MIUNDOMBINU YA ELIMU ZANZIBAR SASA YALINGANA NA MAHITAJI YA KARNE YA 21
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Zanzibar imepiga hatua kubwa katika kuimarisha mazin...
MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR- AFUNGUA KITUO CHA UFUNDI
Written By CCMdijitali on Sunday, June 16, 2024 | June 16, 2024
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla amesema ujenzi wa kituo cha Karakana ya Uchongaji kilichopo Mwera PONGWE ni hatua muhimu ya utekelezaji wa miradi jumuishi ya elimu itakayowawezesha vijana walio nje ya mfumo rasmi wa elimu kupata ujuzi utakaowasaidia katika maisha yao.
Ameyasema hayo katika hafla ya Uzinduzi wa kituo cha ujuzi kwa vijana cha utekelezaji wa mpango changmani wa kuwawezesha vijana rika wenye umri wa miaka 15- 19 iliyofanyika katika viwanja vya skuli ya Mwera Pongwe, Wilaya ya Kati Unguja.
Amesema utekelezaji wa mradi huo unatoa fursa kwa vijana kujifunza kwa vitendo na kuweza kuwa mafundi mahiri wa kuchonga aina mbali mbali za samani pamoja na kupatiwa ujuzi wa kutengeneza vifaa vya aluminium ili kuwajengea uwezo zaidi katika kukabiliana na harakati za kimaisha.
Mhe. Hemed amesema kituo hicho pamoja na kutoa ujuzi kwa vijana pia kitatoa msaada mkubwa wa kufanya ukarabati wa vifaa mbali mbali kama vile meza, viti na madawati yatakayo haribika katika Maskuli sambamba na kuwataka walimu wakuu kuitumia fursa hio kwa kwa kufanya marekebisho ya samani zilizoharibika katika maskuli yao ili ziendelee kutumika kwa muda mrefu.
Aidha Mhe. Makamu wa Pili wa Rais amesema kuwa Bajeti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali imeongezwa na kufikia Bilioni 830 lengo ikiwa ni kuiwezesha wizara hio kufikia mageuzi ya elimu ya juu na kuimarisha miundombinu ya elimu kwa kujenga madarasa 1500 ilj kufikia azma ya Serikali ya kuingia mkondo mmoja wa asubihi kwa idadi ya wanafunzk 45 kwa kila darasa.
Sambamba na hayo amesema katika kuimarisha mafunzo ya Ufundi na Amali Serikali imejipanga kujenga vituo viatano vya Mafunzo ya amali vitakavyojengwa Unguja na Pemba pamoja na kujenga vituo vya ujuzi bunifu katika skuli 33 za Sekondari kwa Unguja na Pemba ambapo kwa sasa zitajengwa katika skuli tatu (3 ) kila Wilaya lengo ikiwa ni kuwatayarisha vijana kupata ujuzi ambao utawasaidia katika kujiajiri baada ya kumaliza masomo yao.
Mhe. Hemed amewashukuru washirika wa maendelo Serikali ya Canada na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto Duniani (UNICEF) Kwa kufadhili mradi huu wenye lengo la kuwasaidia vijana kupata ujizi utakaowadaidia katika kupata ajira na kujikwamua kiuchumi.
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesisitiza suala la kutunza Amani iliyopo ndani ya nchi na kuvitaka vyombo husika kutumia zaidi busara wakati wa kudhibiti vitendo vya uvunjifu wa amani kwa bila ya amani hakuna maendeleo nchini.
Kwa upande wake Kaimu Waziri wa elimu Zanzibar Ali Abulghulam Hussein amesema Serikali ya Awamu ya Nane(8) imeazimia kufanya mabadiliko makubwa katika Sekta ya Elimu kwa kusomesha Mafunzo ya Amali na ubunifu kuanzia ngazi ya msingi hadi vyuoni.
