_______________________________________________
Akizungumza na wadau hao alisema sekta hii ina changamoto mbalimbali zikiwemo za ongezeko la kodi ya utalii pamoja na kadi nyingine ndogondogo wanazotozwa pindi
wakiwa na wageni wao.
“Najua wafanyabiashara wengi hapa wametishika sana nah ii kodi ya utalii ilioanza kutozwa hivi karibuni nakuwafanya muone kuwa biashara zenu zimeanza kuyumba kwa
watalii kutotaka kufika tena nchini.”
Alisistiza kuwa kuna fursa mbalimbali katika sekta hii ya utalii ambazo zinaweza kukuza zaidi biashara hii na kuwavutia zaidi wageni kutoka nje napia ushirikishwaji wa wadau wa
utalii na Serikali ni kitu chamuhimu sana ndio maana nimeamua kuandaa huu
mkutano ili tuweze kuanzimia mambo mbalimbali kwa pamoja.
Akituoa ufafanuzi wa kodi wa utalii iliyoanza kutumika Julai 1,2016 mpaka Agosti 2016 ,
Mkuu wa Kitengo cha elimu na mapato Euginia Mkumbo ,amesem kuna ongezeko la
kodi kwa kiasi cha bilioni 5.8 ambayo ni asilimia 120 kutoka kwenye kodi za
hoteli na utalii wakati mwaka jana ilikuwa bilioni 2.5 kutoka kwenye kodi za hoteli tu.
Aidha ongezeko hilo la kodi ya utalii imeonyesha kunaongezeko kubwa la mapato
yaliyoingia Serikalini na wakati huo wageni wengi hawajapatwa na usumbufu
wowote tokea kodi hii ya utalii ilipoanza kutumia.
Mwenyekiti wa Tanzania Tour Operators (TATO) bwana Wilbad Chambulo,amesema kuanzishwa kwa kodi hiyo ya utalii kwa upande wao haina shida isipokuwa
hawakupewa taarifa mapema na taasisi husika ili waweze kujipanga.
“Kwetu sisi hii kodi haina shida ila tatizo ni taarifa zimetufikia kwa gafla sana na
kutufanya tukose mda wakujianda,”alisema Chambulo.
Pia alilisitiza kwa Serikali kusimamia sheria zaidi ili wafanyabiashara wote wa sekta
waweze kulipa kodi kuliko kwa sasa ni baadhi yao tu ndio wanalipa
na wengine hawalipi.
Aidha aliomba utaratibu wa malipo kwa taasisi husika uwangaliwe upya kwani kwa sasa unamlolongo mrefu sana unaopelekea kuwachukua mda mrefu sana pindi wanapoenda kufanya malipo hayo au kodi zote zingewekwa kwenye fungu moja iliziweze
kulipwa kwa mara moja.
Mambo mbalimbali yameadhimiwa katika mkutano huo ikiwemo kuimalisha ulinzi na
usalama kwa watalii wote watakaoingia mkoani na pia litaanzishwa dawati maalumu
la kusikiliza Changamoto mbalimbali zitakazo kuwa zinawakabiri wadau hao wa
utalii na kuzitafutia ufumbuzi kwa haraka.
----------------------------------------------
Mkurugenzi Mtendaji wa AICC Bwana Elishilia Kaaya na baadhi ya wageni waliohudhulia mkutano wa wadau wa utalii, uliotishwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha(hayupo pichani) katika ukumbi wa AICC Jijini Arusha.