MIUNDOMBINU YA ELIMU ZANZIBAR SASA YALINGANA NA MAHITAJI YA KARNE YA 21
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Zanzibar imepiga hatua kubwa katika kuimarisha mazin...
Latest Post
November 02, 2016
Mkenya anapokiri hakuna kama Magufuli Afrika
Written By CCMdijitali on Wednesday, November 2, 2016 | November 02, 2016
WAKATI akielekea kutimiza mwaka mmoja akiwa madarakani, wiki hii Rais John Magufuli alifanya ziara ya siku mbili nchini Kenya kwa mwaliko wa Rais Uhuru wa Kenyatta wa Jamhuri ya Kenya. Hii ilikuwa ni ziara yake ya tatu nje ya nchi tangu aingie madarakani mwezi kama huu mwaka jana. Ziara nyingine alizokwishafanya nje ya nchi ni pamoja na ya Rwanda na Uganda.
Mwanasheria, mhadhiri na mchambuzi wa mambo mbali wa Kenya, Profesa Patrick Lumumba ni miongoni mwa watu wa nje ya nchi ambao wamekuwa wakikoshwa na uongozi wa Rais Magufuli.
Tangu Desemba mwaka jana, ikiwa ni siku chache tu tangu Rais John Magufuli ashike madaraka, profesa huyu anayeheshimika sana Afrika, alionesha kufurahishwa, kuridhika na kumtabiria makubwa Rais wa Awamu ya Tano wa Tanzania.
Katika mjadala mmoja unaopatikana katika (www.youtube.com/watch?v=9VunShPDovY)
MAGUFULI IS THE REAL DEAL-PLO Lumumba and Barrack Mulaka on Magufuli
MAGUFULI IS THE REAL DEAL-PLO Lumumba and Barrack Mulaka on Magufuli
Profesa huyo wa sheria, maarufu kama PLO Lumumba, anakaririwa akisema kwa Kiingereza kuwa Magufuli ni ‘real deal’, akimaanisha ni kiongozi shupavu ambaye anachokifanya haigizi bali ndivyo alivyo.
Profesa huyo anasema: "Naweza kukuhakikishia kwamba taswira na mtazamo wa Mwalimu Nyerere sasa vinajitokeza dhahiri kwa Rais Magufuli."
Anaendelea: "Na wale wanaodhani kwamba, haya anayoyafanya ni nguvu ya soda wakidhani yanayotokana na msukumo wa uchaguzi, watakuja kushangaa sana.
“Huyu ni mtu ambaye ndani ya miaka 10 ataonesha njia kuhusu uongozi bora na uliotukuka katika eneo hili la Afrika Mashariki.
Mimi si mtabiri …, lakini angalia hali itakavyokuwa." Siku chache baadaye, Profesa Lumumba, ambaye aliwahi kuongoza Kamati ya Maadili na Kupambana na Rushwa ya Kenya, (EACC), pia alisikika akimpongeza Magufuli kupitia mahojiano aliyofanyiwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC).
Alikaririwa akisema, Magufuli amechukua njia sahihi ambayo anaamini muda si mrefu, Watanzania wataanza kunufaika na uongozi wake.
“Rais Magufuli amedhihirisha kwamba yeye kauli yake ni kutenda kazi na amedhihirisha kwamba uongozi mzuri ni utumishi si usultani. Kwa hivyo kwa Watanzania wengi na wadadisi wengi hizi ni hatua ambazo zinashabikiwa na kusifiwa," alikaririwa akisema.
Akaongeza kwamba hatua ya Rais Magufuli ya kupambana na ufisadi na ubadhirifu wa mali za umma ni jambo ambalo wananchi wengi wa kawaida wanatazamia kuliona kwa rais wao na kwamba hilo litaisaidia sana Tanzania kupiga hatua kimaendeleo.
Akasema hatua ya Rais Magufuli kushiriki katika shughuli za usafi mwaka jana, ilimaanisha pia kwamba yuko tayari kuisafisha Tanzania nzima, si katika mazingira pekee bali pia dhidi ya ufisadi na kuhakikisha wananchi wanaishi maisha mazuri.
Alirudia kusema katika mahojiano hayo na BBC kwamba hatua anazochukua Rais Magufuli si za kujionesha bali anafuata nyayo za marais waliofanya kazi ya kutukuka Afrika kwa ajili ya wananchi na si matumbo yao.
