Home » , » MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR- UFUNGUZI WA TAWI LA BANK YA NMB- WETE PEMBA

MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR- UFUNGUZI WA TAWI LA BANK YA NMB- WETE PEMBA

Written By CCMdijitali on Friday, January 10, 2025 | January 10, 2025

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla amesema ufunguzi wa Tawi la Benki ya NMB Wete Pemba ni hatua nyengine muhimu kwa Benki na Serikali zote mbili kufanikisha adhma ya upatikanaji wa huduma za kifedha kwa kila kona ya Tanzania hususan katika maeneo ya Vijijini.

 

Ameyasema hayo katika hafla ya uzinduzi wa Tawi la Benki ya NMB Wete Kisiwani Pemba ikiwa ni muendelezo wa shamra shamra za kutimia miaka 61 ya  Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

 

Amesema kwa kipindi kirefu wakaazi wa Wete na maeneo jirani ambao ni wateja wa Benki ya NMB walikuwa wanategemea zaidi mawakala kupaata huduma za kibenki zilizohotaji matawi ya benki ama kulazimika kusafiri masafa ya mbali kufata huduma hizo jambo ambalo lilihatarisha usalama wao na fedha zao .

 

Makamu wa Pili wa Rais amesema Benki ya NMB imefanya uwekezaji mkubwa katika Teknolojia ambao umerahisisha upatikanaji wa huduma za Kibenki ambapo kwa sasa wateja wa NMB wanaweza kutumia simu zao za mkononi kufanikisha miamala ya kibenki na kupitia mawakala zaidi ya elf 50 wanaendelea kuwawezesha wateja kupata hiduma kwa karibu na nafuu zaidi.

 

Aidha, Mhe.Hemed amefahamisha kuwa NMB ni mdau mkubwa wa Serikali katika kufanikisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii kupitia uwekezaji katika sekta ya kilimo na Biashara ambapo amewataka Benki ya NMB kuendelea kuekeza katika maeneo muhimu ikiwemo kuongeza matawi na Teknoloji ili kuweza kufikia adhma ya Serikali ya Awamu ya Nane (8) ya kuleta mageuzi ya kiuchumi na kijamii na kuahidi kuwa Serikali itaendelea kutoa ushirikiano ili kuhakikisha Sekta za kibenki nchini zinatanua wigo wa utowaji wa huduma bora kwa wananchi.

 

Sambamba na hayo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema ni vyema wananchi wakatambua kuwa ili Taifa lifanikiwe zaidi kimaendeleo ni lazima kuwepo na Amani na Utulivu hivyo amewataka wanachi kuendelea kuitunza Amani na Mshikamano uliopo katika kipendi cha kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

 

Nae Waizi wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Mhe. Dkt Saada Mkuya Salum amesema Benki ya NMB imekuwa ikitoa ushirikiano mkubwa kwa Serikali katika kutoa huduma mbali mbali za jamii pamoja na  kutoa mikopo kwa Serikali kwa ajili ya kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo Nchi.

 

Dkt. Saada amesema uzinduzi wa Tawi la Benki ya NMB ndani ya Mkoa wa Kaskazini Pemba kutawanufaisha na kuwasaidia wanawake na wajasiri amali wadogo wadogo kupitia huduma mbali mbali zitolewazo na Benk hio ikiwomo Mikopo ya fedha na vifaa mbali mbali kulingana na shughuli za wateja wao.

 

Akitoa salamu za Benki ya NMB kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki wa NMB, bwana Juma Kimori ambae ni Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya NMB amesema benki ya NMB imeona changamoto waliyokuwa wakipata wateja wao kwa kukosa huduma za kifedha karibu na makaazi yao na kuamua kujenga Tawi la NMB katika Mkoa wa  Kaskazini Pemba kwa lengo la kuwasogezea karibu huduma za kifedha kupitia NMB Benk  na mawakala wao waliosambaa nchii nzima.

 

Amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeupa kipaombele na kufanya uwekezaji  mkubwa katika Sekta ya uchumi wa buluu hivyo NMB imedhamiria kuendelea kuunga mkono uwekezaji huo kwa kusaidia vifaa mbali mbali vya Uvuvi, kusaidia katika sekta ya Utalii, Mazao ya Baharini na wafanya biashara hasa wajasiriamali wadodo wadogo ili kuweza kukuza biashara zao.

 

Kimori amesema kila mwaka NMB imekuwa ikitenga fedha maalum kwa ajili ya kurudisha faida katika jami kupitia Sekta ya elimu, afya, Mazingira na kusaidia katika Majanga mbali mbali kwa lengo la kuhakikisha ustawi mzuri wa jamii

 
































Imetolewa na Kitengo cha Habari ( OMPR )

Leo tarehe..10 / 01 /  2025.

.........................................................


Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link