MALARIA BADO NI CHANGAMOTO NCHINI – WAZIRI UMMY
Na WAF-DODOMA
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema ugonjwa wa Malaria bado ni changamoto Tanzania na unaipa mzigo mkubwa Serikali katika utoaji wa huduma za afya.
Waziri Ummy amesema hayo leo jijini Dodoma wakati akifunga Mradi wa Okoa Maisha uliokua unatekelezwa katika Mikoa mbalimbali nchini hususan ile yenye maambukizi makubwa na kuzindua miradi miwili ya Shinda Malaria na Dhibiti Malaria inayofadhiliwa na Program ya Malaria ya Rais wa Marekani (PMI) unaogharimu Shilingi Bilioni 45 katika kipindi cha miaka minne.