MIUNDOMBINU YA ELIMU ZANZIBAR SASA YALINGANA NA MAHITAJI YA KARNE YA 21

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Zanzibar imepiga hatua kubwa katika kuimarisha mazin...

Latest Post

"Kesi yeyote ya ardhi itakayoonekana watendaji katika serikali au wenyeviti wa vijiji wanahusika wahusika hao watafikishwa mahakamani kwa majina yao na sio taasisi"- DC Kilindi, Tanga

Written By CCMdijitali on Monday, August 28, 2023 | August 28, 2023


Mkuu wa wilaya Kilindi Mh Hashim Mgandilwa amesema kuanzia Sasa kesi yeyote ya ardhi itakayoonekana watendaji katika serikali au wenyeviti wa vijiji wanahusika wahusika hao watafikishwa mahakamani kwa majina yao na sio taasisi

Mh Mgandilwa ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa akizungumza na watumishi wa tarafa za Mgera,Mswaki na viongozi wa kisiasa katika tarafa hizo kilichofanyika katika kata ya Kwediboma

Alisema ifike wakati tuone kila uhai una thamani kubwa na wanaotumia migogoro ya ardhi kwa manufaa yao hawatavumiliwa tena kwani migogoro ya ardhi na mingine katika Wilaya imekuwa ni tatizo ambalo kila mmoja anapaswa kuhakikisha tatizo hilo linaisha ama kupungua ili masuala mengine ya maendeleo yaendelee

Mh Mgandilwa alisema ikitokea mgogoro Kama vile mfugaji ameingiza mifugo katika shamba la mtu na kesi hiyo ikaripotiwa sehemu husika na baadae mkulima atoe taarifa ya kukataa kuendelea na shauri hilo kwa maamuzi wamemalizana wenyewe mkulima au mhusika huyo aliyesema haendelei na shauri hilo atafikishwa yeye mahakamani

Alisema hatua hiyo itatekelezwa kwa sababu ya kukithiri migogoro ya ardhi katika Wilaya Kilindi

Kikao hicho kilishirikisha waheshimiwa madiwani,wenyeviti wa vijiji na watumishi wa tarafa za Mgera na Mswaki

Mawasiliano Serikalini Kilindi DC


@ofisiyamkuuwamkoawatanga 
@ccm_kilindi @waziriwazirik @ortamisemi

DKT. TAX AWAPA WAKUU WA MIKOA MBINU ZA KUTEKELEZA DIPLOMASIA YA UCHUMI

Written By CCMdijitali on Sunday, August 27, 2023 | August 27, 2023

DKT. TAX AWAPA WAKUU WA MIKOA MBINU ZA KUTEKELEZA DIPLOMASIA YA
 UCHUMI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) amewapa Wakuu wa Mikoa mbinu mbalimbali za kutekeleza Diplomasia ya Uchumi katika Mikoa yao.
Dkt. Tax ametoa mbinu hizo tarehe 26 Agosti, 2023 wakati wa Mafunzo ya Uongozi kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa yanayofanyika katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere iliyopo Kibaha mkoani Pwani.

“Mbinu za kuibua na kutekeleza diplomasia ya uchumi ni nyingi kama vile kufungua balozi, kukusanya taarifa na uchambuzi, majadiliano,……………….lakini kwenu nyie Wakuu wa Mikoa mnaweza kufanya makongamano ya biashara na uwekezaji na kuzitangaza fursa mbailmbali za biashara katika mikoa yenu pamoja na elimu kwa Umma,” alisema Dkt. Tax.

“Kupitia mikoa yenu mnaweza mkafanya makongamano ya biashara na uwekezaji na kuzitangaza fursa za biashara katika mikoa yenu, ninyi ni wadau wakubwa wa kutekeleza diplomasia ya uchumi kwa vitendo na kuchangia maendeleo,” alisema Dkt. Tax

Alisema kuwa Serikali itaendelea kuboresha  mifumo ya sheiria, kiutendaji na kukuza mazingira ya kushindana Kimataifa na Ofisi za Wakuu wa Mikoa zina mchango mkubwa kufanikisha utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi na hivyo kuchangia maendeleo ya kiuchumi nchini.