Akawataja viongozi hao ni Mwalimu Nyerere na Kwame Nkrumah wa Ghana.
“Rais Magufuli ameonesha Unyerere na Unkrumah na nina hakika kwamba atawadhihirishia watu kuwa yeye ni mtu mwenye azma njema na Tanzania itakuwa nchi ya kupigiwa mfano katika siku za usoni,” alisema.
Aidha, hivi karibuni, akiwa kwenye mkutano nchini Ghana, Profesa Lumumba katika kuzungumzia hali ya uongozi katika nchi za Afrika, aliendelea kueleza namna anavyomkubali Magufuli. Katika video fupi iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii, ilimuonesha mwanasheria na mwanasiasa huyo nguli akisema:
"Miongoni mwenu wapo ambao wanatarajia kuwania uongozi kisiasa. Lakini swali la msingi la kujiuliza ni hili: Kwa nini unataka kuongoza?
"Katika Afrika, njia nyepesi ya kupata utajiri wa harakaharaka ambao huwezi kuutolea maelezo namna ulivyopatikana ni kuingia katika uongozi wa kisiasa. Kama unataka kupata utajiri bila kuufanyia kazi kwa namna yoyote basi ingia kwenye siasa za Afrika.
"Huo ndio ukweli, nenda kila mahala Afrika isipokuwa kwa watu wachache sana. Mtu pekee anayeonekana kwa sasa mintarafu suala zima hilo (la kutumikia wananchi na siyo kutafuta utajiri) ni Rais wa Tanzania, John Magufuli.
"Waliobaki katika Afrika... Sijui... Mtanisamehe mimi ni mgeni hapa (Ghana). (Viongozi wetu wengi) wanawinda na kujikusanyia majumba, magari na pesa na hiyo ndio maana uongozi wa Afrika hauwavutii watu wazuri kabisa, wanaume au wanawake.
"Na kwa bahati mbaya sana, wapiga kura nao wanaruhusu kununuliwa kwa pesa, na sina hakika kama hilo linatokea pia hapa Ghana.
"Wapiga kura wa Afrika nao wanatazamia kuhongwa na wagombea ili waweze kuwapigia kura," alisema Profesa huyo ambaye ameshiriki katika mikutano na makongamano kadhaa Afrika.
Katika kipande hicho cha video, Profesa anamalizia kusema kwamba, kama Afrika haitapambana na ukabila (kuchagua mtu kwa ukabila) na rushwa, basi ijue kwamba bara hili halitaweza kamwe kupata viongozi wazuri. Katika baadhi ya nukuu za Profesa Lumumba aliwahi kusema:
"Tunaishi katika bara ambalo tunawapigia makofi na kuwashangilia wezi lakini tunawanyanyasa watu wazuri."
Kadhalika katika nukuu zake maarufu ni hii aliyopata kusema: "Tuna madaktari ambao tumewasomesha lakini tunapokuwa wagonjwa, hasa tabaka la wanasiasa, tunakimbilia London kwa kuwa hatuna imani na madaktari wetu wala hospitali zetu. Hii ni kutokana na ukweli kwamba rushwa imekita mizizi katika mfumo wetu wa maisha kiasi kwamba hatuwezi kufikiria hali za hospitali zetu za taifa." Profesa huyu pia aliwahi kusema katika nukuu yake nyingine:
"Tunachagua wezi kwa kuzingatia ukabila au ukubwa wa pochi zao (pesa) na bado tunatarajia wafanye mema. Haiwezekani." Pia nukuu yake nyingine ni hii: "Kiongozi mzuri na makini lazima atambuliwe kwa uwezo na uzuri wake na kiongozi dhaifu lazima atambuliwe kwa udhaifu wake."
Aliwahi kunukuliwa pia akisema: "Sisi (Afrika) tunachagua wezi, fisi ili wawalinde mbuzi lakini wakati mbuzi wetu wanapoliwa (na hao fisi) tunashangaa. Tunashangaa nini?" Profesa Patrick Lumumba aliyezaliwa Julai 17 mwaka 1962 nchini Kenya, ni Wakili wa Mahakama Kuu za Kenya na Tanzania.
Pia ni Mhadhiri wa Sheria katika Kitivo cha Sheria, Chuo Kikuu cha Nairobi.
