CPA MAKALLA: CCM ITAWALETEA WAGOMBEA WASIO NA MAKANDOKANDO

  Na Richard Mwaikenda, Mwanza   Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla akiwaahidi wananchi kwa...

Latest Post

MHE. RAIS SAMIA AZINDUA CHAMA CHA MAWAKILI WA SERIKALI

Written By CCMdijitali on Friday, September 30, 2022 | September 30, 2022

MHE. RAIS SAMIA AZINDUA CHAMA CHA MAWAKILI WA SERIKALI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa Mawakili wote wa Serikali ambao hawajasajiliwa kwenye rejista ya Mfumo wa Taarifa wa Mawakili wa Serikali kujisajili kabla ya muda kupita ili watambulike na Mfumo wa Kieletroniki wa Taarifa wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ujulikanao kwa jina la OAG-MIS.
Mhe Rais Samia ameyasema hayo leo wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mawakili wa Serikali kabla ya kuzindua Chama cha Mawakili wa Serikali (Public Bar Association) uliofanyika kwenye Ukumbi wa Jakaya Kikwete Dodoma wenye Kauli mbiu isemayo, “Utekelezaji wa Majukumu Unaozingatia Sheria ni Nyenzo Muhimu kwa Maendeleo ya Taifa”.
“Amri inapotoka Wanasheria wajisajili na muda umetolewa kama mtu hajajisali awe na dharura ya maana sana, ama alikuwa mgonjwa hospitalini hawezi au alipokuwa hakuna mtandao hakupata taarifa kwa wakati lakini kama muda utapita na usajili hajafanya basi Mwanasheria Mkuu nakutaka kusimamia hilo”, amesema Mhe. Rais Samia
Amemtaka Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuwahimiza wale ambao bado hawajajisajili wajisajili kwenye mfumo wa OAG-MIS vinginevyo baada ya muda kupita hawatatambulika kama Mawakili wa Serikali na itabidi watafute sekta za nje wajisajili au kupewa msamaha na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Mhe. Rais Samia amepongeza uanzishwaji wa Chama cha Mawakili wa Serikali cha kitaaluma na kusema uwepo wake utasaidia zoezi la kuratibu utendaji kazi wa Mawakili wote wa Serikali walio katika utumishi wa umma nchini na mmepata mlezi mzuri Mwanasheria Mkuu wa Serikali anayeweza kuwasemea katika masuala yenu ya kitaaluma, kikazi, kinidhamu na kimaslahi.
“Lakini nimefurahishwa kusikia kwamba Chama hiki sasa kilichoundwa kitafanya kazi kwa karibu na Chama cha Mawakili cha Tanganyika (TLS), lakini pia nimefurahishwa na kusikia uhusiano wa karibu wa kazi baina yenu na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar”, amesema Mhe. Rais Samia
Aidha, amesema itakuwa ni rahisi kuwasiliana kupitia mfumo huo wa Mawakili wa Serikali ambao ameuzindua na kusema ni dhahiri maboresho hayo yataongeza ari na tija kwa Mawakili wa Serikali wanapotekeleza majukumu yao katika maeneo mbali mbali nchini.
Akimkaribisha Mhe. Rais Samia, Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesema mkutano huo ulitanguliwa na kikao kazi cha Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara, Taasisi, Idara na Halmashaurizote nchi nzima na kuelezwa kuhusu mpango wa kuanzisha Chama cha Mawakili wa Serikali.
Dkt. Ndumbaro amesema chama hiki kitakuwa kikisimamia masuala ya kitaaluma na masuala ya kimaadili ya Wanasheria na ni fursa nzuri ya kutoa changamoto za kimaadili ambazo zimekuwa zikiwakabili na itawezekana tu kama Mhe. Rais Samia atakubali ombi la kuzindua chama hicho.
“Mhe Rais Samia kupitia Chama cha Mawakili wa Serikali tunatarajia kwamba chama hiki kitaleta umoja wenye nguvu na jukwaa mahususi kabisa la kuishauri Serikali katika mambo mbalimbali ya kisheria na tunatarajia kwamba itakuwa ni sehemu ya majidiliano ya kisheria kwa wanasheria wa Serikali ambalo lilikosekana huko nyuma.
Amewakumbusha Mawakili wa Serikali kwamba kuwa Wakili wa Serikali ni heshima kubwa na heshima ya kuwa Wakili inaendana na wajibu hivyo wanapaswa kuitumikia Serikali ipasavyo, kutumia sheria kupunguza migogoro inayoweza kujitokeza ndani ya Serikali.
Awali Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Feleshi amewataka watendaji kuhakikisha wanawatumia vizuri wanasheria waliopo kwenye rejesta ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kupata ushauri kabla hajaingia kwenye mikataba au kabla ya kuvunja mikataba ili wazingatie kanuni na taratibu.
Mhe. Jaji Dkt. Feleshi amesema chama kitakuwa ni jukwaa la Mawakili kujadili masuala mbalimbali ya kisheria yakiwepo ya kimafunzo yanayohusiana na utoaji wa huduma za kisheria na kutatua malalamiko ya kisheria kutoka kwa wadu mbalimbali.
Naye Wakili wa Serikali kutoka Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Bw. Msalama Mkama ameishukuru Serikali kwa kuwa na maono ya mbali na kuanzisha Chama cha Mawakili wa Serikali ambacho kitakuwa kama jukwaa kwa Mawakili hao kujadili masuala yao ya msingi kwenye Sekta ya Sheria.
Bw. Mkama amesema kuwa chama hicho kitaiwezesha Serikali kuwaunganisha Mawakili na kujadili changamoto zao kwa pamoja na kuiwezesha Serikali kufahamu idadi na utendaji kazi wa Mawakili katika Wizara, Taasisi, Sekretariati za Mikoa na Halmashauri zote nchini.
“Chama kitawawezesha Mawakili kushirikishana katika ujuzi walio nao na kubadilishana uzoefu wa utendaji kazi katika kusimamia mashauri ya Serikali kutoka kwenye taasisi zao na pia kutatua changamoto walizonazo kwa kutumia uzoefu walio nao.
Mkutano huo umehudhuriwa na Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Boniphace Luhende, Mkurugenzi wa Mashtaka, Slyvester Mwakitalu, Viongozi waandamizi wastaafu wa Sekta ya Sheria nchini akiwemo Mtemi Andrew Chenge.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali

Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akisalimiana na Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Boniphace Luhende mara baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa mikutano wa Jakaya Mrisho Kikwete, Dodoma kwa ajili ya kuzindua Chama cha Mawakili wa Serikali.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akielekea kwenye banda la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa lengo la kuangalia namna Mfumo wa kuratibu taarifa za Mawakili wa Serikali unavyofanya kazi. Wa kwanza Kulia ni Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali mara baada ya kuzindua Chama cha Mawakili wa Serikali na mfumo wa kuratibu taarifa za Mawakili wa Serikali uliopo Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali jijini Dodoma. Wa kwanza kulia mstari wa nyuma kulia ni Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Boniphace Luhende
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali (waliosimama stari wa nyuma) walioshiriki mkutano na uzinduzi wa Chama cha Mawakili wa Serikali uliofanyika jijini Dodoma.

SERIKALI, SEKTA BINAFSI WAKUBALIANA KUBORESHA MIFUMO KUWAFIKIA DIASPORA

Written By CCMdijitali on Wednesday, September 28, 2022 | September 28, 2022

Mkurugenzi anayeshughulikia masuala ya Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi James Bwana ameeleza kuwa Serikali imejidhatiti kufanya maboresho ya mifumo ya Tehama katika sekta za umma na sekta binafsi ili kuhakikisha fursa mbalimbali zinazopatikana nchini zinawafikia diaspora kwa wakati.

Hayo yameelezwa katika siku ya pili ya mkutano wa wadau wa sekta za umma na binafsi uliojadili masuala mbalimbali kuhusu ushiriki wa Diaspora katika shughuli za maendeleo ya Taifa uliomalizika leo tarehe 27 Desemba 2022 Jijini Dodoma.

“Wadau wa mkutano huu wamepata fursa ya kushirikishana na kupeana uzoefu juu ya huduma mbalimbali wanazozitoa kwa diaspora, kutoa maoni ya namna bora ya kuboresha huduma na umuhimu wa taasisi kushirikiana ili kurahisisha utoaji wa huduma” alisema Balozi James

Miongoni mwa maeneo yaliyopendekezwa na wadau kwa ajili ya maboresho ni pamoja na: kuongeza kazi ya ukamilishwaji wa mapendekezo ya kupatikana kwa hadhi maalum kwa Diaspora, Uandaaji na ukamilishaji wa Sera na sheria ya Diaspora ya Tanzania, taasisi za fedha kuwa na huduma rafiki na zenye riba nafuu kwa Diaspora na ukamilishaji wa mfumo wa kidigitali wa kuhifadhi taarifa muhimu za watanzania wanaoishi na kufanya kazi nje ya nchi, ujulikanao kama “Diaspora Digital Hub”. Mfumo huu utawezesha kuwatambua Diaspora na mahitaji yao pamoja na kuongeza ubunifu katika utoaji huduma.

