Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais( Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt Selemani Jafo ameshiriki katika zoezi la upandaji miti lililofanyika katika shule ya Msingi Mtoni iliyopo katika Wilaya ya Bagamoyo.
Akiwa shuleni hapo amepongeza Benki ya Standard Chattered ambao ndiyo waandaaji na wasimamizi wakubwa wa tukio hilo la upandaji miti katika shule hiyo.
“Nawapongeza sana benki ya Standard Chattered kwa kunialika kuwa Mgeni Rasmi katika shughuli hii ya upandaji miti ambayo ni mwendellezo wa juhudi katika kuendelea kutunza na kuhifadhi mazingira kwa kupanda miti”. Mhe Dkt Jafo
Aidha ameziagiza Halmashauri zote Nchini ambazo hazijafikia malengo ya upandaji miti kama ilivyokua imeelekezwa awali kuhakikisha wanapanda miti na kufanikisha azma hiyo ya Serikali ya ukupanda miti kwa wingi katika kila Halmashauri Nchini ili kuweza kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
“Naagiza Halmashauri zote kuhakikisha zinafikia malengo ya kupanda miti ili kuweza kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Mabadiliko ya tabianchi ni changamoto kubwa inayoikabili dunia kwani husababisha, ukame, kuongezeka kwa kina cha bahari na maziwa”. Mhe Dkt Jafo
Naye Mkurugenzi wa Standard Chattered Bwana Herman Kasekende amesema watendelea kuunga mkono juhudi za Serikali kwa kusimamia zoezi la upandaji miti katika mashule mbalimbali ili kusaidia kutunza na kuhifadhi mazingira.
#Kaziiendelee
#MheDktJafo
#Zoeziendelevulaupandajimiti
#MitiRafikikwaMazingira
#VivulinaMatundaMengineyo
#KupambanaMabadilikoyaTabianchi
#DktJafoktkMazingira 1
#Endeleakuupigamwingi
#SSH2025🇹🇿
#MunguIbariki🇹🇿