Home » » KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UWEKEZAJI WA MITAJI YA UMMA YATUA MKOANI ARUSHA

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UWEKEZAJI WA MITAJI YA UMMA YATUA MKOANI ARUSHA

Written By CCMdijitali on Sunday, March 13, 2022 | March 13, 2022









 Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) imewasili mkoani Arusha kwa ajili ya ziara ya siku 3, mkoani humo.

Baada ya kuwasili Jijini Arusha Kamati ilikwenda kujitambulisha kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha na kupokelewa na Kaimu Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Eng. Richard Ruyango ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru.

Akizungumzia ziara hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya PIC, Mhe. Jerry Silaa amesema Kamati hiyo ipo Mkoani Arusha kwa ajili ya kutembelea na kukagua miradi ambayo Serikali imewekeza fedha za Umma.

Mhe. Silaa ameitaja Miradi hiyo kuwa ni Uboreshaji wa Miundombinu katika Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), kukagua miradi ya Uboreshaji wa huduma za maji na Usafi wa mazingira inayotekelezwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Arusha (AUWASA).

Mhe. Silaa ametaja mradi mwingine kuwa ni ule wa uwekezaji katika Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viwatilifu Tanzania(TPHA).

Kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Eng. Ruyango ameikaribisha Kamati ya PIC na kuihakikishia ushirikiano wa Serikali katika utekelezaji wa majukumu yake.

Aidha, ameihakikishia kamati kuwa Mkoa wa Arusha uko salama.

Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link