“Serikali itaendelea kuboresha mifumo ya kisheria, kiutendaji na kukuza mazingira wezeshi kushindana kimataifa ambapo ofisi za wakuu wa Mikoa zina nafasi na mchango mkubwa wa kufanikisha utekelezaji wa Diplomasia ya uchumi, na kuchangia kasi ya maendeleo nchini,” alisema Dkt. Tax.

Waziri Tax aliongeza kuwa Wakuu wa Mikoa ni wadau wakubwa katika kutekeleza diplomasia ya uchumi kwenye mikoa yao kwani huibua fursa mbalimbali za biashara na uwekezaji zinazopatikana katika mikoa yao.

Pamoja na mambo mengine Waziri Tax aliongeza kuwa ofisi za Wakuu wa Mikoa ni wadau muhimu na wanalo jukumu la kibua fursa katika maeneo yao kama Mamlaka za msingi zinazobuni mipango ya biashara, miradi ya uwekezaji, uzalishaji, na utumiaji wa rasilimali katika ngazi ya mikoa.

Mafunzo ya Uongozi kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere, Kibaha mkoani Pwani yalianza tarehe 21 – 28 Agosti, 2023.

Rais Mwinyi amesema kuna haja kwa Zanzibar kuongeza vivutio vingi vya utalii kwa kubuni matukio maalumu ya kuwavutia wageni wengi na kuviimarisha vivutio vya asili vilivyomo Tanzania.

Written By CCMdijitali on Saturday, August 26, 2023 | August 26, 2023

Zanzibar,

26 Agosti, 2023

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amesema kuna haja kwa Zanzibar kuongeza vivutio vingi vya utalii kwa kubuni matukio maalumu ya kuwavutia wageni wengi na kuviimarisha vivutio vya asili vilivyomo Tanzania.

Akizungumza kwa niaba ya Rais Dk. Samia, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, aliyasema hayo kwenye ufunguzi wa Tamasha la nane la Kizimkazi, huko uwanja wa Paje Mkoa wa Kusini Unguja.

Rais Dk. Mwinyi alisema tamasha hilo linatoa fursa yakuendeleza utalii na kuutangaza mkoa wa kusini kiutalii na Zanzibar kwa ujumla kwa kufungua fursa nyingi za maendeleo ikiwemo biashara, uwekezaji na uchumi.

Alieleza matarajio yake ya baadae kwa tamasha hilo kuweka hitoria nyengine ya mkoa wa Kusini Unguja kwa kuongeza fursa nyingi za Utalii, uwekezaji na maendeleo ya biashara.

Sambamba na kueleza tamasha hilo mbali na kuongeza vivutio vya utalii vya ndani ya mkoa huo kama tukio la asili la ‘mwaka kogwa’ lakini kuendelea kuitangaza Zanzibar na Tanzania kwa ujumla kwa kuendeleza umoja na mshikamano wa Watanzania kwa pande zote za Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuwakutanisha pamoja kwa amani na upendo kupitia Tamasha la Kizimkazi ambako wasanii wengi, wananchi, taasiisi mbalimbali za binafsi, wadau wa maendeleo, wajasiriamali, wenyeji na wageni kukutana na kufurahika kwa pamoja.

Pia alieleza tamasha hilo limeendelea kuezi na kuimarisha utamaduni wa Tanzania kwa kuvienzi vyakula vya asili, kuimarisha makongamano, michezo, burudani na kuwawesha vijana kiuchumi kwa kubuni miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kukuza biashara, aidha, Dk. Mwinyi alieleza fursa za makampuni binafsi kuwekeza miradi mikubwa zikiwemo taasisi binafsi, tasisi za fedha na benki kutanua matawi yao kusini Unguja kutokana na Tamasha la Kizimkazi.

