MIUNDOMBINU YA ELIMU ZANZIBAR SASA YALINGANA NA MAHITAJI YA KARNE YA 21
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Zanzibar imepiga hatua kubwa katika kuimarisha mazin...
Latest Post
April 24, 2016
Diwani wa Chadema azua tafrani,uchaguzi mdogo Mtaa wa Sanare
Written By CCMdijitali on Sunday, April 24, 2016 | April 24, 2016
Diwani wa Chadema Mh Msofe amejikuta chini ya ulinzi kwa kukiuka taratibu na kanuni za uchaguzi kwa kufanya kampeni siku ya kupiga kura za marudio leo katika Mtaa wa Sanare ,Kata ya Daraja II.
Kijana wa Chadema naye ajikuta mikononi mwa Sheria ,baada ya kutumia bendera ya chama chake kutaka kipigiwe kura,katika eneo la kupigia kura.
Madiwani wa Chadema Kata za Themi na Olmoti wakodiwa kuongeza nguvu Uchguzi wa Mwenyekiti wa Serekali ya Mtaa wa Sanare leo.
Diwani wa Chadema Mh Msofe,akiondolewa kwenye eneo linalofanya uchaguzi leo,katika Mtaa wa Sanare,Kata ya Daraja II
Aliyesimama kulia akiwa ameweka mikono mfukoni ni mwanachama wa Chadema aliyekuwa anatumia bendera ya chama hicho kwenye eneo la uchguzi leo
Wananchi wenye hasira kali,wakihakikisha Diwani Msofe anaondolewa kwenye Mtaa huo, kwa kukutwa akifanya Kampeni kwenye Mtaa wa Sanare leo.Uchaguzi huu unarudiwa baada ya matokeo ya awali ,wagombea wote kutoka suluhu kwa idadi ya kura sawa CCM 381 ,Chadema381
Madiwani wa Kata ya Themi (aliyevaa jeans) na Olmoti (mbele ya mama mwenye blausi ya mistari) wakiwa katika eneo la uchaguzi leo, katika Mtaa wa Sanare. Baada ya Wakaazi kuwalalamikia kuwa huo uchaguzi hauwahusu kwani siyo wakaazi wa eneo husika ,ilibidi waondoke.
Wakazi wa Mtaa wa Sanare ,wakitimiza haki yao ya Kikatiba ya kumchagua kiongozi wanayemtaka,katika foleni.
Diwani wa Chadema Mh Msofe,akiongea na baadhi ya Viongozi wa CCM kwenye eneo linalofanya uchaguzi leo katika Mtaa wa Sanare,Kata ya Daraja II
Wakazi wa Mtaa wa Sanare ,wakitimiza haki yao ya Kikatiba ya kumchagua kiongozi wanayemtaka,katika foleni.
Diwani wa Chadema Mh Msofe (aliyevaa kofia),akiongea na Katibu wa CCM Kata ya Daraja II Ndg Mkombozi Kifumba (kushoto mwenye nguo nykundu na mistari meupe) kwenye eneo linalofanya uchaguzi leo katika Mtaa wa Sanare,Kata ya Daraja II
Wakazi wa Mtaa wa Sanare ,wakitimiza haki yao ya Kikatiba ya kumchagua kiongozi wanayemtaka,katika foleni.
Gari ya Polisi ikiwa imemchukua kijana aliyekuwa anatumia nembo ya Chama chake kwenye eneo la Uchaguzi leo,akipelekwa kituo cha Polisi.
Kiongozi wa Polisi akiondoa watu waliokuwa wamejazana kwenye kituo cha kupigia kura,wakitakiwa wawe mbali na kituo hicho mara baada ya kupiga kura.
Picha zote na Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha,Ndg jasper Kishumbua
Labels:
ARUSHA
April 22, 2016
Michelle Obama Pictures - Photos of the First Lady
Written By CCMdijitali on Friday, April 22, 2016 | April 22, 2016
Labels:
MICHEZO NA BURUDANI
April 22, 2016
Kushoto ya Mhe. Haji Omar ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif na Kulia ya Mh. Haji ni Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Mh. Salama Aboud Talib na Naibu wake Mh. Juma Makungu Juma.
Picha na - OMPR – ZNZ.
Press Release:-
Balozi Seifu afanya mazungumzo na Masheha na Viongozi wa Wilaya za Magharibi “ A ” na “ B ”
Balozi Seif akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo yake na Masheha wa Wilaya za Magharibi A na B hapo Makao Makuu ya Kikosi cha Valantia Mtoni.
Balozi Seif afanya mazungumzo na Masheaha Baadhi ya Masheha wa Wilaya za Magharibi A na B
Kulia ya Balozi Seif ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum ya SMZ Mh. Haji Omar Kheir na Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Mh. Salama Aboud Talib.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mh. Abdulla Mwinyi wa kwanza kutoka Kushoto akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Magharibi A Ndugu Mwinyiusi Khamis na yule ya Magharibi “B”Nd. Ayoud Mohammed Mhmaoud wakifuatilia hotuba ya Balozi Seif hayupo pichani wakati akizungumza na masheha wa wilaya zao.
