Latest Post
October 12, 2025
Dkt. Kikwete Aunguruma Visiwani, Awataka Wazanzibari Walinde Amani na Maendeleo
Written By CCMdijitali on Sunday, October 12, 2025 | October 12, 2025
October 12, 2025


MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR- AKIZUNGUMZA NA WANAMICHEZO - JIMBONI KIWANI
Mgombea wa Uwakilishi Jimbo la Kiwani ndugu Hemed Suleiman Abdulla amesema Serikali ya Awamu ya nane Imeboresha sekta ya michezo kwa kujenga viwanja vipya katika maeneo mbali mbali ya Zanzibar na kufanya ukarabati mkubwa wa Uwanja wa New Aman Complex na Uwanja wa Gombani Pemba kwa lengo la kukuza sekta ya Mizo nchini.
Ameyasema hayo alipokutana na kuzungumza na wanamichezo mbali mbali waliomo katika Jimbo la Kiwani na kutumia fursa hio kuwaomba kura ili aweze kuwa mwakilishi wa Jimbo hilo ifikapo Oktoba 29.
Ndugu Hemed amesema anatambua changamoto mbali mbali zinazowakabili wanamichezo wa Jimbo la kiwani hivyo atakapokuwa mwakilishi wa Jimbo hilo atahakikisha anaimarisha na kufufua vuguvugu la michezo jimboni humo.
Mgombea huyo amesema kwa sasa michezo ni ajira hivyo amewaahidi wanamichezo hao kuwapa kila aina ya ushirikiano katika kufikia malengo yao ikiwemo kuwapatia vifaa vya michezo na mahitaji mengine yote yakimichezo.
Amesema kwa kutambua mchango na umuhimu wa michezo Jimboni na Taifa kwa ujumla atahakikisha analeta walimu na wakufunzi wa michezo mbali mbali watakao wafundisha kitaalamu ili kuwa na waamuzi, wachezaji, na timu bora zitakazoweza kushindana na timu yoyote ndani na nje ya Zanzibar.
Amewasisitiza wanamichezo hao kudumisha nidhamu kwa kufuata miiko, maadili na kanuni za michezo mbali mbali jambo litakalowajenga kuwa wanamichezo bora, pamoja na kuwataka kuwa na umoja, upendo na mshikamano baina yao.
Amesema katika kipindi cha uongozi wao wataunda kamati itakayohusisha timu zote zilizomo ndani ya Jimbo la Kiwani ambao watawasilisha kero na changamoto zinazozikabili timu zao kwa lengo la kulifanya jimbo la kiwani kuwa Jimbo la mfano kwa majimbo yote yaliyomo ndani ya Wilaya ya Mkoani na Zanzibar kwa ujumla.
Amewatoa hofu wanamichezo hao juu ya suala la miundombinu ya Viwanja vya kufanyia Mazoezi na mashindano mbali mbali kwa kuwaahidi kuwa kushirikiana na viongozi wa michezo Jimboni humo atalisimamia suala hilo na kulipatia ufumbuzi.
Wakizungumza kwa niaba ya wanamichezo wenzao ndugu Yussuf Mohd Khatib na Ndugu Kassim Rashid Mohd wamesema wamekuwa wanakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo vifaa vya michezo, changamoto ya usafiri wanapokuwa na mashindano mbali mbali pamoja na uhaba wa walimu na wakufunzi wa kuwafundisha katika timu zao.
Wamesema viwanja vyao vya kufanyia mazoezi vimeathiriwa na ujenzi wa miundombinu ya barabara lakini pia wakati wa msimu wa mvuaa baadhi ya viwanja hujaa maji na kupelekea changamoto ya kukaa muda mrefu bila ya kufanya mazoezi jambo linaloathiri viwango vyao vya michezo.
Wanamichezo hao wamemuahidi Mgombea wa uwakilishi na wagombea wote wa chama cha mapinduzi kiwa watawachagua kwa kura nyingi za ndio ifikapo Oktoba 29 ili waweze kuwafanyia maendeleo makubwa zaidi jimboni mwao.
Imetolewa na kitengo cha Habari ( OMPR )
Leo tarehe 12 / 10 / 2025


Labels:
ZANZIBAR
October 12, 2025

Baraza la Vijana Zanzibar kuendelea kushirikiana na taasisi mbali mbali za Vijana ndani na nje ya Nchi kutunza Mazingira
Baraza la Vijana Zanzibar limesema litaendelea kushirikiana na taasisi mbali mbali za Vijana ndani na nje ya Nchi katika kutunza Mazingira na kukabiliana na athari za Mabadiliko ya Tabianchi.
Hayo yameelezwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Vijana Zanzibar ndugu Ali Haji Hassan wakati wa shughuli ya kufanya Usafi na upandaji miti katika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya Kitengo cha Wazazi - META ikiwa ni sehemu ya shughuli za shamrashamra za Wiki ya Vijana Kitaifa inayofanyika Mkoa wa Mbeya.
Amesema athari za Mabadiliko ya Tabianchi zinapotokea basi Vijana,Wanawake na Watoto ndio waathirika wakubwa hivyo hakuna budi kwa Vijana kuungana kwa pamoja katika kuunga mkono jitahada zinazochukuliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Dk.Samia Suluhu Hassan na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Dk.Husein Ali Mwinyi.
"Jukumu la kutunza Mazingira, kuifanya Tanzania kuwa ya Kijani na kupanda miti ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya Tabianchi ni letu sote hasa sisi Vijana." Alihimiza Katibu Mtendaji huyo.
Aidha Ndugu Hassan alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa Vijana wote wa Tanzania kujitokeza na kushiriki kwa wingi siku ya Uchaguzi tarehe 29 Oktoba 2025 kwa kuhakikisha wanapiga Kura ili kuchaguwa Viongozi ambao watawaletea maendeleo na kuwa sauti ya Vijana huku wakidumisha amani na usalama Nchini.
Nae Mkurugenzi wa Taasisi ya Empower Youth Prosperity (EYP) Ipyana Mwakyusa amelipongeza Baraza la Vijana Zanzibar kwa jitahada zao za kushirikiana nao na kufanya shughuli tofauti za maendeleo ya Vijana wakiwa Mbeya katika Wiki ya Vijana.
"Natoa wito na kusisitiza mashirikiano kwa Taasisi hususan katika suala la Mazingira na tunaahidi tutakuwa wasimamizi wazuri na kuhakikisha miti tulioipanda leo inakuwa na kuwa kivutio kwa wanaofika Hospitali hii" Alisisitiza Mwakyusa
Nae Afisa Afya wa Hospitali hiyo Bi Julieth George amewashukuru vijana hao kwa kuichagua Hospital yao kuwa sehemu ya zoezi hilo na kuwataka Vijana hao kuwa zoezi hilo liwe endelevu na sio katika matukio maalum.
Shughuli hiyo imefanyika kwa mashirikiano ya Baraza la Vijana Zanzibar, Taasisi ya Empower Youth Prosperity (EYP) pamoja na wadau Tasisi za Vijana zilizopo Mbeya na zinazotekeleza Mradi wa Vijana Plus uliochini ya Save the Children kwa ushirikiano na Tanzania Bora Iniatives kwa ufadhili wa Umoja wa Ulaya.

Labels:
ZANZIBAR