MIUNDOMBINU YA ELIMU ZANZIBAR SASA YALINGANA NA MAHITAJI YA KARNE YA 21
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Zanzibar imepiga hatua kubwa katika kuimarisha mazin...
Latest Post
October 12, 2015
MWIGULU NDANI YA KANDA YA ZIWA,ASAKA KURA ZA MAGUFULI MAJIMBO 5 HII LEO
Written By CCMdijitali on Monday, October 12, 2015 | October 12, 2015
Mwigulu Nchemba Mjumbe wa Kamati ya Ushindi ya Chama cha Mapinduzi akimnadi Mbunge mtarajiwa wa Jimbo la Busega Dr.Chegeni mapema hii leo.
Mwigulu Nchemba Jimbo la Busega kwa Dr.Chegeni akisisitiza Wananchi kwenda kupiga kura kwa wingi,Hakuna namna CCM itashinda kwa kishindo kama wananchi hawajitokezi kupiga kura,Kura ni kwaajili ya maamuzi makubwa ya Taifa lako.
Sumve wakionesha Umoja wao kwenye zoezi la kwenda Kuichagua CCM kwa nafasi zote.
Mwigulu Nchemba akimnadi Mbunge mtarajiwa wa Jimbo la Sumve Nd.Ndasa.
Mwigulu Nchemba akiondoka Jimbo la Sumve mara baada ya kuomba kura za Urais,Ubunge na Udiwani kwa Chama cha Mapinduzi.
Mwigulu Nchemba akiwasisitiza Wananchi wasipuuzie jambola kupiga kura,Pia ameonya wananchi wanaouza vitambulisho vya Kupigia kura kuwa ni kosa la kisheria na Kila mmoja anapaswa kutunza kitambulisho chake.
Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza Ndg.Anton Diallo,Mwigulu NChemba na Mh.Charles Kitwanga .
Mbunge wa Jimbo la Misungwi Ndg.Charles Kitwanga akizungumza na Wananchi wake kuwa ameshajipanga kuhakikisha Miradi yote aliyoiianzisha anaikamilisha kwa miaka
Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi wa Jimbo la Solwa hii leo.
Mwigulu Chemba akisalimiana na Mgombea Ubunge Jimbo la Solwa ndg.Salum.
Mwigulu Nchemba akiteta Jambo na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida Bi.Azza Hilaly.
Comrade Mwigulu Nchemba akiagana na Wananchi wa Jimbo la Solwa.
Hisia za Mwananchi kwa Rais mtarajiwa Dr.J.Pombe Magufuli.
Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi wa shinyanga hii leo
"Nawaasa wananchi wa shinyanga Mjini,Muacheni Masele aendelee kusimamia malengo yake,ameshaonesha uwezo wa kusimamia shughuli za maendeleo Jimboni na serikalini.Hakuna haja ya kubadilisha Mbunge wakati hivi sasa ndio Vijana wanaotegemewa kusimamia Serikali hii ya CCM inayokuja.Ubunge sio Fashion kwamba kila siku unaweza kubadilisha"Mwigulu.
CCM "Chama kipo Imara
Wananchi wakishangilia moja ya sentensi za Mwigulu Nchemba "Mgombea wa CCM anauwezo wa Kusimamia jambo na likafanikiwa,ameonesha uwezo huo akiwa waziri nasasatumpatie asimamie Wizara zote".
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza Ndg.Anton Diallo akimnadi Mbunge mtarajiwa kwa awamu ya pili Shinyanga Mjini Ndg.Steven Masele.
Wananchi wa wakifuatilia Mkutano wa kampeni wa Chama Cha Mapinduzi hii leo Shinyanga
Mbunge mtarajiwa wa Chama cha Mapinduzi Shinyanga Mjini Ndg.Steven Masele akizungumza na Wananchi wake,Ameahidi kuendelea kusimamia ujenzi wa Viwanda mbalimbali ndani ya Wilaya ya Shinyanga Mjini ambapo hadi sasa viwanda vitano vimeshajendwa kati ya 12 vinavyotakiwa Kujengwa kwa
Mwigulu Nchemba akiagana na Viongozi na Wananchi wa Shinyanga Mjini mara baaada ya Mkutano wa hadhara.
Picha na Sanga Festo Jr.
Picha na Sanga Festo Jr.
Labels:
KITAIFA
October 08, 2015
Amesema wapo madereva wanaochukuwa abiria kupindukia kiwango kinachokubalika hasa kipindi hichi cha Kampeni na kuendesha vyombo vyao kwa mwendo wa kasi licha ya tahadhari zinazoendelea kutolewa kila siku na Jeshi la Polisi.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa tahadhari hiyo baada ya kuwapa pole majeruhi Tisa waliolazwa Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja wakipatia matibabu kufuatia ajali Tatu za vyombo vya moto zilizotokea wakati wafuasi wa Chama cha Mapinduzi wakirejea kutoka kwenye Mkutano wa Kampeni ya Uchaguzi Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Amesema Serikali Kuu kamwe haipendelei kuona Wananchi wake wanakuwa katika hali ya wasi wasi wakati wanapotumia usafiri wa Bara bara katika shughuli na harakati zao za Kimaisha.
Akiwakagua Majeruhi hao mapema asubuhi Balozi Seif Ali Iddi amewatakia matibabu mema na kuwaombea kwa Mungu wapone haraka ili warejee katika familia zao kuendelea na maisha yao ya kila siku.
Mkuu wa Kitengo cha Wagonjwa Mahatuti { ICU } kiliopo Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Raya Moh’d alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba hali za wagonjwa hao zinaendelea vyema na hakuna mtu aliyefariki katika matukio hayo.
Hata hivyo Bibi Raha alisema Said Ali Juma mwenye Umri wa Miaka 23 Mkaazi wa Mtaa wa Sogea aliyelazwa katika chumba Mahatuti { ICU }hivi sasa amepata nafuu kidogo ikilinganishwa na muda aliolazwa hospitalini hapo kwa matibabu.
Alisema Mgonjwa Said ambae amepata mshtuko wa kichwa kwa sasa anaweza kuonyesha ishara ya lile analolihaji kuhudumiwa hali inayoleta matumaini na faraja hata kwa wauguzi wenyewe.
Naye Ramadhan Hussein Masoud akiwa miongoni mwa majeruhi wa ajali hizo alimueleza Balozi Seif kwamba Dereva wa Gari aliyokuwa akisafiria ainaya Noha alikuwa akiendesha gari hiyo kwa mwendo wa kasi na kupuuza ushauri waliokuwa wakimpa.
Katika kukabiliana na ajali zinazoweza kuepukwa Uongozi wa Chama cha Mapinduzi umeagiza Gari zote zinazokwenda kwenye Mikutano ya Kampeni ya Chama hicho Madereva wake watalazimika kufuata utaratibu uliowekwa wa magari yao kurudi mikutanoni kwa pamoja.
Utaratibu huo utakaoongozwa na Gari ya Polisi utasaidia kuepuka ajali pamoja na kuwadhibiti madereva wasiozingatia sheria za usalama Bara barani ambao wengine huamua kufukuzana bila ya kujali maisha ya wenzao.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
5/10/2015.
Balozi Seif Ali Iddi awapa pole majeruhi Tisa waliolazwa Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja
Written By CCMdijitali on Thursday, October 8, 2015 | October 08, 2015
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimkagua na kumpa Pole Kijana Said Ali Juma Mkaazi wa Sogea aliyelazwa chumba cha wagonjwa Mahututi baada ya kupata ajali ya gari akitokea katika Mkutano wa Kampeni ya Uchaguzi Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Kushoto ya Balozi Seif ni Darkati wake Dr. Juma Salum Mambi.

Balozi Seif akimfariji Bwana Ramadhan Hussein Masoud Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja ambako amelzwa baada ya Garei alilokuwa akisafiria kutoka katika Mkutano wa Kampeni ya Uchaguzi Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja Kupata ajali wakati wakirejea Mjini.
Kijana Abdulsamadu Moh’d Juma Mkaazi wa Kijichi akimueleza Balozi Seif jinsi alivyopata ajali wakati yeye na wenzake wakirejea kutoka katika Mkutano wa Kampeni ya Uchaguzi wa CCM uliofanyika katika Kijiji cha Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Picha na – OMPR – ZNZ.
Picha na – OMPR – ZNZ.
Press Release:-
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewatahadharisha Wananchi kuwakataa Madereva wanaoendesha vyombo vya moto ambao baadhi yao wanashindwa kuzingatia sheria za usalama Bara barani.
Amesema wapo madereva wanaochukuwa abiria kupindukia kiwango kinachokubalika hasa kipindi hichi cha Kampeni na kuendesha vyombo vyao kwa mwendo wa kasi licha ya tahadhari zinazoendelea kutolewa kila siku na Jeshi la Polisi.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa tahadhari hiyo baada ya kuwapa pole majeruhi Tisa waliolazwa Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja wakipatia matibabu kufuatia ajali Tatu za vyombo vya moto zilizotokea wakati wafuasi wa Chama cha Mapinduzi wakirejea kutoka kwenye Mkutano wa Kampeni ya Uchaguzi Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Amesema Serikali Kuu kamwe haipendelei kuona Wananchi wake wanakuwa katika hali ya wasi wasi wakati wanapotumia usafiri wa Bara bara katika shughuli na harakati zao za Kimaisha.
