Home » » MAJALIWA – TUTASIMAMIA KIKAMILIFU UTEKEKEZAJI WA BAJETI

MAJALIWA – TUTASIMAMIA KIKAMILIFU UTEKEKEZAJI WA BAJETI

Written By CCMdijitali on Friday, March 11, 2022 | March 11, 2022






 
 

MAJALIWA – TUTASIMAMIA KIKAMILIFU UTEKEKEZAJI WA BAJETI
 

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kuimarisha mifumo ya usimamizi wa miradi pamoja na ufuatiliaji wa karibu wa utekelezaji wa bajeti yake ili rasilimali zilizopo ziweze kuwa na tija inayoendana na thamani ya fedha za walipa kodi.

 
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Ijumaa, Machi 11, 2022) wakati akifungua Mkutano wa Bunge kuhusu Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Kiwango cha Ukomo wa Bajeti wa Serikali kwa Mwaka 2022/2023 uliofanyika kwenye ukumbi wa Msekwa Bungeni jijini Dodoma
 
Mheshimiwa Majaliwa amesema ni azma ya Rais Samia Suluhu Hassan, kuona ukomo wa bajeti hauathiri utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa sambamba na shughuli zilizopangwa kwa mwaka 2022/2023.
 
“Sote tunafahamu nchi yetu sasa iko katika uchumi wa kati ambayo ni ishara ya  kuongezeka kwa uwezo wa Taifa kugharamia huduma muhimu kwa wananchi sambamba na kuongezeka kwa uwezo wa wananchi kumudu mahitaji yao.” Alisema.

 
Pia, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kutoa taarifa ya Utekelezaji wa Uhifadhi katika eneo la Ngorongoro ambapo amesema kuwa Serikali imeendelea kusimamia suala hilo kwa umakini mkubwa ikiwa ni pamoja na kufanya mazungumzo na wananchi na viongozi wa maeneo hayo ili kuhakikisha wanapata uelewa wa kutosha kwa kuzingatia ushauri uliotolewa na wabunge.
 
“Serikali imetenga eneo la hekari 400,000 lililoko katikati ya maeneo ya Wilaya za Handeni, Kilindi, Kiteto na Simanjiro na hekari 220,000 tayari zimepimwa viwanja 2,406 ambapo kati ya hivyo, viwanja 2,070 tumeandaa kwa ajili ya makazi na kila kimoja kina ukubwa wa ekari tatu. Tumeanza na nyumba101 zenye vyumba vitatu vya kulala kwa wale wanaotaka. Tuna viwanja 336 kwa ajili ya huduma kama shule za msingi na sekondari, zahanati na vituo vya afya. Ujenzi wa mifumo ya maji kazi inaendelea.”

Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link