Habari Leo
Labels:
KITAIFA,
Video Category
November 02, 2016
Uongozi wa Chama cha Wafanyakazi (ZAPSWU) wakutana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Uongozi wa Chama cha Wafanyakazi wa Sekta za huduma za Umma{ ZAPSWU } Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Kulia ya Balozi Seif ni Mwenyekiti wa Chama cha ZAPSWU Nd. Nd.Ameir Mwadini na kushoto ya Balozi Seif ni Katibu Mkuu wa Chama hicho Bibi Mwatum Othman.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Sekta za Huduma za Umma Zanzibar { ZAPSWU } Bibi Mwatum Othman aliyesimama akitoa ufafanuzi katika Kikao cha mrejesho wa agizo la Balozi Seif aliloupa Uongozi huo mnamo Tarehe 9 Juni mwaka 2016 wa kukutana na Wizara ya Fedha kuangalia namna ya kulitafutia ufumbuzi wa shamba la mipira Kichwele.
Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Sekta za Huduma za Umma Zanzibar Nd. Ameir Mwadini.
Baadhi ya Viongozi wa Chama cha Wafanyakazi wa Sekta za Huduma za Umma Zanzibar
{ ZAPSWU } wakifuatilia mazungumzo yao na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif.
Picha na – OMPR – ZNZ.
Kulia ya Balozi Seif ni Mwenyekiti wa Chama cha ZAPSWU Nd. Nd.Ameir Mwadini na kushoto ya Balozi Seif ni Katibu Mkuu wa Chama hicho Bibi Mwatum Othman.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Sekta za Huduma za Umma Zanzibar { ZAPSWU } Bibi Mwatum Othman aliyesimama akitoa ufafanuzi katika Kikao cha mrejesho wa agizo la Balozi Seif aliloupa Uongozi huo mnamo Tarehe 9 Juni mwaka 2016 wa kukutana na Wizara ya Fedha kuangalia namna ya kulitafutia ufumbuzi wa shamba la mipira Kichwele.
Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Sekta za Huduma za Umma Zanzibar Nd. Ameir Mwadini.
Baadhi ya Viongozi wa Chama cha Wafanyakazi wa Sekta za Huduma za Umma Zanzibar
{ ZAPSWU } wakifuatilia mazungumzo yao na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif.
Picha na – OMPR – ZNZ.
Press Release:-
Wafanyakazi wa shamba ya mipira Kichwele lililopo Wilaya ya Kaskazini “B” wameiomba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuandaa utaratibu utakaowapa idhini ya kulihudumia shamba hilo kiuzalishaji baada ya Kampuni iliyopewa jukumu la kuliendesha shamba hilo ya Agro Tec kushindwa kuliendeleza.
Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Sekta za huduma za Umma{ ZAPSWU } Tawi la Shamba hilo Bibi Kazija Sheha Mohammed alitoa ombi hilo wakati Uongozi wa Chama hicho Taifa ulipofika Ofisini kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kufanya mrejesho wa agizo aliloupa mnamo Tarehe 9 Juni mwaka 2016 wa kukutana na Wizara ya Fedha kuangalia namna ya kulitafutia ufumbuzi wa shamba hilo.
Bibi Kazija alisema wafanyakazi wa shamba la mipira Kichwele kwa sasa wanaendelea kukabiliwa na ukali maisha kufuatia Uongozi wa Kampuni ya Agro Tek kusitisha uzalishaji wa mipira uliokwenda sambamba na kulimbikiza madeni ya mishahara ya muda mrefu ya wafanyakazi hao.
Alisema endapo Serikali Kuu itaridhia ombi lao upo uwezekano mkubwa kwa ari waliokuwa nayo wafanyakazi hao kuliendeleza shamba hilo kwa nia ya kutafuta faraja ya kupunguza changamoto za muda mrefu zinazowakabili katika mradi huo wa uwekezaji.
Alieleza kwamba changamoto kama hiyo kwa wafanyakazi wenzao wa Kisiwa cha Pemba imeshapatiwa ufumbuzi baada ya Uongozi wa Mkoa kuwapa ruhusa ya kuendeleza mradi huo ili kukidhi mahitaji yao.
Bibi Kazija alieleza kwamba wafanyakazi wa shamba la Mipira Pemba wamerejea tena katika uzalishaji wa zao la mipira na kuwaingizia mapato yanayosaidia kurejesha madeni, kulipa wafanyakazi pamoja na walinzi wa shamba hilo.