Akiwakagua Majeruhi hao mapema asubuhi Balozi Seif Ali Iddi amewatakia matibabu mema na kuwaombea kwa Mungu wapone haraka ili warejee katika familia zao kuendelea na maisha yao ya kila siku.
Mkuu wa Kitengo cha Wagonjwa Mahatuti { ICU } kiliopo Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Raya Moh’d alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba hali za wagonjwa hao zinaendelea vyema na hakuna mtu aliyefariki katika matukio hayo.
Hata hivyo Bibi Raha alisema Said Ali Juma mwenye Umri wa Miaka 23 Mkaazi wa Mtaa wa Sogea aliyelazwa katika chumba Mahatuti { ICU }hivi sasa amepata nafuu kidogo ikilinganishwa na muda aliolazwa hospitalini hapo kwa matibabu.
Alisema Mgonjwa Said ambae amepata mshtuko wa kichwa kwa sasa anaweza kuonyesha ishara ya lile analolihaji kuhudumiwa hali inayoleta matumaini na faraja hata kwa wauguzi wenyewe.
Naye Ramadhan Hussein Masoud akiwa miongoni mwa majeruhi wa ajali hizo alimueleza Balozi Seif kwamba Dereva wa Gari aliyokuwa akisafiria ainaya Noha alikuwa akiendesha gari hiyo kwa mwendo wa kasi na kupuuza ushauri waliokuwa wakimpa.
Katika kukabiliana na ajali zinazoweza kuepukwa Uongozi wa Chama cha Mapinduzi umeagiza Gari zote zinazokwenda kwenye Mikutano ya Kampeni ya Chama hicho Madereva wake watalazimika kufuata utaratibu uliowekwa wa magari yao kurudi mikutanoni kwa pamoja.
Utaratibu huo utakaoongozwa na Gari ya Polisi utasaidia kuepuka ajali pamoja na kuwadhibiti madereva wasiozingatia sheria za usalama Bara barani ambao wengine huamua kufukuzana bila ya kujali maisha ya wenzao.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
5/10/2015.
Labels:
KITAIFA
October 08, 2015
Balozi Seif Ali Iddi awanadi Viongozi , Majimbo ya Kiembe Samaki na Chukwani
Baadhi ya Wanachama wa CCM wa Majimbo ya Kiembe Samaki na Chukwani wakiwa katika mkutano wa Kampeni wa Kuwanadi Wagombea nafasi za Ubunge, Uwakilishi na Udiwani wa Majimbo hayo uliohutubiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kampeni ya CCM Zanzibar
Balozi Seif Ali Iddi.
Balozi Seif akimnadi Mgombea wa nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Kiembe Samaki kupitia Chama cha Mapinduzi Nd. Ibrahin Raza kwenye uwanja wa michezo hapo Kiembe Samaki Wilaya ya Magharibi “B”.
Balozi Seif akimnadi Mgombea nafasi ya Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi kupitia Chama cha Mapinduzi Jimbo la Kiembe Samaki Mh. Mahmoud Thabit Kombo.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Balozi Seif akimuombea kura Bibi Mwanaasha Khamis Juma anayewania nafasi ya Uwakilishi kwa tiketi ya CCM Jimbo la Chukwani Bibi Mwanaasha Khamis Juma kwenye Mkutano wa Kampeni zinazoendelea ndani ya Majimbo hayo.
Balozi Seif akiwanadi wagombe wa nafasi za Udiwani katika wadi zote zilizomo ndani ya Majimbo la Kiembe Samaki na Chukwani hapo Uwanja wa Michezo wa Kiembe Samaki.
Wagombea nafasi hizo za Udiwani wa kwanza kulia ya Balozi Seif ni Nd. Maabada Ali Wadi ya Mbweni, Ndugu Maulidi Mwinyi Mzee Wadi ya Mombasa, Nd. Suleiman Muusa Wadi ya Shakani na Nd. Khamis Abdillah Wadi ya Kisauni.
Picha na –OMPR – ZNZ.

Press Rlease:-
Mwenyekiti wa Kamati ya Kampeni ya Uchaguzi ya CCM Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba endapo CCM itaendelea kushinda tena kwenye uchaguzi Mkuu wa mwaka huu Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itahakikisha kwamba inafuta waraka zote za umiliki wa ardhi zilizochukuliwa kihadaa kwa sura ya uwekezaji.
Alisema wapo baadhi ya watu waliopewa dhamana na Serikali katika kusimamia masuala ya ardhi na wakaamua kutumia vibaya madaraka yao kwa kujilimbikizia maeneo ya ardhi kwa maslahi yao binafsi.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa Kauli hiyo wakati akiwanadi wagombea nafasi mbali mbali za Uongozi katika Majimbo Mawili ya Kiembe Samaki na Chukwani kwenye Mkutano wa Kampeni zinazowendelea Nchini uliofanyika katika uwanja wa michezo wa Kiembe Samaki Wilaya ya Magharibi “ B ”.
Alisema tamaa ya watu hao kujilimbikizia maeneo makubwa ya ardhi imechangia kuikosesha mapato Serikali kuu kwa kipindi kirefu jambo ambalo upo uwezekano wa maeneo hayo kupewa wawekezaji wenye nia thabiti ya kutaka kuisaidia Nchi Kiuchumi.
Akizungumzia siasa za Kampeni zinazoendelea Balozi Seif ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa alisema uwezo wa upinzani wa kudhania kwamba utaking’oa madarakani Chama cha Mapinduzi ni wa kujifurahisha na hatma yake itaishia kuwadanganya wanachama pamoja na wafuasi wao.
Alisema Upinzani utawezaje kuliongoza Taifa wakati viongozi wake wamo ndani ya maamuzi yanayofanywa na Serikali katika Vikao vya Baraza la Wawakilishi na Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania tokea kuanza kwa mfumo wa Vyama vingi vya Siasa Nchini Tanzania kwa takriban Miaka 25 sasa.
Alisema nguvu za Chama cha Mapinduzi katika kutekeleza Sera na Ilani yake iliyofikia zaidi ya asilimia 90% katika kipindi cha Mwaka 2010 hadi 2015 ndio kigezo sahihi kinachotoa ishara kwamba Chama hicho kitaendelea kuungwa mkono na Wananchi walio wengi Tanzania Bara na Zanzibar.
Balozi Seif alijinasibu kwa kuelezea kuwa tabia ya Viongozi na wafuasi wa vyama vya upinzani kuendelea kumlalamikia kila mara hasa kwenye mikutano yao ni dalili za wafuasi hao kuiogopa CCM kutokana na jitihada zake za kuzisimamia Serikali zote mbili katika utekelezaji wa Ilani na sera zake.
Akisisitiza umuhimu wa suala la Amani Nchini hasa katika kipindi hichi cha mpito kuelekea uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika baadae mwezi huu Balozi Seif amnbae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema Serikali kamwe haitokubali kuona Nchi inaelekezwa katika kutiwa kwenye matatizo.
Balozi Seif alitahadharisha na kuwashauri wale watu waliozoea shari, fujo na mchafuko ni vyema wakafanya utaratibu wa kuelekea kwenye nchi zenye vitendo hivyo na sio haa Zanzibar.
Mapema Muasisi wa Jimbo la Chukwani Mzee Ali Hassan Khamis aliwanasihi Wanasiasa hasa wale wa vyama vya upinzani kuacha kutengeneza fitna mbaya na shari kwa kuwahusisha vijana wa Jimbo hilo ambayo kuachiliwa kupaliliwa kwake inaweza kuleta hatari kwa hatma ya vizazi hivyo.
Mzee Ali Hassan alisema Wazee na Wananchi wa Jimbo la Chukwani hawana nia mbaya na viongozi wa Upinzani lakini tabia ya wanasiasa wake ya kupita nyumba hadi nyumba kushawishi pamoja na kuhonga watu ni mwanmzo wa ishara mbaya ya kutaka kuleta fujo na vurugu.
Naye Mbunge Mstaafu wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Mh. Ummy Aley aliitanabahisha jamii kuwa na hadhari dhidi ya Viongozi wa Vyama vya Upinzani walioamua tumia fedha za Umma kujinufaisha wao binafsi.
Mh. Ummy alisema Wabunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Wale wa Baraza la Wawakilishi wa Chama cha Wananchi CUF wametumia karibu shilingi Bilioni 25 katika kipindi cha miaka Mitano na Shilingi Bilioni Mia 100 katika kipindi cha miaka 20 tokea kuanza kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa.
Katika Mkutano huo ulishirikisha Wanachama vindakindaki wa Majimbo ya Kiembe Samaki na Chukwani Balozi Seif aliwaombea kura kwa Wananchi na Wana CCM wagombea wote wa chama cha Mapinduzi wakati utakapowadia.
Wagombea hao ni Ibrahim Raza Hassananali Ubunge Jimbo la Kiembe Samaki, Mahomud Thabit Kombo Uwakilishi Jimbo hilo la Kiembe Samaki, Bibi Mwanaasha Khamis Juma Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi Jimbo la Chukwani, Nd. Maabad Ali Udiwani Wadi ya Mbweni, Nd. Maulid Mwinyi Wadi ya Mombasa, Suleiman Mussa Wadi ua Shakani na Nd. Khamis Abdillah Wadi ya Kisauni.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
5/10/2015.
