Home » » Mwenezi Jiji la Arusha,aendelea na ziara ya Ujenzi wa Chama - Moivaro

Mwenezi Jiji la Arusha,aendelea na ziara ya Ujenzi wa Chama - Moivaro

Written By CCMdijitali on Wednesday, May 11, 2016 | May 11, 2016

Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya Arusha Ndg Jasper Kishumbua akiwataka Viongozi wa ngazi wa ngazi zote kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa kupata taarifa za kila baada ya miezi mitatu,kama inavyoelekezwa kwenye Ilani aliyoishika mkononi kwenye ziara ya Kujenga Chama Kata ya Moivaro 11 Mei 2016
 Katibu wa Kata ya Moivaro Ndg Charles Mollel akimkaribisha Mwenyekiti wa CCM Kata ya Moivaro Ndg Philimon Menjo ili aweze kufungua kikao, katika kikao cha Semina ya Kujenga Chama kwa Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Kata na Matawi ,Wajumbe wa Halamashauri Kuu za Matawi na baadhi ya Viongozi wa Mashina ya Wakereketwa, 11 Mei 2016.

Baadhi ya Viongozi wa Kata ya Moivaro wakifuatili kwa makini mada zilizokuwa zinawasilishwa na Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Arusha, katika kikao cha Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Kata na Matawi ,Wajumbe wa Halamashauri Kuu za Matawi na baadhi ya Viongozi wa Mashina ya Wakereketwa,katika ziara ya Kujenga Chama iliyofanywa na Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya Arusha katika Kata hiyo 11 Mei 2016.

Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya Arusha Ndg Jasper Kishumbua akiagana na baadhi ya Viongozi Wakuu wa Chama Kata ya Moivaro mara baada ya kuhitimisha semina  ya Kujenga Chama Kata ya Moivaro 11 Mei 2016
Picha zote na Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha, Ndg Jasper Kishumbua

Press Release:

Semina hii ni kwa ajili kuhimiza Viongozi kuzingatia Malengo na Madhumuni ya Chama, Masharti ya Uanachama,Haki za Mwanachama na Wajibu wa Mwanachama kwa mujibu wa Katiba ya Chama Cha Mapinduzi 1977 Toleo la 2007 na Kanuni na Taratibu za CCM.
 
Aidha aliwasilisha maelekezo ya Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Arusha iliyoketi Februari 2016.
 
Katika semina hiyo ilyohudhuriwa pia na Viongozi wa Mashina, aliwataka na kuwakumbusha wajibu wao kwa mujibu wa  Katiba ya Chama Cha Mapinduzi 1977 Toleo la 2007 na Kanuni na Taratibu za CCM, Ibara ya 23,24 na 26    Viongozi wa ngazi zote walitakiwa kuwahamasisha Viongozi hao kufanya vikao vya mara kwa mara ,kama njia mojawapo ya kuwa karibu na wananchi kwa kuwatembelea ,kusikiliza kero zao na kuzitafutia majawabu. Aidha uongozi wa Wilaya uliwaambia kuwa wako tayari kushiriki katika vikao vyao wanavyovifanya ,ili mradi wafuate taratibu kwa kuwashirikisha viongozi wao wa Kata.
Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link