Hata hivyo, Rais Dk. Mwinyi aliipongeza Serikali ya Mkoa wa Kusini Unguja na kamati ya maandalizi ya Tamasha la Kizimkazi kwa kuelendeza juhudi za Rais Dk. Samia kwa kulienzi tamasha hilo.

Akizungumzia fursa za Uchumi wa Buluu na uwekezaji wa biashara, Rais Dk. Mwinyi alisema Mkoa wa Kusini Unguja umebarikiwa bahari na eneo kubwa la wazi kwa wilaya zake zote mbili za Kati na Kusini mwa Mkoa huo na kueleza kupitia Tamasha la Kizimkazi na fursa zinazotoka huko, sekta ya uvuvi itaimarika zaidi kwa kilimo cha kisasa cha mwani na kuongezeka tija kwa fursa nyingi za utalii kuendelea kufunguka.

Akitoa salam za mkoa, Mkuu wa Mkoa wa Kusini, Unguja Rashid Hadidi aliipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ushirikiano wanatoa kukuza maendelo ya mkoa huo kwa sekta zote ikiwemo kuimarishwa kwa miundombinu ya barabara za kisasa, ujenzi wa hospitali kubwa za Wilaya zenye mashine na vifaa tiba vya kisasa, skuli za ghorafa pamoja na kukamilika kwa ujenzi wa matangi matatu makubwa ya maji safi yenye uwezo wa kuchukua lita milioni 10 ambayo yatasaidia kusambaza maji kwa mkoa wote wa Kusini Unguja.

Tamasha la Kizimkazi liliasisiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan miaka nane iliyopita likiwa na lengo la kuunganisha umoja, ushirikiano na mshikamo wa Watanzania wa Mkoa wa kusini Unguja na Tanzania yote bila kujali tofauti za asili na siasa zao.

IDARA YA MAWASILIANO IKULU, ZANZIBAR


WAZIRI MABULA AWASILISHA VIPAUMBELE VYA SEKTA YA ARDHI KATIKA SEMINA YA MA-RC NA MA-RAS

WAZIRI MABULA AWASILISHA VIPAUMBELE VYA SEKTA YA ARDHI KATIKA SEMINA YA MA-RC NA MA-RAS

 

KIBAHA

 

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maedeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula amewasilisha vipaumbele vya wizara yake kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala katika semina ya uongozi katika Chuo cha Mwalimu Nyerere kilichopo kibaha mkoani Pwani.

 

Katika wasilisho lake leo tarehe 26 Agosti  202, Waziri Mabula alizungumzia masuala ya ukusanyaji mapato yatokanayo na sekta ya ardhi, mipango miji pamoja na maeneo ya uwekezaji ambayo yote wakuu hao wa mikoa wanalo jukumu la kusimamia kwenye mikoa yao.

 

Dkt Mabula aliwataka wakuu wa mikoa kusaidia katika kuongeza hamasa katika suala la ukusanyaji mapato ya serikali yatokanayo na sekta ya ardhi.

 

"Niwaombe mkasimamie mikakati ya ukusanyaji maduhuli hayo ikiwa ni pamoja na kuwakumbusha wananchi waliopo katika maeneo kulipa kodi ya pango la ardhi.

 

Kwa mujibu wa Dkt Mabula Rais Samia alitoa msamaha wa riba ya kodi kwa miezi 10 mafanikio yalionekana japo si kwa kiwango kilicho tarajiwa.

 

Pia aliwataka wakuu wa mikoa kuzisimamia halmashauri katika kutenga fedha katika bajeti za maendeleo ya sekta ya ardhi ili kuhakikisha ardhi inapangwa, kupimwa na kumilikisjwa.

