Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Prof. Riziki Shemdoe amesema mashindano ya michezo kwa shule za Msingi (UMITASHUMTA) mwaka 2022 yameshirikisha Wanafunzi zaidi ya 3000 kutoka Mikoa 26 ya Tanzania Bara na miwili kutoka Zanzibar.
Ameyazungumza hayo leo Agosti 4, 2022 mkoani Tabora katika hafla ya Uzinduzi wa mashindano hayo yaliyofanywa na Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania.
Prof. Shemdoe ameeleza kuwa wanafunzi wanaoshiriki mashindano hayo Wana vigezo na wameandaliwa vizuri kuanzia ngazi ya shule.
"Mashindano haya yalianza mwaka 2000 ambapo lengo lake ni kukuza vipaji vya Wanafunzi na kuimarisha upendo, ushirikiano na kuboresha afya kwa Wanafunzi", amesema Prof. Shemdoe.
Ametumia nafasi hiyo kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutenga fedha kwa ajili ya kuendesha shughuli za michezo nchini.
Mashindano ya UMITASHUMTA yatahitimishwa Agosti 08 mwaka huu na Agosti 9,2022 yataanza mashindano ya UMISSETA.
Mwisho