TANZANIA YAPONGEZWA KUWA KINARA WA MASUALA YA AMANI NA USALAMA UKANDA WA MAZIWA MAKUU
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepongezwa kwa kuwa kinara katika masuala mbalimbali yanayolenga kuleta amani na usalama katika Ukanda wa...
Latest Post
January 31, 2014
DK EMMANUEL NCHIMBI APATA MAPOKEZI MAKUBWA JIMBONI KWAKE.
Written By CCMdijitali on Friday, January 31, 2014 | January 31, 2014
Juu wananchi waliojitokeza kwa wingi kumpokea mbunge wao Mhe Dkt Emmanuel Nchimbi leo mjini Songea. Chini Dkt Nchimbi akiongea na wapiga kura wake na amewashukuru sana kwa mapenzi waliyoonesha kwake baada ya kurejea kutoka Dar es salaam alikopata ajali ya kisiasa iliyomplekea kuwajibika kwa kujiuzuru nafasi yake ya waziri wa mambo ya ndani.
Labels:
KITAIFA,
National News
January 31, 2014
MKUTANO WA KAMPENI YA UCHAGUZI WA DIWANI CCM KATA YA SOMBETINI
MWENYEKITI WA UVCCM MKOA NDG ROBSON MEITINYIKU AKIMNADI MGOMBEA WA UDIWANI WA CCM NDG MWALIMU DAVID MOLLEL KURA KWA WANANCHI
MWENYEKITI WA UWT MKOA WA ARUSHA NDG ZELOTE AKIINADI ILANI YA CCM KWENYE MKUTANO ULIOFANYIKA JANA HUKO SOMBETINI
(Kulia - kushoto )MHESHIMIWA DIWANI OLE SEKIYANI,WA KATA YA TERRATI,MGOMBEA UDIWANI WA CCM NDG MWALIMU DAVID MOLLEL,MWENYEKITI WA CCM WILAYA YA ARUSHA NDG WILFRED SOILELI NA MWENYEKITI WA UVCCM MKOA WA ARUSHA NDG ROBSON MEITINYIKU WAKIWA MEZA KUU KATIKA MKUTANO WA KAMPENI YA UCHAGUZI WA DIWANI KATA YA SOMBETINI
KATIBU WA CCM WILAYA YA MERU NDG AKYO AKITEREMKA JUKWAANI MARA BAADA YA KUONGEA NA WANANCHI WALIOJITOKEZA KWENYE MKUTANO WA KAMPERNI YA UCHAGUZI WA DIWANI KATA YA SOMBETINI
BAADHI YA WANANCHI NA WAPENZI WA CCM WALIOJITOKEZA KATIKA MKUTANO WA KAMPENI YA UCHAGUZI WA DIWANI KATA YA SOMBETINI
MWENYEKITI NA MGENI RASMI MWENYEKITI WA UVCCM MKOA WA ARUSHA NDG ROBSON MEITIYIKU AKIELEZA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM KATIKA MKUTANO WA KAMPENI YA UCHAGUZI WA DIWANI KATA YA SOMBETINI
WAGENI KATIKA MEZA KUU KATIKA MKUTANO WA KAMPENI YA UCHAGUZI WA DIWANI KATA YA SOMBETINI
BAADHI YA UMATI WA WATU WALIOJITOKEZA KATIKA MKUTANO WA KAMPERNI YA UCHAGUZI WA DIWANI KATA YA SOMBETINI
MGOMBEA UDIWANI WA CCM MWALIMU DAVID MOLLEL LESIKAR AKIJIELEZA NAMNA ATAKAVYOITEKELEZA ILANI YA CCM KATIKA MKUTANO WA KAMPENI YA UCHAGUZI WA DIWANI KATA YA SOMBETINI
MWNDISHI WA HABARI AKICHUKUA HABARI KATIKA MKUTANO WA KAMPENI YA UCHAGUZI WA DIWANI KATA YA SOMBETINI
MWENYEKITI WA UWT MKOA WA ARUSHA NDG ZELOTE AKIINADI ILANI YA CCM KWENYE MKUTANO ULIOFANYIKA JANA HUKO SOMBETINI
(Kulia - kushoto )MHESHIMIWA DIWANI OLE SEKIYANI,WA KATA YA TERRATI,MGOMBEA UDIWANI WA CCM NDG MWALIMU DAVID MOLLEL,MWENYEKITI WA CCM WILAYA YA ARUSHA NDG WILFRED SOILELI NA MWENYEKITI WA UVCCM MKOA WA ARUSHA NDG ROBSON MEITINYIKU WAKIWA MEZA KUU KATIKA MKUTANO WA KAMPENI YA UCHAGUZI WA DIWANI KATA YA SOMBETINI
KATIBU WA CCM WILAYA YA MERU NDG AKYO AKITEREMKA JUKWAANI MARA BAADA YA KUONGEA NA WANANCHI WALIOJITOKEZA KWENYE MKUTANO WA KAMPERNI YA UCHAGUZI WA DIWANI KATA YA SOMBETINI
BAADHI YA WANANCHI NA WAPENZI WA CCM WALIOJITOKEZA KATIKA MKUTANO WA KAMPENI YA UCHAGUZI WA DIWANI KATA YA SOMBETINI
MWENYEKITI NA MGENI RASMI MWENYEKITI WA UVCCM MKOA WA ARUSHA NDG ROBSON MEITIYIKU AKIELEZA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM KATIKA MKUTANO WA KAMPENI YA UCHAGUZI WA DIWANI KATA YA SOMBETINI