Amesema Wizara itahakikisha wanafunzi wanaomaliza katika vyuo hivyo wanapata ujuzi ambao utawasaidia katika kujiajiri na kuajiriwa katika mashirika na Taasisi mbali mbali ndani na nje ya nchi sambamba na kujenga vituo vya elimu amali kila wilaya kwa unguja na pemba.
Akitoka maelezo ya Kitaalamu kuhusu program ya ZIPOSA Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Khamis Abdulla Said amesema uwepo wa mradi huo utawasezesha watoto wa kike na kiume katika kumaliza elimu yao ya lazima ambayo waliikosa kutokana na chamgoto mabali mbali za kimaisha.
Amesema kuwa jumla ya vijana 150 wapo katika vituo vya elimu mbadala Unguja na Pemba wakijifunza fani mbali mbali za ufundi pamoja na kujiongezea ujuzi na maarifa unaoendana na soko la ajira nchini.
Mapema Mwakilishi Mkaazi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto Duniani UNICEF nchini Tanzania Bibi Elke Wisch ameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuendelea kuboresha Sekta ya Elimu nchini na kutoa kipaombele kwa vijana hasa wale walioacha skuli kwa sababu mbali mbali na kuhakikisha wanawarudisha skuli na kuendelea na masomo yao.
Imetolewa na kitengo cha Habari (OMPR)
Tarehe 15.06.2024
..................................................................................
![]() |
| Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa kituo cha ujuzi kwa vijana kilichopo Mwera Pongwe Wilaya ya Kati Unguja. |
![]() |
| Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla akiweka jiwe la zinduzi wa kituo cha ujuzi kwa vijana kilichopo Mwera Pongwe Wilaya ya Kati Unguja. |
NAIBU WAZIRI PINDA AKERWA UCHELEWESHAJI UJENZI MRADI WA MAKATABA CHUO CHA ARDHI TABORA
Na Munir Shemweta, TABORA
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Punda amekerwa na kuchelewa kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa Maktaba ya Chuo cha Ardhi Tabora (ARITA) kwa wakati kutokana na kuchelewa kuletwa kwa baadhi ya vifaa kutoka kwa mzabuni.
Mhe. Pinda ameelezwa na mkandarasi wa mradi huo Wakala wa Majengo Tanzania TBA kuwa, ujenzi wa mradi huo ungekuwa umekamilika kwa wakati lakini kutokana na kuchelewa kwa baadhi ya vifaa kwa ajili ya ukamilishaji ujenzi wa mradi huo wa maktaba kumesababisha mkanadarasi kushindwa kutekeleza kazi yake kwa wakati
.‘’Mhe. Waziri, kazi hii tungeweza kumaliza ndani ya siku sitini lakini changamoto kubwa ni material tumeshindwa kukamilisha kutokana na kuchelewa kufika kwa baadhi ya vifaa kwa wakati na hivyo kutufanya tushindwe kukamilisha kazi hii’’ alisema Meneja wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) mkoa wa Tabora Mhandisi Ebenezer Ngure.
Akizungumza wakati wa kukagua mradi wa ujenzi wa Maktaba ya Chuo cha Ardhi Tabora tarehe 15 Juni 2024, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda amemuagiza mkandarasi wa mradi huo kuandika ripoti inayoonesha mahitaji yote na kumfikia ifikapo jumatano ya tarehe 19, 2024 ili afanyie kazi changamoto zinazokwamisha ujenzi kutokamilika kwa wakati.
Awali Chuo cha Ardhi Tabora, kilimueleza Naibu Waziri Mhe. Pinda kuwa, kuna baadhi ya vifaa ambavyo Mkandarasi Mshauri ameomba vibadilishwe ambapo mzabuni aliombwa kwenda kuvichukua lakini hakufika jambo lililomshangaza mhe. Pinda.
Naibu Waziri wa Ardhi ameagiza ubadilishaji wa vifaa kutoka kwa mzabuni kufanywa haraka kufikia jumanne ya tarehe 18, 2024 kwa kuwa wenye shinda ni chuo hivyo hawapaswi kusubiri mzabuni na badala yake chuo kifuatilie ili ujenzi wa jengo hilo ukamilike.
