Home »
ARUSHA
» Waomba Ubunge wote Jimbo la Arusha wakamilisha zoezi la uridishaji fomu leo.
Waomba Ubunge wote Jimbo la Arusha wakamilisha zoezi la uridishaji fomu leo.
Mikutano ya Kampeni kwa ajili ya kura za maoni kuanza kesho tarehe 20/07/2015 kama ilivyoelekezwa na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa .
Baadhi ya watangaza nia 8 leo 19/07/2015 wamerudisha fomu na kukamilisha jumla ya waliochukua kuwa 14.
Ndg Lukiza Makubo achukua fomu leo na kuirudisha baada ya kukamilisha taratibu na kutimiza idadi yao kuwa 14.
Justin Nyari achukua kimya kimya na kuirudisha kimya.
Kata zote 25 ndani ya Jiji la Arusha zapata waombaji wa Udiwani : Wanaume 89 na Wanawake 6 wajitokeza jumla yao kuwa 89,mmoja aliyeomba Udiwani Kata ya Sekei Ndg Frank Moloimet ashindwa kurudisha.