WAGENI KATIKA MEZA KUU KATIKA MKUTANO WA KAMPENI YA UCHAGUZI WA DIWANI KATA YA SOMBETINI
BAADHI YA UMATI WA WATU WALIOJITOKEZA KATIKA MKUTANO WA KAMPERNI YA UCHAGUZI WA DIWANI KATA YA SOMBETINI
MGOMBEA UDIWANI WA CCM MWALIMU DAVID MOLLEL LESIKAR AKIJIELEZA NAMNA ATAKAVYOITEKELEZA ILANI YA CCM KATIKA MKUTANO WA KAMPENI YA UCHAGUZI WA DIWANI KATA YA SOMBETINI
MWNDISHI WA HABARI AKICHUKUA HABARI KATIKA MKUTANO WA KAMPENI YA UCHAGUZI WA DIWANI KATA YA SOMBETINI
Labels:
KITAIFA,
National News
January 31, 2014
NDG. ABDULRAHMAN KINANA AKUTANA NA WAENDESHA BODABODA JIJINI MBEYA
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Inspekta Isack Lema Mlezi wa Bodaboda Mkoa wa Mbeya kwa upande wa jeshi la Polisi wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Mtenda uliopo Soweto mjini Mbeya kwa ajili ya kuzungumza na waendesha Bodaboda wa mjini Mbeya, ambapo wamemweleza matatizo mbalimbali wanayokumbana nayo na jinsi wanavyoshirikiana na jeshi la polisi na polisi jamii katika kulinda usalama wa wananchi, wao wenyewe na mali kwa ujumla, Chanagamoto mbalimbali za kimaendeleo zimetatuliwa na zitaendelea kutatuliwa ili waendesha bodaboda wafanye kazi zao kwa ufanisi na utulivu. Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia waendesha Bodaboda ambao wameonekana kufurahia sana mkutano huo uliofanyika leo kwenye ukumbi wa mtenda Soweto jijini Mbeya. Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Blogger wa Mbeya yetu Blog Bwana
Joseph Mwaisango.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa katika meza kuu kulia ni Nape Nnauye Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi wakati wa mkutano huo.
Waendesha Bodabona wakimshagilia Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati alipokuwa akiongea nao leo.
Msafara wa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ukitoka uwanja wa ndege wa Songwe kuelekea mjini Mbeya leo mara baada ya kuwasili mkoani humo.
Pikipiki zao zikiwa zimeegeshwa nje ya ukumbi. Waendesha Bodaboda wakifuatilia hotuba za Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Nape Nnauye Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi wakati wa mkutano huo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea risala ya waendesha Bodaboda kutoka kwa Msumba Makya Katibu wa Waendesha Bodaboda.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akibebwa juujuu na waendesha bodaboda mara baada ya kuwahutubia kwenye ukumbi wa Mkenda leo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipiga picha ya pamoja na uongozi wa waendesha Bodaboda kushoto ni mwenyekiti Vicent Mwashoma na kulia ni Msumba Makya Katibu wa Waendesha Bodaboda.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-MBEYA)
Labels:
KITAIFA
January 28, 2014
RAIS KIKWETE AFURAHISHWA NA HUDUMA ZA NMB KATIKA MPANGO WA KILIMO WA STAKABADHI GHARANI
Written By CCMdijitali on Tuesday, January 28, 2014 | January 28, 2014
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Mkuu wa kitengo cha Masuala ya Kilimo katika Benki ya NMB Bw. Robert Pascal alipotembelea banda lao leo baada ya kufungua kongamano la kilimo Afrika Mashariki katika hoteli ya Kilimanjaro jijini Dar es salaam leo.
