Kamishna SULEIMAN KOVA
Zaidi ya watu 500 wanashikiliwa na polisi mjini DSM kufuatia
operesheni iliyofanywa na Jeshi la Polisi kanda Maalum ya DSM kuwatafuta watuhumiwa
wa vitendo vya uhalifu.
Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Kanda
Maalum ya DSM, Kamishna SULEIMAN KOVA amesema watuhumiwa waliokamatwa
wataendelea kushikiliwa na polisi wakati uchunguzi ukiendelea.
Amesema watuhumiwa hao hawatapata dhamana.