Home » » Balozi Seif azindua rasmi Kampeni ya Majimbo na Wadi, Mkoa wa Kusini Unguja

Balozi Seif azindua rasmi Kampeni ya Majimbo na Wadi, Mkoa wa Kusini Unguja

Written By CCMdijitali on Thursday, September 17, 2015 | September 17, 2015

Baadhi ya wafuasi wa Chama cha Mapinduzi wakijimwaga katika burudani mbali mbali zilizokuwa zikitumbuiza kwenye uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi za Mkoa wa Kusini Unguja.
 Baadhi ya wanachama wa CCM waliohudhuria Uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi ya Majimbo na Wadi za Mkoa wa Kusini Unguja iliyozinduliwa na Mwenyekti wa Kamati ya Taifa ya Kampeni ya CCM Balozi Seif Ali Iddi hapo michamvi Wil;aya ya Kati.
 Balozi Seif akizindua rasmi kampeni za Uchaguzi kwa majimbo na Wadi za Mkoa wa Kusini Unguja hapo Michamvi Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusni Unguja.
 Balozi Seif akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chwaka Ndugu Masuria Mshamba kwenye uzi nduzi wa Kampeni za uchaguzi Mkoa wa Kusini Unguja.
 Balozi Seif akiwanadi kwa Wanachama wa Chama cha Mapinduzi na Wananchi wagombea nafasi za Uwakilishi na Ubunge Jimbo la Uzini kwenye uzinduzi huo.
 Wagombea Ubunge na Uwakilishi kupitia chama cha Mapinduzi katika Jimbo la Tunguu wakiomba kura katika mkutano wa uzinduzi wa Kampenzi ya Uchaguzi Mkoa wa Kusini Unguja.

Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Kampeni ya CCM Balozi Seif akiwanadi wagombea Ubunge na Uwakilishi kupitia kupitia chama hicho katika Jimbo la Paje wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uchaguzi ya Mkoa wa Kusini Unguja.
Picha na – OMPR – ZNZ.

 Press Release:-

Mwenyekiti wa Kamati ya Kampeni ya Chama cha Mapinduzi Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba Mzanzibari yeyote ataendelea kuwa huru kuishi mahali popote apendapo ndani ya Visiwa vya Unguja na Pemba ili kutimiza haki yake ya Kikatiba katika kuendesha maisha yake ya kila siku.

Balozi Seif ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM alitoa kauli hiyo wakati akiizindua Rasmi Kampeni ya Majimbo na Wadi zilizomo ndani ya Mkoa wa Kusini Unguja hapo katika uwanja wa Michezo wa Kijiji cha Michamvi kiliomo ndani ya Wilaya ya Kati.

Alisema tabia ya Viongozi wachache wa Kisiasa wa Vyama vya Upinzani wanaotamka hadharani na wakidai kwamba baadhi ya watu Hawana haki ya kujenga au kuishi Kisiwani Pemba waelewe kuwa wanavunja Katiba na Sheria za Nchi.

Balozi Seif alionya kwamba tabia hiyo mbaya inayofaa kukemewa na Viongozi wa Juu wa Kisiasa na hata wale wa Serikali ni kitendo cha ubaguzi kinachopaswa kulaaniwa na watu wote.

Aliwatahadharisha baadhi ya Viongozi wa Kisiasa kuachana na hulka hiyo mbaya ya kibaguzi inayoashiria cheche za kibaguzi zinazotaka kuwagawa wananchi wa Unguja na Pemba.

Balozi Seif ambae ia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwatoa hofu Wananchi kwa kufafanua kwamba Serikali ya Mapinmduzi ya Zanzibar itaendelea kuwatumikia Wananchi wake bila ya kujali upande mmoja wa Visiwa vya Zanzibar.

Alieleza kwamba miundombinu ya Mawasiliano ya Bara bara, umeme na huduma za Maji safi na salama zinaendelea kuimarishwa kwa pande zote mbili za Zanzibar zikilenga kuwajengea mazingira bora Wananchi wote. 

Balozi Seif aliwaomba Wana CCM na Wananchi wote kuwapigia Kura wagombea wote wa Chama cha Mapinduzi ili wapate ridhaa na nguvu za kusimamia utekelezaji wa sera na ilani ya CCM iliyolenga kudumisha Umoja, kuimarisha uchumi wa Taifa sambamba na kuwapunguzia ukali wa Maisha Wananchi wake wote.

Akigusia changamoto ya hudumza maji safi na salama zinazowakumba Wananchi wa Michamvi Balozi Seif alisema Serikali inaelewa vyema matatizo ya Wananchi hayo na jitihada zinaendelea katika kuzipatia ufumbuzi changamoto hizo.

Balozi Seif hivi sasa Wahandisi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar { ZAWA } wanaendelea na juhudi ya kulitafutia ufumbuzi suala hilo na tayari visima Viwili vimeshachimbwa vitakavyotoa huduma za maji safi na salama katika maeneo hayo.

Maema Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kusini Unguja Ndugu Ramadhan Abdulaah Ali alisema Mkoa huo utaendelea kuwa ngome ya CCM kutokana na umoja na mshikamano madhubuti uliopo miongoni mwa Wanachama wake wa CCM amoja na Wananchi wapenda Maendeleo.

Ndugu Ramadhan alisema uthibitisho huo utaonekana wakati wa kupiga kura kutokana na tathmini iliyofanywa inayothibitisha CCM itapata zaidi ya asilimia 90% ya kura katika Majimbo Matano yaliyomo ndani ya Mkoa huo wa Kusini Unguja.

Othman Khamis Ame
Ofisi yha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
17/9/2015.
Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link