‘’Nilidhani hawa ndiyo wenye makosa lakini wenye makosa ni sisi, maelekezo yangu kufikia jumanne nne vifaa hivi vilivyozidi na kumpa mrejesho wa hatua mliyofikia’’ alisema mhe. Pinda
Meneja wa TBA alimhakikishia Mhe, Naibu Waziri wa Ardhi kuwa ndani ya miezi miwili baada ya kupatiwa vifaa watakuwa wamekamilisha ujenzi wa mradi huo wa Maktaba ya Chuo cha Ardhi na watafanya kazi hiyo kwa weledi mkubwa,
Mradi wa ujenzi wa Maktaba ya Chuo cha Ardhi Tabora ulianza tarehe 15/07/2014 ukitekelezwa chini ya Kampuni ya M/S Co Ltd kwa mkataba uliosaniwa na Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ukiwa na thamani ya TSH 2,026,538,726.00 ambapo muda wa mkataba ulikuwa kipindi cha majuma 44 hivyo kutarajiwa kukamilika tarehe 18/05/2024.
Hata hivyo, kutokana na changamoto kadhaa ikiwemo maombi ya nyongeza ya fedha yaliyotokana na ucheleweshaji malipo kwa hati tatu za madai ulisababisha mkataba huo kuvunjwa mnamo mwezi Juni 2021 na kutokana na umuhimu wa mradi huo tarehe 13 /6/2022 wizara ilisaini mikataba miwili kwa ajili ya kukamilisha mradi huo ambapo chuo kiliendelea kutekeleza ujenzi wa makataba kwa kutumia Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) akiwa mkandarasi mshauri.
SHIRIKANENI KUPANGA, KUPIMA NA KUMILIKISHA ARDHI; BALOZI DKT. BATILDA
Written By CCMdijitali on Wednesday, June 12, 2024 | June 12, 2024
SHIRIKANENI KUPANGA, KUPIMA NA KUMILIKISHA ARDHI; BALOZI DKT. BATILDA
Na Eleuteri Mangi, Tanga
Serikali kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kushirikiana na Benki ya Dunia inatelekeza Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi (LTIP) katika halmashauri mbalimbali nchini zikiwemo za Mkoa wa Tanga.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi Dkt. Batilda Burian amewaagiza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri zinazotekeleza Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi (LTIP) kushirikana na timu zinazotekeleza mradi huo ili kuhakikisha ardhi yote inapangwa, kupimwa na kumilikishwa kwa wananchi.
Dkt. Batilda ametoa agizo hilo mkoani Tanga wakati anafungua mkutano wa wadau kujadili utekelezaji wa Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi Juni 12, 2024 jijini Tanga.
Akinukuu maneno ya Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Batilda amesema Baba wa Taifa wakati akifungua mkutano wadau hao amesema “Ili taifa liendelee tunahitaji watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora.”
Mkuu wa Mkoa amesisitiza “Kwa mkoa wa Tanga watu wapo, siasa safi ipo, uongozi bora upo na ardhi ipo, tumeelezwa kuna migogoro ya ardhi katika maeneo mbalimbali katika mkoa wetu, wajanja sasa hivi ni wengi. Mradi huu umekuja kusaidia kutatua changamoto hizi ili kukuza uchumi na kujiletea maendeleo yetu na taifa.”
Kwa upande wake Mratibu Msaidizi wa Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Miliki za Ardhi Dkt. Upendo Matotola amesema mradi huo unatekelezwa nchini na Serikali kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Januari 21, 2022 ilisaini makubaliano na Benki ya Dunia ya mkopo wa Shilingi bilioni 346 sawa na dola za kimarekani milioni 150 kwa ajili ya kutekeleza mradi huo.
Dkt. Matotola Mradi amesema mradi huo unatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano ukiwa na vipengele vinne vikilenga kuongeza usalama wa milki za ardhi, kuimarisha mifumo ya taarifa za ardhi, kujenga miundombinu ya ardhi na usimamizi wa mradi.
