Home » » Katibu wa CCM Wilaya ya Arusha na Mwenezi wake wafanya ziara ya kushtukizia kwenye baadhi Mashina, Kata ya Olmoti.

Katibu wa CCM Wilaya ya Arusha na Mwenezi wake wafanya ziara ya kushtukizia kwenye baadhi Mashina, Kata ya Olmoti.

Written By CCMdijitali on Thursday, June 9, 2016 | June 09, 2016

Katibu wa CCM Wilaya ya Arusha Ndg Feruzy Bano,akitoa bendera iliyochakaa kwenye Shina la Wakerekereketwa la Mama Mpare  , Kata ya Olmoti leo, katika ziara aliyoongozana na  Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha Ndg Jasper Kishumbua(hayupo pichani) .
Katibu wa CCM Wilaya ya Arusha Ndg Feruzy Bano,akiweka bendera mpya kwenye Shina la Wakerekereketwa la Mama Mpare , Kata ya Olmoti leo, katika ziara aliyoongozana na Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha Ndg Jasper Kishumbua(hayupo pichani) .
Mama Mpareee akiwa ameshika mkononi bendera mpya aliyokabidhiwa na Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha leo.




Katibu wa CCM Wilaya ya Arusha Ndg Feruzy Bano,akiweka mpya  kwenye Shina la Wakerekereketwa la Mama Mpare , Kata ya Olmoti leo, katika ziara aliyoongozana na Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha Ndg Jasper Kishumbua(hayupo pichani) .
Tukio hilo lilifanyika ,wakati Viongozi hao wakitokea kwenye Kikao cha Kamati ya Siasa ya Kata Olmoti, na mara walipoona bendera iliyokuwepo imechakaa, iliwalazimu kuacha njia na kwenda kuwabadilishia na kuwawekea bendera nyingine.

Hali hiyo iliwafurahisha sana wanachama waliokuwepo kwa kusema kuwa ni muda mrefu umepita tangu waombe kubadilishiwa bendera hiyo.

Pia waliwashukuru Viongozi hao kwa kuwaondolea aibu, kwani baadhi ya watu walikuwa wanawakejeli,kutokana na hali ya bendera hiyo kutokuwa katika hali nzuri.
Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link