 

"Halmashauri zitambue kuwa jukumu hilo bado ni la kwao na wanahitaji kuendelea kushiriki kikamilifu katika kutenga fedha ili kutekeleza majukumu yao na kuwezesha watumishi waliopo katika halmashauri kufanya kazi" alisema Dkt Mabula.

 

--------MWISHO------

 

Waziri wa Ardhi Mhe. Dkt Angeline Mabula akizungumza katika kikao cha wakuu wa mikoa na makatibu tawala kinachoendelea katika chuo cha uongozi cha Mwalimu J K Nyerere kibaha mkoani Pwani tarehe 26 Agosti 2023.

 

Sehemu ya washiriki semina ya uongozi inayofanyika katika chuo cha uongozi cha Mwalimu Julius Nyerere kibaha mkoa wa Pwani.

 

Waziri wa Ardhi Mhe. Dkt Angeline Mabula akizungumza katika kikao cha wakuu wa mikoa na makatibu tawala kinachoendelea katika chuo cha uongozi cha Mwalimu J K Nyerere kibaha mkoani Pwani tarehe 26 Agosti 2023.

 

Baadhi ya wakuu wa mikoa wakifuatilia wasilisho la Waziri wa Ardhi Mhe. Dkt Angeline Mabula wakati wa semina ya uongozi inayofanyika katika chuo cha uongozi cha Mwalimu Julius Nyerere kibaha mkoa wa Pwani. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)


SERIKALI IMETENGA BILIONI 1.5 KUIMARISHA HUDUMA YA UZAZI SALAMA ZANZIBAR.

Zanzibar,

26 Agosti, 2023

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amesifu jitihada za wadau wa maendeleo wakiwemo Mashirika ya Kimataifa, taasisi binafsi, makampuni na wahisani mbalimbali wanavyojitokeza kuunga mkono juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Dk. Mwinyi aliyasema hayo, viwanja vya Maisra Suleiman alipozungumza kwenye kampeni ya “Uzazi ni Maisha” iliyoandaliwa kwa ushirikiano wa Wizara ya Afya Zanzibar na Shirika la Kimataifa la Amref Afika, tawi la Tanzania yenye lengo la kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga Zanzibar.

“Kwa dhati kabisa napenda niwashukuru Amref Health Africa kwa kutoa msaada wa gari (Mobile van) ambayo itakuwa msaada muhimu kwa Wizara ya Afya kwenye shughuli mbalimbali zikiwemo kusafirisha wataalamu, kusafirisha sampuli na kutoa huduma za upimaji na ushauri nasaha kwa wananchi katika vituo tofauti vya afya hapa Zanzibar” alieleza Dk. Mwinyi.

Rais Dk. Mwinyi alisema, wadau hao wa maendeleo wamekua na mchango mkubwa kwa Serikali hasa kwenye masuala ya jamii na maendeleo kupitia sekta za Afya, Elimu na huduma za upatikanaji wa maji safi na Salama.

Aidha, alilipongeza Shirika la Amref kwa jitihada zao za kuanzisha kampeni za “Uzazi ni Maisha” zilizojumuisha matembezi ya mbio fupi na matembezi ya hiari, yaliyoanzia Kiembe Samaki kwa Butros Wilaya ya Magharibi B na kumalizikia viwanja vya Maisara, Zanzibar.

Alisema, uamuzi huo ni jitihada za kuunga mkono jitihada za Serikali za kupunguza na kuepusha vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga ambapo alieleza bado kiwango cha changamoto hiyo kipo juu.

Rais Dk. Mwinyi alieleza takwimu zinaonesha vifo vya kina mama 134 kati ya vizazi hai 100,000 kwa mwaka na vifo 28 vya watoto wachanga kati ya vizazi hai 1,000 kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2017, husababishwa na changamoto za huduma duni za mama na mtoto katika hospitali na vituo vya afya zikiwemo uhaba wa wahudumu na tatizo la kukosekana kwa dawa.

