MIUNDOMBINU YA ELIMU ZANZIBAR SASA YALINGANA NA MAHITAJI YA KARNE YA 21
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Zanzibar imepiga hatua kubwa katika kuimarisha mazin...
Latest Post
January 31, 2023
KILUPI-AKABIDHIWA OFISI, ASEMA HAKUNA WA KUZUIA USHINDI WA CCM.
Written By CCMdijitali on Tuesday, January 31, 2023 | January 31, 2023
NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.
KATIBU mpya wa Idara ya Organazesheni CCM Zanzibar Ndg.Omar Ibrahim Kilupi,amesema chini ya uongozi wake hakuna Chama chochote cha kisiasa kitakachozuia ushindi wa CCM mwaka 2025.
Msimamo huo ameutoa leo wakati akikabidhiwa ofisi ya idara hiyo Kisiwandui na aliyekuwa Katibu wa Idara ya Organazesheni Ndg. Galos Cassian Nyimbo huko Kisiwandui Zanzibar.
Kilupi alisema Chama hicho kina tiketi ya kudumu ya kuongoza dola kutoka kwa wananchi wanaokiamini na kukipenda kutokana na usimamizi mzuri wa Ilani yake ya Uchaguzi ya mwaka 2020/2022.
Alifafanua kwamba CCM ni Chama mwalimu na kiongozi wa vyama vingine vya kisiasa kwani imejiwekea mfumo imara wa kiuongozi na utendaji kuanzia ngazi ya shina hadi taifa.
Alisema kwamba CCM kupitia ibara ya 5 ya Katiba yake imeweka wazi dhamira yake ya kushinda bila vikwazo kwa kila uchaguzi wa dola.
Alisema idara hiyo inahusika moja kwa moja ma masuala yote ya uchaguzi hivyo jukumu lake la kwanza ni kuhakikisha CCM inashinda kwa kishindo katika uchaguzi wa Dola wa mwaka 2025.
“ Nachukua nafasi hii kwanza kukishukru Chama Cha Mapinduzi kilichoamua kunipa dhamana hii kubwa, naahidi kutumia uwezo wangu wote kuhakikisha kinashinda kwa asilimia kubwa katika uchaguzi wowote utakaotokea kuanzia hivi sasa.
Pia ofisi yangu ipo wazi muda wote nipo tayari kushiriana na wanachama,viongozi na watendaji wote wa CCM na wale wenye mawazo na fikra za kujenga chama chetu.”, alisema Kilupi.
Aidha Kilupi aliahidi kutekeleza majukumu yake kwa uadili,ueledi na ubunifu ili kwenda sambamba na malengo ya Chama Cha Mapinduzi.
Katika maelezo yake Katibu huyo, amewataka maofisa wa idara hiyo kuwajibika katika majukumu yao ya kikazi.
Alisema kama dhamira ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) kinavyotaka ni kufanya kazi kwa ushirikiano na umoja na ndiye na yeye anavyotaka maofisa hao wa idara kuzingatia hilo.
"Kila mtu awajibike kwenye kwenye nafasi yake na ninachoamini ni kuwa tukifanya kazi kwa pamoja tutafanikiwa na hatutoweza kushindwa kufikia dhamira ya CCM ya kuhakikisha ushindi wa chama kila uchaguzi,"alisema
"Ninashukuru kwa mapokezi yenu pia ninampongeza Katibu aliyepita Galos kwa kazi nzuri yenye uadilifu hivyo anastahili pongezi kubwa,"alisema
Alisema kama ilivyokawaida na desturi ya chama ni kukabidhiana vijiti vya uongozi na kinachotakiwa ni kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa.
Kupitia hafla hiyo ya makabidhiano Ndgu.Kilupi, aliwapongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi kwa kasi yao kubwa ya kutatua changamoto za wananchi na kuwaletea maendeleo endelevu.
Naye Katibu mstaafu wa Idara hiyo Ndg. Casian Galos Nyimbo, amesema idara hiyo ndio chombo mahsusi cha kufanikisha masuala yote ya uchaguzi wa Chama hivyo ni muhimu kufanya kazi kwa juhudi kubwa.
