Comoro kushirikiana na Tanzania katika sekta za kimkakati asema Rais Azali Anena

  Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Visiwa vya Comoro Mheshimiwa Saidi Yakubu amekutana na kufanya mazumgumzo na Rai...

Latest Post

HAKUNA KAMA CCM NYAMONGO TARIME

Written By CCMdijitali on Monday, September 23, 2013 | September 23, 2013

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiz0MWIdX-UN5PSHuwIglVx9qyAIZVgIVBZt6HqW38FXx9Bi15QmAGac1vEbmwhNfydkKjlCmIVyPa8gjtVbFj3pleFizBKglvmTzIzei93gYPF_eTDCozUUFAc6AO8VZTAl3v_dwtneFpf/s1600/1.jpg
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kama ishara ya kufungua ofisi ya CCM Tawi la Nyabichune,wilaya ya Tarime mkoani Mara.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi-hsPJGiE1GcmHMgBJ3G416_QoY48wZddSLnhh-usFjKiZCbQ7pXSvwTwUZmKkLdAsOW2ZCrkrMDbNxidG-bfwRZo7jQoLw7XGOKn7cnMZB6UMIDN545Lf8wtzhzrU3gni1cO52YWvvPOy/s1600/9.jpgOfisi ya CCM Tawi la Nyabichune wilaya ya Tarime mkoani Mara ambalo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alilizindua rasmi leo tarehe 23 Septemba 2013.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhwhtn7CexbkYsvvjwVR5AXMeGQ8nEYGt8wYtLozSa0YY2NwiKEuMyKOlWNI9SeqxoCn4yK1YnEG-7Ctv9pD0UvQV_tRWI4AquHtRXw94tRu-TWOSxHF6qIVeCNFEKjfW5r8zFMnQil-ssL/s1600/2.jpg Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Nyamongo na kuwaeleza namna ambavyo wamejipanga kutatua tatizo la muda mrefu baina ya wakazi wa eneo hilo na wamiliki wa mgodi wa North Mara .

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhJS5rVACO2x3H8mpmN8Bp6jK_RYRAGxzrgCmbm7WE0NfrI0Nfx40K7E3EI28xiYxSnHn9TzN-c9rdUt81QRvZamh2msBQO_36kw53-YAwxMNFr_35vMnvglUsy4U6ocXKUy2r80aSXDKMd/s1600/3.jpg Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza mmoja wa wakazi wa Nyamongo Chacha Magayo Butora ambaye alifafanua kwa kina matatizo yanayowakabili wakazi wa eneo hilo,Katibu Mkuu alitumia Demokrasia ya hali ya juu baada ya kuwapa nafasi watu watatu mbali mbali ambao wananchi waliwachagua waje kuelezea matatizo yao.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgZj5NNcdjihoy3TUfM_J0SkowtH2GNhP2yIZNPQQf02mpA9Cy7M0gSsYMWl9XyWWfkv0D0lxtA1BDYn9I5MFoaHUoA7s16Cs5GSbtjSERiAMysDhLOLwI6EzRxsL-4f75ddrGaolF6ysEk/s1600/5.jpg Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Nyamongo wilaya ya Tarime mkoani mara ambapo aliamua kufuta kila kitu kwenye ratiba yake na kutaka wananchi wateue wawakilishi wao ili wakakae kikao na watu wa serikali ili kupata ufumbuzi wa matatizo hayo.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgrnUIXkCybefzt0Jd6-1_xVVuCN3YJ6X06jJnNhfjCZcnqNau3BAUvQ9beKXj_guX2uEqsDwFRQRsho4iDoofUCKnxGuiF0MW2cO8Jp5FdKDo1kBFGh-I2s2X0vJO4DQvBlSMDYbXvWj89/s1600/6.jpg Naibu Waziri wa Nishati na Madini Ndugu Stephen Masele akifafanua mambo kadhaa ambayo Wizara yake inataka wananchi wafaidike na migodi ikiwa pamoja na kuwasaidia wachimbaji wadogowadogo ambao wanatakiwa wajiunge kutengeneza vikundi.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhaoIAyAABWiXhoMKnWg5MISjCuDeXAWxQWXiIoSsA7WXEl_DO0K3Hrrf0mtIAnq4TmRjownNicKy676WKjofTqih1I0z03O_oHwNzusab4hyphenhyphencMaY6psP4kJ1wcet5c3B4hchXCuM0Ii2dV/s1600/7.jpg Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wakiongea na wananchi wa Nyamongo ,Wananchi wa Nyamongo wameshukuru sana kwa kusikilizwa kwa ukaribu haijawahi tokea na wameahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Viongozi hao.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgYpK0MpY5OgY0nz6814WSGcVeZR-nc-vSLThULeBDWW5ECZ2mcMW0CYjI6Ui7iLshJqePZ-eL_0wu59A8CYLiKYjVsIH9AK9qh_7YTlSUDCMjluu36UyKEZf77qfOYmXpL0UoNVgQ1izex/s1600/8.jpgKatibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisoma moja ya taarifa inayofafanua matatizo ya wakazi wa Nyamongo.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiLkrGE2hPBnD_yuRl76uHNFDwMwzpG_8kTu_ZvL3iSGbLAfCyG-qmcIikoxi_LAfM4k1zLyjy5NLZvh187Jq2dFF-TcICYC9F4WkUjgPw4KQ-P31D2xLJjqTXTGzCRlokxAWQCqaRC0Z3a/s1600/10.jpgSehemu ya wakazi wa Nyamongo wakiwa kwenye kikao cha ndani pamoja na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye,Naibu Waziri Nishati na Madini Ndugu Stephen Masele na Viongozi wengine wa Serikali ambapo walikaa na kujadili matatizo yao namna ya kuyatatua.

