Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akimueleza jambo Balozi
wa Marekani nchini Mhe. Dkt. Donald Wright |
Kikao cha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula na Balozi wa Marekani nchini Mhe. Dkt. Donald Wright kikiendelea |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Balozi wa Norway nchini Mhe. Elisabeth Jacobsen katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam |
Balozi wa Marekani nchini Mhe. Dkt. Donald Wright akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam |
Na Waandishi wetu, Dar
Balozi wa Marekani nchini Mhe. Dkt. Donald Wright amepongeza uendeshaji wa michakato ya kisiasa inavyoendeshwa nchini Tanzania.
Balozi
Wright ameyasema hayo wakati alipokutana kwa mazungumzo na Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata
Mulamula (Mb) katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.
Balozi
Wright amesema anaridhishwa na jinsi hali ya kisiasa ilivyo hapa nchini
na kuongeza kuwa anaunga mkono michakato ya kisiasa inavyoendeshwa
nchini na kuelezea kuridhishwa kwake na hali hiyo.
Pamoja
na mambo mengine, viongozi hao wamejadili masuala mbalimbali ya
ushirikiano kati ya Tanzania na Marekani kwa maslahi ya pande zote
mbili.
Naye
Waziri Mulamula amemuahidi Dkt. Wright kuwa Serikali itaendelea kutoa
ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yake wakati wote hapa nchini.
Katika
tukio jingine, Waziri Mulamula amekutana na kufanya mazungumzo na
Balozi wa Norway nchini Mhe. Elisabeth Jacobsen na kujadili masuala ya
ushirikiano katika masuala ya amani na usalama, jinsia na uwezeshaji wa
wanawake.
Pia,
Waziri Mulamula amekutana kwa mazungumzo na Afisa kutoka Mfuko wa
Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) Bibi. Jacqueline Machangu-Motcho
na kujadili masuala ya ushirikiano baina ya mfuko huo na Tanzania.