MAJALIWA AAGIZA USIMAMIAJI NA UDHIBITI WA UBORA WA ELIMU
▪️Asema lengo ni kuendelea kutoa wahitimu wenye uwezo wa kukidhi vigezo vya kimataifa ▪️Rais Dkt. Samia atoa milioni 100 kuchangia maendel...

MAJALIWA AAGIZA USIMAMIAJI NA UDHIBITI WA UBORA WA ELIMU
Written By CCMdijitali on Friday, June 20, 2025 | June 20, 2025
▪️Asema lengo ni kuendelea kutoa wahitimu wenye uwezo wa kukidhi vigezo vya kimataifa
▪️Rais Dkt. Samia atoa milioni 100 kuchangia maendeleo ya Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameitaka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na TAMISEMI pamoja kusimamia na kudhibiti ubora wa elimu inayotolewa kuanzia elimu ya msingi mpaka elimu ya juu ili kuendelea kukidhi viwango vya kitaifa, kikanda na kimataifa.
Ametoa maagizo hayo leo (Ijumaa Juni 20, 2025) alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye maadhimisho ya miaka 20 ya Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro (MUM), kwenye viwanja vya chuo hicho mkoani Morogoro.
“Mamlaka zetu ziendelee kusimamia hilo kwa kufanya hivyo sio tu kutaendelea kukuza ubora wa elimu yetu, bali pia kutawawezesha wasomi nchini kukidhi viwango na mahitaji ya soko la ajira”
Kadhalika, Mheshimiwa Majaliwa amezitaka Taasisi za Elimu nchini ziimarishe mahusiano na vyuo vyote nchini vinavyotoa maarifa kwa vijana wa kitanzania pamoja na kuzalisha wakufunzi ili kuwa sehemu ya mtandao wa utoaji maarifa na taalum hapa nchini.
Aidha, Mheshimiwa Majaliwa kuwa katika kuunga mkono jitihada za wadau mbalimbali katika kuchangia maendeleo ya chuo hicho kupitia mfumo maalum wa (MUM Community Fund), Rais Dkt. Samia ametoa kiasi cha Shilingi milioni 100 ili kiendelee kutoa huduma kwa watoto wa Kitanzania
Mheshimwa Waziri Mkuu ameongeza kuwa Serikali inaendelea na ujenzi wa Mfumo wa Takwimu wa Sekta ya Elimu utakaowezesha upatikanaji wa takwimu zote za sekta hiyo ambao utakuwa na uwezo wa kupokea takwimu mbalimbali zinazohusiana na elimu kutoka katika mifumo mingine ya Serikali ikiwemo NIDA, RITA na Wizara ya Mambo ya Nje.
Kwa Upande wake Naibu Waziri wa Elimu Qs Omar Kipanga amesema kuwa katika kipindi cha miaka 20, chuo hicho kimefanikiwa kuwa na progrma zaidi ya 32 kutoka program mbili wakati kinaanza na kimefanikiwa kutoa wahitimu zaidi ya 15,000.
“Wahitimu hawa wamekuwa wwamekuwa wa kupigiwa mfano katika kazi na maadili inayofanya waaminiwe katika nafasi mbalimbali kwenye jamii na Serikali kaa ujumla”
Kadhalika, ameongeza kuwa Chuo hicho kimeweka mipango inayozingatia dira ya maendeleo ya Taifa ya 2050 na mwelekeo mpya wa Elimu Nchini Tanzania unaolenga kutoa Elimu Ujuzi, Stadi na Maarifa kwa ajili ya kuwajengea wahitimu uwezo na sifa za kujiajiri na
kuajirika katika soko shindani la ajira duniani.
Naye Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Sheikh Dkt. Abubakar Zubeir bin in Ali ametoa wito kwa Waislam na Watanzania kwa ujumla kuweka mikakati ya kukisaidia chuo ili kiendelee kufanya vizuri na kutoa elimu kwa watanzania nchini.