Baadhi ya Masheha wa Wilaya za Magharibi A na B wakisikiliza hotuba ya Balozi Seif wakati alipobadilishana nao mawazo kuhusu suala la migogoro ya ardhi katika maeneo yao.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum ya SMZ Mh. Haji Omar Kheir akitoa msimamo wa Wizara yake katika kutekeleza agizo la Rais wa Zanzibar kuhusu migogoro ya ardhi.
Kushoto ya Mhe. Haji Omar ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif na Kulia ya Mh. Haji ni Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Mh. Salama Aboud Talib na Naibu wake Mh. Juma Makungu Juma.
Sheha wa Shehia ya Tomondo Bwana Moh’d Omar Said akichangia mawazo katika mkutano wao na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar uliofanyika
Makao Makuu ya Kikosi cha Valantia {KVZ} Mtoni.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Masheha wa Wilaya za Magharibi “A “na “ B” pamoja na wakuu wao wa Wilaya na Mkoa hapo katika Ukumbi wa Kikosi cha Valantia {KVZ} Mtoni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Picha na - OMPR – ZNZ.
Press Release:-
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Serikali italazimika kuchukuwa maamuzi magumu katika kukabiliana na watu waliojenga nyumba bila ya vibali wala kuzingatia taratibu za Taasisi za Ardhi hasa maeneo yaliyowekwa kwa ajili ya miradi ya Kijamii,vianzio vya Maji pamoja na mitaro ya kupitishia maji ya mvua.
Alisema hatua inaandaliwa kuchukuliwa na Serikali kupitia Taasisi husika chini ya usimamizi wa Viongozi watakaosimamia taasisi zao katika azma ya kutekeleza agizo la Rais wa Zanzibar alilolitoa wakati akilizindua Baraza la Wawakilishi Zanzibar juu ya kukabiliana na migogoro ya ardhi ndani ya kipindi cha miaka mitano ijayo.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na Masheha pamoja na watendaji wa Taasisi zote zinazohusika na masuala ya Ardhi wa Wilaya zote mbili za Magharibi “A” na “ B” mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Makamu Makao Makuu ya Kikosi cha Valantia { KVZ } Mtoni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Alisema Serikali imebaini kwamba uuzaji holela wa maeneo ya ardhi unaofanywa na baadhi ya watu wakiwemo pia masheha na hata watendaji wa Idara ardhi ni chanzo cha ujenzi mbovu wa makaazi ya watu usiozingatia Mipango Miji na hatimae kusababisha matatizo ya kutowafikia wananchi katika kupatiwa huduma muhimu za kijamii.
Balozi Seif alieleza kwamba Taifa lazima lirejee katika heshima yake ya kuwa na mipango bora ya ardhi itakayozingatia mazingira kwa lengo la kuondosha migogoro ya ardhi inayoonekana kuongezeka kila siku hasa katika Wilaya za Magharibi “A” na “ B”.
Alitolea mfano eneo la chuini lililotengwa maalum na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa Afisi zake, licha ya tangazo lililobandikwa likitoa indhari ya kutofanyika ujenzi wa aina yoyote lakini baadhi ya watu waliamua kuvamia kwa ujenzi wa nyumba za kudumu na viongozi wa eneo hilo wakishuhudia kutendeka kwa mambo hayo.
Alisema kuachiliwa kuendelea kwa tabia hii inaweza kufika wakati hata ikakosekana maeneo ya kilimo cha mboga mboga kwenye Wilaya hizo kama Wilaya ya Mjini ilivyokosa maeneo ya wazi kwa ajili ya shughuli za Jamii.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alitoa agizo kwa Masheha wote wa Wilaya mbili za Magharibi “A” na “ B” kuanza kufanya uhakiki wa kuziorodhesha nyumba zote zilizojengwa bila ya kibali na katika maeneo yasiyostahiki.
“ Tunakusudia kubomoa majengo yote yaliyojengwa bila ya kibali na kwenye maeneo ya njia za maji ikiwa ni mwanzo wa maamuzi magumu yatakayochukuliwa na Serikali ”. Alisema Balozi Seif.
Alisema sambamba na hilo kuanzia sasa hakuna sheha atakayepaswa wala kuruhusiwa kutoa, kuuza au kukata viwanja kwa ajili ya ujenzi wa nyumba jukumu ambalo liko chini ya dhama ya Wizara ya Ardhi, Maji Nishati na Mazingira.
Mapema Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Mh. Haji Omar Kheir alisema katika kukabiliana na migogoro ya Ardhi Sheha ye yote atakayebainika kuhusika na suala la ardhi itakuwa ndio kibali chake cha kuachia madaraka.
Mh. Haji alisema ameamua yeye pamoja na Uongozi wa Wizara yake kuanza ziara za kukagua maeneo mbali mbali Mjini na Vijijini ili kubaini uzembe na udhaifu uliofanywa na baadhi ya viongozi hao na atakapobaini uzembe wowote atalazimika kuchukua hatua zinazofaa hapo hapo.
