Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula |
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju |
Na WMJJWM, Dodoma
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum
Dkt. Zainab Chaula amewataka Wamachinga kutumia fursa zilizopo nchini ikiwemo
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika Shughuli zao ili kupiga hatua
kiuchumi.
Akifungua kikao cha kuwajengea uwezo Viongozi wa shirikisho la Wamachinga,
kilichofanyika Jijini Dodoma leo tarehe Febriary 22, 2022 Dkt. Chaula amesema
kwa sasa Teknolojia inakuwa kwa kasi hivyo uwezekano wa kupata masoko na bidhaa
umerahisishwa ikilinganishwa na kipindi cha Nyuma ambapo Teknolojia ilikuwa
duni.
Dkt. Chaula amesema, fursa nyingine zilizopo ni pamoja na amani na utulivu
uliopo nchini, mikopo ya Maendeleo kutokana na mapato ya Halmashauri, pamoja na
ardhi.
"Tunamshukuru Mhe. Rais kwa kuona umuhimu wa kuanzisha Wizara hii na kuipa Dhamana ya kushughulikia Makundi Maalum ikiwemo wamachinga, maana yake ni kwamba, anawasikiliza, anawatambua na kuwaelewa" amesema Dkt. Chaula.
Dkt Chaula amewataka pia, kuimarisha ushirikiano miongoni mwao, Serikali na Wadau wengine ili kukuza zaidi mitandao ya biashara zao na kuboresha maisha kwani wao wenyewe ni fursa katika kukuza uchumi wa Taifa. Pia wasikubali kutumiwa kwa namna yoyote ili kuwatenganisha.
Dkt. Chaula amebainisha kuwa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, ametoa jumla ya sh. bilioni 5 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya Wamachinga hivyo Serikali itahakikisha fedha hizo zinatumika kwa ufanisi.
Awali Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amon Mpanju akitoa maelezo kuhusu kikao hicho amesema hadi tarehe 31 Januari usajili wa shirikisho la machinga ulikuwa umekamilika.
Mpanju amesema lengo la kikao hicho ni kuwasikiliza na kuwapa fursa ya kupata elimu ya masuala mbalimbali ili kuongeza ufanisi katika shughuli zao.
"Nia ya Serikali ni kuhakikisha kundi hili linapata Maendeleo kupitia shughuli zao hivyo kikao hiki kinawajengea uelewa wa mambo muhimu ikiwemo sheria, kanuni na taratibu za Serikali" amesema Mpanju.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Shirikisho la Machinga nchini (SHIUMA), Ernest Matondo, wameishukuru Serikali kupitia benki ya NMB kwa kuwakutanisha kwani wana imani m
2h