MIUNDOMBINU YA ELIMU ZANZIBAR SASA YALINGANA NA MAHITAJI YA KARNE YA 21

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Zanzibar imepiga hatua kubwa katika kuimarisha mazin...

Latest Post

RAIS KIKWETE AONGOZA MAZISHI YA CHIFU MKWAWA IRINGA

Written By CCMdijitali on Tuesday, February 17, 2015 | February 17, 2015


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji Chifu mpya wa Wahehe, Chifu Adam Abdu Mkwawa, Mtwa Adam wa Pili (14), wakati wa mazishi ya baba yake aliyekuwa Chifu wa Kabila la Wahehe, Chifu Abdu Mfwimi Adam Mkwawa katika eneo la Nyumba ya Makumbusho ya Chifu Mkwawa, Kijiji cha Karenga leo Februari 16, 2015


  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitia saini kitabu cha maombelezo..


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpa pole mjane wa aliyekuwa Chifu wa Kabila la Wahehe, Chifu Abdu Mfwimi Adam Mkwawa leo Kijiji cha Karenga Februari 16, 2015


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya aliyekuwa Chifu wa Kabila la Wahehe, Chifu Abdu Mfwimi Adam Mkwawa leo katika eneo la Nyumba ya Makumbusho ya Chifu Mkwawa,Kijiji cha Karenga  Februari 16, 2015.

MATOKEO YA KIDATO CHA NNE NA QT 2014

Written By CCMdijitali on Sunday, February 15, 2015 | February 15, 2015


Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani nchini,Dk. Charles Msonde 

Shule za sekondari za binafsi zaongoza 10 bora matokeo ya mtihani wa  kidato cha nne uliofanyika mwaka jana.

Akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam,Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani nchini  (NECTA),Dk.Charles Msonde amesema katika matokeo ya kidato cha nne ya mtihani wa mwaka jana ufaulu umeongezeka  kwa asilimia 12.67 ikilinganishwa na mwaka 2013.


Katika matokeo hayo msichana wa shule ya sekondari ya Baobab ,Nyakaho I. Marungu ndio aliyeongoza mtihani huo na kufatia wavulana.


Shule za Sekondari za St.Fransis ya mkoani Mbeya wanafunzi sita na Feza wanafunzi nane na kufanya shule hizo kuingia katika 10 bora kwa kutoa idadi wanafunzi wengi ikilinganishwa na shule zingine.


Msonde amasema matokeo hayo  yanatokana na mfumo mpya  wa GPA kwa kuangalia masomo saba  hivyo ufaulu umetokana na mfumo huo.


Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani nchini,Dk. Charles Msonde akizungumza na wanahabari jijini Dar leo.




BONYEZA HAPA :MATOKEO YA KIDATO CHA NNE NA QT 2014



CHAMA CHA MAPINDUZI KATA YA KALOLENI JIJINI ARUSHA WAWASHUKURU WANANCHI

KATIBU WA SIASA NA UENEZI CCM WILAYA YA ARUSHA NDG JASPER KISHUMBUA AKIWAHIMIZA WANANCHI,KUTUMIA FURSA ZINAZOTOLEWA SEREKALI INAYOONGOZWA NA CHAMA CHA MAPINDUZI KWA  KUJIUNGA NA MFUKO WA BIMA YA AFYA ,ILI KUWEZA KUWAPATIA UNAFUU KATIKA KUJIKWAMUA NA MAISHA YAO  YA KILA SIKU. AIDHA ALIWATAKA KUTOKUZINGATIA KEJELI ZA WAPINZANI KWANI HUDUMA ZOTE IKIWA NI DAWA , MATIBABU, VIPIMO VYA MAABARA NA X RAY ZINAPATIKANA KATIKA ZAHANATI NA HOSPITALI ZOTE ZINAZOTOA HUDUMA HIZO.UNAPOJIUNGA UNALIPIA GHARAMA YA FEDHA ZA KITANZANIA SH 12,500/= TU KWA MWAKA MZIMA IKIJUMUISHA FAMILIA YAKO. 

