Uongozi wa Wilaya ya Arusha ukiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Said Mtanda kwa kushirikiana na Uongozi wa Ubalozi wa Rwanda Nchini unoongozwa na Meja Jenerali Charles karamba katika kudumisha zoezi la Usafi katika Jiji la Arusha Leo wameongoza zoezi la kufanya Usafi katika maeneo mbalimbali yakiwemo maeneo ya Soko kuu pamoja na stendi kuu ya mabasi Jijini humo.
-
Maadhimisho hayo ya Siku ya Usafishaji wa Mazingira Duniani Jijini Arusha yalihudhuriwa na viongozi wengine mbalimbali akiwemo Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Mhe. Maximillian Iranqhe, Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Bw. Hargeney Chitukuro sambamba na Viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Jiji la Arusha.