Dk. Mwinyi, alieleza matumaini yake kupitia kampeni hiyo, kwamba Serikali itaongeza vifaa tiba kwa vituo vya afya 28, sawa na asilimia 40.5 ya vituo vyote 69 vinavyotoa huduma za mama na mtoto Zanzibar. 

Pia, alieleza jitihada za Seriklali kuimarisha huduma za afya ya msingi kwa ajili ya uzazi salama, italeta mafanikio makubwa ya kulinda maisha ya mama na mtoto.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Naibu Waziri wa Afya, Zanzibar Hassan Hafidh alisema lengo la kuanzishwa kwa kampeni ya “Uzazi ni Maisha” ni kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto nchini.

Alisema, katika kulikabili tatizo hilo kivitendo, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeweka mikakati madhubuti ikiwemo kuwachukulia hatua kali za kisheria na nidhamu watumishi wote wa sekta ya Afya wanaokiuka sheria na taratibu za utumishi wao kutokana na uzembe kazini, kauli chafu, utovu wa nidhamu unaosababisha athari mbaya kwa mama na watoto hasa wakati wa kujifungua. Aidha alieleza Wizara imefanikiwa kuzizibidhi hali hiyo kwa asilimi kubwa.

Naye, Mwakilishi mkaazi wa Shirika la Amref Afika kwa upande wa Tanzania, Dk. Folence Temu alisema lengo la kuanzishwa kampeni hiyo ya “Uzazi ni maisha ni kukusanya shilingi Bilioni moja kwajili ya kununuliwa vifaa tiba vya hospitali na vituo vya afya 69 vinavyotoa huduma za mama na mtoto, Zanzibar.

Alisema, wakiwa kwenye mwaka wa pili wa kampeni yao, Shirika la Amref tayari limefanikiwa kukusanya milioni 557 na wamepokea ahadi za shilingi milioni 883 ambayo itafikisha lengo la kampeni hiyo kufikia 2024.

Kampeni ya “Uzazi ni Maisha” ilianza mwaka jana na inatarajiwa kukamilika mwakani inatekelezwa kwa kaulimbiu isemayo ”Changia vifaa tiba kwa uzazi salama” ambayo imechangia kufikia malengo ya kuanzishwa kwake mwaka wa pili sasa wa utekelezaji wake. 


IDARA YA MAWASILIANO IKULU, ZANZIBAR


Jamii yatakiwa kusimamia watoto kwenye Malezi mema ili kupata Taifa bora lenye vijana wazalendo

Written By CCMdijitali on Friday, August 25, 2023 | August 25, 2023

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla ameitaka Jamii kusimamia watoto kwenye Malezi mema ili kupata Taifa bora lenye vijana wazalendo na wenye uchu wa maendeleo ya Zanzibar.

 

Alhajj Hemed ameeleza hayo wakati akiwasalimia waumini wa Masjid Islah Chakechake Pemba alipojumuika nao katika Ibada ya Sala ya Ijumaa.

 

Amesema Zanzibar ni nchi yenye historia nzuri kwa wananchi wake kuwa na Tabia, silka na tamaduni njema zilizofanya kuitangaza Zanzibar Kitaifa na Kimataifa hivyo, Wazazi na Walezi ni vyema kusimamia dhima hiyo ili kupata jamii iliyosalimika na vitendo viovu.

 

Alhajj Hemed amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayoongozwa na Rais Dkt. Hussein Ali inaendelea kuweka mikakati Mizuri ya kielimu kuanzia elimu ya Maandalizi, msingi, Sekondari hadi Chuo ili vijana waweze kupata elimu  ya lazima kwa manufaa yao na Taifa kwa ujumla.

 

Sambamba na hayo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewataka Wazazi na Walezi kuwashauri vijana wao wanaomaliza elimu ya Sekondari kufanya maamuzi sahihi wanapochagua masomo yao elimu ya juu kwa kuzingatia Fani zilizopewa kipaumbele na Serikali ikiwemo Ualimu wa Sayansi pamoja na Madaktari Bingwa wa Magonjwa mbali mbali.