“Waislam na watanzania tukisaidie chuo hichi, hakuna uislam bila ualimu, uislam ulipokuja ulipiga sana vita ujinga, tuwaunge mkono viongozi wetu kwa kukisaidia chuo hiki”
Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof Juma Assad amesema kuwa moja ya changamoto kubwa katika chuo hicho ni kukosekana kwa hosteli za wanafunzi wa kike “Namna tunavyoingeza udahili ndivyo tunavyoibua changamoto nyingine, tunataka watoto wetu wa kike wote wake ndani ya chuo”

MAKAMU WA RAIS DKT PHILIP MPANGO ASHIRIKI MKUTANO WA UBIA WA MAENDELEO NCHINI ITALIA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amesema Ubia wa Maendeleo baina ya Afrika na Italia kupitia mpango wa Mattei (Mattei Plan) na Mpango wa Ulaya (Global Gateway) utasaidia katika kuendeleza miundombinu, rasilimali watu, kilimo na maendeleo ya kidijitali barani Afrika.
Makamu wa Rais amesema hayo mara baada ya kushiriki Mkutano wa Ubia wa Maendeleo kati ya Bara la Afrika na Serikali ya Italia (Mattei Plan) pamoja na Mpango wa Ulaya (Global Gateway) unaofanyika katika Viwanja vya Villa Doria Pamphilj Jijini Roma nchini Italia akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Amesema mkutano huo umejadili zaidi vipaumbele vya nchi za Afrika na kudhamiria kutekeleza miradi kwa vitendo. Ameongeza kwamba majadiliano katika uongezaji thamani ya mazao hususani zao la kahawa yamelenga kuhakikisha Afrika inapata manufaa zaidi kutokana na kilimo hicho pamoja na kuongeza ajira kupitia zao hilo.
Makamu wa Rais amesema Tanzania ikiwa ni nchi ya nne barani Afrika kwa uuzaji wa kahawa nje ya bara hilo itanufaika zaidi na mpango wa uongezaji thamani wa zao hilo.
Pia amesema mkutano huo umejadili uwekezaji unaohitajika katika rasilimali watu ili kutengeneza mazingira mazuri zaidi kwa wananchi wa Afrika na kuwaepusha kukimbia nchi zao kuelekea mataifa ya Ulaya.
Makamu wa Rais amesema Mpango wa Mattei unabadili utoaji wa misaada ya maendeleo na kuleta mfumo mpya wa uwekezaji wa pamoja katika sekta za kimkakati ambao utatengeneza ajira na kuchochea mageuzi kwa maendeleo endelevu.
Katika Mkutano huo masuala yaliyopewa kipaumbele ni pamoja na uongezaji thamani katika zao la kahawa, nishati endelevu, uboreshaji miundombinu ikiwemo ushoroba wa Lobito pamoja na maendeleo ya kidijitali kama vile matumizi ya akili mnemba katika kukuza uchumi. Tanzania ni moja kati ya Mataifa 14 barani Afrika ambayo yanapewa kipaumbele na Italia kupitia mpango mpya wa kimkakati wa Mattei (Mattei Plan). Miradi ya kipaumbele katika Mpango huo ni pamoja na nishati, elimu na kilimo ambapo euro bilioni 5.5 zimetengwa kwaajili ya utekelezaji wa awamu ya kwanza ya miradi hiyo.
Mpango wa Umoja wa Ulaya (EU Global Gateway) ni wa kuboresha miundombinu katika sekta za kidijitali, nishati, usafirishaji, afya, elimu, na utafiti. Mpango huu unalenga uwekezaji wa Euro bilioni 300 ifikapo mwaka 2027, ambapo Euro bilioni 150 zimeelekezwa barani Afrika.
Umoja wa Ulaya wamedhamiria upanuzi wa mradi wa mawasiliano wa kidijiti (blue raman – submarine cable) unaopita chini ya bahari ambao unaunganisha Ulaya na India ili ufike nchini Tanzania na hivyo kuiunga Afrika Mashariki katika mradi huo.