Pamoja na hayo aliwataka watumishi katika idara hiyo kutoa ushirikiano mkubwa kwa kiongozi mpya aliyekabidhiwa ofisi ili wafikie kwa haraka malengo endelevu ya Chama Cha Mapinduzi.
| KATIBU Mstaafu wa Kamati Maalum ya NEC, Idaraya Organaizesheni CCM Zanzibar Ndg. Casian Gallos Nyimbo (kushoto), akimkabidhi nyaraka za kiutendaji Katibu mpya wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Organazesheni Ndg.Omar Ibrahim Kilupi, huku Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui leo Tarehe 31/01/2023. |
January 31, 2023
KILUPI-AKABIDHIWA OFISI, ASEMA HAKUNA WA KUZUIA USHINDI WA CCM.
NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.
KATIBU mpya wa Idara ya Organazesheni CCM Zanzibar Ndg.Omar Ibrahim Kilupi,amesema chini ya uongozi wake hakuna Chama chochote cha kisiasa kitakachozuia ushindi wa CCM mwaka 2025.
Msimamo huo ameutoa leo wakati akikabidhiwa ofisi ya idara hiyo Kisiwandui na aliyekuwa Katibu wa Idara ya Organazesheni Ndg. Galos Cassian Nyimbo huko Kisiwandui Zanzibar.
Kilupi alisema Chama hicho kina tiketi ya kudumu ya kuongoza dola kutoka kwa wananchi wanaokiamini na kukipenda kutokana na usimamizi mzuri wa Ilani yake ya Uchaguzi ya mwaka 2020/2022.
Alifafanua kwamba CCM ni Chama mwalimu na kiongozi wa vyama vingine vya kisiasa kwani imejiwekea mfumo imara wa kiuongozi na utendaji kuanzia ngazi ya shina hadi taifa.
Alisema kwamba CCM kupitia ibara ya 5 ya Katiba yake imeweka wazi dhamira yake ya kushinda bila vikwazo kwa kila uchaguzi wa dola.
Alisema idara hiyo inahusika moja kwa moja ma masuala yote ya uchaguzi hivyo jukumu lake la kwanza ni kuhakikisha CCM inashinda kwa kishindo katika uchaguzi wa Dola wa mwaka 2025.
“ Nachukua nafasi hii kwanza kukishukru Chama Cha Mapinduzi kilichoamua kunipa dhamana hii kubwa, naahidi kutumia uwezo wangu wote kuhakikisha kinashinda kwa asilimia kubwa katika uchaguzi wowote utakaotokea kuanzia hivi sasa.
Pia ofisi yangu ipo wazi muda wote nipo tayari kushiriana na wanachama,viongozi na watendaji wote wa CCM na wale wenye mawazo na fikra za kujenga chama chetu.”, alisema Kilupi.
Aidha Kilupi aliahidi kutekeleza majukumu yake kwa uadili,ueledi na ubunifu ili kwenda sambamba na malengo ya Chama Cha Mapinduzi.
Katika maelezo yake Katibu huyo, amewataka maofisa wa idara hiyo kuwajibika katika majukumu yao ya kikazi.
Alisema kama dhamira ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) kinavyotaka ni kufanya kazi kwa ushirikiano na umoja na ndiye na yeye anavyotaka maofisa hao wa idara kuzingatia hilo.
"Kila mtu awajibike kwenye kwenye nafasi yake na ninachoamini ni kuwa tukifanya kazi kwa pamoja tutafanikiwa na hatutoweza kushindwa kufikia dhamira ya CCM ya kuhakikisha ushindi wa chama kila uchaguzi,"alisema
"Ninashukuru kwa mapokezi yenu pia ninampongeza Katibu aliyepita Galos kwa kazi nzuri yenye uadilifu hivyo anastahili pongezi kubwa,"alisema
Alisema kama ilivyokawaida na desturi ya chama ni kukabidhiana vijiti vya uongozi na kinachotakiwa ni kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa.
Kupitia hafla hiyo ya makabidhiano Ndgu.Kilupi, aliwapongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi kwa kasi yao kubwa ya kutatua changamoto za wananchi na kuwaletea maendeleo endelevu.
Naye Katibu mstaafu wa Idara hiyo Ndg. Casian Galos Nyimbo, amesema idara hiyo ndio chombo mahsusi cha kufanikisha masuala yote ya uchaguzi wa Chama hivyo ni muhimu kufanya kazi kwa juhudi kubwa.