==== ======  =====

Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana ,leo amefanya ziara katika wilaya ya Tarime Mkoani Mara .


 Katibu Mkuu akiwa ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye pamoja na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Ndugu Stephen Masele.


Katika ziara hiyo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alilazimika kupangua ratiba ya ziara ya baada ya kuona kuna jambo la muhimu zaidi angependa kupata muda na wakazi wa Nyamongo ambao wamekuwa na kero za muda mrefu bila kupata majibu.


Baada ya mapokezi katika kijiji cha Mrito, Katibu Mkuu alipokea taarifa ya kamati ya siasa kisha kuelekea katika shughuli ya kufungua Tawi la Nyabichune,mara tu shughuli za ufunguaji Tawi ilipokamilika alipokea taarifa mbali mbali na ndipo akagundua kuna haja ya kupangua ratiba na kwenda kusikiliza ya wananchi.


Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye awaambia mkutano huu ni wa kusikiliza kero na kuzitafutia ufumbuzi kwani CCM peke yake ndio inaweza kutatua hilo tatizo.


Naibu Waziri wa Nishati na Madini Ndugu Stephen Masele asitisha huduma ya kulipiwa ada mpaka taratibu na makubaliano yapangwe upya,asikitishwa na watendaji wazembe,azungumzia mpango wa kugawa maeneo kwa wachimbaji wadogo wadogo,awataka waunde vikundi watafute leseni,ahimiza kuna Dirisha la Mikopo TIB Bank,pamoja na serikali kuwasaidia vifaa.


Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana atoa wawakilishi wa wananchi kutoka kwenye mkutano, akaa nao kikao cha ndani pamoja na viongozi wa Serikali ,chama na wananchi.

Rais Kikwete akabidhi hati za utambulisho kwa maBalozi wa heshima wa Tanzania Washington DC





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, amesema kuwa serikali yake inajitahidi katika kuboresha hali ya uzalishaji wa bidhaa nchini Tanzania, lakini bado kuna hitaji la wawekezaji kuja kuwekeza nchini Tanzania katika kuboresha huduma na bidhaa zinazopatikana nchini humo na kuziuza kama bidhaa zilizo tayari kwa matumizi badala ya 
bidhaa-ghafi.

Rais Kikwete ameyasema hayo usiku wa jumatano wiki hii wakati akiwahutubia watu waliohudhuria hafla fupi ya kukabidhi hati kwa mabalozi wa heshima wa Tanzania kutoka majimbo mbalimbali ya nchini Marekani, sherehe zilizofanyika katika Ubalozi wa Tanzania jijini  Washington DC

Sikiliza ripoti hii ambayo ni sehemu ya ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30am). Hii ilikuwa ripoti ya Septemba 21, 2013.