Labels:
KITAIFA
October 02, 2015
Uzinduzi wa Kampeni za Udiwani CCM - Kata ya Olmot.
Written By CCMdijitali on Friday, October 2, 2015 | October 02, 2015
Olmoti
Hivi ndivyo ilivyokuwa ,wakati Mgombea Ubunge Jimbo la Arusha Ndg Philemon Mollel maarufu kwa jina la MONABAN akiwasili na kupokelewa na baadhi ya wakereketwa wa CCM Kata ya Olmot kwenye mkutano wa uzinduzi wa Kampeni za Udiwani Kata ya Olmot.
Mgombea Ubunge Jimbo la Arusha Ndg Philemon Mollel maarufu kwa jina la MONABAN akiinadi Ilani ya Chama Cha Mapinduzi na kumuombea kura Mgombea Urais wa CCM Ndg Makufuli na Mgombea Udiwani Kata ya Olmot kwenye mkutano wa uzinduzi wa Kampeni za Udiwani Kata ya Olmot.
Hivi ndivyo ilivyokuwa ,wakati Mgombea Ubunge Jimbo la Arusha Ndg Philemon Mollel maarufu kwa jina la MONABAN akiwasili na kupokelewa na baadhi ya wakereketwa wa CCM Kata ya Olmot kwenye mkutano wa uzinduzi wa Kampeni za Udiwani Kata ya Olmot.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Arusha Ndg Soileli akimnadi Mgombea Udiwani Kata ya Elerai Ndg Suvuku Miagie Lukumay kwenye mkutano wa uzinduzi wa Kampeni za Udiwani Kata ya Olmot .
Hapa kazi tu......."
Mgombea Ubunge Jimbo la Arusha Ndg Philemon Mollel maarufu kwa jina la MONABAN akifurahia jambo na Mgombea Udiwani Kata ya Elerai Ndg Suvuku Miagie Lukumay kwenye mkutano wa uzinduzi wa Kampeni za Udiwani Kata ya Olmot .
Mmoja wa wakereketwa wa CCM Kata ya Olmot akiwa na bango la mgombea urais Mkufuli na furaha kwenye mkutano uliohudhuriwa na wananchi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi waliojitokeza kwenye uzinduzi wa Kampeni za Udiwani Kata ya Olmot.

Mgombea Ubunge Jimbo la Arusha Ndg Philemon Mollel maarufu kwa jina la MONABAN akiinadi Ilani ya Chama Cha Mapinduzi na kumuombea kura Mgombea Urais wa CCM Ndg Makufuli na Mgombea Udiwani Kata ya Elerai kwenye mkutano wa uzinduzi wa Kampeni za Udiwani Kata ya Olmot.
Baadhi ya wakereketwa wa CCM Kata ya Olmot wakiwa na furaha kwenye mkutano uliohudhuriwa na wananchi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi waliojitokeza kwenye uzinduzi wa Kampeni za Udiwani Kata ya Olmot.
Mgombea Ubunge Jimbo la Arusha Ndg Philemon Mollel maarufu kwa jina la MONABAN akiinadi Ilani ya Chama Cha Mapinduzi na kumuombea kura Mgombea Urais wa CCM Ndg Makufuli na Mgombea Udiwani Kata ya Elerai kwenye mkutano wa uzinduzi wa Kampeni za Udiwani Kata ya Olmot.
Mgombea Ubunge Jimbo la Arusha Ndg Philemon Mollel maarufu kwa jina la MONABAN akiinadi Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwenye mkutano wa uzinduzi wa Kampeni za Udiwani Kata ya Olmot .
Mmoja wa mashabiki wa mgombea akiwa amevaa t shirt ya mgombea kwenye Kampeni za Udiwani Kata ya Olmot.
Mgombea Udiwani Kata ya Elerai Ndg Suvuku Miagie Lukumay kwenye mkutano wa uzinduzi wa Kampeni za Udiwani Kata ya Olmot .
Mgombea Ubunge Jimbo la Arusha Ndg Philemon Mollel maarufu kwa jina la MONABAN akimnadi Mgombea Udiwani Kata ya Elerai Ndg Suvuku Miagie Lukumay kwenye mkutano wa uzinduzi wa Kampeni za Udiwani Kata ya Olmot .
Picha zote na Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha - Jasper Kishumbua
Labels:
ARUSHA
October 02, 2015
Kutoka kulia ni Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Sekondari ya Fujoni Mwalimu Mbarouk Ishak Daima,Mwakilishi wa Kampuni ya Tigo Bibi Sylvia Balwire, Meneja Uhusiano wa Tigo Bibi Halima Okash pamoja na Mkurugenzi waq Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini B Ndugu Hassan Ali
Kombo.
Aliyesimama nyuma yao ni Mbunge anayemaliza muda wake wa Jimbo la Kitope ambaye pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
Kulia ya Bibi Sylvia Balwire ni Balozi Seif Ali Iddi, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini “B” ambao kushoto ya Bibi Sylvia ni Meneja Uhusiano wa Tigo Bibi Halima Okashi na Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Sekondari ya Fujoni Mwalimu Mbarouk Ishak Daima.
Picha na –OMPR – ZNZ.
Juhudi zilizochukuliwa na Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini “B” Mkoa wa Kaskazini Unguja kwa kushirikiana na Mbunge anayemaliza muda wake wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi hatimae zimezaa matunda yaliyosaidia Skuli ya Sekondari ya Fujoni Wilayani humo kupata vifaa vya Maabara .
Kampuni ya mtandao wa Mawasiliano ya simu za Mkononi ya Tigo
imeikabidhi Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini “B” Vifaa vya Maabara vyenye Thamani ya ya zaidi ya shilingi Milioni 20,000,000/- kwa ajili ya Skuli ya Sekondari ya Fujoni iliyomo ndani ya Jimbo Jipya la Mahonda.
Hafla hiyo fupi iliyoshuhudiwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ambae pia ni mgombea Uwakilishi wa Jimbo la Mahonda Balozi Seif Ali Iddi ilifanyika Nyumbani kwake Mtaa wa Kama Wilaya ya Magharibi “A ”.
Akikabidhi vifaa hivyo vya Maabara kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini “ B” Ndugu Hassan Ali Kombo Mwakilishi wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo Bibi Sylvia Balwire aliishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwajengea mazingira bora wawekezaji wanaoamua kuwekeza miradi yao ya kiuchumi Nchini.
Bibi Sylvia alisema taasisi yake ya Mtandao wa mawasiliano ambayo imekuwa ikitoa huduma za mawasiliano Nchi nzima imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuendesha biashara na faida inayopatikana huelekezwa katika kusaidia miradi ya Kijamii kama elimu, afya na maji safi na salama.
Akipokea msaada huo wa vifaa vya Maabara, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini “ B ” Ndugu Hassan Ali Kombo alieleza kwamba anaamini msaada huo uliofika kwa wakati utaimarisha fani ya sayansi kwa wanafunzi wa Wilaya hiyo.
Ndugu Hassan alisema upungufu wa vifaa vya maabara uliozikumba skuli nyingi za Sekondani Nchini umepelekea Serikali za Wilaya kupitia Halmashauri zake kutafuta mbinu na kuweka mikakati za kutanzua changamoto hiyo.
Alisema Uongozi wa Halmashauri hiyo ulilazimika kufanya juhudi za kutafuta msukumo na msaada kutoka kwa wafadhili na washirika wa Maendeleo katika kuunga mkono Sekta ya Elimu inayobeba nguvu ya maendeleo ya Taifa lolote.
Akitoa shukrani zake Mbunge anayemaliza muda wake wa utumishi wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema Serikali itaendelea kuimarisha miundo mbinu ya uwekezaji ili kuwajengea mazingira ya uhakika wawekezaji wanaoamua kuwekeza miradi yao hapa Zanzibar.
Balozi Seif ameipongeza Kampuni ya Simu za Mkononi ya
Alisema Skuli ya Sekondari ya Fujoni imeweka historia kubwa ndani ya Wilaya ya Kaskazi “B ” kwa kuimarisha masomo ya sayansi kiasi kwamba Halmashauri ya Wilaya hiyo ikalazimika kuiunga mkono katika kusaidia
kukabiliana na changamoto zinazoikabili skuli hiyo.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
2/10/2015.
Tigo yakabidhi Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini “B” Vifaa vya Maabara
Uongozi wa Kampuni ya simu za Mkononi ya Tigo ukikabidhi vifaa vya Maabara kwa Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini “B” vilivyotolewa msaada kwa ajili ya Skuli ya Sekondari ya Fujoni
iliyomo ndani ya Wilaya hiyo.
iliyomo ndani ya Wilaya hiyo.
Kutoka kulia ni Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Sekondari ya Fujoni Mwalimu Mbarouk Ishak Daima,Mwakilishi wa Kampuni ya Tigo Bibi Sylvia Balwire, Meneja Uhusiano wa Tigo Bibi Halima Okash pamoja na Mkurugenzi waq Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini B Ndugu Hassan Ali
Kombo.