Pamoja na hayo aliwataka watumishi katika idara hiyo kutoa ushirikiano mkubwa kwa kiongozi mpya aliyekabidhiwa ofisi ili wafikie kwa haraka malengo endelevu ya Chama Cha Mapinduzi.
January 03, 2023
WAZIRI MABULA AWEKA WAZI MAFANIKIO NA UTEKELEZAJI WA MASUALA YA SEKTA YA ARDHI NCHINI
Written By CCMdijitali on Tuesday, January 3, 2023 | January 03, 2023
Na Munir Shemweta, WANMM
Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan ameridhia ardhi yenye ukubwa wa ekari 1,492,703 iliyokuwa sehemu ya maeneo ya hifadhi na maeneo ya umma zikiwemo Ranchi za Serikali kumegwa na kurasimishwa kwa wananchi.
Aidha, Mapori Tengefu 12 yenye ukubwa ekari 707,962 na Hifadhi za Misitu Misitu 7 zenye ekari 46,715 nayo imefutwa na ardhi hiyo kukabidhiwa kwa wananchi kupitia usimamizi wa Serikali za Mikoa katika kupanga na kuyapima maeneo hayo.
Hayo yamebainishwa leo na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi Mhe. DKt Angeline Mabula wakati akizungumzia masuala mbalimbali ya sekta ya ardhi na muelekeo wa utekezaji wa Wizara hiyo kwa kipindi cha kuanzia januari 2023.
"Kamati ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta imeielekeza Mikoa kusimamia utekelezaji wa uamuzi wa Serikali kwenye maeneo yao yote yalioainishwa na kutolewa uamuzi" alisema Dkt. Mabula.
Kwa mujibu wa Dkt Mabula, mongoni mwa kazi zinazondelea kutekelezwa hivi sasa ni pamoja na uwekaji wa alama za mipaka baina ya maeneo ya hifadhi na maeneo ambayo Serikali imeridhia yabaki kwa wananchi, upangaji na upimaji wa maeneo yaliyorejeshwa kwa wananchi, utambuzi, uhakiki na uthamini wa maeneo ambayo wananchi watatakiwa kupisha shughuli au maeneo yatakayotumika kwa matumizi ya umma na uandaaji wa mipango ya matumizi ya ardhi.
Amechukua fursa kupitia mkutano na vyombo vya habari kuomba kila Mkoa kusimamia utekelezaji wa maamuzi ya Serikali na kuhakikisha kazi zote zinakamilishwa ifikapo tarehe 30 Machi, 2023.
Akizungumzia ulipaji kodi ya pango la ardhi hasa baada ya msamaha wa riba ya malimbikizo ya pango la ardhi uliotolewa na Rais Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan ambapo wananchi wenye malimbikizo walipewa nafuu ya kulipa deni la msingi ili wasamehewe riba ya malimbikizo. Waziri wa Ardhi alieleza kuwa, Kutokana na nafuu uliotolewa Wizara yake imeweza kukusanya jumla ya shs 90,907,939,421 sawa na asilimia 75 ya lengo la nusu mwaka.
Hadi kufikia Novemba, 2022 wananchi 2,819 wamenufaika na msamaha wa riba ya malimbikizo ya kodi ya pango la ardhi yenye jumla ya TZS 6,946,930,272. Idadi hiyo haijumuishi wananchi waliojitokeza ambao wamehudumiwa kuanzia tarehe 1 – 31 hadi Disemba 31, 2022.
Amewashukuru na kuwapongeza wamiliki wa ardhi waliojitokeza kunufaika na msamaha uliotolewa na Mhe. Rais na kubainisha kuwa, katika mwezi Disemba, 2022 Wizara ya Ardhi imeshuhudia idadi kubwa ya wamiliki waliojitokeza kulipa na kiasi cha bilioni 22.6 kimekusanywa katika mwezi Disemba pekee.
Akigeukia suala la utatuzi wa migogoro ya ardhi, Dkt Mabula amezitaka Mamlaka za Serikali za Mitaa kusimamia kikamilifu mipango ya jumla, mipango kina na mipango ya matumizi ya ardhi vijijini kupitia kamati za ardhi za Vijiji ili kudhibiti ujenzi holela usiozingatia mipango iliyoandaliwa na kuidhinishwa kupitia Kamati za Mipangomiji.