KINANA ASHUHUDIA MAABARA INAYOTEMBEA WILAYA YA SERENGETI

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiBLw0RjOJEfG92gYna16p0CPk0LHITXrEH2nFFITbG8Ff9XOU6OiBLIbbkSHA8QGokAk4pgqx5ulFKMYhgPvzUklWbChhW6RlIocKlaMTTgZC10glj0hqwgz3VAWWVy88Z_6377KHR3-CO/s1600/10.jpg Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Wazee wa kata ya Isenya wilaya ya Serengeti waliokuja kumpokea.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhb-JXwQl39mvRlciEmO00MHGG6w832dv539Bsyed17m3BzxQuulZ38K4VUm2UQOwhZCYKZCDEuHt_s3F33Py4l5i5BIKTrutv9CeVpD84pPODZerx78FZTqDqSnYehZ4nBChlRfBFSmCJN/s1600/11.jpg Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza mwalimu wa masomo ya sayansi Ndugu Silvester Joseph , Katibu Mkuu alitembelea shule ya Natta Secondary na kushuhudia jinsi masomo ya sayansi yanavyopewa kipaumbele.
Mwanafunzi wa Kidato cha Nne Peter Semion wa shule ya sekondari ya Natta iliyopo kata ya Natta wilaya ya Serengeti akimuelekeza namna ya kutengeneza sabuni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipotembelea shule hiyo ya Natta iliyopo wilaya ya Serengeti.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj97MGJk86gBq3i6ZO2dxBnblFrpNIJGuuws-6RnC6ZNp_yfUYDremXugysrxhG91S2PiCreyQ2p8PkSJrWYiIpvGDS8YDUVm5fG08rRplg4jlwFndeNojYVOFZw6UCir-zQVc2REzkgdCt/s1600/8.jpg Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na vijana wajasiriliamali wa kuendesha boda boda na ukulima wa mboga mboga mara baada ya kuzindua kikundi hicho ambapo aliwasihi lazima wapate elimu ya biashara wajue namna ya kuweka na kukopa na kulipa madeni kwa wakati.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiiLQ4QwC-JzDHLeoZVPHe1DpOtwyRtB2ZiWU0C_k4f2mZaZqfohdiIRUM9p5EGC3Xh0EdoceGiqAc08RtKfdVnRhyphenhyphenodarelH2hqno9sMYRxY1seSwuqZm0dkyjJ0XfUA7clXiFGvCDw75_/s1600/9.jpg Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitoka ndani ya ukumbi wa mkutano wa MUGUMU CCM ambapo alikutana na vijana wajasiriamali wa wilaya hiyo.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi5_YG67AD4HlZNXFxY7RUYeNdLMp-HZUVkazuxw3zMOUFv-1ZxvW6wUFouYKmFjVftB6PNWlKImO4K73XhH91T1JiZHfOyy5cIpu75crJ1ya3xCl4Fs7WbL2p52KTTWupk0C7hHD6u8KgC/s1600/4.jpg Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Natta mara baada ya kumaliza kikao na balozi wa shina namba 11 Tawi la Natta Majengo.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj3gH888GfOBgKDLkUgGPg59bKQq8K714dXVWybbWG8kEquyo-jBYqMTZNyvD461YH__3jQlZqMym2urRYGFg20aBOtRPz_r01SIO5hN7Oht45Xq6-E-D431bs8bWIdKt0xeoRuzsRM8UQ6/s1600/5.jpg Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitoa shukrani kwa wazee wa Natta baada ya kumpa heshima ya kuwa Mzee wa Natta.

Rais Kikwete awasili New York kuhudhuria Kikao cha 68 cha Umoja wa Mataifa


Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na Waziri wa kazi na Utumishi wa Umma wa Zanzibar, Mhe. Haroun A. Suleiman.
Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na Naibu Mwakilishi wa Kudumu katika Ubalozi wa Tanzania, New York,
 
 Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi wa Iadara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi mara baada ya kuwasili katika Hoteli ya JW Marriot ya Jijini New York, Marekani. Mhe. Rais Kikwete na Ujumbe wake yupo nchini Marekani kwa ajili ya kuhudhuria Kikao cha 68 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) kinachofanyika kuanzia tarehe 17 Septemba hadi 20 Desemba, 2013.
 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) naye akiwasili katika Hoteli ya JW Marriot akiwa amefuatana na Balozi Mushy (kulia) pamoja na Msaidizi wake Bw. Togolani Mavura.
Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Robert Kahendaguza.

Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na  , Bw. Yusuph Tugutu mmoja wa Maafisa katika Ubalozi wa Tanzania, New York waliofika kumpokea Hotelini hapo.

Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na  m Bw. Noel Kaganda, Afisa katika Ubalozi wa Tanzania, New York.

Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na  Bi. Ramla Khamis mmoja wa Maafisa utoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na  Bi. Tully Mwaipopo mmoja wa Maafisa katika Ubalozi wa Tanzania, New York.

Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na Bibi. Ellen Maduhu mmoja wa Maafisa katika Ubalozi wa Tanzania, New York.

Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na  Bibi Maura Mwingira mmoja wa Maafisa katika Ubalozi wa Tanzania, New York.

Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na Bw. Grayson Ishengoma, Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa

Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na Bi. Tuma Abdallah, Mwandishi Mwandamizi wa Gazeti la Daily News.

Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na Bi. Anna Nkinda, Afisa Kutoka Idara ya Habari (MAELEZO).
Na Rosemary Malale, New York


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete amewasili mjini New York, Marekani tarehe 21 Septemba, 2013 kwa ajili ya kuhudhuria kikao cha 68 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (The 68th Session of the United Nations General Assembly (UNGA 68TH) kinachoendela mjini hapa kuanzia tarehe 17 Septemba hadi 20 Desemba, 2013.


Kikao hicho kimeazimia kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili dunia kiusalama, kiuchumi, kisiasa na kijamii. Kaulimbiu ya Mjadala Mkuu (General Debate) ni “Post-2015 Development Agenda: Setting the Stage”. Aidha, Mhe. Rais Kikwete, anatarajiwa kulihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa tarehe 26 Septemba, 2013.


Pamoja na Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na kulihutubia Baraza hilo, Mhe. Rais atashiriki mikutano mingine yenye manufaa kwa maendeleo ya Taifa ikiwemo:- Mkutano wa Mfuko wa Changamoto za Milenia (MCC) kwa ajili ya ufadhili wa miradi ya Awamu ya Pili baada ya Awamu ya Kwanza kumalizika; Mkutano kuhusu Usalama wa Chakula na Lishe; Mkutano wa Kamati ya Marais wa Afrika kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi.


Mingine ni Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali kuhusu biashara haramu ya Wanyamapori na uvunaji haramu wa Magogo; Mkutano kuhusu maendeleo ya Wanawake na Watoto; Mkutano wa Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR) kuhusu hali nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC); na Mkutano kuhusu kuongeza kasi ya utekelezaji wa Malengo ya Milenia.


Katika hatua nyingine, Mhe. Rais atapata nafasi ya kukutana na Viongozi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Rais wa Marekani, Mhe. Barack Obama; Waziri Mkuu wa Norway, Mhe. Jes Stoltenberg; Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. Ban Ki-moon; Mkurugenzi Mtendaji wa MCC, Bw. Daniel Yohannes na Viongozi wa Makampuni mbalimbali.


Aidha, pamoja na mikutano ya ngazi ya juu, Kikao cha Baraza Kuu pia hujumuisha mikutano ya Wataalam kupitia Kamati Sita za Umoja wa Mataifa ambazo ni Kamati inayoshughulikia masuala ya Upokonyaji na Upunguzaji Silaha Duniani; Kamati ya Uchumi na Fedha; Kamati ya Kijamii na Haki za Binadamu; Kamati inayoshughulikia masuala ya Ukombozi Duniani; Kamati ya Bajeti na Utawala; na Kamati ya masuala ya Sheria.


Viongozi wengine watakaoambatana na Mhe. Rais Kikwete ni pamoja na Mke wa Rais, Mhe. Mama Salma Kikwete; Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.); Waziri wa Kazi Zanzibar, Mhe. Haroun Ali Suleiman; Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Khamis Kagasheki (Mb.); Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mhe. Hussein Mwinyi (Mb); na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Mhe. Terezya Huvisa (Mb.).
Wengine ni Mhe. Khalifa Suleiman Khalifa (Mb.), Mhe. Anastazia Wambura (Mb); Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango; na Maafisa Waandamizi kutoka Serikalini.