Maeneo mengine ni uharakishwaji wa mchakato wa kuwapatia Diaspora vitambulisho vya Taifa, kuwepo kwa siku maalum ya Diaspora ili kuwajengea uzalendo, Balozi za Tanzania nje ya nchi kusimamia kwa karibu changamoto mbalimbali za Diaspora, wadau kuwekeza zaidi katika kupata uzoefu kutoka mataifa mengine yaliyofanikiwa katika masula ya Diaspora, maboresho katika taratibu na sheria za ununuzi na umiliki wa ardhi na majengo, kuanzishwa kwa madawati maalum yanayohudumia Diaspora katika sekta za Umma na Binafsi hususan huduma za kidigitali.

Akifunga mkutano huo Naibu Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Diaspora, Ofisi ya Rais – Ikulu Zanzibar, Bi. Maryam Ramadhan Hamoud amewahakikishia wadau kuwa Serikali ya mapinduzi Zanzibar itaendelea kutoa ushirikiano na uzoefu wake katika hatua mbalimbali za uandaji wa sera na sheria ya Diaspora kwa upande wa Tanzania bara kwa kuwa tayari Tanzania-Zanzibar ilishakamilisha taratibu hizo.

Mkurugenzi wa masuala ya Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi James Bwana akiongea na wadau kwenye mkutano wa kujadili masuala yaushiriki wa Diaspora kwenye shughuli za maendeleo nchini uliomalizika tarehe 27 Septemba 2022 jijini Dodoma
Mwakilishi kutoka Benki ya CRDB Bw. Joseph Haule akichangia mada kwenye mkutano wa kujadili masuala yaushiriki wa Diaspora katika shughuli za maendeleo nchini uliokuwa ukiendelea jijini Dodoma
Mkutano wa kujadili masuala yaushiriki wa Diaspora katika shughuli za maendeleo nchini ukiendelea
Afisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushikiano wa Afrika Mashariki Bi. Semeni Nandonde akichangia jambo kwenye mkutano uliokuwa ukijadili masuala yaushiriki wa Diaspora katika shughuli za maendeleo nchini uliokuwa ukiendelea jijini Dodoma
Mkurugenzi wa masuala ya Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi James Bwana akifurahia jambo wakati wa mkutano wa kujadili masuala yaushiriki wa Diaspora kwenye shughuli za maendeleo nchini uliokuwa ukiendelea jijini Dodoma

SERIKALI KUPANGA MIKAKATI YA KUENDELEZA SEKTA YA SHERIA NCHINI

SERIKALI KUPANGA MIKAKATI YA KUENDELEZA SEKTA YA SHERIA NCHINI

Na Mwandishi Wetu, OWMS, Dodoma

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupanga mikakati ya kuendeleza Sekta ya Sheria nchini kwa ajili ya kuwatumikia watanzania. 

Hayo yameelezwa na Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Boniphace Luhende wakati akitoa salamu kwenye kikao kazi cha Wakurugenzi na Wakuu wa Vitengo vya Sheria wa kutoka Wizara mbalimbali, Taasisi za Serikali, Mashirika ya Umma na Halmashauri zote nchini 
Dkt. Luhende ameongeza kuwa kikao kazi hicho kimewakusanya viongozi hao ili kupanga mikakati ya kuendeleza Sekta hiyo ikiwa ni pamoja na kubadilishana uzoefu ili kupata wanasheria wabobezi ndani ya Serikali ili kuisaidia Serikali kutekeleza majukumu yake ambapo maelezo hayo yamejikita kwenye Kauli Mbiu ya Mwaka huu isemayo, 

“Utekelezaji wa Majukumu Unaozingatia Sheria ni Nyenzo Muhimu kwa Maendeleo ya Taifa.” 