Aliyesimama nyuma yao ni Mbunge anayemaliza muda wake wa Jimbo la Kitope ambaye pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
Mwakilishi wa Kampuni ya mtandao wa mawasiliano ya simu za Mkononi wa Tigo Bibi Sylvia Bwalwire aliyepo kati kati akielezea msimamo wa Kampuni yake kusaidia huduma za jamii hapa
Nchini.
Nchini.
Kulia ya Bibi Sylvia Balwire ni Balozi Seif Ali Iddi, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini “B” ambao kushoto ya Bibi Sylvia ni Meneja Uhusiano wa Tigo Bibi Halima Okashi na Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Sekondari ya Fujoni Mwalimu Mbarouk Ishak Daima.
Picha na –OMPR – ZNZ.
Press Release:-
Baadhi ya Halmashauri za Wilaya hapa nchini zinaendelea kufanya
jitihada katika kuimarisha miundo mbinu kwenye masomo ya Sayansi kwa lengo la kuwawezesha Wanafunzi wa Skuli za Sekondari kupata taaluma inayokwenda sambamba na
mabadiliko ya sayansi na teknolijia Duniani .
Juhudi zilizochukuliwa na Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini “B” Mkoa wa Kaskazini Unguja kwa kushirikiana na Mbunge anayemaliza muda wake wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi hatimae zimezaa matunda yaliyosaidia Skuli ya Sekondari ya Fujoni Wilayani humo kupata vifaa vya Maabara .
Kampuni ya mtandao wa Mawasiliano ya simu za Mkononi ya Tigo
imeikabidhi Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini “B” Vifaa vya Maabara vyenye Thamani ya ya zaidi ya shilingi Milioni 20,000,000/- kwa ajili ya Skuli ya Sekondari ya Fujoni iliyomo ndani ya Jimbo Jipya la Mahonda.
Hafla hiyo fupi iliyoshuhudiwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ambae pia ni mgombea Uwakilishi wa Jimbo la Mahonda Balozi Seif Ali Iddi ilifanyika Nyumbani kwake Mtaa wa Kama Wilaya ya Magharibi “A ”.
Akikabidhi vifaa hivyo vya Maabara kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini “ B” Ndugu Hassan Ali Kombo Mwakilishi wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo Bibi Sylvia Balwire aliishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwajengea mazingira bora wawekezaji wanaoamua kuwekeza miradi yao ya kiuchumi Nchini.
Bibi Sylvia alisema taasisi yake ya Mtandao wa mawasiliano ambayo imekuwa ikitoa huduma za mawasiliano Nchi nzima imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuendesha biashara na faida inayopatikana huelekezwa katika kusaidia miradi ya Kijamii kama elimu, afya na maji safi na salama.
Akipokea msaada huo wa vifaa vya Maabara, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini “ B ” Ndugu Hassan Ali Kombo alieleza kwamba anaamini msaada huo uliofika kwa wakati utaimarisha fani ya sayansi kwa wanafunzi wa Wilaya hiyo.
Ndugu Hassan alisema upungufu wa vifaa vya maabara uliozikumba skuli nyingi za Sekondani Nchini umepelekea Serikali za Wilaya kupitia Halmashauri zake kutafuta mbinu na kuweka mikakati za kutanzua changamoto hiyo.
Alisema Uongozi wa Halmashauri hiyo ulilazimika kufanya juhudi za kutafuta msukumo na msaada kutoka kwa wafadhili na washirika wa Maendeleo katika kuunga mkono Sekta ya Elimu inayobeba nguvu ya maendeleo ya Taifa lolote.
Akitoa shukrani zake Mbunge anayemaliza muda wake wa utumishi wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema Serikali itaendelea kuimarisha miundo mbinu ya uwekezaji ili kuwajengea mazingira ya uhakika wawekezaji wanaoamua kuwekeza miradi yao hapa Zanzibar.
Balozi Seif ameipongeza Kampuni ya Simu za Mkononi ya
Tigo kwa uamuzi
wake wa kusaidia sekta ya Elimu katika skuli iliyoonyesha

juhudi kubwa katika kuimarisha masomo ya sayansi ambayo
ndio yenye soko kubwa la ajira kwa hivi sasa.
Alisema Skuli ya Sekondari ya Fujoni imeweka historia kubwa ndani ya Wilaya ya Kaskazi “B ” kwa kuimarisha masomo ya sayansi kiasi kwamba Halmashauri ya Wilaya hiyo ikalazimika kuiunga mkono katika kusaidia
kukabiliana na changamoto zinazoikabili skuli hiyo.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
2/10/2015.
Labels:
KITAIFA
October 02, 2015
Kushoto ya Balozi Seif ni Bibi Khaina Ali Makame anagombea Wadsi ya Kiboje, Kulia ya Balozi Seif ni Nd. Victor Fabian anayegombea Udiwani Wadi ya Koani na Nd. Rashid Abass Othman Udiwani Wadi ya Bambi.
Alisema mpango huo umelenga kupunguza asilimia kubwa ya ushindi wa Chama cha Mapinduzi kwenye uchaguzi Mkuu ujao wa mwezi Oktoba ambao uko wazi kutokana na utekelezaji makini wa Sera na Ilani yake ya mwaka 2010 – 2015 iliyoleta maendeleo makubwa ya Kiuchumi na Kijamii Nchini Tanzania.
Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati akizungumza na Wana CCM na Wananchi wa Jimbo la Uzini akiizindua rasmi Kampeni za Uchguzi za Jimbo hilo hapo katika uwanja wa michezo wa Kiboje Muembe Shauri Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Alisema Viongozi pamoja na wafuasi wa Vyama vya Upinzani Nchini tayari wameshabaini kwamba nguvu ya ushindi wa CCM Kwenye uchaguzi Mkuu ujao wa mwezi huu inatisha kasi ambayo inavijengea mazingira ya kifo vyama hivyo kwa kukosa uhimili wa kuungwa mkono na wananchi walio wengi.
Balozi Seif ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliendelea kuwatoa hofu Wananchi hasa wale wenye asili ya Tanzania Bara kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia vyombo vyake vya Dola itakuwa makini katika kulinda usalama wao.
Alisema cheche ya baadhi ya watu kujaribu kujiandaa kutaka kufanya fujo kabla na baada ya uchaguzi zimetambuliwa licha ya baadhi ya viongozi wa Upinzani kutafuta mbinu za kukanusha mpango huo wa hatari.
Aliwakumbusha Wananchi na Wana CCM wote kujitokeza kwa wingi Tarehe 25 Mwezi huu katika kupiga kura na kuwachagua wagombea wote wa Chama Tawala cha CCM.
Balozi Seif aliwaomba wananchi hao kurejea nyumbani mara wanalizapo zoezi hilo ili kulinda amani ya nchi pamoja na kusaidia kuepusha ile shari ambayo tayari baadhi ya watu wametia nia ya kuianzisha kipindi hicho.
Mapema Mwenyekikti wa CCM Jimbo la Uzini Ndugu Haji Shaaban alisema watu wanaoeneza uzushi kuwa hakuna Maendeleo Zanzibar wanastahiki kuzomewa kwani ushahidi wa huduma za kijamii kama Maji safi na salama, umeme na Bara bara ndani ya kipindi cha miaka 50 upo wazi.
Nd. Shaaban alisema miaka 100 ya utawala wa Kikoloni wazee walishuhudia madhila, ugaguzi na ukosefu wa maendeleo ambayo yale finyu yaliyokuwepo yaliyolenga zaidi kwa watawala hasa mji Mkongwe.
Katika Mkutano huo wa uzinduzi wa Kampeni ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi Jimbo la Uzini Balozi Seif aliwanadi wagombea nafasi mbali mbali za Uongozi wa Jimbo hilo kupitia CCM.
Wagombea hao ni Nd. Salum Reheni anayegombea Nafasi ya Ubunge, Nd. Moh’d Raza Hassanali nafasi ya Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi, Bibi Khania Ali Makame nafsi ya Udiwani Wadi ya Kiboje, Nd.Rashid Abass Othman Udiwani Wadi ya Bambi na Nd.Victor Fabian Udiwani Wadi ya Koani.
Wakiomba kura kwa Wana CCM na Wananchi wa Jimbo hilo la Uzini Wagombea hao wameahidi kusimamia vyema Sera na Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2015 – 2020 ambayo wana uwezo nayo katika kuwaletea maendeleo Wananchi wa Jimbo la Uzini.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
1/10/2015.
Picha na –OMPR – ZNZ.
Balozi Seif Ali Iddi azungumza na Wana CCM na Wananchi wa Jimbo la Uzini
Baadhi ya wana CCM na wananchi wa Jimbo la Uzini wakiwa katika Mkutano wa uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi za Jimbo hilo zilizofanyika katika uwanja wa Michezo wa Kiboje Muembe Shauri.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kampeni ya CCM Balozi Seif Ali Iddi akimnadi mgombe nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Uzini kwa Tiketi ya Chama hicho Ndugu Salum Rehani wakati wa uzinduzi wa Kampeni za uchaguzi za Jimbo hilo.
Balozi Seif akimnadi kwa wapiga kura Ndugu Moh’d Raza Hassanali anayewanifa nafasi ya Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi Jimbo la Uzini liliopo Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Balozi Seif akiwanadi wagombea wa nafasi za Udiwani wadi zilizomo ndani ya Jimbo la Uzini wakati akizindua rasmi Kampeni za Uchaguzi za Jimbo hilo.