Yanga 2-3 Azam

  https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjP5VUhsHZbicfP7VH2OUebxK0XebT8zmu_OEzZ9L3YLOMBc7hQWGO6XNzjIyotHlIo666xV0dK0ox8NlyZ6L2we4MIYnpzUGJASq5iBsE9b5tlW53o1pf9K8t0sFyU9viGgWsGIsyV4Wg/s1600/1.JPG
Mshambuliaji wa Yanga, Hamisi Kiiza akichuana na beki wa Azam FC, Waziri Salum (kulia) katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Azam FC ilishinda 3-2.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiUDB7Vdgm_3wXWoII2Bi_3V-PsD5wXw4HBUhZZQNz3AK8p6EyRPZI6D9hPrM3VbXQUF8ZWmnbMDDZqhiDE51yLLCe-1daXKouABtYLp8H5Y7lF7dEqfdWhusdyMpaDg6sHNj1YIyWPk5s/s1600/2.JPG Mshambuliaji wa Yanga, Didier Kavumbagu (kushoto) akioneshana ubabe na beki wa Azam Fc, Kipre Balou katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo. Azam imeshinda bao 3-2.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiCvMHtH-RPGTzLLITt94yC_XddwPqg9AnIgwUJ2_7Z189tlVUxoy7XvhgMpI6vuE7uwznRcVROL2-sAMbs59t-gfwsFfHUmzNA7yd0NyVJvFdC5H35MCpzS3UhzbM31iFvv6qI10fMe44/s1600/IMG_3605.JPGWachezaji wa Azam FC wakishangilia bao la tatu la timu yao. (Picha zote na Francis Dande).

DK. SEIF KHATIB AKUTANA NA KATIBU WA MAMBO YA NJE WA CHAMA CHA ANC CHA AFRIKA KUSINI.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEinhrYIh_ywrq8zh-bYDXyN4d3gLzMN08NGGNLwZK6Dbr75-Fnk7nSiMbLF_MbguhtZCpH_McJHYB0CUMs7zNQeZ8xhOfmsmWals4AftqMwZUbt7u9OaMWrXjUYr7sHbArYUl6W-YZ6S5w/s1600/2.jpg
 KATIBU wa NEC, Oganaizesheni Dk. Mohamed Seif Khatib, akimkaribisha Katibu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Chama Cha ANC cha Afrika Kusini Billy Masetlha (kushoto) alipowasili Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, jana, kwa ajili ya mazungumzo na kuwasilisha, Makubaliano ya viongozi wa vyama vya mstari vya ukombozi kusini mwa Afrika,  yaliyofikiwa na viongozi hao katika mkutano wao wa Machi 7, mwaka huu mjini Pretoria, Afrika Kusini.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgzkpTQ-zNlTFg0CNfE2x8ejjfkvgtb7PrIGWxEuBA0HJc7clAutnG22VrIzQV69h8kvSMhsMmIKQOVCujvLV8Z0yG546xmVn_H2SnVj31pbSG6xp4ZthByO1hBHNhME-lPqbYLp3_PjuE/s1600/3.jpg KATIBU wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Chama Cha ANC cha Afrika Kusini Billy Masetlha (kushoto) alikimkabidhi Katibu wa NEC ya CCM, Ogamaizesheni, Muhamed Seif Khatib, kabrasha la Makubaliano ya viongozi wa vyama vya mstari vya ukombozi kusini mwa Afrika,  yaliyofikiwa na viongozi hao katika mkutano wao wa Machi 7, mwaka huu mjini Pretoria, Afrika Kusini, jana, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjin4K6VVPNAHiFLEvg0MLfjcHs1PH8wVDP7omKoyd7SESWBnEFsJqVfFjOskBoUrkgfu470YqEtePT_aXQmcPGBSip1D5a9KHn_4tB7msvGVw5frqjxbOB5kpLQfFmBWBITAiIahsf0bI/s1600/4.jpg KATIBU wa NEC, Oganaizesheni Dk. Mohamed Seif Khatib, akizungumza na Katibu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Chama Cha ANC cha Afrika Kusini Billy Masetlha (kushoto) alipowasili Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya mazungumzo na kuwasilisha, Makubaliano ya viongozi wa vyama vya mstari vya ukombozi kusini mwa Afrika,  yaliyofikiwa na viongozi hao katika mkutano wao wa Machi 7, mwaka huu mjini Pretoria, Afrika Kusini.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhmaWcFkcsYyqIY8SttYTJVh9IFKJBKdBXCOJWNxSiuXVAcpxZPz0tUk53E5rm-lmT6hYsqDi7_uFmm-BZUAjIwnQbDv0p2MTMHqSJAgHp4niK0rZt81ZbrhiOGebA2JGAkt_WmNpBINyU/s1600/5.jpg KATIBU wa NEC, Oganaizesheni Dk. Mohamed Seif Khatib, akiwa katika picha ya pamoja na Katibu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Chama Cha ANC cha Afrika Kusini Billy Masetlha (kushoto) alipowasili Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya mazungumzo na kuwasilisha, Makubaliano ya viongozi wa vyama vya mstari vya ukombozi kusini mwa Afrika,  yaliyofikiwa na viongozi hao katika mkutano wao wa Machi 7, mwaka huu mjini Pretoria, Afrika Kusini. Wengine kushoto ni Ofisa kutoka ANC Lebogang Matshaba na kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiFzbFps_cMhyphenhyphenoUqpwT7VvvWHPYF2nk2JEnvXi1sdHfNy6iyxWl8kL6hGAAgh4oNvShdPP1wi9xJW0L6Dk1T7pI7MYFHj0FPQZdycqO-dmyV8UklZMn2Zy3XYXlPi-jVHit7bL_3qpEck8/s1600/6.jpg Katibu wa Mambo ya Nje Chama cha ANC cha Afrika Kusini Billy Masetlha akiongea na Dk. Khatib wakati akiaga nje ya Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, baada ya mazungumzo yao,