Mradi huo utatoa fursa katika kijamii kwa kuzingatia makundi maalum na kuleta usawa wa kijinsia na kuwezesha wamiliki wa ardhi kumiliki ardhi zao kisheria hatua inayosaidia kupunguza migogoro ardhi katika maeneo mbalimbali inayohusiana na matumizi ya ardhi hasa ya wakulima na wafugaji pamoja na maeneo yaliyotengwa kwa shughuli maalumu.
Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi katika Mkoa wa Tanga unatekelezwa katika halmashauri miji za Tanga jiji, Korogwe DC na Mheza wakati kwa upande wa vijijini unatekelezwa katika halmashauri za Kilindi, Handeni na Mkinga.








MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR- AFUNGA KAMPENI- JIMBO LA KWAHANI
Written By CCMdijitali on Thursday, June 6, 2024 | June 06, 2024

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndugu Hemed Suleiman Abdulla amesema Chama cha Mapinduzi kiko imara na kitaendelea kushinda kwa kishindo katika Uchaguzi wa Jimbo la Kwahani na uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2020-2025 kutokana na kuitekeleza vyema Ilani ya CCM katika kuwaletea wananchi maendeleo.
Akimnadi Mgombea wa Ubunge wa Jimbo la Kwahani kupitia tiketi ya CCM Ndg Khamis Yussuf Mussa Pele wakati wa kufunga kampeni za jimbo hilo katika viwanja vya kibanda maiti , Mhe. Hemed amewataka wananchi wa Jimbo la kwahani kumpigia kura za ndio mgombea huyo ili aendeleze kuinadi na kitekeleza vyema ilani ya CCM.
Amesema endapo wananchi wa jimbo la Kwahani hawatafanya makosa na watamchagua ndugu Pele kuwa mbunge wa jimbo hilo ambae atashirikiana na wabunge na viongozi wengine katika kuitekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi hasa katika kuwaletea wananchi wa Zanzibar maendeleo.
Mhe. Hemed amewataka wana CCM wa jimbo la kwahani kudumisha amani na utulivu wakati wote wa zoezi la uchaguzi na kuwasihi watakapomaliza kupiga kura kuŕudi majumbani kusubiri matokeo yatakayotangazwa na Tume ya Uchaguzi.
Nae Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Talib Ali Talib amesema wana CCM wa jimbo la kwahani wanaahidi kumchagua kwa kishindo ndugu Khamis Pele ambae anatosha kuwa Mbunge kutokana na uchapa kazi wake katika chama, uaminifu na kujitoa kwake katika kuitumikia CCM vinatosha kuipeperusha bendera ya CCM katika Bunge.
Talib ametoa onyo kali kwa wale wote wanaotumia majukwaa kwa kuwatukana na kuwakashifu Viongozi wakuu wa nchii na kusema kuwa CCM haitakuwa tayari kuvumilia uovu huo na itaviomba vyombo vya sheria kufanya kazi yake kwa maslahi ya Taifa.
Akiomba ridhaa ya kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Kwahani ndugu Kahamis Yussuf Pele ameahidi ataitekeleza vyema Ilani ya CCM kwa kukaa pamoja na viongozi wengine wa Jimbo kupanga mikakati ya kimaendeleo ili kuweza kuleta Ustawi ndani ya Jimbo hilo la kwahani.
Pele amewashukuru Viongozi wa Chama cha Mapinduzi kwa imani kubwa waliyompa ya kumteuwa kuwa mgombea wa ubunge wa Jimbo la Kwahani ambapo amesema kazi yake kubwa ni kuhakikisha anayatekeleza kwa vitendo yale yote yaliyoelezwa katika Ilani ya Chama Cha Mapinduzi.





