ZANZIBAR KUWA KITOVU CHA UTALII WA MICHEZO | RAIS MWINYI
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali itaendelea kuwekeza katika ujenzi na u...
Latest Post
January 01, 2026

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali itaendelea kuwekeza katika ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya michezo kwa lengo la kuifanya Zanzibar kuwa kituo maalum cha utalii wa michezo kitaifa na kimataifa.
Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 01 Januari 2026, aliposhiriki Bonanza la 16 la Mazoezi ya Viungo lililoandaliwa na Chama cha Mazoezi ya Viungo Zanzibar (ZABESA), lililofanyika katika Uwanja wa New Amaan Complex, Mkoa wa Mjini Magharibi. Bonanza hilo limehusisha vikundi 165 vya mazoezi kutoka vilabu 25 vya Pemba, 100 vya Unguja na 40 kutoka Tanzania Bara, likiwa na washiriki zaidi ya 500.
Amesema mazoezi ya viungo ni nguzo muhimu ya afya ya mwili na akili, na husaidia kuongeza kinga dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo kisukari, shinikizo la damu na magonjwa ya moyo.
Aidha, amebainisha kuwa bonanza la kila mwaka ni jukwaa muhimu la kuwakumbusha wananchi umuhimu wa afya njema kwa maendeleo ya mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
Rais Dkt. Mwinyi amewahimiza wananchi kuendelea kushiriki michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, volleyball, riadha pamoja na michezo ya asili ya kitamaduni ili kuimarisha afya zao. Ameeleza pia kuwa Serikali itaendelea kuhimiza mabonanza, matukio ya michezo, ligi na mashindano ya kitaifa na kimataifa ili kuongeza mvuto wa utalii wa michezo Zanzibar.
Amefafanua kuwa michezo ni sekta muhimu inayochangia maendeleo ya utalii na uchumi wa Taifa kwa kuvutia watalii na wawekezaji, kuongeza fursa za ajira kwa vijana na kukuza pato la Taifa. Serikali, kwa kushirikiana na wadau wa michezo, itaendelea kuimarisha miundombinu ili kufikia viwango vya kitaifa na kimataifa na kuendeleza vipaji kuanzia ngazi ya chini hadi ya juu.
Rais Dkt. Mwinyi amesema kupitia programu madhubuti za mafunzo, nidhamu na usimamizi bora, Zanzibar inaweza kuzalisha wanamichezo bora watakaoshindana kimataifa na kuinua hadhi ya Taifa pamoja na kuboresha maisha yao na familia zao. Ameongeza kuwa Serikali imeimarisha kwa kiwango kikubwa miundombinu ya michezo ikiwemo Uwanja wa Amaan Complex, Gombani na Mao Tse Tung, sambamba na ujenzi wa viwanja 17 unaoendelea katika mikoa yote, ambapo baadhi tayari vimekamilika.
Mapema, Rais Dkt. Mwinyi aliwaongoza mamia ya wana mazoezi katika matembezi maalum kutoka Michenzani kupitia Muembe Kisonge hadi Uwanja wa New Amaan Complex, kabla ya kushiriki mazoezi ya pamoja. Amewapongeza ZABESA na wadau wote kwa kufanikisha bonanza hilo na kuwakabidhi vyeti vya shukrani, huku akihimiza kuendelea kuliunga mkono. Aidha, alipata fursa ya kusalimiana na mwanariadha wa kimataifa wa Tanzania, mshindi wa medali ya dhahabu ya mbio za marathon, Alphonce Simbu, aliyeshiriki bonanza hilo.

ZANZIBAR KUWA KITOVU CHA UTALII WA MICHEZO | RAIS MWINYI
Written By CCMdijitali on Thursday, January 1, 2026 | January 01, 2026

Labels:
ZANZIBAR