Home » » WIZARA YA ARDHI YAWAJENGEA UWEZO WADAU WA MRADI WA UIMARISHAJI MIUNDOMBINU YA UPIMAJI

WIZARA YA ARDHI YAWAJENGEA UWEZO WADAU WA MRADI WA UIMARISHAJI MIUNDOMBINU YA UPIMAJI

Written By CCMdijitali on Friday, January 31, 2025 | January 31, 2025

Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani Bw. Hamdouny Mansoor akifungua semina ya wadau wa Mradi wa Kuimarisha Miundombinu ya Upimaji na Ramani (LDI) kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhandisi Anthony Sanga Januari 30, 2025 katika Kituo cha Ubunifu na Mafunzo ya Kijiografia kilichopo (UDOM) jijini Dodoma. Kulia ni Mkuu wa kituo hicho Dkt. Aidan Kawinga na kushoto ni Makurugenzi Msaidizi Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu wizara hiyo.


Mratibu wa Mradi wa Kuimarisha Miundombinu ya Upimaji na Ramani (LDI) Dkt. Erick Mwaikambo akiwasilisha mada kwenye semina kwa wadau wa Mradi wa LDI Januari 30, 2025 katika Kituo cha Ubunifu na Mafunzo ya Kijiografia kilichopo (UDOM) jijini Dodoma.

Mkuu wa Kituo cha Ubunifu na Mafunzo ya Kijiografia kilichopo chou Kikuu cha Dodoma, Dkt. Aidan Kawinga akiwaeleza na kuwaonesha washiriki wa semina vifaa vinavyotumiwa kutekeleza kazi za upimaji kwenye Mradi wa Kuimarisha Miundombinu ya Upimaji na Ramani (LDI).

 
Washiriki wa semina ya wadau wa Mradi wa Kuimarisha Miundombinu ya Upimaji na Ramani (LDI) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa semina hiyo Januari 30, 2025 ambayo ilifanyika Kituo cha Ubunifu na Mafunzo ya Kijiografia kilichopo UDOM jijini Dodoma.

Baadhi ya washiriki wa semina ya wadau wa Mradi wa Kuimarisha Miundombinu ya Upimaji na Ramani (LDI) wakifuatilia mada Januari 30, 2025 katika Kituo cha Ubunifu na Mafunzo ya Kijiografia kilichopo UDOM jijini Dodoma.

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kupitia Mradi wa Kuimarisha Miundombinu ya Upimaji na Ramani (LDI) imeendesha semina ya kuwajengea uwezo wadau wa mradi huo kutoka taasisi mbalimbali kuhusiana na namna mradi mradi huo unavyorahisisha kazi katika maeneo yao.

Semina hiyo imefanyika Januari 30, 2025 katika Kituo cha Ubunifu na Mafunzo ya Kijiografia kilichopo eneo la Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) jijini Dodoma ambayo imehusisha wataalamu kutoka taasisi mbalimbali za serikali zinazotegemea na kutumia taarifa za kijiografia kutekeleza majukumu yao.

Alizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhandisi Anthony Sanga, Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani Bw. Hamdouny Mansoor amesema amesema semina hiyo inalenga kuwajengea uwelewa zaidi wataalamu hao kuhusu mradi wa LDI ili kuimarisha uhusiano mzuri uliopo miongoni mwa taasisi za Serikali hatua itakayosaidia kutekeleza mradi huo kwa pamoja kwa ufanisi zaidi.

Kutokana na umuhimu wa taasisi, tumeandaa semina hii ili kuwajengea uwelewa zaidi kuhusu mradi tukiamini hatua hii itaongeza uhusiano mzuri uliopo na taasisi na kwa pamoja kutekeleza mradi kwa ufanisi;. amesema Bw. Mansoir.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Mkurugenzi huyo wa Upimaji na Ramani ameongeza kuwa mradi huo wa LDI unaboresha miundombinu ya upimaji inayoleta taarifa zote za ardhi katika ukamilishaji wake.

Amesema, lengo kubwa la mradi huo wenye thamani ya dola milioni 65 unafadhiliwa na serikali ya Jamhuri ya Korea Kusini utasaidia kuandaa ramani za msingi kwa nchi nzima pamoja na kuboresha teknolojia ya upimaji.

Mradi huu una umuhimu wa kipekee katika sekta nyingine zinazotegemea taarifa za kijiografia katika kutekeleza majukumu yake na mfano ni katika miradi mikubwa ya kimkakati ya ujenzi wa miundombinu, utunzaji mazingira, utalii na udhibiti wa maliasili pamoja na ulinzi wa usalama wa nchi; amesema Mansoor.

Mradi huo ni uwekezaji mkubwa unaofanywa na serikali ili kuboresha huduma upatikanaji huduma na taarifa sahihi za kijiografia kwa wakati zikiwemo ramani za msingi ambazo ni nyenzo muhimu katika utawala wa ardhi hususan kupanga, kupima na kumilikisha.


-----------mwisho-----------

Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link