MKUTANO NA SHEREHE HIZO  ZA KUWASHUKURU NA KUWAPONGEZA WAKAZI WA KATA HIYO KWA KUICHAGUA  KWA KISHINDO CCM KATIKA NAFASI WENYEVITI NA WAJUMBE WA SEREKALI ZA MITAA (MTAA WA KALOLENI MASHARIKI MKT HASSAN SHARIF NA MAGHARIBI MKT ABDALLAH NASSORO), ULIFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA OFISI YA MTENDAJI WA KATA YA KALOLENI NA KUHUDHURIWA NA MAELFU YA WATU BILA KUZINGATIA ITIKADI.
 KATIBU WA SIASA NA UENEZI CCM WILAYA YA ARUSHA NDG JASPER KISHUMBUA AKIFURAHIA NYIMBO  MPYA YA CCM ILIYOIMBWA CAPT JOHN KOMBA, AKIUNGWA MKONO NA BAADHI YA VIONGOZI NA WANACHAMA WA CCM WALIOJITOKEZA KWA MAELFU KATIKA MKUTANO NA SHEREHE ZA KUWASHUKURU NA KUWAPONGEZA WAKAZI WA KATA HIYO KWA KUICHAGUA  KWA KISHINDO CCM KATIKA NAFASI WENYEVITI NA WAJUMBE WA SEREKALI ZA MITAA (MTAA WA KALOLENI MASHARIKI MKT HASSAN SHARIF NA MAGHARIBI MKT BDALLAH NASSORO).
MWENYEKITI WA CCM WILAYA YA ARUSHA NDG WILFRED SOILELI AKIWASHUKURU MAELFU YA WAKAZI  WA KATA YA KALOLENI  YA  JIJINI ARUSHA KATIKA VIWANJA VYA OFISI YA MTENDAJI WA KATA, WALIOHUDHURIA MKUTANO NA SHEREHE ZA KUWASHUKURU NA KUWAPONGEZA WAKAZI WA KATA HIYO KWA KUICHAGUA  KWA KISHINDO CCM KATIKA NAFASI WENYEVITI NA WAJUMBE WA SEREKALI ZA MITAA (MTAA WA KALOLENI MASHARIKI MKT HASSAN SHARIF NA MAGHARIBI MKT BDALLAH NASSORO).
 MWENYEKITI WA CCM KATA YA KALOLENI NDG H. NGALAWA AKIMKARIBISHA MGENI RASMI NDG WILFRED SOILELI KATIKA MKUTANO NA SHEREHE ZA KUWASHUKURU NA KUWAPONGEZA WAKAZI WA KATA HIYO KWA KUICHAGUA  KWA KISHINDO CCM KATIKA NAFASI WENYEVITI NA WAJUMBE WA SEREKALI ZA MITAA (MTAA WA KALOLENI MASHARIKI MKT HASSAN SHARIF NA MAGHARIBI MKT BDALLAH NASSORO).


 BAADHI YA WAKAZI WA KATA YA KALOLENI WALIOHUDHURIA  MKUTANO NA SHEREHE ZA KUWASHUKURU NA KUWAPONGEZA WAKAZI WA KATA HIYO KWA KUICHAGUA  KWA KISHINDO CCM KATIKA NAFASI WENYEVITI NA WAJUMBE WA SEREKALI ZA MITAA (MTAA WA KALOLENI MASHARIKI MKT HASSAN SHARIF NA MAGHARIBI MKT BDALLAH NASSORO).
 MWENYEKITI WA SEREKALI YA MTAA WA KALOLENI MAGHARIBU NDG ABDALLAH NASSORO AKIWASHUKURU NA KUWAPONGEZA WANANCHI HAO WALIOJITOKEZA KWA WINGI KWA KUMPA KURA ZA HESHIMA,KATIKA  MKUTANO NA SHEREHE ZA KUWASHUKURU NA KUWAPONGEZA WAKAZI WA KATA HIYO KWA KUICHAGUA  KWA KISHINDO CCM KATIKA NAFASI WENYEVITI NA WAJUMBE WA SEREKALI ZA MITAA (MTAA WA KALOLENI MASHARIKI MKT HASSAN SHARIF NA MAGHARIBI MKT BDALLAH NASSORO).