Naye Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Feleshi ambaye ndiye muandaaji wa kikao kazi hicho alisema kuwa ni muhimu kwa viongozi hao kuelewa dira na dhima ya Ofisi wanazotumikia; kufanya tathmini nakujipima namna wanavyotekeleza majukumu; kufanya uchambuzi wa wadau wa ndani na nje ya taasisi wanayofanyia kazi; kuweka mikakati endelevu ya kujengeana uwezo; kuepuka kujenga uadui na makundi; kufurahia kukoselewa na kufanyia kazi maeneo waliyokosolewa; na kuwa wadilifu ili wawe na nguvu ya kuchukua hatua.

“Utumishi wa umma tunaoutaka kwenye Sekta ya Sheria ni kuhakikisha kuwa kila mtumishi wa umma wa kada ya sheria atumike kutokana na uwezo wake mahali alipo ambapo anaweza kuwa mwajiriwa wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali lakini akatumika kufanya kazi kwenye Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kuwa siku hizi tunasoma kuwa mahiri na sio kusoma bora tu kusoma na mpaka sasa tuna jumla ya Mawakili wa Serikali 2,661 ambapo kati ya hao Mawakili 18 wana shahada ya uzamivu, 789 wana shahada ya uzamili, 863 wana astashahada ya juu na 855 wana shahada ya kwanza ya masuala ya sheria kwa mujibu wa takwimu zilizopo kwenye Mfumo wa Taarifa wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu (OAG-MIS) ambapo Mawakili hao wamejisajiri,” amesema Mhe. Jaji Dkt. Feleshi.

Akizungumza kwa niaba ya viongozi waliotoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) ambao wameshiriki kikao kazi hicho, Shaban Ramadhan Abdallah, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesema kuwa wamekuja kujifunza ili nao waweze kuiga na Kwenda kutekeleza masharikiano hayo baina ya Ofisi hiyo ya SMZ na za Tanzania Bara
Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini, Slyvester Mwakitalu amesema kuwa baada ya kikao kazi hicho na Mkutano wa Mawakili wa Serikali utakaofanyika tarehe 29 na 30m Septemba, 2022 utawawezesha viongozi na washiriki kupata maarifa mapya pamoja na uzoefu kwa kuwa taasisi moja inafanya mambo yanayotekelezwa na taasisi nyingine kwa kuwa taasisi za Serikali zinafanya kazi kwa kutegemeana.

Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Boniphace Luhende akizungumza na Wakurugenzi na Wakuu wa Vitengo vya Sheria (hawapo pichani) kutoka Wizara mbali mbali, Taasisi za Umma, Mashirika ya Umma na Halmashauri zote nchini wakati wa kikao kazi kilichofanyika Jijini Dodoma.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji. Dkt. Eliezer Feleshi akifungua kikao kazi cha Wakurugenzi na Wakuu wa Vitengo vya Sheria (hawapo pichani) wa Wizara mbalimbali, Taasisi za Umma, Mashirika ya Umma na Halmashauri zote nchini kilichofanyika Jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Slyvester Mwakitalu, akizungumza na Wakurugenzi na Wakuu wa Vitengo vya Sheria (hawapo pichani) kutoka Wizara, Taasisi za Umma, Mashirika ya Umma na Halmashauri zote nchini wakati wa kikao kazi chao kilichofanyika Jijini Dodoma.

Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Boniphace Luhende (wa pili kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mawakili wa Serikali wa Mikoa mbalimbali kutoka Ofisi hiyo wakati wa kikao kazi cha Wakurugenzi na Wakuu wa Vitengo vya Sheria wa Wizara na Taasisi mbalimbali za Umma, Mashirika ya Umma na Halmashauri zote nchini kilichofanyika jijini Dodoma. Wa tatu kushoto ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji. Dkt. Eliezer Feleshi.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

Msemaji Mkuu wa Serikali azungumza siku ya Kimataifa ya Upatikanaji Habari kwa wote

Hatumzuii Mtu kuanzisha Televisheni ya Mtandaoni-Msigwa

Na Grace Semfuko, MAELEZO

Septemba 28, 2022

Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO Bw. Gerson Msigwa amesema Tanzania ni moja kati ya Nchi Duniani zenye vyombo vingi vya Habari na kwamba bado inaendelea kusajili vyombo hivyo ili viweze kuuhabarisha umma.

Amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha watanzania wanapata habari kupitia vyombo hivyo huku Waandishi nao, wanakuwa huru katika kukusanya, kuchakata na kusambaza habari za ukweli ambapo Sheria ya Huduma za Habari Namba 12 ya mwaka 2016 imeanisha masuala hayo.

