogo wa bara hilo katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, na kutoa wito wa kupitishwa kwa angalau viti viwili vya kudumu vya Afrika vyenye nguvu ya kura ya turufu.
 
Amesema Tanzania inaungana na nchi nyingine katika kudai mageuzi ya haraka na ya kina ya mfumo wa fedha wa kimataifa. Ametoa wito wa kuongeza ufadhili wa masharti nafuu wa muda mrefu, kurekebisha mifumo huru ya ukadiriaji wa mikopo, na kufikiria upya tathmini ya uhimilivu wa deni, ili kupatikana mtaji wa uwekezaji katika miundombinu, elimu, afya na kuhimili mabadiliko ya tabianchi. Amesisitiza nia ya kuongezeka kwa sauti na uwakilishi wa Afrika katika miundo ya utawala ya Shirika la Fedha Duniani (IMF) na Benki ya Dunia ambayo haijafanyiwa kazi kwa muda mrefu.
 
Makamu wa Rais amesema Tanzania imejitolea na imepiga hatua katika utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG’s 2030) ikifikisha asilimia 60. Amesema kwa lengo namba 3, Tanzania imefanikiwa kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi kutoka vifo 750 kwa kila vizazi hai 1000 mwaka 2000 hadi 104 mwaka 2022. Kwa lengo namba 6, upatikanaji wa maji safi na salama uliongezeka katika maeneo ya vijijini na mijini kutoka asilimia 32 na 55 mwaka 2000 hadi asilimia 79.9 na 94 mwaka 2024. Kwa nishati safi ya bei nafuu ambayo ni lengo namba 7, Tanzania imefanikiwa kuunganisha nishati ya umeme kwa vijiji 8,587 mwaka (2000) hadi 12,318 mwaka 2024 ambapo ni vijiji 15 pekee vilivyobaki bila umeme.
 
Makamu wa Rais amehimiza jumuiya ya kimataifa kuimarisha mwitikio wa pamoja wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Ametoa wito wa kutumia vyema fursa ya Mkutano wa wa COP30 nchini Brazil kuhakikisha ahadi zinatekelezwa ikiwemo uchangiaji wa Mfuko wa Hasara na Maafa kutokana na athari za mabadiliko ya tabianchi (Loss and Demage Fund) pamoja na kuongezwa kwa ufadhili wa masharti nafuu wa muda mrefu, uhamishaji wa teknolojia, na masharti ya kibiashara yanayozingatia haki ili kufanikisha ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa mataifa na kutafuta ushirikiano wa manufaa kwa pande zote katika matumizi ya rasilimali.
 
Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
26 Septemba 2025
New York – Marekani.
Published from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android App

MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR ASHIRIKI DUA YA KUIOMBEA NCHI

Written By CCMdijitali on Thursday, September 25, 2025 | September 25, 2025

 Wazazi na walezi wametakiwa kuwahimiza vijana wao katika kuitunza amani iliyopo nchini hasa katika kipindi hichi cha kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao.

 

Hayo yamesemwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt Hussein Ali Mwinyi katika dua ya kuiombea nchi iliyoandaliwa na ofisi ya mufti mkuu kanda ya Pemba na kufanyika katika Masjid Rahman uliopo Gombani Pemba.

 

Amesema kuwa  ni lazima kukaa pamoja na kushirikiana kwa kila jambo ili kuhakikisha wanapiga vita viashiria vyote vya uvunjifu wa amani na kusisitiza kuwa bila ya amani hakuna chochote cha kimaendeleo kinachoweza kufanyika nchini.

 

Alhajj Hemed amefahamisha kuwa wazizi na walezi ndio wahusika wakuu katika kuwaandalia vijana mazingira wezeshi ili kuweza kuishi katika hali ya amani na utulivu sambamba na kuyafaidi matunda ya kimaendeleo yanayoendea kutekelezwa na serikali ya Awamu ya Nane.

 

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewataka waumini kutokukubali kushawishiwa kuingia katika uvunjifu wa amani kwa  kisingizio cha siasa jambo ambalo sio sahihi.

 

Sambamba na hayo Alhajj Hemed amewashukuru waumini kwa kuendelea kuiombea dua nchi hasa katika kipindi hichi cha kuelekea uchaguzi mkuu wa nchi unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao.

 

Kwa upande wake Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh. MAHMOUD MUSSA WADI amewataka waumini wa dini ya kiislamu na wananchi kwa ujumla kuiombea dua nchi na viongozi wake kila wakati ili Mwenyezi Mungu aweze kuiepusha nchi na machafuko hasa kipindi hichi cha kuelekea uchaguzi mkuu wan chi.

