TFS kutumia mikoko ya Tanga kuzalisha asali
Na Mashaka Mgeta, TANGA
Wakala wa Misitu (TFS) kupitia Shamba la Nyuki Mwambao wilayani Handeni, umeazimia kutumia maeneo ya ukanda wa mikoko, kufuga nyuki ili kuzalishaji asali itakayokidhi lengo la kufikia tani 50 kwa mwaka 2023/2024.
Afisa Nyuki Msaidizi katika Shamba la Nyuki Mwambao, Nkwimba Maige, ameyasema hayo kwenye kikao cha wataalamu wa uvuvi na nyuki mkoani Tanga, kilichoitishwa na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Waziri Kindamba.
Maige amesema Shamba la Nyuki Mwambao lenye maeneo ya uhifadhi katika kata za Kabuku na Kang’ata wilayani Handeni, limeyapitia maeneo ya ukanda wa mikoko kwenye wilaya za Pangani, Tanga na Mkinga na kubaini kuwa yanafaa kwa uzalishaji mkubwa wa asali.
‘’Sasa tunakwenda kuweka mizinga 140 ya awali wakati tukisubiri mingine 800…lengo letu ni kwamba, asali itakayopatikana kwenye maeneo hayo ichangie kufikia lengo la uzalishaji wa tani 50 kwa mwaka huu wa fedha,’’ amesisitiza zaidi Maige
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Kindamba amesema asali na mazao mengine ya baharini na kwenye misitu, ni miongoni mwa rasilimali zinazopewa kipaumbele kupitia mikakati ya uwekezaji na kukuza uchumi wa mkoa huo.
Mhe. Kindamba amesema, azma ya kuwekeza mizinga ya nyuki kwenye maeneo ya mikoko, itasaidia kuibua fursa kubwa za kiuchumi zitakazoacha alama ya mafanikio mkoani humo.
Amesema ili kutoa hamasa kubwa kwa wakazi wa mkoa huo kujihusisha na uzalishaji wa asali, anatafuta maeneo yakiwamo ya ukanda wa mikoko na mashamba ya mkonge yenye muda mrefu, ili awekeze katika ufugaji wa nyuki.
Naye Mhifadhi Msaidizi wa TFS wilayani Tanga, Issa Mziray amesema eneo la hifadhi ya mikoko lina ukubwa wa hekta 9,501 ambapo Tanga ina hekta 2,966, Mkinga (4813) na Pangani (1,722).
@wazirikindamba
@tanzania_forest #tanzaniaforestservices
@matukio_tanga @tanga_jiji @ccm_dijitali @wizarayamaliasilinautalii @wizara_ya_kilimo @michuzijr @millardayo @
Home »
MIKOANI
» "asali na mazao mengine ya baharini na kwenye misitu, ni miongoni mwa rasilimali zinazopewa kipaumbele kupitia mikakati ya uwekezaji na kukuza uchumi Mkoani Tanga.”- RC KINDAMBA
"asali na mazao mengine ya baharini na kwenye misitu, ni miongoni mwa rasilimali zinazopewa kipaumbele kupitia mikakati ya uwekezaji na kukuza uchumi Mkoani Tanga.”- RC KINDAMBA
Written By CCMdijitali on Friday, September 22, 2023 | September 22, 2023
Labels:
MIKOANI