Kushoto ya Balozi Seif ni Bibi Khaina Ali Makame anagombea Wadsi ya Kiboje, Kulia ya Balozi Seif ni Nd. Victor Fabian anayegombea Udiwani Wadi ya Koani na Nd. Rashid Abass Othman Udiwani Wadi ya Bambi.
Press Release:-
Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Kampeni ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amewatahadharisha Wana CCM na Wananchi kuwa na tahadhari na baadhi ya watu walioamua kupita mitaani kununua Vitambulisho vya kupigia kura.
Alisema mpango huo umelenga kupunguza asilimia kubwa ya ushindi wa Chama cha Mapinduzi kwenye uchaguzi Mkuu ujao wa mwezi Oktoba ambao uko wazi kutokana na utekelezaji makini wa Sera na Ilani yake ya mwaka 2010 – 2015 iliyoleta maendeleo makubwa ya Kiuchumi na Kijamii Nchini Tanzania.
Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati akizungumza na Wana CCM na Wananchi wa Jimbo la Uzini akiizindua rasmi Kampeni za Uchguzi za Jimbo hilo hapo katika uwanja wa michezo wa Kiboje Muembe Shauri Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Alisema Viongozi pamoja na wafuasi wa Vyama vya Upinzani Nchini tayari wameshabaini kwamba nguvu ya ushindi wa CCM Kwenye uchaguzi Mkuu ujao wa mwezi huu inatisha kasi ambayo inavijengea mazingira ya kifo vyama hivyo kwa kukosa uhimili wa kuungwa mkono na wananchi walio wengi.
Balozi Seif ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliendelea kuwatoa hofu Wananchi hasa wale wenye asili ya Tanzania Bara kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia vyombo vyake vya Dola itakuwa makini katika kulinda usalama wao.
Alisema cheche ya baadhi ya watu kujaribu kujiandaa kutaka kufanya fujo kabla na baada ya uchaguzi zimetambuliwa licha ya baadhi ya viongozi wa Upinzani kutafuta mbinu za kukanusha mpango huo wa hatari.
Aliwakumbusha Wananchi na Wana CCM wote kujitokeza kwa wingi Tarehe 25 Mwezi huu katika kupiga kura na kuwachagua wagombea wote wa Chama Tawala cha CCM.
Balozi Seif aliwaomba wananchi hao kurejea nyumbani mara wanalizapo zoezi hilo ili kulinda amani ya nchi pamoja na kusaidia kuepusha ile shari ambayo tayari baadhi ya watu wametia nia ya kuianzisha kipindi hicho.
Mapema Mwenyekikti wa CCM Jimbo la Uzini Ndugu Haji Shaaban alisema watu wanaoeneza uzushi kuwa hakuna Maendeleo Zanzibar wanastahiki kuzomewa kwani ushahidi wa huduma za kijamii kama Maji safi na salama, umeme na Bara bara ndani ya kipindi cha miaka 50 upo wazi.
Nd. Shaaban alisema miaka 100 ya utawala wa Kikoloni wazee walishuhudia madhila, ugaguzi na ukosefu wa maendeleo ambayo yale finyu yaliyokuwepo yaliyolenga zaidi kwa watawala hasa mji Mkongwe.
Katika Mkutano huo wa uzinduzi wa Kampeni ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi Jimbo la Uzini Balozi Seif aliwanadi wagombea nafasi mbali mbali za Uongozi wa Jimbo hilo kupitia CCM.
Wagombea hao ni Nd. Salum Reheni anayegombea Nafasi ya Ubunge, Nd. Moh’d Raza Hassanali nafasi ya Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi, Bibi Khania Ali Makame nafsi ya Udiwani Wadi ya Kiboje, Nd.Rashid Abass Othman Udiwani Wadi ya Bambi na Nd.Victor Fabian Udiwani Wadi ya Koani.
Wakiomba kura kwa Wana CCM na Wananchi wa Jimbo hilo la Uzini Wagombea hao wameahidi kusimamia vyema Sera na Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2015 – 2020 ambayo wana uwezo nayo katika kuwaletea maendeleo Wananchi wa Jimbo la Uzini.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
1/10/2015.
Picha na –OMPR – ZNZ.
Labels:
KITAIFA
October 01, 2015
NA LILIAN JOEL ARUSHA
SADIFA"LOWASA NI MCHAFU HATUNA SABUNI WALA DODOKI LA KUMSAFISHA"
Written By CCMdijitali on Thursday, October 1, 2015 | October 01, 2015
MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Taifa, Sadifa Juma Hamis akihutubia mkutano wa hadhara katika kata ya Dumbechand Wilayani Karatu.
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepata pigo wilayani karatu mkoani hapa bada ya wananchama wake zaidi 30 kukihama chama hicho na kuhamia chama cha Mapinduzi (CCM).
Wananchama hao awalikihama chama hicho juzi wakati wa mkutano wa hadhara wa kampeni wa mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa chama Cha Mapinduzi taifa Sadifa Juma Hamis (UVCCM) wa kumuombea Dk John magufuli kura,mbunge wa Karatu Dk Wilbard Lory pamoja na madiwani wa CCM wilayani humo.
Mkutano huo uliofanyika katika kata ya Dumbechand ambapo ulihudhuriwa na mamia ya wananchi waliofika kusiliza ilani ya CCM na wakati mwenyekiti huyo akihutubia wanachama wa CHADEMA waliokuwa katika mkutano huo walikunwa na ilani hiyo na kujikuta wakirudisha kadi hizo.
Akizungumza kwa niaba ya wananchama wenzake hao aliyejitambulisha kwa jina la Anna Bohay alisema kata yao inakabiliwa na changamoto kubwa ya maji pamoja na miundo mbinu mingine mingi na kila kipindi cha uchaguzi CHADEMA uwaahidi kuwaletea maendeleo lakini wakishapata kura hawarudi nyuma kutimiza ahadi zao.
“Tulipotea njia tumedanganywa vya kutosha hatudanganyiki tena na sasa tumeamua kurudi CCM kwa kuwa ahadi zake zinatekelezeka na tutafanya kampeni usiku na mchana kuhakikisha CCM inashinda kwa kishindo katika wilaya ya karatu.
Akizungumza katika mkutano huo Sadifa aliwataka wananchi kuichagua CCM Oktoba 25 ili iweze kuwaletea maendeleo ya uhakika na kwa wakati.
Alisema serikali itakayoongozwa na Dk Magufuli itakuwa ni mapinduzi ya viwanda ambapo itatoa ajira za uhakika kwa vijana ili kutatua changamoto hiyo kubwa ambayo kwa sasa inawakabili vijana wengi hap nchini wasomi na wasiyokuwa wasomi.
Kuhusu migogoro ya Ardhi katika kata ya Mang’ola inayosababishwa na wawekezaji amabo wamehodhi ardhi kinyemela alisema mara baada ya uchaguzi mkuu kumalizika kero hiyo itatatuliwa mara moja na kurejesha mashamba hayo kwa wananchi inadapo watakuwa hawayamiliki kihalali .
“Mwekezaji hawezi kuhodhi ardhi na kukaa nayo bila kuiendeleza mashamba yote ambayo hayaendelezwi nitamuomba rais ayafutie hati na kuwamilisha wanachi ili muweze kulima na kuongeza
kipato cha familia .
Labels:
ARUSHA
October 01, 2015
Jaji Warioba alisema hayo jana kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika Uwanja wa Jamhuri, mjini hapa. “Tusipojua historia yetu… kama kuna kiongozi anakuja hajui historia ya nchi hii, tusije tukamkubali,” alisema Jaji Warioba. Aliendelea kusema, “Mtu yeyote ambaye hajui historia hiyo, hana haki ya kuomba uongozi,” alisema.
Warioba alisema ikichukuliwa historia hiyo, na kuangalia hali ya mwaka 1985 na kuilinganisha na mwaka 1961, atabaini mambo yaliyofanyika. “Ukiangalia Tanzania ambayo Mkapa (Rais Benjamin) aliiacha mwaka 2005 ni tofauti kabisa na jinsi Mwinyi alivyoiacha mwaka 1995,” alisema.
Hata hivyo alisema, zipo changamoto kwenye elimu, afya, maji, kilimo, miundombinu, ufugaji, uvuvi ambazo alisema, baadhi zinatokana na mafanikio. “Kama ni kiongozi, angalia msingi uliopo, anza kujenga huo msingi usije ukadharau kila kitu,” alisema na kuhoji, “Mtu gani anaweza asitambue maendeleo.”
Aliwataka wananchi kuhakikisha wanachuja mambo ya kampeni wanayoyasikia. “Mtu asije kuua historia ya nchi hii, ni lazima tuilinde historia ya nchi hii,” alisisitiza. Magufuli mzalendo Warioba ambaye alisema Magufuli ndiye anayefaa kuwa Rais kutokana na uzalendo wake wa kuhimiza amani, alieleza maeneo ambayo nchi ilipitia hadi kufika hatua hii ambayo hayapaswi kubezwa.
“Amekuwa (Magufuli) akisisitiza sana amani…sasa hasa vijana mnisikilize. Kwa sababu amani ililetwa na vijana, inalindwa na vijana, wazee huwa hawafanyi vurugu, akina mama huwa hawafanyi vurugu,” alisema na kuongeza kuwa kulinda amani ni lazima kufahamu ilivyokuja.