Ameyasema hayo leo Septemba 28, 2022 Jijini Dar es Salaam aliposhiriki kwenye mahojiano katika kipindi cha Baragumu kinachorushwa na Televisheni ya Channel Ten ikiwa ni siku ya kimataifa ya upatikanaji wa habari kwa wote ambapo ameongeza kuwa, wingi huo wa vyombo vya habari umewekwa kwa makusudi ili watanzania wawe huru kupata habari huku waandishi nao waweze kufanya kazi zao kwa uhuru.

“Sisi Tanzania tumerahisisha sana, na nchi yetu ni moja kati ya nchi Duniani ambayo ina idadi kubwa ya vyombo vya habari, na tumefanya hivi makusudi ili watanzania wawe huru kupata habari, na Vyombo vya habari pia pamoja na waandishi wawe huru kufanya kazi zao, hivi ninavyozungumza nchi yetu ina idadi ya magazeti na majarida yaliyosajiliwa 303, TV za Mtandaoni zaidi ya 667 Redio za mtandaoni 23, redio za kawaida zaidi ya 210, na tunaruhusu hata leo ukitaka kuanzisha redio, unaanzisha, sasa zipo nchi ambazo zina vyombo vya habari havizidi hata vitano” amesema Bw. Msigwa.

Amesema jukumu la Serikali ni kufungua milango ya kuanzisha vyombo vya habari ambapo mtu yeyote anaruhusiwa kuanzisha ili mradi tu afuate sheria. 

“Kuna sheria kwa mfano ya huduma za habari namba 12 ya mwaka 2016 tumeiweka pale kwa ajili ya kusimamia sekta ya habari lakini wakati huo huo tunawasikiliza wadau, mfano hivi karibuni Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan alishatoa maelekezo, Mheshimiwa Waziri Nape alishatoa maelekezo anasimamia utekelezaji” amesema Bw. Msigwa.

Mwisho. 

Viongozi Toeni Taarifa kuhusu Mafanikio ya Serikali-Msigwa

Viongozi Toeni Taarifa kuhusu Mafanikio ya Serikali-Msigwa 

Na Grace Semfuko, MAELEZO

Septemba 28, 2022

Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO Bw. Gerson Msigwa amewataka Viongozi wa Taasisi za Serikali Nchini, kutoa taarifa za mafanikio ya utendaji kazi wa taasisi hizo kwa Vyombo vya Habari, ili kuwaonesha Wananchi maendeleo yanayofanywa na Serikali yao.

Amesema yapo mambo mengi yanayofanywa na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan na hivyo ni muhimu kuyaweka wazi ili wananchi wayaone.

Ameyasema hayo leo Septemba 28, 2022 Jijini Dar es Salaam aliposhiriki mahojiano katika kipindi cha Baragumu kinachorushwa na Televisheni ya Channel Ten ikiwa ni Siku ya Kimataifa ya Upatikanaji wa Habari kwa Wote, na kubainisha kuwa wapo baadhi ya watendaji wanaokwepa kutoa taarifa za mafanikio ya taasisi zao kwa wananchi na kuwataka kuzitoa taarifa hizo.

“Wapo baadhi ya viongozi ni wakwepaji kuja kutoa taarifa kwenye vyombo vya Habari Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema, Mhe Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye ametoa maelekezo na Mimi Mwenyewe Msemaji Mkuu wa Serikali nimesema mara nyingi kwamba taasisi zote zinatakiwa kutoa taarifa kwa wananchi, zinatakiwa kuja kutoa ufafanuzi mbalimbali kwenye vyombo vya habari, wasije tu kwenye kampeni za kazi zao, wakati wote waje waseme wanafanya nini” amesema Bw. Msigwa.

Aidha amewataka Maafisa Habari wa Taasisi hizo pia kushirikiana na vyombo vya habari katika kutoa taarifa muhimu zinazohusu maendeleo ya taasisi zao.

“Lakini kwa kutambua kuna changamoto ya baadhi ya Viongozi kuwa na majukumu mengi, Serikali iliunda vitengo vya habari na nyie vyombo vya habari mkihitaji habari mnapaswa kuwasiliana nao ili muweze kupata taarifa na kuzitoa” amesema Bw. Msigwa.