 MWENYEKITI WA SEREKALI YA MTAA WA KALOLENI MASHARIKI NDG HASSAN SHARIFU AKIWASHUKURU NA KUWAPONGEZA WANANCHI HAO WALIOJITOKEZA KWA WINGI KWA KUMPA KURA ZA HESHIMA,KATIKA  MKUTANO NA SHEREHE ZA KUWASHUKURU NA KUWAPONGEZA WAKAZI WA KATA HIYO KWA KUICHAGUA  KWA KISHINDO CCM KATIKA NAFASI WENYEVITI NA WAJUMBE WA SEREKALI ZA MITAA (MTAA WA KALOLENI MASHARIKI MKT HASSAN SHARIF NA MAGHARIBI MKT BDALLAH NASSORO).



BAADHI YA WAKAZI WA KATA YA KALOLENI WALIOHUDHURIA  MKUTANO NA SHEREHE ZA KUWASHUKURU NA KUWAPONGEZA WAKAZI WA KATA HIYO KWA KUICHAGUA  KWA KISHINDO CCM KATIKA NAFASI WENYEVITI NA WAJUMBE WA SEREKALI ZA MITAA (MTAA WA KALOLENI MASHARIKI MKT HASSAN SHARIF NA MAGHARIBI MKT BDALLAH NASSORO).


 MWENYEKITI WA SEREKALI YA MTAA WA KALOLENI MASHARIKI NDG HASSAN SHARIFU AKIPEANA MKONO WA HONGERA NA KATIBU WA FEDHA NA UCHUMI CCM WILAYA YA ARUSHA NDG VICTOR MOLLEL,MARA BAADA YA KUONGEA NA KUWASHUKURU WAKAZI WAKAZI WA KATA YA KALOLENI.
MWENYEKITI WA SEREKALI YA MTAA WA KALOLENI MASHARIKI NDG HASSAN SHARIFU AKIPEANA MKONO WA HONGERA NA KATIBU WA SIASA  NA UENEZI CCM WILAYA YA ARUSHA NDG JASPER KISHUMBUA ,MARA BAADA YA KUONGEA NA KUWASHUKURU WAKAZI WAKAZI WA KATA YA KALOLENI.
 KATIBU WA SIASA NA UENEZI CCM WILAYA YA ARUSHA NDG JASPER KISHUMBUA AKITETA JAMBO NA NDG RAMA RAMADHANI WAKATI AKIENDA KUUTAMBULISHA UONGOZI WA WILAYA ULIOFUATANA NA MWENYEKITI WA CCM WILAYA YA ARUSHA.
 


KATIBU WA SIASA NA UENEZI CCM WILAYA YA ARUSHA NDG JASPER KISHUMBUA  NA BAADHI YA VIONGOZI WA KATA NA WILAYA (ALIYEVAA KOFIA NYEUSI NI KATIBU WA WAZAZI WILAYA YA ARUSHA NDG REHEMA MOHAMED) WAKIONYESHA KUFURAHIWA NA WIMBO MPYA WA TOT.....
 MWENYEKITI WA CCM WILAYA YA ARUSHA NDG WILFRED SOILEL NA MEZA KUU WAKIONYESHA FURAHA ZAO NA KUJIKUTA WAKIMSHANGILIA  KATIBU WA SIASA NA UENEZI WA CCM WILAYA YA ARUSHA NDG JASPER KISHUMBUA NA BAADHI YA VIONGOZI WENGINE  WALIPOKUWA WAKICHEZA WIMBO WA MPYA WA TOT.