"wizara imekuwa ikipokea taarifa na malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu ukiukwaji wa taratibu mbalimbali zinazohusu Usimamizi wa Ardhi Mijini na Vijijini" alisema Dkt Mabula
Miongoni mwa malalamiko ni baadhi viongozi wa vijiji na Mitaa kuuza ardhi kinyume na utaratibu, kukosekana kwa udhibiti wa uendelezaji ardhi katika maeneo ya Vijiji na Miji. Hali hiyo imesabisha kuongezeka kwa migogoro ya ardhi na uendelezaji ardhi kinyume na mipango iliyoandaliwa na kuidhinishwa.
Dkt Mabula alisema Wizara yake inaandaa programu maalum ya kufanya ukaguzi wa uzingatiaji wa mipango ya matumizi ya ardhi kwa Mamlaka za Upangaji. Taarifa hizi zitatolewa kwa umma kama sehemu ya uwajibikaji wa mamlaka zetu kwa wananchi.
Kuhusu ujenzi wa vituo vya mafuta, Dkt Mabuka alisema hadi kufikia tarehe 31 Disemba, 2022 Wizara imepokea taarifa ya uendelezaji wa vituo vya mafuta kutoka Halmashauri 129 kati ya 184 zilizopo nchini sawa na asilimia 70.1.
Uchambuzi uliofanywa na Wizara ya Ardhi umebaini katika Halmashauri 129, kuna vituo 2,063 ambapo kati ya hivyo vituo vya mafuta ni 1269 (asilimia 61.6) na vituo vidogo vya mafuta ni 794 (asimilia 38.5) huku Vituo 1,868 vimejengwa katika umbali wa zaidi ya mita 200 kutoka kituo kimoja na kingine sawa na asilimia 90.5 kama inavyoelekezwa na kanuni ya viwango vya umbali
Aidha, Vituo 195 vimejengwa umbali wa chini ya mita 200 sawa na asilimia 9.5. Wizara inaendelea kufanya uchambuzi zaidi ili kubainisha vituo ambavyo vimejengwa kabla au baada ya kanuni za mwaka 2018 zinazoendelea kutumika ili hatua stahili ziweze kuchukuliwa.
Pia Waziri wa Ardhi alizungumzia suala la program ya miaka 10 ya urasimishaji makazi holela ambapo Wizara inayo Programu ya Urasimishaji Makazi iliyoanza kutekelezwa mwaka 2013. Programu hiyo mwisho wake ni mwaka huu 2023 na imekuwa ikitekelezwa katika Mitaa 3,397 kwenye Mikoa yote 26.
Dkt Mabula alisema, Mitaa 1,961 imerasimishwa sawa na asilimia 57.7 na Mitaa 1,436 haijarasimishwa sawa na asilimia 42.3 na kubainisha kuwa prrogramu hiyo imewezesha upangaji wa viwanja 2,338,926 na kati ya hivyo, viwanja 1,170,638 upimaji wake umekamilika. Aidha, jumla ya milki 177,330 zimeandaliwa na kutolewa kwa wananchi.
Hata hivyo, alisema katika kutekeleza Programu hiyo, kumekuwepo na changamoto mbalimbali licha ya mafanikio yaliyopatikana na kuzitaja baadhi ya changamoto kuwa ni pamoja na Uelewa mdogo wa wananchi juu ya umuhimu na namna zoezi la urasimishaji linavyofanyika, baadhi ya wananchi kutokuwa tayari kuchangia ardhi inayohitajika kwa ajili ya miundombinu na matumizi ya umma, baadhi ya wananchi kutolipa gharama za urasimishaji kwa wakati hali inayosababisha baadhi ya kampuni kushindwa kumudu gharama za utekelezaji na baadhi ya kampuni za urasimishaji kutokamilisha kazi kwa wakati pamoja na kutumia wataalam wasiokuwa na sifa.