Alifahamisha wazi kwamba katika kuhakikisha mradi huo wa mipira kwenye shamba la Kichwele unarejea katika uhalisia wake Wafanyakazi hao karibu 350 waioachwa kabla ya kufungwa mradi huo tayari wameshajipanga hata Kiuongozi katika kuona kazi za uendelezaji na ugemaji wa utomvu zinafanyika kama awali.
Mapema akitoa mrejesho wa agizo la Balozi Seif la kukitaka Chama cha Zapswu kukutana na Wizara ya Fedha kutafuta ufumbuzi wa tatizo la shamba hilo Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho Nd. Suleiman Juma alisema Wizara ya Fedha haikuwa na kipengele cha moja kwa moja kinachoruhusu njia ya ulipaji wa madeni ya Wafanyakazi wa Shamba hilo.
Nd. Suleiman alisema Uongozi wa Wizara ya Fedha ulifafanua wazi kwamba inakuwa vigumu kwa wafanyakazi hao kupatiwa haki zao kupitia Wizara hiyo kwa vile Kampuni iliyowaajiri ilikuwa binafsi.
Naye Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Sekta za Huduma za Umma Zanzibar { ZAPSWU } Bibi Mwatum Othman aliiomba Serikali Kuu kuwaagiza watendaji wake waandamizi na wale wa ngazi za Kati kutoa ushirikiano wa karibu na Vyama vya Wafanyakazi kwa nia ya kupunguza migogoro kati ya waajiri na Wafanyakazi.
Bibi Mwatum alisema yapo malalamiko mengi kwa baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi tofauti yanayokosa kushughulikiwa licha ya kuripotiwa kwenye vyama vya Wafanyakazi sababu ni dharau za watendaji waandamizi wenye tabia ya kuwakimbia kwa mazungumzo viongozi wa vyama vya wafanyakazi.
Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alisema Taifa halina nia ya kulikataa ombi la wafanyakazi hao, lakini kinachopaswa kuzingatiwa kwa sasa ni kulifikisha Serikalini ili kuangalia hatua zinazostahiki kuchukuliwa.
Balozi Seif alisema Ilani ya CCM Imekuwa ikitoa miongozo kwa wananchi kutafuta mbinu za kujiajiri ili kuendesha maisha yao ya kila siku na lazima yasimame katika njia na misingi ya halali.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliupongeza Uongozi wa Chama cha Wafanyakazi wa Sekta za huduma za Umma{ ZAPSWU } kwa jitihada unazochukuwa za kufuatilia changamoto zinazowakabili wanachama wao katika taasisi mbali mbali hapa nchini.
Kampuni ya Agro Tec ilikuwa ikikabiliwa na madeni ya zaidi ya shilingi Milioni 284,839,982/- ikiwa ni pamoja na Mishahara ya wafanyakazi wa mashamba ya Mipira Unguja na Pemba, fedha za Likizo pamoja na deni la ZSSF kwa wafanyakazi wake katika kipindi kati ya miezi Mitatu hadi Minane.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
2/11/2016.
Labels:
KITAIFA
November 02, 2016
Taarifa ya ziara ya Siku tano ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Gambo,Wilayani Longido - ARUSHA.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha
Mhe. Mrisho Gambo (aliyeko kwenye mtaro) akishiriki ujenzi wa daraja la chini
linalojengwa na wananchi wa Mundarara,Wilayani Longido .
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
OFISI YA MKUU WA MKOA ARUSHA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo katika utaratibu wake aliojiwekea wakutembelea Wilaya zote za Mkoa huu amekamilisha ziara ya kikazi ya SIKU TANO aliyoifanya katika Wilaya ya Longido kuanzia tarehe 24 -28/10/2016. Lengo ni kujitambulisha kwa wananchi, kufahamu changamoto na kuzitafutia ufumbuzi, kuona fursa zilizopo, kushiriki pamoja shughuli za maendeleo na kukagua miradi ya Maendeleo.
