Home » » ZIARA YA KATIBU TAWALA MKOA WA SONGWE Bi HAPPINESS SENDEDA

ZIARA YA KATIBU TAWALA MKOA WA SONGWE Bi HAPPINESS SENDEDA

Written By CCMdijitali on Monday, October 23, 2023 | October 23, 2023

ZIARA YA KATIBU TAWALA MKOA WA SONGWE Bi HAPPINESS SENDEDA YA UKAGUZI WA MIRADI YA MAENDELEO NA KUSIKILIZA KERO ZA WATUMISHI INAENDELEA WILAYA YA MBOZI.

Katibu Tawala Mkoa wa Songwe (RAS), Bi Happiness Seneda


Katibu Tawala Mkoa wa Songwe (RAS), Bi Happiness Seneda Amendelea na ziara ya kukagua na kufanya tathimini ya miradi ya maendeleo na kusikiliza kero za watumishi katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi .

Katika Ziara hiyo ya ukaguzi na tathimini ya miradi ya maendeleo kwa robo ya kwanza imeanza imeendelea leo Jumatatu Oktoba 23, 2023. Miongoni mwa miradi aliyotembelea RAS Seneda ni pamoja na umaliziaji boma la zahanati ya Chizumbi, Zahanati ya Ipunga na jengo la CTC Zahanati ya Ihanda.

Pia, katika ziara hiyo Katibu Tawala Bi. Happiness Seneda ambaye ameambatana na Sekretarieti ya Mkoa amekagua miundombinu ya maji safi katika Zahanati ya Hanseketwa, boma la Zahanati Kilimampimbi, ujenzi wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, jengo la uchunguzi Saratani ya shingo ya kizazi pamoja na ukarabati wa wodi ya magonjwa ya mlipuko pamoja na baadhi ya shule mpya, nyumba za walimu na ujenzi wa barabara.













@happinessseneda 
@mbozidc
Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link