Mkutano huo umeshirikisha Viongozi mbalimbali wa Afrika, Umoja wa Ulaya pamoja na Taasisi za Fedha za Kimataifa ikiwemo Benki ya Dunia, Shirika la Fedha Duniani (IMF) na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).
Taasisi za fedha za kimataifa, Umoja wa Ulaya pamoja na Serikali ya Italia zimeahidi kutoa fedha kwaajili ya kugharamia miradi mbalimbali itakayotekelezwa katika Mpango huo.
Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
20 Juni 2025
Roma - Italia






MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR AFANYA ZIARA YA KICHAMA - KASKAZINI UNGUJA
Written By CCMdijitali on Wednesday, June 18, 2025 | June 18, 2025
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amewataka wanachama wa CCM kuzidisha mshikamano ndani ya chama kwa kipindi chote cha maandalizi ya uchaguzi hadi utakapomalizia mwezi Oktoba.
Ameyasema hayo alipokutana na Viongozi wa Halmashauri Kuu ya Wilaya, Kamati za Siasa za Jimbo na wadi ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kuimarisha chama ndani ya Wilaya ya Kaskazini "A", Mkoa wa kazkazini ungaja katika Tawi la CCM Chaani.
Amesema ili kuwa na nguvu kubwa ya ushindi katika uchaguzi wa mwezi oktoba, ni lazima wanachama kuwa na umoja na kuzungumza sauti moja ya kukisemea chama vizuri kwa wananchi jambo litakalorahisisha ushindi wa chama hicho.
Mhe. Hemed amesema katika kuelekea kwenye viakao vya uteuzi wa wagombea ni vyema viongozi na wajumbe wa kamati kufanya maamuzi kwa kufuata katiba ya chama inavyoelekeza ili kuweza kupata wagombea watakaweza kuwatetea wananchi majimboni mwao.
Amesema uaminifu, uadilifu, kuacha utashi binafsi, visasi na chuki ni jambo pekee litakalopelekea kupata wagombea wenye sifa na uwezo wa kukiletea ushindi wa kishindo chama cha mapinduzi.
Amewaasa viongozi wa CCM kutokubali kutumiwa vibaya kwa kukununuliwa ama kupokea rushwa katika kipindi chote cha harakati za uchaguzi Mkuu ili kiendelea kulinda heshima na hadhi zao pamoja na chama chao.
Mhe.Hemed amewataka wanachama wa CCM kufanya kazi kwa umoja na mshikamano katika kukijenga na kukiimarisha chama cha Mapinduzi hasa kipindi hiki muhimu cha kukipambia chama kiweze kushinda katika uchaguzi wa mwezi oktoba na kuebelea kushikilia dola.
Amesisitiza kuwa kila mwanachama wa CCM ana haki ya kugombea akiwa na sifa zinazokubalika hivyo hakuna haja ya kutishana, kubezana na kudharauliana badala yake watiane mioyo na kusaidiana.
Amewahamasisha wanawake na vijana kujitokeza kwa wingi katika kitumia haki yao ya kikatiba kwa kugombea nafasi mbali mbali ili waweze kukitumikia chama chao na Taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake Katibu wa Idara ya Siasa, Itikadi, Uwenezi na Mafunzo ya chama ndugu Khamis Mbeto amesema Bajeti ya Serikali ya mwaka 2025/2026 iliyosomwa jana Baraza la Wawakilishi inaenda kumaliza changamoto ndogo ndogo zilizobakia na kuendeleza utekelezaji wa miradi ya kimkati kwa lengo la kuwaletea wananchi maendeleo.
Mbeto amesema Rais Dkt Samia Suluhu na Rais Dkt Hussein Mwinyi hawana deni kwa wananchi kwani kupitia uongozi wao kero na changamoto nyingi za wananchi zimetatulia hivyo amewataka wana CCM kuendelea kuwaunga mkono viongozi hao ili wawndelee kuwatumikia Watanzania.
Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa kazi za Chama cha Mapinduzi kwa kipindi cha Januari hadi Mei, Katibu wa CCM Wilaya ya Kaskazini "A" ndugu Aboud Said Mpate amesema wamejipanga Kimikakati kukiletea ushindi chama chao katika uchaguzi Mkuu kwa kushinda kwenye Majimbo yote yaliyomo ndani ya Mkoa huo.
Mpate amesema Wilaya ya Kaskazini "A" haina shaka na kazi itakayofanywa na kamati ya uteuzi wa wagombea na kusema kuwa wanaamini watapatikana wagombea wenye sifa ya kukitumikia chama kwa uzalendo na kutatua kero na changamoto za wazanzibari.
Viongozi wa CCM waaswa kutokubali kutumika vibaya kwa kununuliwa na kupokea rushwa
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amewataka viongozi wa CCM kutokubali kutumika vibaya kwa kununuliwa na kupokea rushwa hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi Mkuu.
Ameyasema hayo alipokutana na Viongozi wa Halmashauri Kuu ya Wilaya, Kamati za Siasa za Jimbo na wadi ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kuimarisha chama ndani ya Wilaya ya Kaskazini "B", Mkoa wa kaskazini ungaja katika Tawi la CCM Mahonda.
Amesema ni vyema kwa viongozi kuwa wazalendo kwa kuweka mbele maslahi ya chama na kuwa tayari kujitoa kwa hali na mali katika kukitumikia chama cha Mapinduzi.
Mhe. Hemed amesema kwa kipindi chote cha kuelekea uchaguzi Mkuu viongozi na wanchama wa CCM wanatakiwa kuwa wavumilivu na wastahmilivu na kuachana na mambo yote yanayokitia dosari chama ili kuwa mfano bora wa kuigwa na vyama vyengine.
Amesisitiza uminifu, uadilifu na kuacha utashi binafsi kwa viongozi na wajumbe watakaofanya kazi ya uteuzi wa wagombea jambo litakalopelekea kupata wagombea wenye sifa na uwezo wa kuwatetea majimboni mwao pamoja na kukiletea ushindi wa kishindo chama cha mapinduzi.
Mhe.Hemed amewataka wanachama wa CCM kufanya kazi kwa umoja na mshikamano katika kukijenga na kukiimarisha chama cha Mapinduzi hasa kipindi hiki muhimu cha kukipambia chama kiweze kushinda katika uchaguzi wa mwezi oktoba na kuebelea kushikilia dola.
Amesema cha Mapinduzi ni Chama cha wana CCM wote hivyo kila mmoja ana haki ya kugombea akiwa na sifa zinazokubalika ndani ya chama na kwa jamii iliyomzunguka.
Amewahamasisha wanawake na vijana kujitokeza kwa wingi katika kitumia haki yao ya kikatiba kwa kugombea nafasi mbali mbali ili waweze kukitumikia chama chao.
Katibu wa Idara ya Siasa, Itikadi, Uwenezi na Mafunzo ya chama ndugu Khamis Mbeto khamis amesema maendeleo makubwa yamefanywa na Serikali ya Awamu ya nane ikowemo ujezi wa miradi mbali mbali ya maendeleo ambayo inaendelea kuwanufaisha wanachi wa Mkoa wa Kaskazini.
Mbeto amesema kuna kila sababu ya kuendelea kuwarejesha madarakani ifikapo Oktoba Rais Dkt Mwinyi na Rais Dkt samia ili waedelee kuiimarisha na kuijenga vyema Tanzania.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kaskazini "B" ndugu Ali Khamis Ali amesema wakati utakapofika wa kupitisha wagombea kamati hazitakwenda kinyume na matakwa ya katiba ya chama na watafanya kazi kwa haki uwazi na hakuna mgombea atakae onewa kila mtu atapewa haki yake anayostahiki.
