Home » » WAZIRI DKT MABULA AMSHUKURU RAIS SAMIA KWA PESA ZA PROGRAMU YA UPIMAJI ARDHI

WAZIRI DKT MABULA AMSHUKURU RAIS SAMIA KWA PESA ZA PROGRAMU YA UPIMAJI ARDHI

Written By CCMdijitali on Wednesday, September 14, 2022 | September 14, 2022

SEPT 13, 2022 MWANZA

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe Samia Suluhu Hassan kwa  kuiwezesha wizara yake kupata fedha kiasi cha Shilingi Bilioni 50 kwa ajili ya programu ya kupanga, kupima na kumilikisha ardhi nchini.

Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango iliipatia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi shilingi bilioni 50 kwa ajili ya kuzikopesha Halmashauri 55 kutekeleza Programu ya Kupanga, Kupima na Kumilikisha Ardhi nchini. 

Alisema, utolewaji wa kiasi hicho cha fedha kumewezesha mkoa wa Mwanza kupatiwa  shilingi Bilioni 4.691 zilizosaidia kutekeleza miradi ya kupanga, kupima na  kumilikisha ardhi katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo. 

Dkt Mabula ametoa shukran hizo tarehe 13 Septemba 2022 mbele ya Makamu wa Rais Mhe. Dkt Phillip Isdori Mpango wakati wa uzinduzi wa stendi mpya na ya kisasa ya mabasi na maegesho ya malori iliyopo eneo la  Nyamhongolo wilayani  Ilemela.




Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link