 KATIBU WA SIASA NA UENEZI CCM WILAYA YA ARUSHA NDG JASPER KISHUMBUA AKIWAHIMIZA WANANCHI,KUTUMIA FURSA ZINAZOTOLEWA NA SEREKALI INAYOONGOZWA NA CHAMA CHA MAPINDUZI KWA KUHAKIKISHA WANAJIUNGA NA MFUKO WA BIMA YA AFYA ,ILI KUWEZA KUPATA UNAFUU KATIKA KUJIKWAMUA NA MAISHA YAO  YA KILA SIKU.
AIDHA ALIWATAKA WAPUUZE KEJELI ZA WAPINZANI KWANI HUDUMA ZOTE IKIWA NI DAWA , MATIBABU, VIPIMO VYA MAABARA NA X RAY ZINAPATIKANA KATIKA ZAHANATI NA HOSPITALI ZOTE ZINAZOTOA HUDUMA HIZO.MARA UNAPOKUWA MWANACHAMA WA BIMA YA AFYA, NA PINDI UNAPOJIUNGA UNALIPIA GHARAMA YA FEDHA ZA KITANZANIA SH 12,500/= TU KWA MWAKA MZIMA IKIJUMUISHA FAMILIA YAKO. 

MKUTANO NA SHEREHE HIZO  ZA KUWASHUKURU NA KUWAPONGEZA WAKAZI WA KATA HIYO KWA KUICHAGUA  KWA KISHINDO CCM KATIKA NAFASI WENYEVITI NA WAJUMBE WA SEREKALI ZA MITAA (MTAA WA KALOLENI MASHARIKI MKT HASSAN SHARIF NA MAGHARIBI MKT ABDALLAH NASSORO), ULIFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA OFISI YA MTENDAJI WA KATA YA KALOLENI NA KUHUDHURIWA NA MAELFU YA WATU BILA KUZINGATIA ITIKADI.
 KATIBU WA JUMUIYA YA WAZAZI YA CCM WILAYA YA ARUSHA NDG REHEMA MOHAMED AKIWASALIMIA WANANCHI NA WAKAZI WA KATA YA KALOLENI WALIOJITOKEZA KWA MAELFU KATIKA MKUTANO NA SHEREHE ZA KUWASHUKURU NA KUWAPONGEZA WAKAZI WA KATA HIYO KWA KUICHAGUA  KWA KISHINDO CCM KATIKA NAFASI WENYEVITI NA WAJUMBE WA SEREKALI ZA MITAA (MTAA WA KALOLENI MASHARIKI MKT HASSAN SHARIF NA MAGHARIBI MKT BDALLAH NASSORO).
 KATIBU WA UCHUMI NA FEDHA  CCM WILAYA YA ARUSHA NDG VICTOR MOLLEL AKIWASALIMIA WANANCHI NA WAKAZI WA KATA YA KALOLENI WALIOJITOKEZA KWA MAELFU KATIKA MKUTANO NA SHEREHE ZA KUWASHUKURU NA KUWAPONGEZA WAKAZI WA KATA HIYO KWA KUICHAGUA  KWA KISHINDO CCM KATIKA NAFASI WENYEVITI NA WAJUMBE WA SEREKALI ZA MITAA (MTAA WA KALOLENI MASHARIKI MKT HASSAN SHARIF NA MAGHARIBI MKT BDALLAH NASSORO).
 MWENYEKITI WA CCM WILAYA YA ARUSHA NDG WILFRED SOILELI  AKIWAHIMIZA WANANCHI WA KATA YA KALOLENI  YA  JIJINI ARUSHA KUJITOKEZA KWENDA KUIPIGIA KURA YA NDIYO RASIMU YA KATIBA ILIYOPENDEKEZWA SIKU ITAKAPOWADIA ILI IWEZE KUPITA KWA KISHINDO, KATIKA VIWANJA VYA OFISI YA MTENDAJI WA KATA, KATIKA MKUTANO NA SHEREHE ZA KUWASHUKURU NA KUWAPONGEZA WAKAZI WA KATA HIYO KWA KUICHAGUA  KWA KISHINDO CCM KATIKA NAFASI WENYEVITI NA WAJUMBE WA SEREKALI ZA MITAA (MTAA WA KALOLENI MASHARIKI MKT HASSAN SHARIF NA MAGHARIBI MKT BDALLAH NASSORO).