Katibu Ali amesema wanachama wa CCM wa Wilaya ya Kaskazini "B" wanaahidi ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu na hawatopoteza jimbo hata moja ndani ya Mkoa huo.
SIASA za kutakiana Heri kwenye majimbo zatawala katika Mkutano wa Chama cha Madaktari Arusha(M.A.T)
Kauli hiyo ambayo ameitoa leo juni 18,2025 katika mkutano huo unaofanyika aicc Arusha,ni wazi kwamba Makonda ameingiza miguu yote kulinyakua jimbo hilo kutoka kwa mbunge wa Sasa Mrisho Gambo ambaye umaarufu wake umeendelea kuporomoka kutokana na mnyukano wa wawili hao unaoendelea.
Kadhalika Makonda amemtakia kila la heri waziri Mkuu Kasimu Majaliwa katika jimbo lake la Ruangwa huku akisisitiza kuwa isingekuwa uchaguzi alikuwa amepania jiji la Arusha kuwa kama dubai kutokana na mipango aliyokuwa nayo.
"Mhe. Waziri Mkuu katika mipango bora iliyopo ya kulifanya jiji la Arusha kuwa kitovu cha utalii na sasa katika usafiri wa anga kwa kipindi cha miaka mitano Arusha ingekuwa ni kitu kingine ni vile tu kuna uchaguzi na tumebakiza siku chache". Amesema Makonda.
"Nasema hivi ni uchaguzi tu naimani waziri Mkuu amenielewa na mimi nikutakie kila lenye kheri Ruangwa na mimi usiache kunitakia kheri ili baada ya uchaguzi utakapo malizika na tutakapo kutana tufurahie kwa pamoja kuwa tulitakiana kheri". Amesisitiza Makonda.
Naye naibu waziri wa Afya Dr Godwin Mollel alisema kuwa katika jimbo lake la SIHA amemaliza uchaguzi na kumtakia heri waziri Mkuu Majaliwa na kumuomba asiache kufika jimbo la Siha ili kuhakikisha kura zake zinaendelea kujaa.
"Mhe. Waziri Mkuu mimi ni kama M'bunge wa pili Ruangwa maana nimefika mara nyingi katika kuteleza majukumu katika sekta ya Afya nimejione kwamba umesha maliza na unasubilia kuongoza tena kwa miaka mitano na mimi pale Siha nimeshamaliza nasubilia kusheherekea na kuendelea kuchapa kazi". Amesema Mollel.
"Na kwa vile tunahitaji viongozi wanaochapa kazi na sio maneno nikutakie Mhe. Makonda kila la kheri pale ulipo panga kulitumikia taifa letu umefanya mengi katika uongozi wako kama Mkuu wa Mkoa na matunda yanaonekana". Ameongeza Mollel.
Kwa upande wake waziri Mkuu amewahamasisha wananchi kujitokeza kugombea nafasi yoyote ya uongozi kama haki yao ya msingi ya kila mwananchi.
Aliwataka wananchi kutafakari lugha za wagombea iwapo kama zinafaa kwa ushawishi .


FANYENI TAFITI ZENYE TIJA KWA WANANCHI-MAJALIWA
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ametoa wito kwa watafiti na wapangaji wa Sera kuwekeza katika tafiti zenye tija kwa wananchi. Amesema kufanya hivyo, kutawezesha kuwa na matokeo ambayo yatatumika kutengeneza sera na mipango ya utekelezaji yenye kuleta mabadiliko halisi katika jamii.
- Ataka matokeo ya tafiti hizo yatumike badala ya kuyafungia
- Awataka wadau wa Sekta ya Afya kuongeza uwekezaji katika vifaa tiba na teknolojia mpya
Ametoa wito huo leo Jumatano (Juni 18, 2025) kwenye Kongamano la 13 la Kisayansi la Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) lililofanyika chuoni hapo kampasi ya Mloganzila, jijini Dar es Salaam.