Mhe.Gambo alitembelea Tarafa zote nne za Longido, Enduimet, Kitumbeine pamoja na Engarenaibor kwenye Kata za GelaiLumbwa, GelaiMerugoi, Kitumbeine, Engarenaibor, Matale, Tingatinga, Olmolog, Sinya, Namanga, pamoja na Kata ya Longido. Pia alifanya mikutano ya hadhara na wananchi wa Vijiji na vitongoji vipatavyo kumi na tano.
Vilevile, Mkuu wa Mkoa alitembelea eneo la mpaka wa Tanzania na Kenya (Normans Land) na aliweza kukutana na wafanyakazi wa Taasisi za Serikali zinazotoa huduma eneo la mpakani pamoja na wafanyakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido.
Kupitia ziara hiyo ya kazi Mhe.Gambo alibaini na kutoa maelekezo katika maeneo yafuatayo:
i. Mtandao wa Barabara – Barabara ya Esokonoi yenye urefu wa Km 25 iliyofunguliwa na kujengwa na wananchi kwa kutumia zana za asili iingizwe kwenye mtandao wa barabara za Halmashauri na kutengewa Fedha kwa ajili ya kukamilisha ujenzi ili kuunga mkono jitihada za wananchi. Pia aliwajulisha wananchi kuwa barabara ya Namanga – Sinya – Elerai imepandishwa hadhi kuwa barabara ya Mkoa kupitia kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa cha tarehe 22/10/2016; Aliwataka Halmashauri kukamilisha haraka miradi ya Barabara iliyopo ili kuwaondolea kero wananchi.
ii. Afya ya Jamii na uboreshaji wa miundombinu ya Afya – Wananchi walilalamikia upungufu wa dawa vituoni pamoja na huduma za afya kupatikana mbali na makazi yao. Rc Gambo alisema “Serikali ya Wilaya lazima ianze ujenzi wa Vituo vya Afya kwenye Kata za Kitumbeine na Namanga ili kuwasogezea wananchi huduma na ukizingatia wananchi wa Namanga huenda kutibiwa Kenya kutokana na kukosekana kwa huduma hii; Ujenzi wa Kituo cha Afya Namanga ufanyike kwenye eneo ilipokuwa Kambi ya Mkandarasi Namanga na kwa kuanza nachangia Bati 100 pamoja na mifuko ya saruji 100 nahitaji ujenzi huo uanze mara moja”.
Aliongeza kuwa Idara ya Afya iendelee kutoa elimu na kuhamasisha wananchi kuendelea kujiunga na mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) ili kupunguza changamoto ya uhaba wa dawa na watumishi wasio waadilifu waache mara moja tabia ya wizi wa dawa kwani huleta madhara makubwa kwa wananchi wanyonge.
iii. Elimu Msingi na Sekondari - Walimu wanaofanya kazi katika Halmashauri ya Longido walisema wanaidai Serikali zaidi Tsh Million 250 za malimbikizo yasiyo kuwa ya mishahara, mishahara ya mwanzo pamoja na nauli. Kutokana na hilo, RC Gambo aliahidi kufuatilia kwa karibu ili madeni hayo yaweze kulipwa haraka iwezekanavyo.
iv. Upatikanaji wa Maji – Iliripotiwa kuwa changamoto kubwa kwa wananchi wa Longido na upatikanaji wa maji. Kutokana na hali hiyo RC Gambo aliagiza kuletewa taarifa ya miradi ambayo haijakamilika kutokana na Fedha kutowasilishwa kwa wakati ili aweze kufuatilia Fedha hizo Wizarani pia alisisitiza mradi mkubwa wa maji utakaogharimu Bilioni 13 uanze kutekelezwa mara moja. Mradi huo utaanzia Mto Simba (Siha) hadi vijiji vya Longido, Ollepes, Orbombo, Engikarate mpaka Ranchi na ukikamilika upatikanaji wa maji utaongezeka hadi kufikia asilimia 80.
v. Nidhamu kwa Watumishi – Rc Gambo alisema “Nakuagiza katibu Tawala Mkoa kumuandikia barua Katibu Mkuu Tamisemi ili awarudishe aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Longido Bw. Julius Challya na Eng. Edwin Rwezaura waje kujibu tuhuma za matumizi mabaya ya Fedha za mradi wa maji uliogharimu zaidi ya Tsh Mil 400”.