 BAADA YA MKUTANO , MAMBO YALIKUWA KAMA INAVYOONEKANA,KWENYE PICHA ZA JUU KWANI WASWAHILI HUSEMA  KWANI "KAZI NA DAWA"

KATIBU WA UVCCM WILAYA YA ARUSHA NDG JAMAL KHIMJI AKITETA JAMBO NA KATIBU WA UVCCM KATA YA KATI NDG JAMILA MARA BAADA YA SHEREHE HIZO.

JIKO LA HOTELI YA KENDWA ROCKS , MKOA WA KASKAZINI UNGUJA LAUNGUA MOTO.

 Baadhi ya Sehemu za jengo la Jiko la Hoteli ya Kendwa Rocks iliyoko Mkoa wa Kaskazini Unguja ambalo iliuungua moto ulisababishwa na hitilafu za umeme.
 Wahandisi wa Hoteli ya Kendwa wakijaribu kurejesha miundo mbinu ya umeme iliyoathirika kutokana na moto mkubwa uliotokea kwenye Hoteli hiyo.
 Jengo la Jiko la Hoteli ya Kendwa Rocks lililoungua vibaya mwa moto uliosababishwa na hitilafu ya umeme.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimfariji Mwakilishi wa Hoteli ya Gold Zanzibar iliyopo Nungwi  Mkoa wa Kaskazini Unguja Bwana Andrea Azzala baada ya paa la jengo lao kuungua moto.
Balozi Seif akikaguzwa kuangalia maeneo yaliathirikia kutokana na moto kwenye Hoteli ya Kendwa Rocks Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Kulia ya Balozi Seif ni  Msaidizi Menja Mkuu wa Kendwa Rocks Bwana Omar Ibrahim Kilupi, Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Kanal Mstaafu Juma Kassim Tindwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Moh’d Aboud Moh’d.

Picha na – OMPR – ZNZ.

Press Release:-

Hitilafu ya umeme iliyotokea mapema  asubuhi imesababisha moto mkubwa   ulioteketeza jengo la jiko, Duka ,sehemu ya burdani ya Hoteli Kendwa Rocks pamoja na Hoteli ya Gold Zanzibar zilizopo katika Kijiji cha Nungwi Mkoa wa kaskazini Unguja.

Moto huo ulioripuka kwa kusaidiwa na upepo mkali uliokuwa ukivuma majira ya saa nne za asubuhi umeteketeza vitu na vifaa mbali  vilivyokuwemo ndani ya majengo hayo na kusabisha hasara inayokisiwa kufikia shilingi za Kitanzania Bilioni Moja { 1,000,000,000/- }.


 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiambatana pamoja na Waziri wa  Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar  Mh. Moh’d Aboud Moh’d walifika eneo la tukio kuwafariji wamiliki wa Hoteli hizo.

Meneja wa Kendwa Rocks Bwana Ali Ibrahim Kilupi alimueleza Balozi Seif kwamba wafanyakazi  kwa kushirikiana na wananchi wanaozizunguuka Hoteli hizo walijaribu kuuzima moto huo uliokuwa ukiwaka kwa kasi kutokana na upepo mkali uliovuma wakati huo.