Hata hivyo, alisema kutokana na uwepo wa changamoto hizo, Wizara imechukua hatua mbalimbali kuhakikisha kazi za urasimishaji zinakamilika na hatua hizo ni pamoja na Wizara kwa kushirikiana na Halmashauri, kukwamua baadhi ya kazi zilizokwama, kuchukua hatua kwa kampuni zilizoshindwa kutimiza wajibu wao ikiwa ni pamoja na kusimamisha au kufungia baadhi ya kampuni hizo, kuhusisha taasisi za kifedha katika miradi ya urasimishaji na kuandaa na kusambaza mwongozo wa urasimishaji ikiwemo kupunguza gharama za urasimishaji hadi kufikia shilingi 130,000 kwa kiwanja.
Pamoja na jitihada hizo, Wizara ya Ardhi kwa kushirikiana na Halmashauri na Sekta Binafsi inatekeleza programu ya Kupanga, Kupima na kumilikisha ardhi ili kuwa na miji nadhifu na iliyopangwa.
Kwa mujibu wa Waziri wa Ardhi, Matokeo ya programu hii, yatasaidia kupunguza Mitaa isiyorasimishwa na kudhibiti kuendelea kukua kwa makazi yasiyopangwa. Aidha, baadhi ya Mitaa ambayo haijarasimishwa (Mitaa 559) imeingizwa kwenye Mradi wa Kuboreshaji Milki za Ardhi (Land Tenure Improvement Project) unaofadhiliwa na Benki ya Dunia ambapo utekelezaji wake umeanza.
Wizara imeandaa Mkakati wa kushughulikia changamoto za urasimishaji baada ya kikao baina ya Wataalam wa Wizara na wadau wa urasimishaji kilichofanyika tarehe 22 Disemba, 2022. Mkakati huo, utawasilishwa kwenye kikao nilichopanga kukiongoza mapema wiki ijayo hapa Dar es Salaam ambapo ndiyo penye changamoto kubwa ya zoezi la urasimishaji.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula alikutana na kuzungumza na vyombo vya habari kutoa salam za mwaka mpya kwa kuelezea masuala mbalimbali ya sekta ya ardhi na muelekeo wa utekelezaji kwa mwaka 2023.
---------MWISHO-----------
![]() |
| Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula akizungumza kwenye mkutano na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam tarehe 3 Januari 2022. (PICHA NA WIZARA YA ARDHI) |
November 30, 2022
Nape na vijana wadeki barabara kumpokea Rais
Written By CCMdijitali on Wednesday, November 30, 2022 | November 30, 2022
![]() |
| Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, akideki barabara pamoja na vijana wa mkoa wa Lindi |
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, ameungana na vijana wa mkoa wa Lindi kufanya usafi maeneo mbalimbali ya mkoa huo ikiwa ni maandalizi ya kumpokea Rais Samia Suluhu Hassan, ambaye atawasili mkoani humo kesho Desemba Mosi, 2022.
Vijana hao walifanya zoezi hilo la kusafisha barabara baada ya kumaliza matembezi maalum katika maeneo mbalimbali ambapo walitumia fursa hiyo kufikisha salamu zao kwa Rais Samia kupitia kwa Waziri wa Habari Nape.
"Sisi Vijana wa Lindi ilifikia hatua baadhi ya wanasiasa walituita watoto tuliotengwa lakini walisahau licha ya mkoa wa Lindi kutotembelewa na Rais kwa muda mrefu Mama yetu Samia Suluhu akiwa Makamu wa Rais alitutembelea sana" Amesema Mustafa Dumbo kwa niaba ya vijana wa Lindi
Akiwajibu vijana hao Waziri Nape Nnauye amewataka vijana hao kutambua Rais Samia anaupenda sana mkoa wa Lindi na ndiyo maana Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa, anatokea huko.
November 30, 2022
7th SWAPO PARTY CONGRESS
7th SWAPO PARTY CONGRESS
24-28 NOVEMBER 2022
MBUNGE wa Jimbo la Mlalo, Rashid Abdallah Shangazi amewakilisha Chama Cha Mapinduzi (CCM)-katika Mkutano Mkuu wa Saba wa Chama cha Ukombozi wa Nchi ya Namibia -SWAPO(Southe West Africa Peoples Organization)
SWAPO kimeendelea kuwa Chama cha Siasa chenye Malengo Makuu ya Kushika Dola na kutengeneza umoja na Mshikamano kuelekea Maendeleo makubwa ya kijamii na kiuchumi (Socio-Economic Development )kwa wananchi wa Namibia.