“Tunataka kuona matokeo ya tafiti hizi yanatumika, msiweke tafiti hizi kwenye makabati tu, matokeo haya yanapaswa kuleta tija katika sekta ya afya, Ni matarajio yangu kuwa kongamano hili litatumika kutoa mapendekezo yatakayoimarisha mifumo, sera, na ushirikiano baina ya sekta ya umma na binafsi ili kuhakikisha Watanzania wananufaika kikamilifu na mapinduzi haya”
Kadhalika, Mheshimiwa Majaliwa amewataka wadau wa sekta binafsi na washirika wa maendeleo kuongeza uwekezaji katika vifaa tiba, na teknolojia mpya ili kuimarisha uwezo wa kukabiliana na magonjwa kwa wakati.
Amesema kuwa Serikali kwa upande wake itaendelea kuboresha sekta ya afya kwa kuwekeza zaidi katika miundombinu, rasilimali watu, tiba za kibingwa, na mifumo ya kukabiliana na milipuko ya magonjwa.
“Tutaendelea kushirikiana na wadau wote kuhakikisha kila Mtanzania anapata huduma bora, salama na rafiki bila kujali mahali alipo”.
Pia, Amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoomgozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kuweka mazingira wezeshi ya kuvutia uwekezaji katika uzalishaji wa dawa, chanjo na vifaa tiba ndani ya nchi. “Tayari tumeanza kushuhudia hatua chanya katika maeneo haya, tukijivunia mchango wa wataalamu wetu wa ndani”.
“Serikali yetu imeendelea kuimarisha mazingira ya matumizi ya teknolojia katika sekta ya afya.
Leo hii, hospitali zetu zinatumia mifumo ya kidijitali kubaini magonjwa, kutoa tiba sahihi, na kufuatilia maendeleo ya wagonjwa.”
Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Naibu Katibu Mkuu Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu Prof. Daniel Mushi amesema kuwa Serikali imeweka vipaumbele kwenye elimu, sayasi na teknolojia.
“Tunajivunia mageuzi makubwa chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, uongozi wake umeleta mageuzi mapya katika kuimarisha taasisi za elimu nchini”.
Amesema kuwa maboresho yaliyopo chuoni hapo ni ushahidi mkubwa wa namna serikali inavyoweka mipango ya kuboresha mazingira ya Ujifunzaji na Kufundishia. Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Appolinary Kamuhabwa
Ameipongeza Serikali kwa jitihada za dhati ambazo zimewezesha kuungwa mkono na wadau mbalimbali wa maendeleo na hivyo kufanikisha utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati inayoleta mageuzi makubwa katika mazingira ya elimu ya juu na afya nchini.
Prof. Appolinary amesema ujenzi wa Kituo cha Umahiri cha Magonjwa ya Moyo na Mishipa ya Damu cha Afrika Mashariki (yaani "East African Centre of Excellence for Cardiovascular Sciences") unaofadhiliwa na Serikali kupitia mkopo wa masharti nafuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika ni moja ya miradi itakayotekelezwa.
“Mradi huu unaingia katika awamu ya pili, baada ya kukamilisha awamu ya kwanza ya ujenzi wa kituo hiki muhimu hapa Mloganzila, Awamu ya kwanza iligharimu shilingi bilioni 21.62 na Awamu ya pili ya mradi huu ambayo imeanza rasmi mwezi Mei 2025, inalenga kujenga Hospitali ya Kisasa ya Kufundishia wataalamu bingwa na bobezi wa magonjwa ya Moyo na Mishipa ya damu”.
Alisema Prof. Appolinary Amesema kuwa Hospitali hiyo itakaongeza uwezo wa kutoa huduma za kibingwa, kufundisha wataalamu wa ndani na nje ya nchi, na kufanya tafiti zinazolenga kukabiliana na changamoto za magonjwa ya moyo na mishipa.