Bwana Ali alifahamisha kwamba Uongozi wa Hoteli hiyo ulijaribu kuwasiliana na Kikosi cha Zima moto na Uokozi  Zanzibar kujaribu kusaidia uokozi huo lakini wakati huduma hizo zinakaribi kufika kasi ya moto huo iliyochukuwa baina ya dakika 15 na 20 tayari ilikuwa imeshateketeza vifaa na vitu vyote.

Alieleza kwamba licha ya wageni wengi kuvutiwa na mazingira ya nyumba zinazoezekwa makuti lakini Uongozi wa Hoteli hiyo umeamua kubadilisha mfumo huo kwa kutumia vitage ili kujaribu kujikinga na majanga kama hayo.

Naye Mwakilishi wa Hoteli ya Gold Zanzibar Bwana Andrea Azzala alisema kwa kwa hivi sasa  ni mapema mno kujua hasara iliyopatikana kutokana na kuungua kwa paa la jengo lao moja.

Bwana Andrea aliwashukuru wafanyakazi na baadhi ya wananchi wa vijiji jirani vilivyozuunguka Hoteli hizo kwa jitihada zao zilizosaidia kukabiliana na moto huo uliovumba ghafla mapema asubuhi.

Akitoa pole kwa wamiliki wa miradi hiyo ya Hoteli Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesikitishwa kutokea kwa janga hilo la moto litakalorejesha nyuma malengo ya wamiliki wa hoteli hizo.

Hata hivyo Balozi Seif amefurahishwa na Uongozi wa Hoteli hiyo kwa uamuzi wake wa kuuwekea  bima ya moto mradi wao  kwani itasaidia kupunguza machungu ya hasara iliyotokea.

Alisema maafisa wa Idara ya Maafa Zanzibar ambayo iko chini ya Ofisi yake  itafanya tathmini kujuwa harasa kamili iliyotokea ya janga hilo na kuripoti Serikalini ili kuangalia namna ya kusaidia wawekezaji hao wazalendo.

Akitoa shukrani kwa niaba ya Uongozi wa hoteli ya Kendwa Rocks Msaidizi meneja Mkuu wa Hoteli hiyo Bwana Omar  Ibrahim Kilupi ameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibaf kwa  kuwa karibu na Wananchi wake.

Majanga ya miripuko ya moto yamekuwa yakitokea mara kwa mara katika kipindi cha kiangazi na kusababisha hasara kubwa inayochukuwa muda mrefu hasa kwenye miradi ya hotel.


Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
14/2/2015.


BALOZI SEIF ALI IDDI AIPONGEZA SERIKALI YA WATU WA MAREKANI

Written By CCMdijitali on Wednesday, February 11, 2015 | February 11, 2015


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya siku tano kuhusu zoezi la kukabiliana na maafa Zanzibar yanayofanyika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort.

Kushoto ya Balozi Seif ni Mwakilishi wa shirika la Usafricom Kamanda Philip Knightsheen, Waziri wa Afya Zanzibar Mh. Rashid Seif , Kaimu Kamanda wa Brigedia Nyuki Zanzibar na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Abdulla Mwinyi.

Kulia ya Balozi Seif ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Moh;d Aboud Moh’d, Mwakilishi wa shirika la Misaada la Marekani Us Aid Bibi Anna Senga, Waziri wa Nchio Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum Mh. Haji Omara Kheir, na Msadizi Kamishna wa Polisi Kamanda Hassan Nassir.