Aidha Mheshimiwa Shangazi amefurahishwa kuona bado vyama vingi vya ukombozi wa eneo la kusini mwa Africa vipo imara sana na kukumbuka wema wa watanzania wakati wote wa harakati za ukombozi wa Kusini mwa Afrika kupitia Jukwaa la Nchi zilizo Mstari wa Mbele chini ya Utendaji mahiri wa aliyekuwa Katibu Mkuu wake Hayati Brigedier Hashim Mbita (RIP)
Aidha vita dhidi ya siasa za ubaguzi wa rangi yaani (Apartheid)katika Nchi ya Afrika ya Kusini vilihusisha pia vyama hivi vya ukombozi kwa nyakati tofauti.
Historia hii imevikutanisha vyama rafiki vya-
1- Chama Cha Mapinduzi -Tanzania
2- Zanupf-Zimbabwe
3- MPLA-Angola
4- Communist Party of Cuba
5- Communist Party of China
6- Communist Party of Russia
7- FRELIMO -Mozambique
8- ANC -South Africa
9- Palestine Liberation Movement
10- United Socialist Party of Venezuela (PSUV)
Shukrani za dhati kwa Mwenyekiti wetu Mama Samia Suluhu Hassan kwa uongozi bora na mahiri katika stratejia na mikakati madhubuti ya kukuza diplomasia na kuimarisha undugu kichama na kisiasa.
Ahsante comrade Daniel Chongolo kupitia idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa kwa kuimarisha na Kuyaenzi Mahusiano Yetu na Vyama rafiki.
Kidumu Chama Cha Mapinduzi.
November 26, 2022
Wafanyakazi KADCO watakiwa kuwa Wazalendo.
Written By CCMdijitali on Saturday, November 26, 2022 | November 26, 2022
Wafanyakazi KADCO watakiwa kuwa Wazalendo.
Na Jamal Zuberi, Tanga
Serikali mkoani Tanga imesema kuwa mikutano ya Baraza la Wafanyakazi itumike kujadili malengo na mipango ya Taasisi ikiwa ni pamoja na maslahi ya watumishi.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omary Mgumba akifungua Mkutano wa kwanza 2022/2023 wa Baraza la Wafanyakazi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro (KADCO) katika ukumbi wa Tanga Beach Hoteli, Jijini Tanga.
"Mabaraza haya ni jukwaa muhimu kujadili utendaji wa kazi wa kila siku na jinsi ya kuboresha utendaji huo zaidi" alisisitiza zaidi Mgumba.
Amesema kuwa ni muhimu tija na maslahi lazima yawe na uwiano ili kuwa na matokeo chanya ya utendaji bora, unaolenga kutoa huduma bora zaidi kwa wananchi tunaowatumikia.
"Tuelewane utendaji bora zaidi unaongeza tija, tija ikiongezeka ni rahisi kuongeza maslahi ambayo hatimae yanawawezesha watumishi kuishi maisha bora zaidi.
" Naomba kama watumishi katika Sekta ya Usafirishaji wa Anga, lazima mfanye kazi kwa uzalendo, maadili na nidhamu ya juu muonyeshe mfano wakuigwa " alisisitiza Mkuu huyo
Mgumba amewapongeza Wafanyakazi hao wa KADCO kuwa kiwanja bora cha ndege Afirka na Duniani kwa jumla kwa kupewa Tunzo mbali mbali za kimataifa kwa huduma bora pamoja na kuwa na Hati Safi ya matumizi ya fedha.
November 25, 2022
PROFESA MBARAWA AWATAKA TRC KUTOA TAARIFA KWA WAKATI
Written By CCMdijitali on Friday, November 25, 2022 | November 25, 2022
PROFESA MBARAWA AWATAKA TRC KUTOA TAARIFA KWA WAKATI
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amelitaka Shirika la Reli nchini (TRC), kutoa taarifa kwa wakati kuhusu maendeleo ya reli ya kisasa ya sgr na mchakato wa ununuzi na mapokezi ya vifaa vyote vya reli hiyo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa mapokezi ya mabehewa 14 kati ya 59 ya awamu ya kwanza ya SGR yaliyowasili Prof. Mbarawa amesema zaidi ya shilingi bilioni 882 tayari zimetumika katika kununua vichwa vya treni, mabehewa na vifaa vingine muhimu vitakavyotumika katika uendeshaji wa reli hiyo na vitawasili kwa awamu.
