Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza kwenye Mkutano wa 19 wa Umoja Wakuu wa Shule za Sekondari za Umma na Binafsi, kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma, Desemba 12, 2024
Akizungumza kwenye mkutano huo, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Serikali inatambua kazi kubwa inayofanywa na walimu wote nchini katika kuhakikisha sekta ya elimu inaendelea kufanya vizuri.