Kamanda Philip Knightsheen akitoa salamu za Shirika lake linalosimamia huduma za Kibinaadamu na Afya la Usafricom kwenye mafunzo ya siku tano ya zoaezi la kukabiliana na maafa Zanzibar hapo Zanzibar Beach Resort Mazizini.
 Mwakilishi wa shirika la Misaada la Marekani Us Aid Bibi Anna Senga akizungumza katika mafunzo ya siku tano kuhusu zoezi la kukabiliana na maafa Zanzibar.
Waziri wa Ncho Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Moh’d Aboud Moh’d akimkabidhi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ripoti ya Maafa Zanzibar.
 Mkurugenzi wa Idara ya Maafa Zanzibar Nd. Ali Juma Hamad wa kwanza kutoka kulia akiwa na baadhi ya watendaji wa Idara hiyo wanaoshiriki mafunzo ya sku tano kuhusu zoezi la kukabiliana na maafa Zanzibar.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya siku tano kuhusu zoezi la kukabiliana maafa Zanzibar yanayofanyika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini.
 Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya siku tano kuhusu zoezi la kukabiliana maafa Zanzibar yanayofanyika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini.
 Mwakilishi wa shirika la Misaada la Marekani Us Aid Bibi Anna Senga akibadilishana mawazo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif nje ya ukumbi wa Zanzibar Beach Resort mara baada ya kufunguliwa rasmi mafunzo ya zoezi hilo.

Nyuma ya Balozi Seif ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais ,Tawala za Mikoa na Idara Maalum Mh. Haji Omara Kheir. Kulia ya Balozi Seif ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Moh’d Aboud Moh’d na Mwakilishi wa Shirika linalosimamia huduma za Kibinaadamu na Afya la Usafricom Kamanda Philip Knightsheen.


Picha na – OMPR – ZNZ.

 Press Release:-

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameipongeza Serikali ya Watu wa Marekani kupitia Shirika lake la Misaada ya Maendeleo la Us aid kwa jitihada zake za kuisaidia Zanzibar katika mipango yake ya kutafuta mbinu za kuwa tayari kwa kukabilana na maafa wakati wowote yatapotokezea.

Alisema Zanzibar imekuwa na historia pana ya majanga mbali mbali yaliyowahi kuikumba na kusababisha maafa makubwa yatayoendelea kukumbukwa na vizazi vya sasa na vile vijavyo.

Balozi Seif alitoa pongezi hizo wakati akifungua rasmi mafunzo ya siku tano kuhusu zoezi la kukabiliana na maafa Zanzibar yanayofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

Alisema Marekani imekuwa mshirika mkubwa katika kusaidia harakati mbali mbali za maendeleo ya miundo mbinu ya mawasiliano ya Bara bara, huduma za Afya na ustawi wa Jamii wa Zanzibar jambo ambalo limekuwa likileta faraja kwa Wananchi walio wengi hapa Nchini.

Balozi Seif alifahamisha kwamba juhudi za Zanzibar katika kujiweka tayari kukabiliana na maafa yoyote yatakayoweza kutokea zimekuja kufuatia majanga tofauti yaliyowahi kutokea kama maradhi ya Kolera, ajali za vyombo vya usafiri wa Baharini na majanga ya moto ambayo yamesababisha vifo vya watu kadhaa.

“ Zanzibar imeshuhudia maradhi ya kolera karibu miaka 20 iliyopita na kukumbwa na ajali za usafiri wa Baharini miaka michache iliyopita na kulazimika kuchukuwa jitihada za tahadhari katika kukabiliana nayo endapo yatatokezea tena “. Alisema Balozi Seif.

Alifahamisha kwamba Zanzibar ikiwa miongoni mwa Mataifa machanga Duniani inawajibika kuimarisha Idara yake ya Maafa kwa kushirikiana na taasisi za ulinzi, Afya na Mawasiliano ili kuona huduma za kukabiliana na maafa Nchini zinapatikana kwa ubora unaokusudiwa.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alieleza kuwa ile nia ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kujenga vituo vya mafunzo na uokozi wakati yanapotokea maafa katika eneo la Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja na Chake chake kwa Pemba bado iko pale pale.

Alisema kilichokwamisha utekelezaji wa mpango huo kwa sasa ni upatikanaji wa vifaa na fedha licha ya juhudi kadha zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali kuu katika kuomba misaada ya kiufundi kwa Taasisi za Kimataifa zilizobobea katika taaluma hiyo muhimu.