Mh. Lowassa aongoza Kikao cha Wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Sweden leo

Written By CCMdijitali on Sunday, September 22, 2013 | September 22, 2013

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg4E9xPXlYEFZer6dju4vAO0Yi2qcOV1FmR3Rzdw_VfAMiszpnzJ9A7ZBCAjdUwP5OAzPKs8RPUfBRelTY0kO3COGhOkNjmZVfizZtrSTRtJX3nQ-QzEuY3qrnqOL73qsvlaQenrB-U6RN_/s1600/photo.JPG

Mwenyekiti wa Kamati ya BUNGE, Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Mhe. Edward Lowassa akimsikiliza mmoja wa wajumbe wa kikao alichokiongoza wakati alipokutana na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania jijini Stockholm,Sweeden.Waliohudhuria kwenye kikao hicho ni Balozi Muhammed Mzale,Mhe. Juma Nkamia,Mhe. Suzanne Lyimo,Bw. Jacob Msekwa,Bw. Athuman Brambath,Bw. Yusuf Mndolwa,Bw. Arthur Mwambene na Bi Apronia Rutaihwa.Kikao hicho kimefanyika leo kwenye ukumbi wa Mikutano wa Ubalozi huo.

Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete atunukiwa Shahada ya Uzamivu katika Chuo Kikuu Guelph jimboni Ontario