“Waelezeni wananchi ukweli kuwa kuna mabehewa ya aina tatu yaliyoagizwa yaani daraja la kwanza, la juu na la tatu ili wasipotoshwe pindi yanapowasili”, amesema Prof. Mbarawa.
Prof. Mbarawa amesisitiza kuwa mabehewa 45 yaliyosalia ya daraja la tatu yatawasili mwezi mei mwakani.
Amezungumzia umuhimu wa wanahabari kufanya utafiti na kujiridhisha kwa vyanzo sahihi kabla ya kuandika na kutangaza taarifa za miradi mikubwa ya kitaifa ili kuondoa upotoshaji kwa wananchi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Bw. Masanja Kadogosa amesema wamejipanga kuongeza mabehewa katika reli ya kati na kaskazini katika kipindi cha mwisho wa mwaka ili kuondoa changamoto za usafiri.
“Tumejipanga kuhakikisha usafiri wetu unakuwa salama na safari zote zinafuata ratiba iliyopangwa ili kutoa huduma bora kwa wananchi’ amesisitiza Kadogosa.
Naye Balozi wa Korea Kusini, Kim Sun Pyo amesema nchi yake itaendeleza ushirikiano na Tanzania katika uimarishaji wa miundombinu nchini.
@tzrailways
November 25, 2022
MAJALIWA: MRADI WA SGR UTAKAMILIKA KAMA ULIVYOPANGWA
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ameridhishwa na maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) na kwamba Serikali itaendelea kuhakikisha mradi huo unajengwa kwa viwango na kukamilika kama ilivyobainishwa kwenye mkataba.
Amesema kuwa ujenzi wa reli hiyo unaendelea vizuri katika vipande vyote na kwamba Serikali itahakikisha mradi huo haukwami na itakabiliana na viashiria vyote vinavyoweza kukwamisha utekelezaji wake.
Ameyasema hayo leo (Alhamisi, Novemba 24, 2022) wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa stesheni kuu ya Dodoma katika eneo la Mkonze, jijini Dodoma.
Akizungumza baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa stesheni hiyo, Mheshimiwa Majaliwa amewataka Watanzania wanaoshiriki katika ujenzi wa mradi huo wasimamie usalama wa mradi na wawe walinzi ili ukamilike kama ilivyokusudiwa.
Aidha, Waziri Mkuu amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassam inaendelea kufanya maboresho kwenye sekta mbalimbali ikiwemo ya usafirishaji.
“Rais Samia anaendelea na mkakati wake wa ujenzi wa reli, endeleeni kuwa na imani na Serikali yenu, lengo lake ni kuhakikisha anainua uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla”
Aidha, Mheshimiwa Majaliwa amemtaka Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma kuwa na mkakati wa maeneo ya uwekezaji kutokana na fursa ya ujenzi wa reli hiyo ikiwemo ujenzi wa kituo cha mabasi jirani na stesheni hiyo.
Kwa upande wake, Mkurgenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa amesema kuwa Shirika hilo lipo kwenye mpango wa ununuzi wa vichwa vya treni na mabehewa ya mizigo. “Hadi sasa TRC imesaini mkataba wa ununuzi wa vichwa vya treni vya umeme 19, seti za treni 10 zenye uniti 80.”
Amesema pia shirika hilo itanunua mabehewa ya kawaida ya abiria 89, mabehewa ya ghorofa 30 ambayo yanakuja, mabehewa ya mizigo 1,430 na vifaa vya matengenezo 26.