Rais Jakaya Kikwete akipata maelezo ya jinzi mpango wa Stakabadhi Gharani ulivyo na manufaa kwa mkulima toka kwa Mkuu wa kitengo cha Masuala ya Kilimo katika Benki ya NMB Bw. Robert Pascal alipotembelea banda lao leo baada ya kufungua kongamano la kilimo Afrika Mashariki katika hoteli ya Kilimanjaro jijini Dar es salaam leo.
Mkuu wa kitengo cha Masuala ya Kilimo katika Benki ya NMB Bw. Robert Pascal akitoa maelzo kwa Rais Kikwete juu ya mafanikio ya benki hiyo katika mpango wa Stakabadhi Gharani ambao amesema unaendeshwa kwa mafanikio makubwa.
Labels:
BIASHARA
January 28, 2014
BONANZA LA MAVETERANI YOMBO MAKANGARAWE,TEMEKE LAZINDULIWA
Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Matemvu akikagua timu ya Veterani ya Yombo Kilakala wakati wa uzinduzi wa michuano ya maveterani ya Ujirani Mwema, katika Kata ya Yombo Kilakala, Temeke, Dar es Salaam juzi. Timu 12 kutoka sehemu mbalimbali za jiji zilishiriki kwenye michuano hiyo. Timu hiyo ilicheza na Kigamboni Veterani.
Mtemvu akikagua timu ya Kigamboni Veterani. Kushoto ni Diwani wa Kata ya Makangarawe, Victor Mwakasendile.
Mtemvu akihutubia wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo, ambapo aliahidi kuyadhamini kwa timu zote kuzinunulia jezi za TMK. Kushoto ni Mwakasendile na Mungia Mbwana mratibu wa michuano hiyo.
Timu za New Kivule Veterani (waliovaa Bluu) na Kitunda (waliovaa bluu nyeusi) wakipepetana
Ni mtanange kwa kwenda mbele
Hapiti mtu hapa
Sasa nawatoka
Wanachi wakishuhudia mpambano huo
Timu za Yombo Makangarawe Veterani (BLUU) wakicheza na Kigamboni Veterani huku wananchi wakishuhudia
Mlinda mlango wa Kigamboni akiwania mpira na mchezaji wa Yombo Makangarawe
PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG.
Labels:
MICHEZO NA BURUDANI
January 28, 2014
Rais Kikwete aamuru Jeshi kusimamia utoaji huduma kwa waathirika wa mafuriko Morogoro
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikagua Daraja la Mto Mkundi mkoani Morogoro linalokarabatiwa baada ya kuharibiwa na mafuriko hivi karibuni.Rais Kikwete alitembelea eneo hilo na sehemu nyingine zilizokumbwa na mafuriko hayo kujionea uharibifu. Picha na Freddy Maro wa Ikulu.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi la Ulinzi na
Usalama, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameliamuru Jeshi la Wananchi wa
Tanzania (JWTZ) kuanza mara moja kazi ya kusimamia utoaji huduma kwa watu
walioathiriwa na mafuriko katika Mkoa wa Morogoro, ikiwa ni pamoja na kusimamia
ujenzi wa nyumba za muda wa wahanga hao.
Rais
pia ameliamuru Jeshi kupeleka mashine za kusafisha maji katika makambi ambako
wahanga hao wa mafuriko ya Januari 22, mwaka huu wanaishi kwa muda.
Aidha,
Rais Kikwete amewahakikishia wahanga wa mafuriko hayo kuwa Serikali
itahakikisha inawapatia huduma zote za msingi ikiwa ni pamoja na chakula,
malazi, maji na huduma za afya hadi hapo watakapokuwa na uwezo wa kuanza
kujitegemea tena.