Akihimiza umma kuepuka kutenganishwa na mchakato, Jaji Warioba alieleza namna vijana na wazee walivyokutana katika miaka ya 1950 wakaunda Chama cha Tanu na kumchagua Mwalimu Nyerere awe kiongozi akiwa na umri wa miaka 32.
Alisema vijana hao ndiyo walioleta amani kwa kuunganisha watu wa makabila, dini zote likapatikana taifa moja na kuondoa ubaguzi wa kikabila na kiimani. Warioba aliendelea kusema vijana hao ndiyo waliounda Muungano wa Tanzania.
Aliwaambia vijana ndiyo taifa la leo na viongozi wa kesho. “Uchaguzi ni utaratibu wa kupata uongozi na siyo kututenganisha,” alisema Jaji Warioba. Alisema nchi ina kila sababu ya kumchagua Magufuli kwa kuwa ni mzalendo, anayehubiri amani muda mwingi.
“Wengine wanaona kama ni utani,” alisema Jaji Warioba na kusisitiza kuwa anaamini Magufuli ataunganisha na kuimarisha umoja wa nchi. Uadilifu, ufisadi Aidha, Jaji huyo mstaafu alisema kipindi hiki panahitajika mtu mwadilifu kutokana na ufisadi kuwa tatizo kubwa nchini.
Alisema anaamini Magufuli ndiye mwenye uwezo huo. Alimsifu namna ambavyo aliongoza wizara ya Ujenzi na kufanya kiwango cha rushwa katika wizara hiyo kupungua. Alitoa ushuhuda kwamba mwaka 1996, Rais Mkapa alimpa heshima ya kuwa mwenyekiti wa tume ya kuchunguza rushwa, ambayo miongoni mwa iliyobaini, rushwa kubwa ilikuwa kwenye sekta ya ujenzi.
Lakini, alisema tangu Magufuli alipoanza kuongoza wizara hiyo, rushwa imepungua katika sekta ya ujenzi.
Akihimiza wananchi kuhakikisha Oktoba 25 wanapiga kura, Jaji Warioba alisema, watu wengine kauli wanazotoa, ni za kujiandaa kukataa kura. Mkutano huo uliofurika watu, ulihudhuriwa na wanasiasa wakongwe, licha ya Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Warioba, ulihudhuriwa pia na Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela.
Wakongwe wengine waliohudhuria ni Pancras Ndejembi na Job Lusinde. Kimbisa: Magufuli hadaiwi fadhila Mwenyekiti CCM Mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa, alisema mgombea wa chama hicho, Dk John Magufuli hana deni la fadhila kwa kuwa hakuna mtu au kikundi cha watu watakaodai kwamba ndiyo waliomfikisha hapo.
“Hana deni la Kamati Kuu, nilikuwapo hakuna mjumbe wa kamati kuu atakayedai yeye ndiye yeye, nilikuwepo NEC hakuna aliyembeba… Halmashauri Kuu hana deni, Mkutano Mkuu hana deni. Nani anamdai Magufuli?,” alihoji Kimbisa. Wananchi wa Tanzania watamdai Magufuli fadhila.
“Naomba mumchague ili mpate muda wa kumtaka awalipe aliyowaahidi. Kimbisa alisema Magufuli ni mfuatiliaji na si mkali kama inavyodhaniwa na watu. Alihoji akifuatilia mishahara ya wafanyakazi, kwa watu wanaokula fedha , alihoji kama huo ni ukali au ufuatiliaji?
Kwa upande wake, Waziri Mkuu mstaafu, Malecela aliwashukuru wakazi wa Dodoma akisema mkoa huo kila wakati kunapokuwa na uchaguzi, huwa ni namba moja. “Wewe mwana Dodoma tunakuomba kazi yako iwe ni kumtafutia Magufuli kura kuanzia leo hadi Oktoba 25,” alisema.
Alisema katika safari ya kumpeleka Ikulu Magufuli, ni lazima wana Dodoma wawe mstari wa mbele, ikizingatiwa aliteuliwa mkoani hapa. Alisisitiza kuwa kura nyingi lazima zitoke hapa.
Warioba: Msichague wasiojua historia
![]() |
| Mzee wa Chama Cha Mapinduzi, Joseph Sinde Warioba. |
WAZIRI Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba amehadharisha umma wa Watanzania kuepuka kumkubali na kumchagua kiongozi asiyejua historia ya nchi, ilikotoka na ilipo. Akieleza kushangazwa na kile alichokiita ‘wimbo’ kwamba CCM haijafanya chochote katika miaka 54 tangu ipate huru, aliwashangaa zaidi watu wanaotumia jina la Mwalimu Julius Nyerere, mwasisi wa taifa, huku wakimuona dira, lakini wakisisitiza kwamba, hakufanya chochote.
Jaji Warioba alisema hayo jana kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika Uwanja wa Jamhuri, mjini hapa. “Tusipojua historia yetu… kama kuna kiongozi anakuja hajui historia ya nchi hii, tusije tukamkubali,” alisema Jaji Warioba. Aliendelea kusema, “Mtu yeyote ambaye hajui historia hiyo, hana haki ya kuomba uongozi,” alisema.
Warioba alisema ikichukuliwa historia hiyo, na kuangalia hali ya mwaka 1985 na kuilinganisha na mwaka 1961, atabaini mambo yaliyofanyika. “Ukiangalia Tanzania ambayo Mkapa (Rais Benjamin) aliiacha mwaka 2005 ni tofauti kabisa na jinsi Mwinyi alivyoiacha mwaka 1995,” alisema.
Hata hivyo alisema, zipo changamoto kwenye elimu, afya, maji, kilimo, miundombinu, ufugaji, uvuvi ambazo alisema, baadhi zinatokana na mafanikio. “Kama ni kiongozi, angalia msingi uliopo, anza kujenga huo msingi usije ukadharau kila kitu,” alisema na kuhoji, “Mtu gani anaweza asitambue maendeleo.”
Aliwataka wananchi kuhakikisha wanachuja mambo ya kampeni wanayoyasikia. “Mtu asije kuua historia ya nchi hii, ni lazima tuilinde historia ya nchi hii,” alisisitiza. Magufuli mzalendo Warioba ambaye alisema Magufuli ndiye anayefaa kuwa Rais kutokana na uzalendo wake wa kuhimiza amani, alieleza maeneo ambayo nchi ilipitia hadi kufika hatua hii ambayo hayapaswi kubezwa.
“Amekuwa (Magufuli) akisisitiza sana amani…sasa hasa vijana mnisikilize. Kwa sababu amani ililetwa na vijana, inalindwa na vijana, wazee huwa hawafanyi vurugu, akina mama huwa hawafanyi vurugu,” alisema na kuongeza kuwa kulinda amani ni lazima kufahamu ilivyokuja.
Akihimiza umma kuepuka kutenganishwa na mchakato, Jaji Warioba alieleza namna vijana na wazee walivyokutana katika miaka ya 1950 wakaunda Chama cha Tanu na kumchagua Mwalimu Nyerere awe kiongozi akiwa na umri wa miaka 32.
Alisema vijana hao ndiyo walioleta amani kwa kuunganisha watu wa makabila, dini zote likapatikana taifa moja na kuondoa ubaguzi wa kikabila na kiimani. Warioba aliendelea kusema vijana hao ndiyo waliounda Muungano wa Tanzania.
Aliwaambia vijana ndiyo taifa la leo na viongozi wa kesho. “Uchaguzi ni utaratibu wa kupata uongozi na siyo kututenganisha,” alisema Jaji Warioba. Alisema nchi ina kila sababu ya kumchagua Magufuli kwa kuwa ni mzalendo, anayehubiri amani muda mwingi.
“Wengine wanaona kama ni utani,” alisema Jaji Warioba na kusisitiza kuwa anaamini Magufuli ataunganisha na kuimarisha umoja wa nchi. Uadilifu, ufisadi Aidha, Jaji huyo mstaafu alisema kipindi hiki panahitajika mtu mwadilifu kutokana na ufisadi kuwa tatizo kubwa nchini.
Alisema anaamini Magufuli ndiye mwenye uwezo huo. Alimsifu namna ambavyo aliongoza wizara ya Ujenzi na kufanya kiwango cha rushwa katika wizara hiyo kupungua. Alitoa ushuhuda kwamba mwaka 1996, Rais Mkapa alimpa heshima ya kuwa mwenyekiti wa tume ya kuchunguza rushwa, ambayo miongoni mwa iliyobaini, rushwa kubwa ilikuwa kwenye sekta ya ujenzi.
Lakini, alisema tangu Magufuli alipoanza kuongoza wizara hiyo, rushwa imepungua katika sekta ya ujenzi.
Alieleza kushangazwa na wapinzani, ambao alisema, anachoona CCM ndiyo inayofanya kazi kwao kwa kuwa wapiga debe anaowaona huko ni wa kutoka CCM.
Akihimiza wananchi kuhakikisha Oktoba 25 wanapiga kura, Jaji Warioba alisema, watu wengine kauli wanazotoa, ni za kujiandaa kukataa kura. Mkutano huo uliofurika watu, ulihudhuriwa na wanasiasa wakongwe, licha ya Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Warioba, ulihudhuriwa pia na Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela.
