Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima |
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima |
Na WMJJWM
Waziri
wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy
Gwajima, amewapongeza Ngariba waliokuwa wanajihusisha na vitendo vya
ukeketaji baada ya kuacha kufanya vitendo hivyo na kisha kugeuka kuwa
wanaharakati wa kukemea vitendo vinavyo dhalilisha utu wa mtoto wa kike
na kumuachia maumivu makali.
Akifunga Kongamano Maalum kwajili ya
mapambano ya kutokomeza Ukeketaji lilichofanyika mkoani Mara katika
Wilaya ya Tarime, Dkt. Gwajima alisema, kitendo cha Ngariba hao kuacha
suala la Ukeketaji na kujiunga na Serikali katika mapambano hayo ni
ujasiri wa hali ya juu na nicha kupongezwa.
“Mmewasikia wenyewe wakijieleza hapa, kwamba wapo baadhi yao walikata shauri na kuacha kuendelea kukeketa, lazima tuwapongeze sana kwa hatua hii. Lakini baadhi yao wanatishiwa hata kutengwa na jamii zao baada ya kuacha vitendo hivyo vya kikatili, tuseme kama Serikali na wadau tutakuwa nao bega kwa bega kuwatetea kwa nguvu zote bila kuchoka” alisema Waziri Dkt. Gwajima.
Dkt. Gwajima alisema dhana ya kwamba, mtoto kumvusha rika kutoka usichana kwenda kuwa mama au mtu mzima sio lazima akeketwe zipo njia mbadala za kumvusha binti rika ikiwepo kuwapatia mafunzo yakujitambua bila kumuathiri mwili wake.
Ameongeza kuwa, zipo athari wanazo kumbana nazo Mabinti wanaokeketwa ikiwepo athari za kisaikolojia na msongo wa mawazo, kwani, vitendo hivyo hufanywa bila ridhaa ya wahusika, kupata maumivu makali, kutokwa damu nyingi, kuuguza kidonda, changamoto za kujifungua na uwezekano wa kupoteza maisha.
“Madhila mengine kusababisha maambukizi ya magonjwa ya ngono, Virusi vya UKIMWI pamoja na magonjwa ya njia ya mkojo (UTI), lakini pia uwepo wa kovu la ukeketaji linalo kusababisha mimba kinzani na unaweza kusababisha fistula”. alisisitiza Dkt. Gwajima, na kuongeza kuwa,
“Mtoto anaweza kupata changamoto wakati wa kujifungua ambapo zinaweza kumsababishia mtindio wa ubongo, na kupata mateso katika maisha yake yote. aliongeza Waziri Dkt. Gwajima.
Awali kabla ya kufunga mafunzo hayo, wakichangia mada zilizowasilishwa katika Kongamano husika, Mangariba hao waliiomba Serikali iwalinde,