Katika hatua nyingine Bw. Msigwa amewataka Wamiliki wa vyombo vya habari nchini, kuwalipa mishahara waandishi wao ili kuwajengea weledi katika kufanikisha kazi zao za kila siku.

“Nitoe wito kwa wamiliki wa vyombo vya habari tujitahidi sana kuwalipa watumishi tulionao ambao ni Waandishi wa Habari, wakifanya kazi zao walipwe kwa sababu tumepata hizo changamoto, na vyombo vya habari vinafanya kazi, waandishi wa habari hawana mishahara, wanategemea wakienda kufanya kazi kwenye taasisi fulani ndio walipwe posho, sasa hii sio sawa, ni vizuri vyombo vya habari vikawa na mipango madhubuti ya kuhakikisha waandishi wa habari wanapofanya kazi zao wanalipwa mishahara ili wafanye kazi kwa weledi” amesema Bw. Msigwa.

Mwisho.

RAIS WA KENYA WILLIAM RUTO ATANGAZA BARAZA LAKE LA KWANZA LA MAWAZIRI

Written By CCMdijitali on Tuesday, September 27, 2022 | September 27, 2022

Nairobi, Kenya.

Rais wa Kenya William Ruto ametangaza Baraza lake la kwanza la Mawaziri saa chache baada ya kufanya kikao na Baraza la Mawaziri waliohudumu chini ya Utawala wa Serikali ya Uhuru Kenyatta.

Taarifa zimesema, katika Baraza hilo, Ruto amemteua Kiongozi wa Chama cha Amani National Congress, Musalia Mudavadi kuwa Waziri Kiongozi. 

Mudavadi atamsaidia Rais na Naibu Rais, Rigathi Gachagua kufuatilia shughuli katika wizara za Serikali.

Wengine aliowateua katika Baraza hilo ni;

1. Waziri wa Usalama wa Ndani – Prof Kithure Kindiki

2. Waziri wa Masuala ya Kigeni – Dkt Alfred Mutua

3. Waziri wa Elimu – Ezekiel Machogu

4. Waziri wa Kawi – Davis Chirchir

5. Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki – Rebecca Miano

6. Waziri wa Ulinzi – Aden Duale

7. Waziri wa Utalii – Penina Malonza

8. Waziri wa Afya – Susan Nakumicha Wafula

9. Waziri wa Michezo – Ababu Namwamba

10. Waziri wa Ardhi – Zacharia Mwangi Njeru

11. Waziri wa Leba – Florence Bore

12. Waziri wa Biashara – Moses Kuria

13. Waziri wa Maji – Alice Wahome

14. Waziri wa Mazingira – Roselinda Soipan Tuya

15. Waziri wa Fedha – Profesa Njuguna Ndung’u

16. Waziri wa Habari na Mawasiliano – Eliud Owalo

17. Waziri wa Kilimo – Franklin Mithika Linturi

18. Waziri wa Huduma za Umma, Jinsia na Usawazishaji – Aisha Jumwa

19. Waziri wa Barabara – Kipchumba Murkomen

20. Waziri wa Sekta ya Biashara Ndogo na za Wastani (SMEs) – Simon Chelugui

21. Waziri wa Uchimbaji Madini – Salim Mvurya

22. Mshauri wa Shirika la Masuala ya Wanawake – Harriet Chigai

23. Mshauri wa Masuala ya Usalama wa Ndani – Monica Juma

24. Mwanasheria Mkuu – Justin Muturi

25. Katibu katika Baraza la Mawaziri – Mercy Wanja.

Rais wa Kenya William Ruto.

SERIKALI YAAHIDI KUJENGA VITUO 15 VYA KUPOZA UMEME.

Written By CCMdijitali on Monday, September 26, 2022 | September 26, 2022

SERIKALI YAAHIDI KUJENGA VITUO 15 VYA KUPOZA UMEME. 

Na Godfrey Mwemezi, Dodoma. 

Serikali inaendelea na mchakato wa kujenga vituo vya kupoza umeme katika maeneo mbalimbali nchini kwa lengo la kuimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika. 

Vituo 15 vya kupoza umeme vinatarajiwa kujengwa kwa mwaka 2022/2023 na vipo kwenye mpango wa gridi imara, ambapo taratibu za kuwapata wakandarasi wajenzi wa vituo hivyo zinaendelea. 