 

Sheikh Mahmoud amesema historia inaonesha kuwa nchi nyingi duniani kila ifikapo kipindi cha uchaguzu hupatwa na taharuki ya kutoweka k wa amani katika nchi zao  hivyo ni wajibu wa kila mwananchi kuhakikisha anailinda amini kwa gharama yoyote kabla ya uchaguzi, wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi.

 

Imetolewa na Kitengo cha Habari (OMPR)

25.09.2025



SEKTA YA MADINI IMEENDELEA KUWA NGUZO YA UKUAJI WA UCHUMI-MAJALIWA

Written By CCMdijitali on Monday, September 22, 2025 | September 22, 2025



WAZIRI MKUU,Kassim Majaliwa amesema kuwa Sekta ya madini imeendelea kuwa nguzo ya uchumi nchini ambapo katika mwaka 2022 sekta hiyo imekua kwa asilimia 10.9 na kufikia mchango wa asilimia 10.1 kwenye Pato la Taifa mwaka 2024, ikilinganishwa na asilimia 9.0 mwaka 2023.

Ametoa kauli hiyo Leo (Jumatatu, Septemba 22, 2025) wakati wa uzinduzi wa Maonesho ya Nane ya Teknolojia ya Madini Mkoa wa Geita, yaliyofanyika katika viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Amesema kuwa hatua hiyo imetokana na jitihada mbalimbali za Serikali ya awamu ya sita ikiwemo kuimarishwa kwa mifumo ya ukusanyaji wa mapato na udhibiti wa biashara ya madini, matumizi ya mifumo ya kielektroniki (online mining cadastre system), uwepo wa masoko ya madini na ufuatiliaji wa mikataba ya uwekezaji.

"Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuweka kipaumbele katika kuimarisha mazingira ya uwekezaji kwenye sekta ya madini ili rasilimali za madini zichangie kwa katika ukuaji wa uchumi na ustawi wa Watanzania wote".

Waziri Mkuu ametoa rai kwa wadau wa sekta ya madini kuendelea kuwekeza katika teknolojia kwani ndiyo daraja la mageuzi kuanzia utafiti na uchimbaji, usafishaji na biashara ya madini. "Bila teknolojia sahihi, haiwezekani kuongeza tija, kuhakikisha usalama wa wachimbaji, kulinda mazingira, wala kufanya uongezaji thamani wa madini yetu".

Ameongeza kuwa kupitia maonesho hayo, katika kiipindi cha mwaka 2021 hadi 2025 Wachimbaji wadogo wa Geita wamezalisha zaidi ya kilo 22,000 za dhahabu zenye thamani ya Shilingi Trilioni 3.44, huku Serikali ikipata zaidi ya Shilingi Bilioni 235.5 kama mrabaha. "

Aidha, makampuni makubwa kama Geita Gold Mine na Buckreef katika kipindi hicho wamezalisha kilo 76,530 za dhahabu zenye thamani ya Shilingi Trilioni 11.38, na Serikali kupata zaidi ya Shilingi Bilioni 793 kama mrabaha."

Kwa Upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Mhandisi Yahya Samamba amesema kuwa Tanzania sasa imepiga hatua kwa kuwa na viwanda vya kutengeneza zana mbalimbali za uchimbaji wa madini.

"Katika mwaka wa fedha 2024-2025 tumeweza kuzalisha tani 62 za dhahabu tofauti na nyuma tulikuwa tukizalisha tani 40-50 kila mwaka hii inatufanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi tano bora Afrika katika uzalishaji wa dhahabu."

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigela amesema huo umefanya kazi kubwa ya kusambaza umeme vijijini na kwa kuwa kazi ya uchimbaji unahitaji umeme tayari umeme umepelekwa katika maeneo mengi ya wachimbaji wadogo.

"Tumefanyia kazi maagizo ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kupeleka umeme katika maeneo ya wachimbaji wadogo ili wafanye kazi zao na kuwa na uzalishaji wa uhakika katika maeneo yao."

Published from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android App

WASIRA: DK. SAMIA, CCM WAMEDHARIA KULETA MABADILIKO KATIKA MAISHA YA WATANZANIA

Written By CCMdijitali on Thursday, September 18, 2025 | September 18, 2025


WASIRA: DK. SAMIA, CCM WAMEDHARIA KULETA MABADILIKO KATIKA MAISHA YA WATANZANIA

Na MWANDISHI WETU, MBEYA

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira, amesema Chama kinafanya kazi kubwa ya kuleta mabadiliko ili kuwaletea maendeleo wananchi.

Aidha, amesisitiza wananchi wandelee kukiamini na kukipa nafasi Chama kiendelee kudumisha amani kwa kuwa maendeleo hayatapatikana iwapo itatoweka.

