Mkuu
wa Wilaya ya Njombe, Mhe Kissa Gwakisa Kasongwa amefanya ziara katika
Taasisi ya mamlaka ya Maji ya Makambako (MAKUWASA) tarehe 14/03/2022
Lengo
la ziara hio nikufahamiana na Watumishi wa secta hio , pamoja
nakujionea maendeleo ya Mradi wa Uviko 19 ambao umefikia Asilimia 90% ya
Fedha zilizo letwa.
Mhe, Kissa ameongea na watumishi juu ya
uweledi katika kufanya kazi yao, maana sekta ya maji ni moja ya sekta
muhimu katika jamii. Na wafanye kazi bila makando kando ili kuhakikisha
wananchi hawakosi imani nao.
Kutengeneza kamati zitako fatilia na
kuhakikisha watu wanao iba maji na kuharibu miundombinu ya maji wana
kamatwa na kuadhibiwa ili kuhakikisha hakuna upotevu wa maji kiholela,
asema Mhe Kissa.
Mwisho awaomba Makuwasa kushiriki kikamilifu
kwenye Uzinduzi wa MWENGE WA UHURU utakao fanyika Mkoani Njombe katika
viwanja vya Saba saba, asema Mhe Kissa.
DC NJOMBE AFANYA ZIARA KATIKA TAASISI YA MAMLAKA YA MAJI MAKAMBAKO
Written By CCMdijitali on Tuesday, March 15, 2022 | March 15, 2022
Labels:
KITAIFA