Home » » GAMBO AWAKUNA WANANCHI WA TERRATI – ARUSHA

GAMBO AWAKUNA WANANCHI WA TERRATI – ARUSHA

Written By CCMdijitali on Friday, October 21, 2016 | October 21, 2016

 Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (kwanza kulia) akizungumza na wananchi wa Kata ya Terrati kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya Msingi Mkonoo.


 Baadhi ya wananchi wa Kata ya Terrati waliohudhuria Mkutano wa hadhara ulioitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha

 Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Ndg. Athumani Kihamia (aliyesimama) akiwatambulisha wakuu wa Idara za Jiji (hawapo Pichani) kwenye Mkutano wa hadahara.
 Mhandisi wa barabara Jiji la Arusha Fordia Mwankenja (anayepunga mkono)akiwasalimia wananchi wa Kata ya Terrari kwenye Mkutano wa hadhara
 Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Fabian Gabriel Daqarro akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha kuzungumza na wananchi wa Kata ya Terrati kwenye Mkutano wa hadhara.


Mwenyekiti wa Mtaa wa Ilaitayoki Mhe. Long’ida Lomayani Kupitia Chadema akiwasilisha kero za mtaa wake kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.


Nteghenjwa Hosseah – Arusha


Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo amechangia Lita 600 za mafuta kwa ajili ya greda la Halmashauri ili liweze kutengeneza miundombinu ya barabara kwenye maeneo yote korofi yanayozunguka kata ya Terrati.

Rc Gambo amefanya hivyo wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi wa Kata ya Terrat uliofanyika kwenye Shule ya Msingi Terrat wenye lengo la kufahamu changamoto za muda muda mrefu zinazowakabili wananchi wa maeneo hayo.

Katika Mkutano huo Mkuu wa Mkoa alianadamana na watalaamu wa Taasisi mbalimbali zinazotoa huduma katika Mkoa huu pamoja na menegiment ya Jiji ili kuwezesha upatikanaji wa majawabu ya kero zote zilizo wasilishwa na wananchi hao ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa haraka ili kumaliza kabisa changamoto hizo.

Wananchi wa Kata hiyo wamesema kwa muda mrefu wamekuwa wakikabiliwa na kero ya ubovu wa miundombinu ya barabara, kukosekana kwa maji safi na salama pamoja na umeme katika eneo hilo na pia walitoa shukrani zao kwa Mkuu wa Mkoa kwa kuwapa kipaumbele katika ziara zake za kutambua changamoto za Mkoa wake.

Sisi wakazi wa huku tumekua kama hatuishi kwenye Jiji la Arusha kwa sababu huduma zote muhimu zimekuwa kikwazo sana kwetu mpaka zinasababisha kudorora kwa uchumi kwa wakazi wa maeneo haya kwa kuwa hapavutii wafanyabiashara kuja kuwekeza wala wanunuzi kutoka mjini hivyo tumekua tukiuziana sisi kwa sisi ambao wote tuna vipato duni alisema Jumanne Juma Kingu.

Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa Jina la Eliakim Mason kutoka Mtaa wa bondeni kati alisema kuwa Gari lakubebea wagonjwa katika kituo cha Afya Mkonoo limeharibika kwa kipindi kirefu sana na wanapata tabu ya kusafirisha mgonjwa hadi kufikia kwenye Hospital za Mjini Arusha inawalazimu kukodi Gari kwa gharama kubwa ili kunusuru maisha ya ndugu zao pia alilalamikia uhaba wa watumishi katika Kituo cha Afya Mkonoo na kudai kwamba inakuwa vigumu kupata hudma bora wagonjwa wanapokua wengi katika kituo hicho.

Akitoa majibu ya malalamiko hayo Mkuu wa Mkoa wa Arusha alisema changamoto hizi zimekuwa za kipindi kirefu lakin hivi sasa zimefika mwisho kwa sababu Serikali ya Awamu ya Tano ni ya kutatua kero na vitendo ndivyo vinavyotawala hivyo ndani ya muda mfupi eneo hili litakua sehemu nzuri ya kuishi kwa kuwa kero hizi zitakuwa historia.

Rc Gambo alimuagiza Maneja wa Tanesco Mkoa kuhakikisha umeme unawafikia wananchi wa Kata ya Tarati ndani ya miezi mitatu pia aliwataka viongozi wengine wa Taasisi zinazolalamikiwa kutolea ufafanuzi na mikakati ya haraka ya kumaliza kabisa matatizo ya wananchi wa Terrat.

Naye Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Ndg. Athumani Kihamia aliahidi mbele ya Mkutano huo kwamba ndani ya wiki mbili gari la kubebea wagonjwa kwenye Kituo cha Afya Mkonoo litakuwa limeshatengenezwa na kuanza kutoa huduma na pia ataongeza watumishi wa kutosha ili kuboresha utoaji wa huduma za Afya katika Kituo hicho.

Eng. Ruth Koya ni Mkuu wa Idara ya Maji safi na maji Taka (AUWSA) alieleza kuwa Taasisi yake imeanza kutekeleza mradi mkubwa wa uboreshaji wa miundombinu pamoja na upatikanaji wa maji safi na salama na Kata ya Terrati ni miongoni mwa maeneo ambayo yatafikiwa na mradi huo na utamaliza kabisa changamoto hii ya maji.

Mkutano huu ulihudhuriwa na wananchi wa chama cha demokrasia na maendeleo
akiwemo Mwenyekiti wa Mtaa wa Ilaitayok Mhe. Long’ida Lomayani.
Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link