MAONYESHO YA WAJASIRIAMALI
NJOMBE KUELEKEA UZINDUZI WA
MWENGE KITAIFA
Mkuu
wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Waziri Kindamba . amezindua maonyesho ya
kibiashara (Wajasiriamali) yaliyofanyika katika viwanja vya Sabasaba.
kama amsha amsha kuelekea Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa
utakaofanyika katika Mkoa wa Njombe Tarehe 02 Aprili, 2022.
Mhe,Waziri
ameipongeza Benki ya CRDB kwakudhamini Uzinduzi huu wa Mwenge wa Uhuru
pamoja na kufanya maboresho ya uwanja ambao utatumika katika uzinduzi wa
Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa .
Aidha Mhe.Waziri Kindamba
amewasisitiza Wananchi kushiriki kikamilifu kwenye Sensa ya watu na
Makazi ambayo itafanyika Mwezi wa Nane mwaka huu ili kuunga mkono
Kaulimbiu ya Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2022 isemayo-
"SENSA NI MSINGI WA MIPANGO YA MAENDELEO: SHIRIKI KUHESABIWA TUYAFIKIE MAENDELEO YA TAIFA".
Pamoja na mambo mengine Mhe.Kindamba amewaasa Wananchi kuendelea kujitokeza kupata chanjo ya UVIKO -19.
".. Chanjo ya UVIKO-19 ni muhimu kwajili ya Kujikinga na maambukizi ya Ugonjwa wa UVIKO ambalo ni gonjwa hatari sana linalo shambulia mataifa mengi, nawaomba Wananjombe mzidi kujitokeza kuchoma chanjo ya Uviko 19 na hapa kwenye maonyesho kuna Mabanda maalumu ya kutolea chanjo." Mhe.Kindamba.
Mwisho Mhe.Kindamba amewakaribisha Wananchi wote kushiriki katika Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2022.
"..Napenda kuwaalika wananchi wote kwenye *Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa utakaofanyika Katika viwanja vya Sabasaba Njombe..".
Mhe.Kindamba.
#Njombetupotayari
# VisitNjombe
#vijanawamamasamia🇹🇿