Rais
Kikwete ametoa amri hizo kwa Jeshi leo, Januari 27, 2014, wakati alipotembelea
kambi za wahanga wa mafuriko hayo kuwajulia hali walioathirika katika makambi
yaliyoko Shule ya Sekondari ya Magole katika eneo la Dumila na katika Kijiji
cha Mateteni kilichoko Dakawa, Wilaya ya Kilosa.
Katika
hotuba zake fupi baada ya kuwa ametembelea na kuona mahema ambamo wahanga hao
wanalala, Rais Kikwete amesema ameagiza
Jeshi kuongoza harakati za kuwahudumia wahanga hao kwa sababu zikifuatwa
taratibu za kawaida za Kiserikali huduma zitachelewa sana kuwafia waathirika.
“Kazi
yetu ni kusimamia maisha ya watu hasa
kipindi cha shida za namna hii. Tukifuata taratibu za kawaida za
Kiserikali za tenda tutachelewesha sana huduma za dharura kwa waathirika. Ndiyo
maana nimeliamuru Jeshi kufanya kazi hii ikiwa ni pamoja na kujenga haraka
makazi ya muda wa waathirika,” amesema Rais Kikwete na kuongeza:
“Katika
mazungumzo hayo na Mkuu wa Majeshi, nimemwagiza pia kuleta mashine za kusafishia
maji ili kuhakikisha kuwa watu wanakunywa maji salama kwa sababu katika hali ya
sasa maji yasiyokuwa salama yanaweza kuwa chanzo cha magonjwa.”
Kuhusu
upatikanaji wa chakula cha msaada kwa wahanga, Rais Kikwete amesema kuwa
Serikali inacho chakula cha kutosha kwa ajili yao. “Tunacho chakula cha kutosha
na hata kile tusichokuwa nacho tutanunua. Tutabanana ndani ya Serikali ili
tupate fedha za kutosha za kuwahudumia.”
Kuhusu
malazi, Rais amesema:”Naambiwa kuna upungufu wa magodoro. Tutahakikisha kuwa
yanapatikana na yatafika katika siku mbili zijazo. Hatutaki watu walale chini
na waje kupata vichomi.”
Kuhusu
maji, Rais Kikwete amesema kuwa Serikali itaendelea kutoa huduma ya maji bure
kwa wahanga. “Tutaendelea kutoa bure huduma hii mpaka hapo huduma ya kawaida ya
maji itakapoanza kupatikana tena.”
Kuhusu
huduma za afya, Rais amesema kuwa anafurahi kuwa kila kambi ya wahanga inayo
huduma ya afya ambayo itaendelea kutolewa kwa kadri watu wanavyozidi kuishi
kwenye makambi.
Rais
ameagiza kuwa baada ya muda mfupi viongozi wa Mkoa wa Morogoro na wilaya husika
wakae chini ya viongozi wa ngazi za chini na wahanga kujadili na kutafuta
mwafaka kuhusu maisha ya baadaye ya wahanga – hasa kuhusu namna gani wanaweza
kupatiwa maeneo yaliyoko nje ya mikondo ya mafuriko.
“Hili
ni lazima kwa sababu hata kama imechukua miaka mingi kwa mafuriko ya sasa
kutokea ni dhahiri kuwa iko siku yatakuja tena – inaweza kuwa hata mwaka huu
kwa sababu zipo mvua za masika. Kwa hiyo ni lazima tukubaliane jinsi gani ya
kurudi ama kutokurudi katika maeneo yetu tulikotoka.”
Labels:
KITAIFA
January 28, 2014
KIKWETE AKABIDHIWA JEZI YA TIMU YA CHICAGO CUBS TOKA KWA MWENYEKITI WA TIMU HIYO,JOE RICKETTS,PIA APOKEA TABLET 61 KWA AJILI YA WANAFUNZI WA SHULE YA WAMA NAKAYAMA
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea jezi ya timu ya baseball ya Chicago Cubs toka kwa mmiliki wa timu hiyo na Mwenyekiti wa taasisi ya kusaidia elimu ya Opportunity Education Foundation wa Marekani Bw. Joe Ricketts wakati alipomtembelea Ikulu Jumapili Januari 27, 2014.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea akipokea moja ya Tabuleti 61 kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Wama Nakayama iliyoko kijijini Nyamisati, Rufiji, Mkoa wa Pwani toka kwa Mwenyekiti wa taasisi ya kusaidia elimu ya Opportunity Education Foundation wa Marekani Bw. Joe Ricketts wakati alipomtembelea Ikulu Jumapili Januari 27, 2014.
