Na. Chrispin Kalinga - Njombe
Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya DP World ya Dubai Sultan Ahmed bin Sulayem mara baada ya kusaini Mkataba wa Uendeshaji wa Gati namba 4 mpaka 7 za Bandari ya Dar es Salaam Jana Oktoba 22,2023 alianza safari kwenda Mkoa wa Njombe kwa lengo la kutazama fursa mbalimbali za uwekezaji.
Leo Oktoba 23, 2023 amekutana na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi. Kissa Gwakisa na viongozi wengine wamekutana na kufanya mazungumzo katika Uwanja wa Ndege wa Mkoa wa Njombe.
Pamoja na Mambo mengine wamejadili kuja kufanya uwekezaji kwenye eneo la Utalii,Ujenzi wa Hotel kubwa yenye hadhi ya nyota 5, Kilimo cha chai na mazao ya Miti pamoja na Uwekezaji mkubwa kwenye eneo la Madini ya Chuma na Makaa ya Mawe.
"Ninamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dokta Samia Suluhu Hassan kwa kufungua fursa za kiuwekezaji nchini kwetu Tanzania, Leo hii muwekezaji mkubwa katika bandari yetu ya Tanzania amefika Mkoani Njombe akiongozana na mfanyabiashara mkubwa kwenye Mkoa wetu akitokea nchini kenya Bw. David Lang'ati na ameahidi kuwa atafanya uwekezaji kwenye eneo la Ujenzi wa Hotel kubwa za Kitali, lakini pia tumetumia nafasi hii kama Mkoa kumkaribisha kwenye uwekezaji kwenye eneo la Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Mkoa wa Njombe". Alisema Mhe. Mtaka