Wasira alieleza hayo alipokuwa akizungumza na viongozi na wanachama wa CCM kutoka Jimbo la Mbeya, akiwa katika ziara ya kumwombea kura mgombea urais wa CCM Dk. Samia Suluhu Hassan pamoja na wagombea wa ubunge na udiwani mkoani Mbeya, jana.

Alitumia mkutano huo kumwombea kura Dk. Samia, wagombea ubunge na udiwani waliosimamishwa kupeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, mwaka huu.

"Kazi yetu ni kuleta mabadiliko katika maisha ya watu, maendeleo ni mabadiliko katika maisha ya watu, ukitengeneza barabara unamwezesha huyu mtu aweze kufikisha bidhaa zake sokoni kwa hiyo ataongeza kilimo na uchumi wake utaongezeka kwa sababu ana mahali pakuuza.

"Ukimnyima barabara analima chakula chake cha kula na kufa, anakula ashibe angojee kifo maana hakuna maendeleo hapo," alisema.

Alisema kuwajengea wananchi miundombinu muhimu ikiwemo ya hospitali ni kuwapunguzia safari ya kwenda kutafuta dawa maeneo ya mbali kutoka katika makazi yao.

"Tumepiga hatua lakini maendeleo hayana kikomo na wala hayamalizi matatizo yote kwa mpigo kwa sababu hata ukifanya maendeleo makubwa zaidi unaweza ukazalisha matatizo mapya.


MIAKA MINNE YA MAFANIKIO

Alieleza kuwa, katika miaka CCM i.esimamiamaendeleo makubwa katika ngazi mbalimbali ambayo yamewagusa wananchi moja kwa moja.

"Tukisema Samia mitano tena ni kwa sababu kuna kazi amefanya na ameifanya kwa uzuri na ana uzoefu wa kuifanya, ametekeleza vema miradi mikubwa iliyoachwa na mtangulizi wake likiwemo bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere.

"Amejenga lile bwawa limefikia asilimia 100, sasa tuna megawati 4000 badala ya 16,000 alizoachiwa na mtangulizi wake na sasa hakuna shida ya umeme labda matatizo ya miundombinu lakini hakuna shida ya mahitaji ya umeme," alisema.

Kwa miaka minne na nusu serikali imejenga shule tisa mpya za msingi hapa kwenye wilaya yenu na amejenga madarasa 280 mapya tena sio mapya tu bali mapya mazuri, amejenga sekondari mpya nane katika wilaya hii katika muda wa miaka minne na nusu, amejenga madarasa ya sekondari 218 na hamkuchangishwa kwa madarasa hayo.

KUHUSU AMANI
Alisisitiza Watanzania kulinda amani kwa kuwa ndiyo nyenzo muhimu ya kuleta maendeleo ya sekta zote.

Wasira alisema ukipoteza amani unapoteza maendeleo kwa sababu hata maendeleo yaliyofikiwa hayawezi kuwa na msaada kwa maisha ya watu.

"Amani ikipotea hata madaraja tuliyojenga hayana maana, hata barabara zinachimbika kwa sababu amani imetoweka kwa hiyo kqzi yetu kama chama cha Mapinduzi pamoja na kulinda u.oja wa taifa tunataka kuhakikisha amani amani inakuwepo kwa sababu ikitoweka hakuna maendeleo na haya yote mnayosema hapa hayatakuja," alieleza.

Kwa upande wake Kaimu Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya, Ndele Mwaselela alisema Chama mkoani humo kimejipanga vema kuhakikisha uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, mwaka huu wagombea wake wote wanapata kura za kishindo.

Mwaselela alisema wamejipanga kumtafutia kura nyingi Dk. Samia zitakazomwezesha kuibuka mshindi aendelee kuiongoza nchi kwa mafanikio.

Mgombea ubunge katika Jimbo la Mbeya Vijijini, Patali Shida, alisema iwapo ataibuka mshindi ataendelea kusimamia vema kasi ya maendeleo kuendeleza iliyofanyika katika miaka mitano iliyopita.

Published from Blogger Prime Android App
== ==
VV1
Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Stephen Wasira akimnadi mgombea ubunge wa Jimbo la Mbeya Vijijini, Patali Shida katika mkutano wa viongozi wa CCM Jimbo la Mbeya Vijijini, Mbalizi mkoani Mbeya, jana. (Na Mpigapicha Wetu).
...

...

Viongozi wa CCM Jimbo la Mbeya Vijijini wakimsikiliza
Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Stephen Wasira alipozungumza nao katika mkutano uliofanyika Mbalizi, mkoani Mbeya, jana (Na Mpigapicha Wetu).

WASIRA- ILANI YA UCHAGUZI CCM INAGUSA MAISHA YA WATU ,WATAICHAGUA

Written By CCMdijitali on Wednesday, September 17, 2025 | September 17, 2025



NA MWANDISHI WETU, MBEYA

MAKAMU MMwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira amesema Watanzania wataichagua CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu kwa kuwa Ilani yake ya Uchaguzi inagusa maisha na maendeleo yao.

