Home » » UTEKELEZAJI WA ILANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

UTEKELEZAJI WA ILANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

Written By CCMdijitali on Wednesday, October 12, 2022 | October 12, 2022

📍 Igunga, Tabora

"SERIKALI YA AWAMU YA SITA YA CCM IMETENGA BILIONI 21 ZA KUNUFAISHA WANANCHI KWA MAJI YA ZIWA VICTORIA"

Serikali ya awamu ya Sita ya Chama Cha Mapinduzi inayoongozwa na Mwenyekiti wetu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan imetenga Shilingi Bilioni Ishirini na Moja kuweza kusambaza Maji ya Ziwa Viktoria katika Kata za Jimbo la Igunga, Wilayani Igunga.

Mradi huo wa Upanuzi umekabidhiwa kwa Mkandarasi wa maji ambae tayari ameingia 'SITE' na kuanza kazi ya Uchimbaji mitaro, kulaza Bimba na kuanza kuunganisha katika Miradi ya Umma, Taasisi za Umma (Shule, Hospitali, Misikiti na Makanisa) pamoja na Makazi ya watu chini ya Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA).

Pichani, Mbunge wa Jimbo la Igunga Mhe. Nicholaus George Ngassa ameambatana na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Waheshimiwa Madiwani, Wahandisi wa Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA) na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kumkabidhi eneo la mradi (site) Mkandarasi kwa ajili ya kufanya upanuzi wa mradi wa Maji ya Ziwa Victoria kutoka Igogo (Nanga) kwenye Bomba Kuu. 

Sehemu zitakazonufaika ni Vijiji vya Kata za Mwamashiga, Mbutu, Kining'inila, Isakamaliwa, Mwamakona, Igurubi na Kinungu na kusababisha Mradi wa Maji ya Ziwa Viktoria kuzifikia Kata nyingi za Wilaya ya Igunga.

Imetolewa na:
Ofisi ya Katibu Itikadi na
Uenezi Wilaya ya Igunga

11 Oktoba, 2022








Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link