Home » » TIC yanadi fursa za Uwekezaji za Tanzania Nchini Ureno.

TIC yanadi fursa za Uwekezaji za Tanzania Nchini Ureno.

Written By CCMdijitali on Sunday, October 23, 2022 | October 23, 2022

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimeshiriki katika kunadi fursa mbalimbali za uwekezaji zinazopatikana hapa nchini kupitia kongamano la Uwekezaji kati ya Tanzania na Ureno lilifanyika jijini Lisbon Ureno leo Alhamisi tarehe 20 Oktoba, 2022 .

Kongamano hilo ambalo limeandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa Afrika Mashariki, Wizara ya Biashara za Kimataifa na Uwekezaji wa Nje ya Ureno, TIC na Taasisi inayohamasisha biashara na Uwekezaji ya Ureno (AICEP Portugal Global). 

Kongamano limehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Tanzania na Ureno wakiongozwa na Mhe. Dkt. Stagomena Lawrence Tax, Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mhe. Bernado Ivo Cruz, Waziri wa Nchi, Biashara za Kimataifa na Uwekezaji kutoka Nje. Kongamano hilo lilihudhuriwa na wawekezaji zaidi ya 50 chini ya mwavuli wa AICEP Portugal Global taasisi inayotekeleza majikumu kama ya TIC nchini Ureno.

Kongamano hilo ni mojawapo ya kazi katika ratiba ya ziara ya kikazi ya Mhe Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Nchini Ureno katika mikakati na juhudi zinazoendelea za Wizara hiyo katika kuhamasisha Uwekezaji kupitia Diplomasia ya Uchumi. 

Katika ziara hiyo, TIC inawakilishwa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uhamasishaji Uwekezaji Bw, Revocatus Rasheli ambaye alitoa mada kuhusu mazingira ya uwekezaji na fursa zilizopo katika sekta za kimkakati hapa nchini pamoja na kuwasilisha “Offer” kwa wawekezaji wa Ureno ya miradi zaidi ya 130 ya uwekezaji iliyofungashwa na TIC kutoka kwa wadau mbalimbali wa sekta ya Umma na Binafsi inayotafuta mitaji, teknolojia, ujuzi nk ili kuitekeleza kwa ufanisi. 

Aidha, TIC imefanya mazungumzo na AICEP Portugal Global kwa lengo la kuwa na makubaliano ya mashirikiano yanayolenga katika kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo Tanzania na kuwasaidia wawekezaji wa Ureno wanaopanga kuwekeza Tanzania kupata taarifa na taratibu za uwekezaji nchini.

Lisboa, Portugal 20 Oktoba, 2022










Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link