Mwenyekiti wa taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi Dkt Shukuru Kawambwa, Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya WAMA Nakayama Dkt Ramadhani Dau na Mkuu wa Shule hiyo wakipokea moja ya Tabuleti 61 alizozitoa kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Wama Nakayama iliyoko kijijini Nyamisati, Rufiji, Mkoa wa Pwani leo Januari 27, 2014 toka kwa Mwenyekiti wa taasisi ya kusaidia elimu ya Opportunity Education Foundation wa Marekani Bw. Joe Ricketts akikabidhi moja ya Tabuleti 61 alizozitoa kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha pili katika Shule hiyo.
Mwenyekiti wa taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi Dkt Shukuru Kawambwa, Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya WAMA Nakayama Dkt Ramadhani Dau na Mkuu wa Shule hiyo wakiangalaia matumizi ya ya Tabuleti 61 katika darasa la kidato cha pili katika Shule ya Wama Nakayama iliyoko kijijini Nyamisati, Rufiji, Mkoa wa Pwani leo Januari 27, 2014 toka kwa Mwenyekiti wa taasisi ya kusaidia elimu ya Opportunity Education Foundation wa Marekani Bw. Joe Ricketts akikabidhi moja ya Tabuleti 61 alizozitoa kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha pili katika Shule hiyo.PICHA NA IKULU.
Labels:
MICHEZO NA BURUDANI
January 26, 2014
Mkutano wa Uzinduzi wa Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM
Written By CCMdijitali on Sunday, January 26, 2014 | January 26, 2014
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM Taifa Abdulrahman Kinana,wakati alipowasili katika viwanja vya Mpira Kiembesamaki katika Mkutano wa maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM,sambamba na kumnadi Mgombea wa CCM wa uwakilishi Jimbo la Kiembesamaki Mahmoud Thabit Kombo leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na vijana Chipukizi alipowasili viwanja vya Mpira Kiembesamaki katika Mkutano wa maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM,sambamba na kumnadi Mgombea wa CCM wa Uwakilishi Jimbo la Kiembesamaki Mahmoud Thabit Kombo leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akivalishwa Skafu na vijana Chipukizi wakati mapokezi alipowasili viwanja vya Mpira Kiembesamaki katika Mkutano wa maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM,sambamba na kumnadi Mgombea wa CCM wa uwakilishi Jimbo la Kiembesamaki Mahmoud Thabit Kombo leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akipokea salamu ya heshma baada ya kuvalishwa Skafu na vijana Chipukizi wakati mapokezi alipowasili viwanja vya Mpira Kiembesamaki katika Mkutano wa maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM,sambamba na kumnadi Mgombea wa CCM wa uwakilishi Jimbo la Kiembesamaki Mahmoud Thabit Kombo leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akiwapungia mkono wanaCCM waliohuduria katika Mkutano wa maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM,sambamba na kumnadi Mgombea wa CCM Jimbo la Kiembesamaki Mahmoud Thabit Kombo leo,mara alipowasili katika uwanja mpira Kiembesamaki palipofanyika mkutano huo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akimnadi na kumuombea kura kwa wanaCCM na Wananchi, Mgombea wa CCM wa uwakilishi Jimbo la Kiembesamaki Mahmoud Thabit Kombo leo,katika Mkutano wa maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM katika viwanja vya mpira Kiembesamaki.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na wananchi na wanachama wa CCM katika Mkutano wa maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM,sambamba na kumnadi Mgombea wa CCM Jimbo la Kiembesamaki Mahmoud Thabit Kombo leo, katika uwanja mpira Kiembesamaki palipofanyika mkutano huo
Katibu Mkuu wa CCM Taifa Abdulrahman Kinana,alipkuwa akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein kuzungumza na wananchi na wanachama wa CCM katika Mkutano wa maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM,sambamba na kumnadi Mgombea wa uwakilishi wa CCM Jimbo la Kiembesamaki Mahmoud Thabit Kombo leo, katika uwanja mpira Kiembesamaki palipofanyika mkutano huo.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.
Labels:
KITAIFA