“Wafanyakazi wa mpakani acheni kupokea rushwa, inaonekana vitendo vya rushwa, urasimu na ubadhirifu vimekithiri hapa Namanga hakika sisi kama Serikali hatutasita kuwachukulia hatua wale wote watakaobainika kupokea na kutoa rushwa au kushirikiana na wahalifu kuhujumu mapato ya Serikali kwa namna yeyote ile tutamshughulikia pasipo kujali nafasi yake”.
vi. Uwekezaji – Kutokana na wingi wa mifugo katika Wilaya ya Longido RC Gambo alishauri Halmashauri kuangalia uwezekano wa kuwekeza kwenye ujenzi wa viwanda vya Nyama na maziwa pia Viwanda vya kusaga nafaka ili kusitisha biashara inayoendelea sasa ya kusafirisha mazao ya nafaka ambapo inaweza kupelekea baa la njaa kwa wananchi; Uwekezaji huu utasaidia kuongeza mnyororo wa thamani pamoja na kuongeza ajira.
vii. Ukuaji wa mji Namanga – Kutokana na ongezeko la Idadi ya watu kumekuwa na uhitaji mkubwa wa huduma za kijamii katika eneo la Namanga hivyo Mkuu wa Mkoa ameagiza uongozi wa Wilaya kupitia madai ya wananchi wake ya kutaka kuanzishwa kwa Mamlaka ya Mji mdogo katika eneo hilo na kuchukua hatua stahiki.
viii. Ajira kwa Vijana – Mkuu wa Mkoa aliahidi kutoa boda boda kumi kwa vijana wanaofanya shughuli hizo katika Wilaya ya Longido, na kuangalia uwezekano wa kuongeza pikipiki hizo kwa kadiri atakavyoridhishwa na utendaji kazi wao lengo ni kuwajengea uwezo na kuinua pato la Vijana. Pia aliwaagiza Halimashauri kuhakikisha 10% ya mapato yao inawafikia vijana na kina mama kama Serikali ilivyoelekeza.
ix. Kuchangia miradi ya Maendeleo – Kupitia ziara hiyo Mkuu wa Mkoa wa Arusha alichangia Mifuko ya saruji 580, Mabati 856, mbao 466, madawati 100 pamoja na mchango wa Fedha zaidi ya Tsh Mil 1.5 pia aliungwa mkono na Umoja wa waendesha Noah za Arusha – Namanga kwa kuchangia mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya ukamilishaji wa ujenzi unaondelea wa madarasa, zahanati, vituo vya afya, madaraja pamoja na barabara.
Mkuu wa Mkoa alihitimisha ziara yake kwa kuwataka Viongozi na wataalam kuendelea kujipanga namna gani ya kuwatumikia wananchi kwa uadilifu na kujitoa ili kupunguza malalamiko.
“Hakikisheni mnawatembelea wananchi vijijini, kusikiliza na kujibu hoja, mtatue changamoto zinazowakabili na kuwafariji katika harakati zao za kujitafutia kipato na kuleta maendeleo” Alisisitiza RC Gambo.
Imetolewa na:
Nteghenjwa Hosseah
Afisa Habari
Labels:
ARUSHA
November 02, 2016
Kamati ya kuwaenzi Viongozi wa Kitaifa ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar chafanyika - ZANZIBAR
Mwenyekiti wa Kamati ya kuwaenzi Viongozi wa Kitaifa ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar Jimbo la Konde Mh. Omar Seif Abeid wa Pili kutoka Kushoto akizungumza katika Kikao kilichowakutanisha Wajumbe wa Kamati hiyo pamoja na Uongozi wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.
Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Vuga Mjini Zanzibar.
Wa kwanza kutoka kushoto ni Waziri Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Mohammed Aboud Mohammed, wa kwanza kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Nd. Joseph Abdulla Meza, Naibu Katibu Mkuu Ahmad Kassim Haji na Mkurugenzi Mipango, Sera na Utafiti - OMPR - Nd. Ameir Ussi.
Picha na – OPMR – ZNZ.
Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Vuga Mjini Zanzibar.
Wa kwanza kutoka kushoto ni Waziri Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Mohammed Aboud Mohammed, wa kwanza kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Nd. Joseph Abdulla Meza, Naibu Katibu Mkuu Ahmad Kassim Haji na Mkurugenzi Mipango, Sera na Utafiti - OMPR - Nd. Ameir Ussi.
Picha na – OPMR – ZNZ.
Labels:
KITAIFA