“Awamu hii itagharimu kiasi cha shilingi bilioni 221.57.”








KAENI KIMYA KAMA HAMJUI NCHI ILIKOTOKA - WASIRA

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Stephen Wasira amesema tangu kupata uhuru Tanzania imepata maendeleo makubwa na kwamba wanaosema hakuna kilichofanyika ni vema wakakaa kimya, wasiwe na tabia ya kasuku kukariri wasiyoyajua.
Wasira ameyasema hayo leo Juni 17, 2025 alipokuwa akizingumza katika mkutano wa hadhara Katoro, mkoani Geita akiwa katika ziara ya kukagua uhai wa Chama na kuzungumza na wananchi.
Akieleza kuhusu maendeleo yaliyofanyika nchini tangu kupatikana kwa uhuru alisema ni makubwa na wenye umri mkubwa wanajua vizuri nchi ilivyokuwa na wamekuwa wakishuhudia hatua mbalimbali zinazofanywa na serikali inayoundwa na CCM.
“Labda ninyi vijana hamwelewi lakini niwaambie wakoloni wa Kijerumani na wakoloni wa Kiingereza wamekaa Tanganyika miaka 75, Wajerumani wamekaa miaka 35, wamejenga reli kwa viboko bila malipo.
Waingereza wamekaa miaka 40 walitumwa na Umoja wa Mataifa (UN) watuendeleze tujitawalie, lakini miaka 40 ya Waingereza wametuacha na wahandisi wawili katika nchi isiyo na barabara.
“Wametuachia nchi hakuna daktari hata mmoja walikuwepo madaktari kutoka India na Pakistani nao walikuwa Dar es Salaam. Wakati tunapata uhuru akina mama walikuwa hawajifungui ila wanazaa maana hakukua na kliniki, hivyo walikuwa wanazaa kama ng’ombe anavyozaa ndama.
Ng’ombe umeona wapi ana kliniki (ya uzazi)? Hiyo ndio hali waliyotuacha nayo (wakoloni) wametuacha hatuna barabara.
“Leo anakuja mtu hajafikisha umri wa miaka 30 au miaka 40 anawaambia hakuna maendeleo. Wewe uliwahi kutembea kwa miguu, kuna maendeleo, hao wanaosema hakuna maendeleo ambayo yamefanyika akija muulizeni hivi kwako maendeleo ni kitu gani?.
Wasira amesema inawezakana wanaosema hakuna kilichofanyika anazungumza kama kasuku, maana kasuku huwa anakariri tu haelewi hata maana ya maneno anayosema na hao ndio wanasiasa wapya, sisi tumejitawala tulikuwa na msomi mmoja tu mwenye ‘Master’ (shahada ya uzamili) Julius Nyerere ndio alikuwa ameandaliwa na Wakoloni kwa miaka 75.
“Leo wala sio Tanganyika nilikuwa namuuliza Mkurugenzi wa Bukombe asubuhi anasema ana wahandisi 12, nikasema wewe ni tajiri kuliko Tanganyika ya mwaka 1970 maana kulikuwa na wahandisi wawili wewe unao 12. Namuuliza madaktari anasema wengi tu sisi hatukuwa na daktari.
“Hiyo ndio nchi tuliyorithi, leo unaweza kwenda mkoa wowote wa Tanzania kwa lami. Zamani wakati tunakabidhiwa nchi lami ilikuwa inatoka Dar es Salaam mpaka Morogoro kwa sababu kulikuwa na wazungu wanalima mkonge, ilikuwa inatoka Tanga mpaka Korogwe kwa sababu kulikuwa na wazungu wanalima mkonge.