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato alipokuwa akizungumza kwenye semina ya wabunge wa kamati ya Nishati na Madini iliyofanyika katika ukumbi wa jeongo la Osha Jijini Dodoma, Septemba 24, 2022. 

Alisema serikali imetenga sh. bilioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya kupoza umeme katika wilaya ya Mkuranga, Tunduru, Mpanda, Mlele, Sikonge, Uvinza, Urambo, Ngara, Handeni, Bariadi, Ukerewe, Lushoto, Rombo, Kilindi na Kishatu ambapo ujenzi wa vituo hivyo utaanza mwezi Oktoba mwaka huu. 

Byabato alisema Shirika la Umeme nchini (TANESCO) limefanya upembuzi yakinifu na kubaini maeneo yenye mahitaji makubwa ambayo vituo hivyo vya kupoza umeme vitajengwa. 

"Serikali imezingatia zaidi maeneo yenye changamoto kubwa ya upatikanaji wa umeme wa uhakika na hivyo Wizara tumeamua kuanza na hayo ili wananchi wapate umeme wa uhakika," alisema Byabato. 

Alisema kuwa mwaka 2023/2024 TANESCO itaendelea kujenga vituo vya kupoza umeme kupitia mpango wake wa gridi imara katika maeneo yenye mahitaji ya kati ambayo hayakufikiwa katika awamu ya kwanza ya mradi. 

"Lengo la Serikali ya awamu ya sita ni kuhakikisha kila mtanzania mwenye uhitaji wa kupata huduma ya umeme anafikiwa na huduma hiyo," alisema Byabato. 

Pia Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Mhe. Felchesmi Mramba, alisema kuwa serikali inaendelea na mikakati mbalimbali ili kuhakikisha inasimamia vyanzo vya kuzalisha umeme ukiwemo mradi wa kuzalisha umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) pamoja na Ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha chalinze ambacho Ujenzi wake unaendelea vizuri. 

Kadhalika Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya Nishati na Madini Dunstan Kitandula, alishauri serikali kuongeza usimamizi wa ujenzi wa mradi wa kufua umeme wa maji ya Julius Nyerere ili uweze kukamilika.

BALOZI MULAMULA ASHIRIKI MKUTANO WA 12 WA MAWAZIRI MARAFIKI WA UN WA USULUHISHI

Written By CCMdijitali on Thursday, September 22, 2022 | September 22, 2022

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe Balozi Liberata Mulamula  ameshiriki Mkutano wa 12 wa Mawaziri Marafiki wa Umoja wa Mataifa wa Usuluhishi unaofanyika sambamba na Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York. 

Akizungumza katika mkutano huo Balozi Mulamula amesema usuluhishi ni njia muhimu  katika kutatua changamoto za migogoro duniani na kuusihi Umoja wa Mataifa kuliingiza suala la usuluhishi katika mifumo ya utatuzi wa migogoro ya Umoja wa Mataifa.

Amesema usluhishi ukiingizwa katika mifumo ya utatuzi ya migogoro ya Umoja huo utasaidia shughuli za upatanishi na utatuzio wa migogoro na hivyo kuufanya Umoja huo kufikia lengo la utatuzi wa migogoro na kuifanya dunia kuwa sehemu salama .

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe Balozi Liberata Mulamula  akishiriki Mkutano wa 12 wa Mawaziri Marafiki wa Umoja wa Mataifa wa Usuluhishi unaofanyika sambamba na Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe Balozi Liberata Mulamula  akijadiliana jambo na washiriki wa Mkutano wa 12 wa Mawaziri Marafiki wa Umoja wa Mataifa wa Usuluhishi uliofanyika  jijini New York.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe Balozi Liberata Mulamula  akiwa katika Mkutano wa 12 wa Mawaziri Marafiki wa Umoja wa Mataifa wa Usuluhishi ujijini New York.
Wenyeviti wenza wa Mkutano wa 12 wa Mawaziri Marafiki wa Umoja wa Mataifa wa Usuluhishi Uturuki na Finland wakiwasikiliza washiriki wa kikao hicho

Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango ahutubia Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Philip Mpango  ametoa wito kwa mataifa ulimwenguni kuungana katika kutoa mchango kwa mfuko wa kimataifa wa kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria (Global Fund) ili uweze kufikia lengo la kukusanya kiasi cha dola za kimarekani bilioni 18 zitakazotumika kutokomeza magonjwa hayo duniani kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.
 