Alisema kazi iliyo mbele ya Viongozi hao kwa sasa ni kuhakikisha kwamba agizo la Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein linaanza kuchukuliwa hatua mara moja.
Naye kwa upande wake Waziri wa Ardhi, Maji,Nishati na Mazingira Mh. Salama Aboud Talib aliwaahidi Masheha na Viongozi hao wa Wilaya za Magharibi “A” na “ B ” kwamba atasimamia kwa uadilifu jukumu alilokabidhiwa ili kuona haki ya kila raia wa Nchi hii inapatikana.
Waziri Salama alisema wapo baadhi ya watendaji wakiwemo pia wa Taasisi zilizo chini ya Wizara yake ambao wamekuwa wakisababisha kuibuka kwa migogoro ya ardhi katika maeneo mengi kwa kuendekeza tama na kukosa uadilifu.
Mh. Salama Aboud aliwahakikishia masheha na Viongozi hao wa Wilaya za Magharibi “ A ” na “ B ”kwamba Maamuzi magumu yanayopaswa kuchukuliwa na Serikali Kuu dhidi ya wanaosababisha migogoro hiyo atakuwa wa kwanza kuanza kuyatekeleza.
Mkutano huo umewashirikisha Masheha wote wa Wilaya za Magharibi “A” na “B”, Wakuu wa Wilaya hizo, Watendaji wa Ardhi, Mazingira, na Mkoa wa Mjini Magharibi akiwemo pia Meya wa Manispaa ya Zanzibar Mstahiki Khatib Abdulrahman Khatib.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
21/4/2016.
Labels:
KITAIFA
April 21, 2016
Picha zote na Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha - Ndg jasper Kishumbua
Mama Samia apokelewa na maelfu ya wakazi wa Mkoa wa Arusha
Written By CCMdijitali on Thursday, April 21, 2016 | April 21, 2016
Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu,leo amewasili Jijini Arusha ,tayari kwa Mkutano wa Udhibiti wa Silaha ndogo ndogo katika Kanda ya Afrika,ukikutanisha Washiriki wa Nchi zaidi ya 15.
Mapokezi hayo yameongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh Daudi Felix Ntibenda katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro
Wakazi wengi walionekana kujipanga kando kando ya barabara kuu ya Moshi -Arusha
Baadhi ya Viongozi wa Serekali na Chama Cha Mapinduzi walishiriki katika mapokezi hayo leo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro
Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu,akishuka kutoka kwenye ndege ,mara baada ya kutua Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro leo.
Baadhi ya umati wa watu waliojitokeza kumlaki katika Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro leo.
Kama inavyoonekana ,pembezoni mwa barabara kuu ya Moshi -Arusha, baadhi ya watu waliacha shughuli zao ,kumlaki Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu
Baadhi ya Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi kutoka nafasi mbalimbali, (kushoto) ni Bi Esther Maleko,Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Arusha,Mwenyekiti wa CCM Kata ya Unga Ltd - Bi Sophia Munisi,Kada wa CCM Bi Tausi na aliyesimama nyuma yao ni Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Arusha Ndg Martin Munisi.
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha NdgSabaya akisalimiana na Mkurugenzi wa Maji Safi na Maji Taka Mkoani Arusha.
Wamama nao hawakuwa nyuma,pichani ni Muasisi wa Chama Cha Mapinduzi ,maarufu kwa jina la Bibi Ndoyee wa Kaloleni,Jijini Arusha.
Kada na Kiongozi wa Chama Cha Mapinduzi na Mfanyabiashara maarufu Jijini Arusha
Alhaji H.Migire
Katibu wa UVCCM Wilaya ya Arusha Ndg jamal Kimji,Katibu Msaidizi wa CCM Wilaya ya Arusha Ndg Elia Ngowi na Rajabu Mshana Kiongozi wa UVCCM Kata ya Sokon I
Katibu Hamasa wa UVCCM Mkoa wa Arusha Ndg Lucas Paschal Nsomi na Mwenyekiti wa Serekali ya Mtaa wa Olmuriaki,Kata ya Sombetini alipita bila kupingwa kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika tarehe 17/04/2016, baada ya mgombea wa Chadema ,kuandika barua ya kujitoa,bada ya kuona majimazito. 
Mwenyekiti wa UWT Mkoa Bi Zelote na Katibu wake Bi Fatuma Hasan
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh Daudi Felix Ntibenda,akiwa tayari kwenda kumpokea mgeni wake.
Bi Viola ,Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Arusha akiwa na Bi Anna Msuya, tayari kumlaki Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu,kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro leo.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh Daudi Felix Ntibenda,akisalimiana na baadhi ya Viongozi wa dini kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro leo.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh Daudi Felix Ntibenda,akimlaki Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro leo.
Picha zote na Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha - Ndg jasper Kishumbua
Labels:
ARUSHA











