Home » » BALOZI WA TANZANIA NCHINI SUDANI AWASILISHA HATI ZA UTAMABULISHO NCHINI SUDANI YA KUSINI

BALOZI WA TANZANIA NCHINI SUDANI AWASILISHA HATI ZA UTAMABULISHO NCHINI SUDANI YA KUSINI

Written By CCMdijitali on Thursday, February 10, 2022 | February 10, 2022

 

Balozi wa Tanzania nchini Kenya ambaye pia anaiwakilisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Sudani Kusini, Dr. John S Simbachawene (kulia) akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mheshimiwa Salva Kiir Mayardit, Rais wa Jamhuri ya Sudani Kusini mjini Juba.


Balozi wa Tanzania nchini Kenya ambaye pia anaiwakilisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Sudani Kusini, Dr. John S Simbachawene amewasilisha Hati za Utambulisho kwa Mheshimiwa Salva Kiir Mayardit, Rais wa Jamhuri ya Sudani Kusini mjini Juba.

Katika mazungumzo, Mhe. Balozi Simbachawene pia amewasilisha salamu kutoka kwa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwenda kwa Mhe. Rais Salva Kiir Mayardit. Mhe. Salva Kiir ameeleza kufurahishwa na mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Tanzania na Sudani Kusini na ameahidi kuendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania kukuza mahusiano hayo. 

Kufuatia majadiliano hayo, Tanzania na Sudani Kusini zitachukua hatua za kuimarisha mahusiano ya kisiasa na kibiashara kati ya nchi hizo mbili. Maeneo ya kipaumbele yaliyoanishwa katika kuimarisha uhusiano ni ushirikiano wa kimataifa, kilimo, utalii, elimu na nishati. 

Vilevile, Tanzania na Sudani Kusini zimekubaliana kuingia Makubaliano ya Ushirikiano kwa ajili ya kuanzisha Tume ya Pamoja ya Ushirikiano, na pia kushirikiana katika kufundisha lugha ya Kiswahili nchini Sudani Kusini
Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link