NSSF YATUMIA MAONYESHO YA 11 YA BIASHARA NA UTALII KUITANGAZA NSSF TAARIFA
Written By CCMdijitali on Tuesday, June 4, 2024 | June 04, 2024
MKUTANO WA BARAZA LA KISEKTA LA MAWAZIRI LINALOSHUGHULIKIA MASUALA YA EAC NA MIPANGO WAANZA ARUSHA
Written By CCMdijitali on Monday, June 3, 2024 | June 03, 2024
Mkutano huo wa siku tano kuanzia Juni 3-7, 2024 umeanza kwa Ngazi ya Wataalam na na baadaye utafuatiwa na Ngazi ya Makatibu Wakuu utakaofanyika tarehe 6 Juni 2024 na kuhitimishwa na Mkutano Ngazi ya Mawaziri ukaofanyika tarehe 7 Juni 2024.
Mkutano huo katika Ngazi ya Wataalam pamoja na mambo mengine utapokea na kujadili mapendekezo na taarifa mbalimbali za Jumuiya ikiwemo: Utekelezaji wa Itifaki ya Soko la Pamoja la Jumuiya; Mapendekezo ya kuhuisha Mipango ya Jumuiya na Mipango ya Nchi Wanachama; Taarifa ya Wakurugenzi wa Masuala ya Kazi kuhusu Ukamilishaji wa Rasimu Iliyorekebishwa ya Sera ya Uhamiaji ya Wafanyakazi wa Jumuiya.
Masuala mengine yatakayo jadiliwa ni pamoja na taratibu za Uanzishwaji wa Jukwaa la Mashauriano kuhusu Uhamaji katika Jumuiya ya Afrika Mashariki; Kuidhinisha Sera na Mkakati wa Pili wa Mawasiliano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki; na Kuidhinisha Kalenda ya Shughuli za Jumuiya kwa kipindi cha Julai – Desemba 2024.
Akifungua mkutano huo Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayesimamia masuala ya forodha, biashara na fedha Bi. Annette Ssemuwemba amehimiza kuhusu umuhimu wa mkutano huo katika kusimamia utekelezaji na ufanisi wa sera na mipango ya Jumuiya ili kukidhi matarajio ya Wananchi.
“Mtakumbuka kuwa takriban miaka miwili sasa hakupata fursa ya kufanya mkutano huu, kwa sababu hiyo kwa umoja wetu tutumie fura hii hadhimu kujadili na kutafuta majawabu yatakayotupa uelekeo mpya na sahihi wa kutekeleza na kusimamia kwa ufanisi sekta mbalimbali ikiwemo bishara na fedha kwa maendeleo ya Jumuiya yetu” Alieleza Bi. Annette Ssemuwemba
Vilevile mkutano huo unatarajiwa kufanya tathimini ya hatua iliyofikiwa kwenye utekelezaji wa masuala mbalimbali yaliyoamuliwa kwenye mikutano iliyopita ikiwemo mpango wa Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) na Uondoaji wa Vikwazo vya Biashara visivyokuwa vya kikodi.
Mkutano huo umehudhuriwa na nchi zote Wanachama wa Jumuiya, huku ujumbe wa Tanzania ukijumuisha Mkurugenzi wa Mawasiliano Balozi Mindi Kasiga, Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii Mhandisi Abdillah Mataka, na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji Bw. Benjamini Mwesiga ambaye pia ni kiongozi wa ujumbe huo, wote kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
![]() |
| Meza kuu wakiongoza Mkutano 33 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri linaloshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango ngazi ya Wataalam unaofanyika jijini Arusha |
AGIZO LA WAZIRI SILAA LA KUHAMISHIA HUDUMA ZA ARDHI OFISINI KWAKE LAANZA KUTEKELEZWA DODOMA
Na Eleuteri Mangi, WANMM-Dodoma
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeanza kutekeleza agizo la Waziri Mhe. Jerry Silaa alilolitoa Mei 28, 2024 baada ya kufunga Masijala ya Ardhi jijini Dodoma.
Zoezi la Ardhi Kliniki limeanza Juni 3, 2024 katika Ofisi za Halmashauri ya jiji la Dodoma ambapo Waziri Silaa alitoa maelekezo msijala hiyo irudishwe Ofisini kwake iwe chini ya usimamizi na uangalizi wa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Anthony Sanga ili kuwahudumia wananchi kutatua changamoto za ardhi zinazowakabili.
