Wanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari
Mpenchi iliyopo katika Wilaya ya Njombe, wamemuhaidi Rais wa Jamuhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan @samia_suluhu_hassan .
kufaulu asilimia 100% kwenye Mitihani yao ya Kidato cha Nne ifikapo
2025 , na pia wamemshukuru kwa kuwaletea miradi mizuri ya madasa 5 ya
fedha za UVIKO-19,
Mkuu
wa Wilaya ya Njombe, Mhe Kissa Gwakisa Kasongwa, akipokea salamu hizo
katika shule hio ya sekondari ya Mpechi, Amefurahishwa sana na Mwitikio
wa wazazi kwa kuwasajili na kuwapeleka watoto kujiunga na Kidato cha
kwanza maana ni Haki yao ya msingi.
Awasisitiza wanafunzi kusoma kwabidii na kuepukana na vishawishi na Vikwazo ambayo vitawazuia kufikia malengo yao kwenye maisha, na wawe na uvumilivu ili waweze kufanikiwa kama yeye na Walimu ambao wametimiza malengo waliokuwa nayo , asema Mhe.Kissa.
Mhe.
Kissa amesisitiza maendeleo ya watu wa Njombe na Mkoa wa Njombe
yataletwa na wananjombe, kwahio tuendelee kuhamasisha jamii iwapeleke
watoto shule ili wakapate Elimu itakayo wasaidia kuja kuleta maendeleo
kwatika Mkoa wetu wa Njombe.