November 25, 2022
MKUTANO MKUU WA KUMI WA UMOJA WA WAZAZI TANZANIA 24 NOVEMBA 2022 DODOMA
UCHAGUZI MKUU JUMUIYA YA WAZAZI TAIFA
MATOKEO YA UCHAGUZI MKUU JUMUIA YA WAZAZI
MWENYEKITI
1.ALLY KHAMIS MASUDI-5
2.HASSAN HAJI ZAHARA-6
3.BAKARI NAMPENYA KALEMBO-21
4.SAID MOHAMED SAID-43
5.ALLY MAULID OTHMAN-57
6.MWANAMANGA JUMA MWADUGA-61
7.DR.EDMUND BENARD MNDOLWA-64
8.FADHIL RAJAB MAGANYA-578
MAKAMU MWENYEKITI
1.FATMA ABEID HAJI-25
2.AMEIR AHMED-44
3.HAIDARY HAJI ABDALLAH-48
4.ZAHORO SALEHE MOHAMED (MKULIMA)-56
5.SAID MOHAMED DIMWA-77
6.DOGO IDD MABROUK-530
NAFASI YA HALMASHAURI KUU YA CCM(NEC) TANZANIA BARA NAFASI TATU(3)
1.NYIRIZA MAKONGORO NYIRIZA-21
2.BUPE NELSON MWAKANG'ATA-26
3.MECKTRIDIS FRATERN MDAKU-27
4.DANIEL GEORGE SAYI-41
5.MOHAMED NASORO NGINGITE-46
6.MGORE MIRAJI KIGERA-58
7.ANGELA CHARLES KIZIGHA-163
8.KELVIN PASCHAL TEGWA-176
9.ADAMU KIGHOMA ALLY MALIMA-195
10.PAUL HERMAN KIRIGINI-215
11.DR.ANGELA LUBALA MABULA-234
12.GEORGE BRUNO GANDYE-238
13.DR.DOTO MASHAKA BITEKO-535
14.HAMOUD ABUU JUMA-569
NAFASI YA HALMASHAURI KUU YA CCM (NEC) TANZANIA VISIWANI NAFASI MBILI(2)
1.ZAWADI SULEIMAN ABDULA-21
2.SAID MUSA ZUBERI-26
3.SULEIMAN AME KHAMIS-32
4.SAID MUSA ZUBERY-41
5.DR.HAJI MWITA HAJI-65
6.KHAMIS JUMA MWALIM-86
7.RAMADHAN ISSA KIPAYA-160
8.SULEIMAN JUMA KIMEA-205
9.AMINA ALLY MOHAMED-266
10.HABIBA ALLY MOHAMED-335
11.KHADIJA SALUM ALLY-387
November 25, 2022
RAIS SAMIA AIPONGEZA CCM MANYARA KWA UCHAGUZI USIO NA PURUKUSHANI
November 24, 2022
MKUTANO MKUU WA KUMI WA UMOJA WA WAZAZI TANZANIA 24 NOVEMBA 2022 DODOMA
Written By CCMdijitali on Thursday, November 24, 2022 | November 24, 2022
UCHAGUZI MKUU JUMUIA YA WAZAZI TAIFA
NAFASI YA HALMASHAURI KUU YA CCM(NEC) TANZANIA BARA NAFASI TATU(3)
1. NYIRIZA MAKONGORO NYIRIZA-21
2. BUPE NELSON MWAKANG'ATA-26
3. MECKTRIDIS FRATERN MDAKU-27
4. DANIEL GEORGE SAYI-41
5. MOHAMED NASORO NGINGITE-46
6. MGORE MIRAJI KIGERA-58
7. ANGELA CHARLES KIZIGHA-163
8. KELVIN PASCHAL TEGWA-176
9. ADAMU KIGHOMA ALLY MALIMA-195
10. PAUL HERMAN KIRIGINI-215
11. DR.ANGELA LUBALA MABULA-234
12. GEORGE BRUNO GANDYE-238
13. DR.DOTO MASHAKA BITEKO-535
14. HAMOUD ABUU JUMA-569
NAFASI YA HALMASHAURI KUU YA CCM (NEC) TANZANIA VISIWANI NAFASI MBILI(2)
1. ZAWADI SULEIMAN ABDULA-21
2. SAID MUSA ZUBERI-26
3. SULEIMAN AME KHAMIS-32
4. SAID MUSA ZUBERY-41
5. DR.HAJI MWITA HAJI-65
6. KHAMIS JUMA MWALIM-86
7. RAMADHAN ISSA KIPAYA-160
8. SULEIMAN JUMA KIMEA-205
9. AMINA ALLY MOHAMED-266
10. HABIBA ALLY MOHAMED-335
11. KHADIJA SALUM ALLY-387
