“Watendaji wote wakae sehemu moja, mwananchi kama anashida ahudumiwe katika eneo moja. Mhe. Jerry Willam Silaa amelionge hili Bungeni, ameliongea mara kwan mara katika mikutano yake lengo la msingi ni kuwahudumia wananchi katika eneo moja na wasipate adha ya nenda ofisi fulani, wala njoo kesho hii ndiyo dhana halisi ya kituo kinmoja jumuishi (one stop centre). Hapa ni watu wa ardhi bila kuangalia mipaka ya utawala,” amesema Mhandisi Sanga.
Zoezi hilo la Kliniki litafanyika kwa muda wa wiki mbili ambapo wananchi watahudumia kwa kutatua migogoro yao na kupatiwa hati miliki ya ardhi yao kwa kuzingatia wananchi wana migogoro mingi ambayo inatokana ama kwa kutapeliwa au ardhi yao kupewa zaidi ya mtu mmoja na baadhi ya watumishi wasio waadilifu.
Mamia ya wananchi wamemiminika katika viwanja vya Ofisi za Halmashauri ya jiji la Dodoma kutatua madhila ya ardhi yanayowakabili ili watumie ardhi na muda wao kwa shughuli za kiuchumi kujiletea maendeleo.
Akizungumzia zoezi hilo linaloendelea jijini Dodoma, Katherine Mwimbe Mwekezaji na Mkurugenzi wa Taasisi ya Domaiya Estate Dodoma Tanzania inayojishughulisha na usindikaji wa mvinyo na huduma za hoteli ni miongoni mwa waliopata huduma kwenye Kliniki ya Ardhi inayoendelea jijini Dodoma ambapo amesema ameridhishwa na huduma zinazotolewa katika zoezi hilo.
“Tumekuwa na changamoto za ardhi katika uwekezaji wetu, tumepata simu tukakaribishwa katika kambi hii maalum inayozungumzia masuala ya ardhi, tuliambiwa tufike saa 2:30, tumefika kwa wakati mara moja tumepata huduma tunayohitaji, tumekuja na nyaraka zetu. Vitu vimefanyiwa kazi, tunapata matumaini na tuanweza kuendelea na uwekezaji na biashara” amesema Mwimbe.
Mwimbe ameongeza “Sisi kama kampuni ya kimataifa tumepata huduma nzuri, hiyo imetupan sana moyo, naamini tunaweza kwenda kufanya maendeleo zaidi hasa katika sekta ya mvinyo hapa Dodoma.
Zoezi hilo linaongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Anthony Sanga, Naibu Katibu Mkuu Lucy Kabyemera, Kamishna wa Ardhi Methew Nhonge, watendaji wa wizara hiyo pamoja na watendaji wa Ardhi mkoa wa Dodoma.
![]() |
| Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhandisi Anthony Sanga akiongea na waandishi wa Habari wakati wa zoezi la Kliniki ya Ardhi inayoendelea jijini Dodoma. |
![]() |
| Viongozi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakiongozwa na Katibu Mkuu Mhandisi Anthony Sanga wakiwahudumia wananchi wakati wa zoezi la Kliniki ya Ardhi inayoendelea jijini Dodoma. |
![]() |
| Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhandisi Anthony Sanga (katikati kulia) akiwahudumia wananchi wakati wa zoezi la Kliniki ya Ardhi inayoendelea jijini Dodoma. |
![]() |
| Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhandisi Anthony Sanga akiongea na waandishi wa Habari wakati wa zoezi la Kliniki ya Ardhi inayoendelea jijini Dodoma. |
NAIBU WAZIRI PINDA AHIMIZA KULIPA KODI YA ARDHI
Na Munir Shemweta
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda amewahimiza wamiliki wa ardhi nchini kuhakikisha wanalipa kodi ya pango la ardhi kwa wakati ili kuepuka kuchukuliwa hatua za kisheria.