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akisindikizwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mheshimiwa Dkt. Shukuru Kawambwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe kuelekea ukumbini kutunukiwa Shahada Ijumaa Septemba 20, 2013.
Nyimbo za taifa zikipigwa wakati wa sherehe za kumtunuku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete atunukiwa Shahada ya Uzamivu katika Chuo Kikuu Guelph jimboni Ontario, Canada, Ijumaa Septemba 20, 2013.
Sehemu ya umati ulioshuhudia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa kutunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Chuo Kikuu cha Guelph jimboni Ontario Ijumaa Septemba 20, 2013.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akitunukiwa Shahada ya Uzamivu na Provost na Makamu wa Rais wa Chuo Kikuu cha Guelph jimboni Ontario, Dkt Maureen Mancuso , Ijumaa Septemba 20, 2013.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akishangiliwa katika Chuo Kikuu Guelph baada ya kutunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Chuo Kikuu cha Guelph jimboni Ontario Ijumaa Septemba 20, 2013 Ijumaa Septemba 20, 2013.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia Chuo Kikuu Guelph baada ya kutunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Chuo Kikuu cha Guelph jimboni Ontario Ijumaa Septemba 20, 2013.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Guelph pamoja na na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mheshimiwa Dkt. Shukuru Kawambwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe baada ya kutunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Chuo Kikuu cha Guelph jimboni Ontario Ijumaa Septemba 20, 2013 Ijumaa Septemba 20, 2013.
Umati ulioshuhudia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa kutunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Chuo Kikuu cha Guelph jimboni Ontario Ijumaa Septemba 20, 2013.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Wakuu wa Chuo Kikuu Guelph pamoja na na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mheshimiwa Dkt. Shukuru Kawambwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe baada ya kutunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Chuo Kikuu cha Guelph jimboni Ontario Ijumaa Septemba 20, 2013 Ijumaa Septemba 20, 2013.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akipongezwa baada ya kutunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Chuo Kikuu cha Guelph jimboni Ontario Ijumaa Septemba 20, 2013.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mheshimiwa Dkt. Shukuru Kawambwa (kulia) na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe baada ya kutunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Chuo Kikuu cha Guelph jimboni Ontario Ijumaa Septemba 20, 2013.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete Ijumaa, Septemba 20, 2013, ametunukiwa Shahada ya Uzamivu (PHD) na Chuo Kikuu cha Guelph katika jimbo la Ontario nchini Canada kwa kutambua mchango na uongozi wake katika kuleta mageuzi ya kilimo katika Afrika.
Viongozi wa Chuo hicho wanasema kuwa wamefanya uamuzi wa kumtunuku Rais Kikwete kutokana na jitihada zake za kukabiliana na changamoto zinazokabili kilimo, jitihada zake za kuleta usalama wa chakula na pia majaribio makubwa ya kuongeza matumizi ya technolojia katika kilimo cha Tanzania na Afrika.
Rais Kikwete ambaye amewasili Canada usiku wa Alhamisi, Septemba 19, 2013 akitokea Washington, D.C., Marekani ambako alikuwa kwa siku mbili akitokea Jimbo la California amekuwa Mtanzania wa kwanza kutunukiwa shahada ya juu kabisa katika historia ya Chuo hicho.
Chuo cha Guelph ni moja ya vyuo vikuu vinavyoheshimiwa zaidi katika Canada na duniani katika Nyanja za kilimo na kilianzishwa rasmi kama Chuo cha Kilimo cha Jimbo la Ontario Mei Mosi, mwaka 1874.
Chuo hicho ambacho kimejipatia umaarufu kutokana na ubora wa shughuli zake za utafiti kimekuwa katika mstari wa mbele kutafuta majawabu ya changamoto zinazoikabili dunia katika masuala ya kilimo, raslimali za maji, matatizo makubwa ya magonjwa ya mimea, matatizo ya ukuaji haraka wa miji duniani na changamoto za biashara za kimataifa.
Katika miaka ya karibuni kufuatia tishio kubwa kimataifa la ongezeko la bei za vyakula duniani na hasa katika nchi masikini, mabadiliko ya tabianchi, ongezeko la uchafuzi wa hali ya hewa, uharibifu wa mazingira, changamoto za upatikanaji wa maji safi na salama duniani, kazi ya Chuo hicho imeongezeka sana.
Chuo hicho kimeichagua Tanzania kama nchi ya kufanya nayo kazi katika Afrika kukabiliana na changamoto hizo na kimemtambua Rais Kikwete kutokana na mchango wake mkubwa katika sekta ya kilimo katika miaka yote ya uongozi wake na mipango yake ya kuboresha kilimo katika Tanzania kama ASDP, Kilimo Kwanza na SAGCOT ambayo yote inasifiwa sana kimataifa.
Chuo hicho kina mahusiano ya karibu na Vyuo Vikuu vya Dar es Salaam, Sokoine cha Mzumbe – Morogoro na UDOM – Dodoma. Kati ya mwaka jana na mwaka huu, Chuo hicho kimetiliana saini Makubaliano ya Ushirikiano (MOU) na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine cha Mzumbe – Morogoro na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
Mara nne kati ya Januari, mwaka jana, 2012 na Juni, mwaka huu, 2013, uongozi wa Chuo hicho ukiongozwa na Rais na Makamu Mkuu wa Chuo, Dkt. Alastair Summerlee na Makamu wa Rais wa Utafiti Dkt. Kevin Hall umetembelea Tanzania na kukutana na viongozi wa Serikali pamoja na wale wa Vyuo Vikuu vya Dar Es Salaam na Sokoine cha Mzumbe, Morogoro.
Mbali na ujumbe ambao unaongozana na Rais Kikwete, sherehe za kutunukiwa kwa Kiongozi Mkuu huyo wa Tanzania pia zimehudhuriwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mheshimiwa Dkt. Shukuru Kawambwa, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe, Jumuia ya Watanzania wanaoishi Canada pamoja na maofisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini humo.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
20 Septemba, 2013
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link