Wakongwe wengine waliohudhuria ni Pancras Ndejembi na Job Lusinde. Kimbisa: Magufuli hadaiwi fadhila Mwenyekiti CCM Mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa, alisema mgombea wa chama hicho, Dk John Magufuli hana deni la fadhila kwa kuwa hakuna mtu au kikundi cha watu watakaodai kwamba ndiyo waliomfikisha hapo.
“Hana deni la Kamati Kuu, nilikuwapo hakuna mjumbe wa kamati kuu atakayedai yeye ndiye yeye, nilikuwepo NEC hakuna aliyembeba… Halmashauri Kuu hana deni, Mkutano Mkuu hana deni. Nani anamdai Magufuli?,” alihoji Kimbisa. Wananchi wa Tanzania watamdai Magufuli fadhila.
“Naomba mumchague ili mpate muda wa kumtaka awalipe aliyowaahidi. Kimbisa alisema Magufuli ni mfuatiliaji na si mkali kama inavyodhaniwa na watu. Alihoji akifuatilia mishahara ya wafanyakazi, kwa watu wanaokula fedha , alihoji kama huo ni ukali au ufuatiliaji?
Kwa upande wake, Waziri Mkuu mstaafu, Malecela aliwashukuru wakazi wa Dodoma akisema mkoa huo kila wakati kunapokuwa na uchaguzi, huwa ni namba moja. “Wewe mwana Dodoma tunakuomba kazi yako iwe ni kumtafutia Magufuli kura kuanzia leo hadi Oktoba 25,” alisema.
Alisema katika safari ya kumpeleka Ikulu Magufuli, ni lazima wana Dodoma wawe mstari wa mbele, ikizingatiwa aliteuliwa mkoani hapa. Alisisitiza kuwa kura nyingi lazima zitoke hapa.
Labels:
KITAIFA
October 01, 2015
Na Charles Charles
MWENYEKITI wa Taifa wa Chama cha NCCR - Mageuzi, James Mbatia hatimaye amejipachika rasmi jukumu la kuwa ni "msemaji" wa mgombea wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa.
Tayari hali hiyo pia imemkera Makamu Mwenyekiti wa NCCR - Mageuzi, Leticia Mosore aliyesema, Alhamisi ya wiki iliyopita kuwa Mwenyekiti wake huyo amejigeuza kuwa Msemaji wa Chadema, na kwamba amekisahau na kukiacha chama chake hicho mwenyewe kikidhoofika.
Kutokana na hali hiyo, Mosore alimtaka bosi wake kuacha kuisemea Chadema (na Lowassa), badala yake afanye za kuijenga NCCR - Mageuzi ikiwemo ya kuitisha na kuongoza vikao vya chama chake hicho.
Makamu Mwenyekiti huyo alitoa tuhuma hizo jijini Dar es Salaam, mbele ya waandishi wa habari akiwa pamoja na Katibu Mkuu wa NCCR - Mageuzi, Mosena Nyambabe.
Karibu wiki tano zilizopita, Mbatia ambaye pia ni Mwenyekiti Mwenza wa genge linalojiita Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), alijitokeza hadharani, mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kumtetea Lowassa kutokana na tuhuma za ufisadi dhidi yake.
Katika kufanya hivyo, mwanasiasa huyo anayegombea ubunge wa jimbo la Vunjo, Moshi mkoani Kilimanjaro, alikwenda mbali zaidi kwa kutaka iundwe Tume ya Maridhiano na Mafisadi ili wasifungwe jela!
Siku kadhaa zilizopita, Mbatia yuleyule na kwa kutumia mtindo uleule wa vyombo vya habari, safari hii kwa kuongea 'live' na wananchi kupitia vituo kadhaa vya televisheni nchini, alimtetea Lowassa kwa ujinga aliofanya akiwa Tabora, wakati wa kampeni zake za urais.
Akiwa kwenye ibada katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) mjini humo, Lowassa aliwaomba waumini wa dhehebu hilo nchini kote, wamchague kuwa Rais wa Serikali ya Awamu ya Tano kwa vile wote waliotangulia hakuna hata mmoja kati yao ambaye ni Mlutheri!
"Naomba mniombee, (tena) mniombee kwelikweli. Nyie Walutheri mna sababu ya kuomba zaidi kwa sababu tangu nchi hii iumbwe haijapata Rais Mlutheri. (Hayati) Mwalimu (Julius Kambarage) Nyerere alikuwa Mkatoliki, (halafu) Rais (Benjamin) Mkapa (naye) alikuwa Mkatoliki", alisema kwa kinywa chake mwenyewe na kuongeza:
"Sasa nadhani Mungu atatuongoza ili nasi (Walutheri) tuweze kuipata nafasi hiyo. Kwa hivyo naomba mniombee sana" (mwisho wa kunukuu).
Hivyo ndivyo Lowassa alivyosema alipopewa fursa hiyo muhimu ya kusalimia kanisani, nafasi aliyoipata kwa vile alikuwa akisali kwa mara yake ya kwanza kanisani hapo.
Alipewa kwa vile ni utaratibu maalum wa kanisa hilo kuwatambulisha, wakati wa matangazo waumini wote wageni wanaokuwa na vyeti vya utambulisho kutoka sharika wanazosali, na pia huwapa nafasi ya kusimama na kujitambulisha wenyewe wasiokuwa na barua hizo.
Badala ya kusalimia kwa Neno la Mungu kama "Bwana Yesu asifiwe, tumsifu Yesu Kristu" au kusema "haleluya", kisha akajitambulisha na kuketi ili asimame mtu mwingine, yeye alitumia mwanya huo kuwaomba Walutheri nchini wamchague kuwa Rais wa Serikali ya Awamu ya Tano kwa vile naye ni Mlutheri!
Aliomba wamuombee kwa sala zao zote ili dhehebu hilo nchini nalo litoe rais, ujinga ambao wananchi hawakutarajia kama ungeweza ukafanywa na mgombea wa nafasi hiyo muhimu kwa taifa!
Lakini bila wasiwasi wala aibu usoni, Mbatia alijitokeza hadharani, mbele ya kamera za televisheni kadhaa nchini kumtetea Lowassa kwa kupotosha waziwazi.
Alidanganya, kwamba alichosema eti ni kuomba aombewe ili ashinde siku ya uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani mwezi ujao, jambo linalofanywa na kila mmoja anayegombea nafasi yoyote ile ya madaraka ya kisiasa wakiwemo hata washirikina.
Sitaki kuamini kuwa Mbatia ni muongo sana, mzushi sana, zuzu sana, tapeli wa kisiasa, mvivu wa kufikiri, mpotoshaji mkubwa na hata vinginevyo, lakini imebidi nimtathimini kwa kutumia sifa hizo ili kupata undani wake.
Hata kwa akili ya kawaida ni je, hivi ni kweli Lowassa aliposema "nyie Walutheri mna sababu ya kuomba zaidi kwa sababu tangu nchi hii iumbwe haijapata Rais Mlutheri", maneno aliyoyasema mwenyewe alikuwa eti anaomba aombewe ushindi na Walutheri hao?
Je, ni kweli kwamba alipotolea mfano wa Rais wa Serikali ya Awamu ya Kwanza, hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Rais wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa kwa kusema wote walikuwa Wakatoliki huyo alikuwa anaomba aombewe ushindi kwa sababu za kawaida za imani yake Kiroho?
Au, Lowassa aliposema kwamba "sasa nadhani Mungu atatuongoza ili nasi (Walutheri) tuweze kuipata nafasi hiyo (ya urais)" alikuwa akiomba, kwamba aombewe kwa taratibu za kawaida na siyo kwa sababu ni Mlutheri?
Ni kweli kuwa kwa maneno yake hayo, kauli zake hizo na hata vinginevyo alikuwa akitaka aombewe ushindi?
Nimesema sitaki kuamini kuwa Mbatia ni tapeli wa kisiasa, muongo sana, mzushi, mpotoshaji na kadhalika, lakini nina haki ya kutilia wasiwasi uwezo wake wa kufilkiri, uadilifu wake na hata ubora wake wa kuongoza watu akiwa mbunge au Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Siasa.
Ni vigumu katika hali ya kawaida hasa kwa mtu asiyehongwa, kiongozi mwadilifu na anayejua na kuthamini ukweli kupata ujasiri ulioonyeshwa na Mbatia wa kwenda kutetea upuuzi na tena hadharani!
Najaribu kutafakari endapo kweli ni adui mkubwa wa watuhumiwa wa wizi wa fedha za serikali, ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma.
Najiuliza kwa sababu siamini kuwa Mbatia aliyekuwa mmoja kati ya vinara wa kukemea ufisadi, mafisadi wenyewe au wanasiasa na watumishi wa umma wenye tuhuma hizo za jinai hivi sasa ndiye wakili wao mkubwa!
Najiuliza sana kama sasa ni mmoja kati ya viongozi wa kisiasa wanaohongwa sana, kwamba inawezekana akawa tayari amehongwa kwa namna moja ama nyingine ili awe mstari wa mbele kujibu tuhuma zote, kutetea maovu yote na upuuzi wote wa kisiasa unaofanywa na mgombea huyo wa urais wa Chadema.