"Naomba kusisitiza kwa wamiliki wote wa ardhi nchini, kutekeleza sharti la kulipa kodi ya ardhi kwa kuwa sasa tumeboresha njia za ukadiriaji na ulipaji wa kodi husika kidigitali". Amesema Mhe. Pinda.
Amewakumbusha wamiliki wa ardhi maelekezo yaliyotolewa na Mhe. Waziri wa Ardhi Jerry Silaa wakati wa kuhitmisha Hotuba ya Bajeti 2024 Bungeni kwamba, Wizara imedhamiria kuchukua hatua kwa wamiliki wote wa ardhi watakaoshindwa kutimizi masharti ikiwemo kuwafikisha mahakamani ili kuuza mali zao kufidia kodi ya ardhi na kupendekeza ubatilisho wa milki zao.
Amesema, wamiliki wa ardhi wanaweza kupokea Ankara za malipo kupitia ofisi za ardhi za mikoa na halmashauri na mara baada ya kupata makadirio ya kodi wanayodaiwa wanaweza kulipa kupitia benki au mawakala wa benki sambamba na njia ya simu ya kiganjani kwa kufuata taratibu za miamala ya malipo ya Serikali kupitia simu.
Aidha, Naibu Waziri wa Ardhi amefafanua kuwa, malipo ya Kodi ya Pango la Ardhi hufanyika kwa kuzingatia ukubwa wa ardhi inayomilikishwa, matumizi ya ardhi yaliyoidhinishwa, thamani ya ardhi na kiwango cha malipo ya mbele (premium) ya ardhi inayomilikishwa.
Mhe, Pinda amewataka wamiliki wa ardhi waliopimiwa ardhi kuhakikisha wanakwenda ofisi za ardhi kwa ajili ya kumilikishwa kwa kuwa wasipofanya hivyo baada ya siku tisini wataingizwa kwenye mfumo na kuanza kudaiwa kama wamiliki wengine.
Mhe. Pinda amegusia pia mkanganyiko uliopo baina ya kodi ya pango la ardhi na kodi ya majengo ambapo amesema Kodi ya Pango la ardhi hutozwa kwa wamiliki wa ardhi tofauti na Kodi ya Majengo ambayo hutozwa kwenye majengo/nyumba na kuwekewa utaratibu wa ulipaji na ukusanyaji wake ambapo kwa sasa inalipwa kwa njia ya malipo ya ununuaji wa umeme kupitia mfumo wa LUKU.
CDE.MBETO : AKEMEA SIASA ZA CHOKO CHOKO ZINAZOFANYWA NA ACT-WAZALENDO.
Written By CCMdijitali on Sunday, June 2, 2024 | June 02, 2024
![]() |
| KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Zanzibar Khamis Mbeto Khamis,akizungumza katika moja ya mikutano yake ya kikazi aliyofanya hivi karibu Unguja. |
MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR- KUFUNGA KONGAMANO MKOKOTONI - KWA NIABA YA RAIS WA ZANZIBAR
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kushirikiana na Jumuiya ya wasioona Zanzibar (ZANAB) na Jumuiya nyengine za watu wenye ulemavu ili kuhakikisha inaweka mazingira wezeshi ambayo yatawasaidia watu wenye ulemavu kufaidika na fursa mbali mbali nchini.
Ameyasema hayo katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla wakati wa kuahirisha maadhimisho ya kuongeza uwelewa kwa jamii juu ya watu wenye Ulemavu katika Viwanja vya Mpira wa Mto wa Pwani Wilaya ya Kaskazini 'A' Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Amesema kwa kutambua kuwa watu wenye ulemavu wamekuwa wakikumbana na chamgamoto mbali mbali katika jamii, kumeanzishwa Baraza la Taifa la watu wenye ulemavu na mabaraza ya Wilaya ya watu wenye Ulemavu yenye dhamana ya kusimamia , kutekeleza, kutetea na kulinda haki nafursa za watu wenye Ulemavu ambapo jumla ya shilingi za Kitanzania Bilioni 1.2 zimetenga kwa mwaka wq fedha 2024-2025 kwa ajili ya kuendeshea mabaraza hayo.