Makamu wa Rais ametoa wito huo wakati akihutubia Mkutano wa saba wa kuwezesha mfuko wa kimataifa wa kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria (Global Fund) uliofanyika New York nchini Marekani. Amesema Migogoro ya sasa ya kimataifa imepunguza juhudi za kurejesha uchumi wa nchi nyingi ulioathirika na janga la UVIKO19 na kuongeza changamoto mpya katika kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu hivyo hakuna budi wote kwa pamoja kuona haja ya kuunga mkono kazi nzuri ya Mfuko huo wa Kimataifa ili kuendeleza mafanikio katika kukabiliana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria.
 
Aidha Makamu wa Rais amesema Tanzania inathamini ushirikiano wa kihistoria uliopo baina yake na Global Fund, ambao umekuwa na matokeo chanya yaliopelekea kupunguza idadi ya vifo kwa magonjwa ya Ukimwi ,Kifua Kikuu na Malaria. Ameishukuru Bodi ya Global Fund kwa kuinga mkono Tanzania kwa miaka mingi pamoja na kuzishukuru na kuzipongeza Serikali, Mashirika, Taasisi na watu binafsi wote kwa michango yao kwa Mfuko huo kwa kipindi cha miaka 20 iliyopita.
 
Makamu wa Rais amesema Tanzania imejitolea kufikia lengo la kimataifa la kukomesha ugonjwa wa Ukimwi ifikapo 2030 kwa kutumia teknolojia mpya na mikakati ya kibunifu. Ameongeza kwamba licha ya mafanikio yaliopatikana katika kukabiliana na Ugonjwa wa Ukimwi , Kifua Kikuu na Malaria , bado Tanzania inakabiliwa na changamoto ya maambukizi mapya hususani kwa vijana wenye umri wa miaka 15-24. Pia amesema katika kukabiliana na Kifua Kikuu bado taifa linakabiliwa na vikwazo kama vile upatikanaji mdogo wa huduma za uchunguzi wa ugonjwa huo hasa katika maeneo yenye watu muhimu na walio hatarini ikiwa ni pamoja na wafanyakazi wa migodini, wavuvi na wafungwa.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Philip Mpango amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) Bi. Samantha Power, Mazungumzo yaliofanyika Jijini New York, Marekani.

Katika Mazungumzo hayo Makamu wa Rais ametaja juhudi mbalimbali zinazofanywa zinazofanywa na serikali ya Awamu ya Sita katika kuboresha sekta ya afya hususani Afya ya mama na mtoto kwa kuanzisha programu mbalimbali za kuokoa Maisha ya Mama na mtoto kwa kushirikiana na wadau ikiwemo programu ya M- Mama. Amesema serikali imeendelea kushirikiana na wadau wa afya katika kuboresha huduma za afya na kuongeza juhudi katika ujenzi wa miundombinu ya afya ikiwemo vituo vya afya pamoja na hospitali.
 
Makamu wa Rais ameishukuru serikali ya Marekani kwa kushirikiana na Tanzania katika kupambana na Uviko 19 kwa kutoa msaada wa dozi milioni  5 za chanjo ya ugonjwa huo.
 
Amesema serikali imeweka mkazo katika kuboresha mazingira ya uwekezaji kwa kuweka sera rafiki na kuunganisha taasisi zinazohusika na uwekezaji ili kuondoa urasimu kwa wenye nia ya kuwekeza Tanzania. Pia Makamu wa Rais ametaja juhudi zinazofanywa katika kuboresha miundombinu ya usafirishaji pamoja na nishati ili kuwa na mazingira rafiki kwa wawekezaji.
 
Katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, Makamu wa Rais amekaribisha USAID kushirikiana na Tanzania katika kupata teknolojia rafiki ya mazingira itakayowezesha wananchi kuendelea na shughuli za kiuchumi na kijamii bila kuathiri mazingira.
 
Kwa upande wake Mkuu wa Shirika la Maendeleo  ya Kimataifa la Marekani (USAID) Bi. Samantha Power amesema Shirika hilo litaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuunga mkono juhudi mbalimbali za mageuzi hususani katika sekta ya afya na kilimo.
 
Bi Samantha ameongeza kwamba shirika hilo linaiunga mkono Tanzania katika kuifanya kuwa tegemeo la upatikanaji wa chakula kwa kuwezesha kupatikana kwa mbolea ya gharama nafuu itakayosaidia kuinua sekta ya kilimo.

Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link