Na Angela Msimbira MARA
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Innocent Bashungwa amemuagiza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais - TAMISEMI kuhakikisha Mameneja TARURA wa Mkoa yote nchini wanatoa Ripoti kila mwezi kuhusu kazi zao kwa kuwa moja ya kigezo cha kuwapima ni utendaji kazi uliotukuka.
Mhe.
Bashungwa ametoa agizo hilo Leo kwenye uwekaji wa Jiwe la msingi kwenye
Mradi wa Majisafi wa Mugambo-Kiabakari-Butiama katika Halmashauri ya
Wilaya ya Musoma, Mkoani Mara.
Amesema
kazi ya Mameneja Mkoa ni kuhakikisha fedha zinazotolewa na Serikali
katika ujenzi wa miundombinu ya barabara zinasimamiwa kwa weledi na
kuhakikisha thamani ya fedha ya fedha inaonekana kwenye ubora wa
miundombinu ya barabara inayotekelezwa.
Mhe.
Bashungwa amesema Ofisi ya Rais - TAMISEMI inaendelea kufanya maboresho
kwa Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) ili iweze kusimamia
kikamilifu fedha zinazotolewa na Serikali katika ujenzi ya miundombinu
ya barabara nchini ili kuwafungulia wananchi barabara za vijijini na
kufika kusikofikika.