Rais Dkt Mwinyi amesema Serikali imeweza kutoa nafasi za Uongozi kwa watu wenye ulemavu katika Wizara mbali mbali ambapo wamekuwa wakitekeleza majukumu kwa ufanisi mkubwa jambo ambalo linazidi kutoa hamasa lwa Serikali kuendelea kuweka mazingira mazuri kwa watu wenye ulemavu ili kuwawezesha kufikia katika ndoto zao walizojipangia.
Dkt. Mwinyi amesema Serikali itahakikisha sheria ya watu wenye Ulemavu inafanyiwa kazi na kupelekwa Baraza la Wawakilishi kwa ajili ya kujadiliwa na hatimae kupitishwa kuwa Sheria kamili ambayo itatoa miongozo mbali mbali kwa Taasisi na Jumuiya za watu wenye ulemavu ili kuwawezesha kufanikisha malengo yao walkyojipangia.
Rais Dkt Mwinyi amesema kupitia Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020-2025 Serikali imekuwa ikichukua hatua za kuweka mazingira bora kwa watu wenye ulemavu ikiwemo kutunga Sheria ya watu wenye Ulemavu Namba (8) ya mwaka 2022 kwa lengo la kulinda na kutetea haki na fursa za watu wenye ulemavu.
Aidha Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Amesema Serikali kupitia Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais itaandaa program maalum itakayowajengea uwelewa wananchi juu ya kutambua haki na wajibu wa watu wenye ulemavu katika Mikoa yote ya Zanzibar.
Sambamba na hayo Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi ametoa wito kwa Jumuiya za watu wenye Ulemavu kuongeza nguvu zaid ya uwajibikaji na kuwahamasisha watu wenye ulemavu kuchangamkia fursa mbali mbali zinazojitokeza katika Taifa.
Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Mhe. Dkt KHALID SALUM MUHAMMED amesema Serikali zote mbili zimefanya mapitio ya Sera na Sheria kuhakikisha watu wote wanapata haki sawa ikiwa ni pamoja na makundi maalum katika nyanja zote za kiuchumi na kijamii.
Dkt Khalid amefahamisha kuwa Serikali kupitia Mfuko wa uwezeshaji imejipanga kumaliza kilio cha muda mrefu cha watu wenye ulemavu kwa kuwapatia mikopo itakayowasaidia kujiendeleza kiuchumi katika miradi yao pamoja na kujikimu kimaisha.
Akisoma Risala iliyoandaliwa na Jumuiya ya watu wasioona Zanzibar Ndugu AWENA HASSAN SEIF amesema (ZANAB) inaiomba Serikali kuongeza uwelewa kwa jamii katika kushirikiana na watu wenye ulemavu katika kutambua haki na ustawi wao katika mambo mbali mbali ya kijamii.
Amesema kuwa changamoto kubwa inayowakabili watu wenye ulemavu ni kutokufikishwa katika Baraza la Wawakilishi sheria ya Hati miliki ya Zanzibar kwa ajili ya kufanyiwa marekebisho ili iendane na Mkataba wa Markesh ambayo itatoa fursa kwa watu wasioona kupata nyaraka za maandishi kwa mfumo sikivu.
Mapema Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja RASHID HADID RASHID amesema jamii inapaswa kutambua kuwa watu wenye ulemavu wanaweza kuleta maendeleo katika jamii, hivyo tunapaswa kuwashirikisha na kuwapa kipaombele katika kushiriki mambo mbali mbali ya kimaendeleo.
Hadid amesema Serikali ya Mkoa wa Kaskazini Unguja imekuwa ikifanya kazi kwa karibu na watu wenye ulemavu kwa kuwashirikisha katika mambo muhimu ya kimaendeleo ili kutoa mchango wao katika mambo yanayowahusu.
Imetolewa na Kitengo cha Habari (OMPR)
Tarehe 02.06.2024




