RAIS SAMIA ATEMBELEA MAJERUHI WA AJALI MEATU
Written By CCMdijitali on Tuesday, June 17, 2025 | June 17, 2025
WADAU SEKTA YA MILKI WATAKIWA KUWA NA UMOJA
Na Munir Shemweta, WANMM MWANZA
Wadau wa sekta ya milki nchini wametakiwa kuendelea kuwa na umoja ili kuhakikisha sekta ya milki inakuwa.
Hayo yameelezwa tarehe 17 Juni 2025 na Mkurugenzi wa Kitengo cha Milki Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Upendo Matotola wakati wa kikao cha wadau wa sekta ya milki kilichofanyika mkoani Mwanza.
Kikao hicho ni muendelezo wa mijadala mbalimbali kati ya kitengo cha Milki Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na wadau wa Sekta ya Milki kwa lengo la kujenga ufahamu na kupata maoni kuhusiana na sekta ya milki nchini.
Tayari kitengo hicho kimefanya vikao vya mijadala katika majiji ya Dar es Salaam, Arusha na Dodoma.
" Ni lazima tuwe wamoja na kuhakikisha sekta yetu ya milki inakuwa sambamba na kuwa na sura nzuri" amesema
Kwa mujibu wa Dkt Matotola, wananchi wakishaiamini sekta ya milki kazi itakuwa rahisi ikiwemo upatikanaji kazi nyingi kwa kuwa wananchi hawatakuwa na haja ya kuhangaika kutokana na uwepo wa watu wanaowaamini.
" Kwa sababu mtu hana sababu ya kuhangaika kutafuta nyumba au kiwanja maana kuna watu wanawaamini na serikali inawaamini pia hivyo tunaweza kufanya kazi vizuri". Ameeleza
Mkurugenzi huyo wa Kitengo cha Milki ameweka wazi kuwa, kikubwa serikali inachotaka ni kujua kutoka kwa wadau zile changamoto wanazozipata katika uendeshaji na kile wanachotegemea kutoka kwa serikali ili kutengeneza mazingira bora ya kuwafanya wadau kufanya kazi vizuri.
Kwa upande wake Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Mwanza Wilson Luge amesema, serikali imeona ipo haja ya kuzungumza na wadau wa sekta ya milki ili kuwa na uelewa wa pamoja.
" Tutembee pamoja, sisi tuna malengo ya kufikia hatua fulani lakini na ninyi mna malengo fulani hivyo malengo yetu yaende sambamba na malengo yenu" amesema Luge.
Katika kikao hicho cha wadau wa sekta ya milki washiriki walipata uelewa wa majukumu ya kitengo cha milki, mfumo wa usajili na faida zake kwa mawakala, utakatishaji fedha katika sekta na wajibu wa mawakala katika kupambana na utakatishaji pamoja na mwongozo wa usajili wa mawakala.
Washiriki wakiwa katika kikao cha wadau wa sekta ya milki kilichofanyika jijini Mwanza tarehe 17 Juni 2025. |
Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Mwanza Wilson Luge akizungumza kwenye kikao cha wadau wa sekta ya milki kilichofanyika jijini Mwanza tarehe 17 Juni 2025. |
RAIS MHE. DKT. SAMIA AZINDUA KIWANDA CHA KUCHAKATA PAMBA CHA BIOSUSTAIN TANZANIA LIMITED MEATU
![]() |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa kuashiria uzinduzi wa Kiwanda cha kuchakata pamba cha Biosustain Tanzania Limited Meatu mkoani Simiyu tarehe 17 Juni, 2025.
![]() |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Kiwanda cha kuchakata pamba cha Biosustain Tanzania Limited Meatu mkoani Simiyu tarehe 17 Juni, 2025.
![]() |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe kuhusu Kiwanda cha kuchakata pamba cha Biosustain Tanzania Limited Meatu mkoani Simiyu tarehe 17 Juni, 2025.
![]() |
Mandhari ya kiwanda cha kuchakata pamba cha Biosustain Tanzania Limited kilichopo Meatu mkoani Simiyu ambacho kimezinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, tarehe 17 Juni, 2025.