Home » » "Wajumbe wa Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi wapongezwa" - WAZIRI MKUU MAJALIWA

"Wajumbe wa Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi wapongezwa" - WAZIRI MKUU MAJALIWA

Written By CCMdijitali on Monday, February 7, 2022 | February 07, 2022

📷Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa ambae pia Ni Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kitaifa ya Sensa ya Watu na Makazi akifungu kikao cha tatu  kamati hiyo kilichofanyka ukumbi wa Kambarage Dodoma.

 

📷Mwenyekiti  mwenza wa Kamati Kuu ya Kitaifa ya Sensa ya Watu na Makazi ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleman Abdulla akifunga kikao cha tatu  kamati hiyo kilichofanyka ukumbi wa Kambarage Dodoma


📷Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Albina Chuwa akitoa ufafanuzi juu ya maandalizi ya sense ya watu na makazi kwa wajumbe wa kamati ya kitaifa ya sensa ya watu na makazi katika kikao cha tatu cha kamati hiyo kiichofanyika ukumb wa kambarage jijini Dodoma.


📷Wajumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Sensa ya Watu na Makazi wakifuatilia kwa makini kikao cha tatu cha kamati hiyo kilichofanyika ukumbi wa kambarage jijini Dodoma.


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa amewapongeza wajumbe wa Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa ya watu na  Makaazi kwa hatua waliyofikia katika maandalizi ya Sensa ya mwaka huu.

Mhe. Majaliwa ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa ya watu na makazi ameyasema hayo katika kikao cha tatu cha kamati hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa kambarage jijini Dodoma.

Amesema ni jambo la kupongezwa kwa hatua iliyofikia sasa katika maandalizi ya Sensa  hio  inayotarajiwa kufanyika mwezi  Agosti mwaka huu ambapo hatua hiyo inatokana na mashirikiano yailiyopo baina yao, amesema kuwa ni mategemeo ya Serikali zoezi hili liweze kufanikiwa vizuri zaidi.

Mhe. Majaliwa ametaka wajumbe hao kuhakikisha wanaendeleza kushirikiana kwa pande zote za Muungano jambo ambalo litasaidia kufanikisha  zoezi hilo.

Kwa upande wake Mwenyekiti mwenza wa kamati hio kitaifa ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdalla amesema kuwa hatua iliofikiwa hadi sasa katika maandalizi ya Sensa hio ni jitihada za Marais wote wawili, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hasan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt  Husein Ali Mwinyi wanazoendelea kuzichukua katika kufanikisha zoezi hilo

Aidha, Mhe. Hemed amewataka wajumbe wa kamati hio kuhakikisha kuwa wanasimamia vyema majukumu yao ili Sensa hii iweze kufikia lengo la Serikali zote mbili kuweza kupanga mipango Imara ya kimaendeleo kwa maslahi ya Taifa

 

Sambamba na hayo, Mhe.Hemed amesema Serikali zote mbili zimejipanga kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa na linakamilika kwa wakati uliopangwa kwani Sensa ya mwaka huu ni ya kipekee  ambayo itaibua mambo mbali mbali yatakayozisaidia Serikali zote katika kuwaletea Maendeleo wananchi wake.

Nae Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Ndugu JOHN JINGU amesema kuwa jitihada mbali mbali zinaendelea kuchukuliwa kwa kuelimisha jamii kuhusu suala zima la Sensa na kueleza kuwa hadi sasa tayari wameshayafikia makundi ya wananchi tofauti kwa semina nakutumia vyombo vya habari ili kuhakikisha elimu ya Sensa inamfikia kila mmoja katika jamii.

Kwa upande wake, mtakwimu mkuu wa Serikali wa Jamuhuri  ya Muungano wa Tanzania Dr. ALBINA CHUWA amesema mashirika ya ndani na nje ya nchi  tayari wameshaonesha ushirikiano wao ili kuhakikisha zoezi hilo linakamilika bila ya changamoto yoyote.

Aidha, amesema Ofisi zote mbili za takwimu zimejipanga kuhakikisha makarani watakao kusanya taarifa wanatoka katika maeneo husika ili kupata taarifa za usahihi.

 

……………………

Abdulrahim khamis

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais

07/02/2022

Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link