Amesema hakuna chama chochote cha siasa miongoni mwa vyama vinavyoshiriki uchaguzi huo ambacho kimejipanga kufanya mambo mazuri kama ilivyo CCM, hivyo wananchi hawataona sababu ya kuvichagua.

Wasira alieleza hayo jana mjini Mbeya alipozungumza na viongozi wa Chama kutoka majimbo ya Mbeya mjini na Uyole, alipokuwa akimwombea kura Mgombea Urais wa CCM, Dk. Samia Suluhu Hassan na kuweka mikakati ya ushindi katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, mwaka huu

"Yako mambo mengi tumedhamiria kuyafanya kupitia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2030 kwa manufaa ya wananchi.

"Elimu tumekubaliana tubadili mfumo wa elimu ili kijana akienda sekondari 'school' (shule ya sekondari) akitoka anajua ujuzi wa kazi. Tumeeneza umeme, tunapeleka maji, ukiwa na maji ya bomba endapo bomba likiharibika unafanyaje, lazima uwe na watu hapo mtaani kwako ambao wanaweza kurekebisha bomba na ndio kazi yao watakuwa wamesoma," alisema.

Alisema kutokana na kazi kubwa inayofanyika kutanua fursa mbalimbali ikiwemo ya kusambaza umeme, ni muhimu kuwa na mafundi wenye uwezo wa taaluma za umeme hadi vijijini na hiyo ni moja ya sababu za kubadili mfumo wa elimu uendane na mahitaji ya wakati.

"Tumesema katika Ilani hii vijana wasome, waanzishe kampuni zao zinazoendana na ujuzi wao na sisi tuwape mitaji waweze kufanya kazi ya kujiajiri na kuajiri wenzao na hii wamefanya Korea Kusini na wameweza, kwa nini sisi hatuwezi," alieleza.

Kwa mujibu wa Wasira, CCM inakusudia kuimarisha zaidi huduma za afya, kuwapa bima Watanzania wote wenye uwezo na wasiokuwa nao na kwamba sasa Bunge linatafuta vyanzo vya mapato kuona namna ya kugharimia bima kwa wasio lna uwezo.

Aliwataka viongozi hao kuhakikisha wanafikisha kwa wananchi elimu kuhusu ahadi za maendeleo zilizomo ndani ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM.

"Sasa tukiyajua hayo tunaenda kwa wananchi maana mimi nawatuma nyie mwende kwa wananchi na elimu ninayowapa muipeleke kwa wananchi waelewe kumbe ndiyo mambo ya CCM haya, kumbe kuna bima, kumbe kuna elimu yenye ujuzi, kumbe maji yataongezeka," alisisitiza.


MBEYA MJINI KUNG'ARISHWA

Akizungumzia ahadi za Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa jiji la Mbeya, alisema kuhusu elimu ya msingi na sekondari inakusudia kujenga madarasa 1,600 kwa kuwa idadi ya watoto wanaozaliwa inaendelea kuongezeka.

Kwenye Afya alisema zahanati 10 na vituo vya afya vitano vipya vitajengwa pamoja na kuboresha huduma.

Ili kuzidi kuling'arisha jiji hilo alisema zitawekwa taa za barabarani, "taa zile kubwa takribani 100 kwa ajili ya kuleta mwanga na tutasimamia ujenzi wa barabara za mjini kwa ajili ya kuwa na mitaa inayovutia na kama nilivyosema tutaongeza huduma ya maji pamoja na yale ambayo niliyasema kuhusu uchumi.


HAKUNA WA KUSHINDANA NA CCM

Alisema kwa sasa hakuna chama cha siasa miongoni mwa vinavyowania nafasi katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu ambacho kina sera na ilani bora kama ya CCM.

"Sasa chama chenye sera na ilani ya kutushinda kiko wapi, maana tulipotoa hii ilani kiongozi mmoja wa chama cha siasa alitupigia simu akasema sasa CCM mmeandika mambo yote sisi tutaandika nini, nikasema hayo yetu muwe mnasoma halafu mnanukuu mnasema kama CCM ilivyosema.

Aliwahimiza wana CCM kuwauelimisha wananchi waielewe Ilani hiyo, pia kuweka mkakati wa kuhakikisha wananchi hususa wana CCM wanapiga kura.


Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Stephen Wasira akimkabidhi Ilani ya Uchaguzi ya CCM Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Patrick Mwalunenge katika mkutano wa viongozi wa CCM kutoka Jimbo la Uyole na Mbeya Mjini, mjini Mbeya. (Pich na CCM).




 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link