Balozi Seif alieleza kuwa katika kuimarisha huduma za kukabiliana na maafa Nchini Mswada wa Sheria ya Kuanzisha Sheria ya Kupunguza na Kukabiliana na Maafa Zanzibar uliwasilishwa na kujadiliwa na Baraza la Wawakilishi Zanzibar hivi karibu na hatimae kupitishwa katika Mkutano wa 18 wa Baraza hilo.

Alisema Mswada huo ulikusudiwa kuweka sheria mpya inayoweka mfumo wa kisheria katika shughuli za kukabiliana na maafa na mambo ambayo yataondosha mapungufu yanayoonekana katika sheria iliyopo hivi sasa.

Balozi Seif alisisitiza kwamba Sheria hiyo mpya itawiana na Sera ya Kukabiliana na Maafa ya mwaka 2011 pamoja na Makubaliano na Mikataba ya Kikanda na Kimataifa inayohusiana na masuala ya kukabiliana na maafa iliyoridhiwa na nchi yetu.

Mapema Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Ahmad Kassim alisema lengo la zoezi hili la kukabiliana na maafa Zanzibar ni kujenga nguvu za pamoja kati ya Taasisi za Umma, binafsi zikiungwa mkono na washirika wa maendeleo .

Nd. Ahmad alisema kwa vile majanga yanapotokea yanakumba kila kilichoko mbele yake ushirikiano wa karibu unahitajika kwa pande zote zinazohusika ili kujiweka tayari kukabiliana na majanga yoyote yanapotokezea.

Wakitoa salamu za Taasisi zao za kimataifa zinazoshiriki zoezi hilo Mwakilishi wa Shirika linalosimamia huduma za Kibinaadamu na Afya la Usafricom Kamanda Philip Knightsheen na Mwakilishi wa shirika la Misaada la Marekani Us Aid Bibi Anna Senga walisema suala la ulinzi wa maisha ya Mwanadaamu linamuhusu kila mwana jamii.

Walisema licha ya kwamba nguvu kubwa imewekwa kwa vikosi vya ulinzi na uokozi kukabiliana na maafa yanapotokea, lakini bado jukumu hilo litaendelea kusimamiwa kwa pamoja na taasisi zote za umma,binafsi kwa kushirikiana na washirika wa maendeleo.

Wawakilishi wa taasisi hizo za Kimataifa walisema kwamba Nchi za Malawi, Msumbiji na Senegal zinazokuwa zikikabiliana na mafuriko ya mara kwa mara zimekuwa zikipata msaada ya kibinaadamu kwa lengo la kuwapa matumaini wananchi wake wanaokumbwa na kadhia hiyo.

Waliahidi kwamba Taasisi na mashirika ya maendeleo ya Kimataifa wakiyatolea mfano yale ya Unicef, WHO,Usafricom,CDHAM na mengine ya kujitolea yataendelea kuunga mkono juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kukabiliana na majanga na maafa wakati yanapotokea.

Akimkaribisha mgeni rasmi kufungua zoezi hilo Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Moh’d Aboud Moh’d alizishukuru Taasisi inayohudumia masuala ya Kibinaadamu na Afya { USAFRICOM } na ile ya kujikinga na Majanga ya Kibinaadamu { CDHAM } kupitia Serikali ya Marekani kwa kukubali kugharamia mafunzo ya zoezi hilo.

Waziri Aboud alisema msaada wa Taasisi hizo utasaidia kuwawezesha washiriki wa mafunzo hayo kutoka Mataifa mbali mbali rafiki kupata taaluma pana itayoweza kuwasaidia katika kutekeleza majukumu yao kwenye taasisi wanazotokea.

Mafunzo hayo ya siku tano kuhusu zoezi la kukabiliana na maafa Zanzibar yanayofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort yameshirikisha wawakilishi wa Taasisi za ulinzi, maafa, Utawala, pamoja na wataalamu wa Afya kutoka nchi mbali mbali Duniani.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
9/2/2015.
 



 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link