Najiuliza kuwa kwa nini, wakati Lowassa alipotuhumiwa na Dk. Slaa kuwa fisadi, bila kujifichaficha na hata vinginevyo alijitokeza hadharani na haraka ili 'kumkingia kifua' kwa Watanzania!
Najiuliza sana ilikuwaje afikie mpaka hatua ya kutaka eti mafisadi wasamehewe, msimamo ambao unatia mashaka endapo ulikuja kwa utashi wake mwenyewe ama la.
Najiuliza sana kama hafanyi hivyo kwa sababu amehongwa fedha za Lowassa mwenyewe, wapambe wake, Chadema yenyewe au kundi lolote ili afanye kazi hiyo isiyowezekana kwa 'macho makavu'.
Ili aweze kuniondolea mashaka ya wingu hilo dhidi yake, Mbatia anaweza kutuambia kuwa ni nani hafahamu Kiswahili mpaka ashindwe kuijua kauli ile ya Lowassa kanisani na kudai eti hakueleweka?
Au, kama siyo msemaji rasmi wa mgombea huyo wa urais, Mbatia anaweza kutuambia kuwa analinda maslahi gani kwa Lowassa?
Mwandishi wa makala hii anapatikana kwa Simu Na. 0659 220 220 na 0762 633 244
Mbatia anaona nani hafahamu Kiswahili au analinda maslahi gani kwa Lowassa?
![]() |
| MWENYEKITI wa Taifa wa Chama cha NCCR - Mageuzi, James Mbatia |
Na Charles Charles
MWENYEKITI wa Taifa wa Chama cha NCCR - Mageuzi, James Mbatia hatimaye amejipachika rasmi jukumu la kuwa ni "msemaji" wa mgombea wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa.
Tayari hali hiyo pia imemkera Makamu Mwenyekiti wa NCCR - Mageuzi, Leticia Mosore aliyesema, Alhamisi ya wiki iliyopita kuwa Mwenyekiti wake huyo amejigeuza kuwa Msemaji wa Chadema, na kwamba amekisahau na kukiacha chama chake hicho mwenyewe kikidhoofika.
Kutokana na hali hiyo, Mosore alimtaka bosi wake kuacha kuisemea Chadema (na Lowassa), badala yake afanye za kuijenga NCCR - Mageuzi ikiwemo ya kuitisha na kuongoza vikao vya chama chake hicho.
Makamu Mwenyekiti huyo alitoa tuhuma hizo jijini Dar es Salaam, mbele ya waandishi wa habari akiwa pamoja na Katibu Mkuu wa NCCR - Mageuzi, Mosena Nyambabe.
Karibu wiki tano zilizopita, Mbatia ambaye pia ni Mwenyekiti Mwenza wa genge linalojiita Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), alijitokeza hadharani, mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kumtetea Lowassa kutokana na tuhuma za ufisadi dhidi yake.
Katika kufanya hivyo, mwanasiasa huyo anayegombea ubunge wa jimbo la Vunjo, Moshi mkoani Kilimanjaro, alikwenda mbali zaidi kwa kutaka iundwe Tume ya Maridhiano na Mafisadi ili wasifungwe jela!
Hatua yake hiyo ilikuja siku mbili tu baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa kuanika hadharani ufisadi wa Lowassa kuhusu sakata la kampuni tata ya kufua umeme ya Richmond Development LLC.
Siku kadhaa zilizopita, Mbatia yuleyule na kwa kutumia mtindo uleule wa vyombo vya habari, safari hii kwa kuongea 'live' na wananchi kupitia vituo kadhaa vya televisheni nchini, alimtetea Lowassa kwa ujinga aliofanya akiwa Tabora, wakati wa kampeni zake za urais.
Akiwa kwenye ibada katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) mjini humo, Lowassa aliwaomba waumini wa dhehebu hilo nchini kote, wamchague kuwa Rais wa Serikali ya Awamu ya Tano kwa vile wote waliotangulia hakuna hata mmoja kati yao ambaye ni Mlutheri!
"Naomba mniombee, (tena) mniombee kwelikweli. Nyie Walutheri mna sababu ya kuomba zaidi kwa sababu tangu nchi hii iumbwe haijapata Rais Mlutheri. (Hayati) Mwalimu (Julius Kambarage) Nyerere alikuwa Mkatoliki, (halafu) Rais (Benjamin) Mkapa (naye) alikuwa Mkatoliki", alisema kwa kinywa chake mwenyewe na kuongeza:
"Sasa nadhani Mungu atatuongoza ili nasi (Walutheri) tuweze kuipata nafasi hiyo. Kwa hivyo naomba mniombee sana" (mwisho wa kunukuu).
Hivyo ndivyo Lowassa alivyosema alipopewa fursa hiyo muhimu ya kusalimia kanisani, nafasi aliyoipata kwa vile alikuwa akisali kwa mara yake ya kwanza kanisani hapo.
Alipewa kwa vile ni utaratibu maalum wa kanisa hilo kuwatambulisha, wakati wa matangazo waumini wote wageni wanaokuwa na vyeti vya utambulisho kutoka sharika wanazosali, na pia huwapa nafasi ya kusimama na kujitambulisha wenyewe wasiokuwa na barua hizo.
Badala ya kusalimia kwa Neno la Mungu kama "Bwana Yesu asifiwe, tumsifu Yesu Kristu" au kusema "haleluya", kisha akajitambulisha na kuketi ili asimame mtu mwingine, yeye alitumia mwanya huo kuwaomba Walutheri nchini wamchague kuwa Rais wa Serikali ya Awamu ya Tano kwa vile naye ni Mlutheri!
Aliomba wamuombee kwa sala zao zote ili dhehebu hilo nchini nalo litoe rais, ujinga ambao wananchi hawakutarajia kama ungeweza ukafanywa na mgombea wa nafasi hiyo muhimu kwa taifa!
Lakini bila wasiwasi wala aibu usoni, Mbatia alijitokeza hadharani, mbele ya kamera za televisheni kadhaa nchini kumtetea Lowassa kwa kupotosha waziwazi.
Alidanganya, kwamba alichosema eti ni kuomba aombewe ili ashinde siku ya uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani mwezi ujao, jambo linalofanywa na kila mmoja anayegombea nafasi yoyote ile ya madaraka ya kisiasa wakiwemo hata washirikina.
Sitaki kuamini kuwa Mbatia ni muongo sana, mzushi sana, zuzu sana, tapeli wa kisiasa, mvivu wa kufikiri, mpotoshaji mkubwa na hata vinginevyo, lakini imebidi nimtathimini kwa kutumia sifa hizo ili kupata undani wake.
Hata kwa akili ya kawaida ni je, hivi ni kweli Lowassa aliposema "nyie Walutheri mna sababu ya kuomba zaidi kwa sababu tangu nchi hii iumbwe haijapata Rais Mlutheri", maneno aliyoyasema mwenyewe alikuwa eti anaomba aombewe ushindi na Walutheri hao?
Je, ni kweli kwamba alipotolea mfano wa Rais wa Serikali ya Awamu ya Kwanza, hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Rais wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa kwa kusema wote walikuwa Wakatoliki huyo alikuwa anaomba aombewe ushindi kwa sababu za kawaida za imani yake Kiroho?
Au, Lowassa aliposema kwamba "sasa nadhani Mungu atatuongoza ili nasi (Walutheri) tuweze kuipata nafasi hiyo (ya urais)" alikuwa akiomba, kwamba aombewe kwa taratibu za kawaida na siyo kwa sababu ni Mlutheri?
Ni kweli kuwa kwa maneno yake hayo, kauli zake hizo na hata vinginevyo alikuwa akitaka aombewe ushindi?
Nimesema sitaki kuamini kuwa Mbatia ni tapeli wa kisiasa, muongo sana, mzushi, mpotoshaji na kadhalika, lakini nina haki ya kutilia wasiwasi uwezo wake wa kufilkiri, uadilifu wake na hata ubora wake wa kuongoza watu akiwa mbunge au Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Siasa.
Ni vigumu katika hali ya kawaida hasa kwa mtu asiyehongwa, kiongozi mwadilifu na anayejua na kuthamini ukweli kupata ujasiri ulioonyeshwa na Mbatia wa kwenda kutetea upuuzi na tena hadharani!
Najaribu kutafakari endapo kweli ni adui mkubwa wa watuhumiwa wa wizi wa fedha za serikali, ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma.
Najiuliza kwa sababu siamini kuwa Mbatia aliyekuwa mmoja kati ya vinara wa kukemea ufisadi, mafisadi wenyewe au wanasiasa na watumishi wa umma wenye tuhuma hizo za jinai hivi sasa ndiye wakili wao mkubwa!
Najiuliza sana kama sasa ni mmoja kati ya viongozi wa kisiasa wanaohongwa sana, kwamba inawezekana akawa tayari amehongwa kwa namna moja ama nyingine ili awe mstari wa mbele kujibu tuhuma zote, kutetea maovu yote na upuuzi wote wa kisiasa unaofanywa na mgombea huyo wa urais wa Chadema.
Ni vigumu katika hali ya kawaida kupata ujasiri mkubwa kiasi hicho, ule ambao umeshindikana kwa Lowassa mwenyewe, familia yake, Chadema yenyewe na hata washauri wake wa karibu, badala yake umekuwa ukifanywa na Mbatia ambaye hana uhusiano naye wowote!