 

Aidha Alhajj Hemed ameitaka jamii kuyasaidia makundi Maalum ikiwemo watu wenye ulemavu, Mayatima, wazee na vijana jambo ambalo litaongeza mashirikiano na mapenzi katika Jamii.

 

Akitoa khutba ya Sala ya Ijumaa Shekh Walid Muhsin Juma ameikumbusha jamii ya waislamu kuwa na mapenzi baina yao na kuwa na tabia ya kustiri aibu za wengine na kueleza kuwa huo ni msingi wa kupata radhi za Allah (S.W).

 

Amesema Muumini wa kweli ni vyema kufanya mema kwa kufuata maamrisho ya Qur-an na Sunnah ili kutafuta radhi za Allah (S.W) Duniani na kesho Akhera.

 

         


WAZIRI DKT. CHANA AFUNGUA TAMASHA LA PILI LA UTAMADUNI, NJOMBE YANEEMEKA



Na Shamimu Nyaki

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amefungua Tamasha la pili la kitaifa la Utamaduni Agosti 25, 2023 katika viwanja vya Stendi ya zamani mkoani Njombe.

Katika Tamasha hilo wananchi wa Mkoa wa Njombe wameendelea kupata burudani na fursa ya kuuza na kuonesha bidhaa zao, huku mikoa mbalimbali iliyohudhuria tamasha hilo kupitia vikundi na Sanaa na ngoma vikionesha Utamaduni na kuuza kazi zao za ubunifu.

Akifungua Tamasha hilo Waziri Mhe. Pindi Chana amesema tamasha hilo ni utekekezaji wa Sera ya Utamaduni ya mwaka 1997 ambayo inatoa fursa kwa jamii kuenzi na kulinda mila na desturi pamoja na kuzirithisha kwa vizazi cha sasa na vijavyo.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Kissa Gwakisa Kasongwa amesema Tamasha hilo limetoa fursa kwa wananchi wa Njombe hatua inayowaongezea kipato katika biashara zao, kuona utamaduni wa mikoa mingine pamoja na kuonesha kuonesha utamaduni wao. 

Awali akitoa maelezo juu ya tamasha hilo Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Saidi Yakubu amesema tamasha hilo ni utekekezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alilolitoa Septemba mwaka 2021 mkoani Mwanza, lengo likiwa ni kurithisha Utamaduni, mila na desturi za makabila yote Tanzania Bara na Zanzibar pamoja na kutangaza Utamaduni wa Mtanzania.


Katibu Mkuu Bw. Yakubu amesema Tamasha hilo linajumuisha mashindano ya ngoma za asili, vyakula, maonesho ya flamu ikiwemo za Harakati za Ukombozi wa Bara la Afrika, kuitangaza Royal Tour, Mada mbalimbali kuhusu maadili na utamaduni pamoja na huduma ya upimaji wa afya na elimu ya lishe, uchangiaji wa damu pamoja na kuwepo kwa mechi za kirafiki na matembezi mafupi.

NHC YATAKIWA KUTILIA MKAZO UKUSANYAJI MADENI



Na Munir Shemweta, WANMM

Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii imelitaka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kuhakikisha linatilia mkazo ukusanyaji madeni ya wapangaji katika nyumba zake.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo Timetheo Mnzava amesema, pamoja na shirika hilo kujitahidi katika ukusanyaji malimbikizo ya kodi za wapangaji wake lakini bado linatakiwa kuongeza kasi ya ukusanyaji madeni kutoka kwa wadaiwa.

Akizungumza wakati wa Kikao cha kupokea taarifa ya utendaji kazi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) jijini Dodoma tarehe 25 Oktoba 2023, Mhe. Mnzava amelitaka pia shirika hilo kuweka msisitizo zaidi katika kuzuia kuzalisha madeni badala ya kusubiri mpaka wapangaji kuwa na malimbikizo makubwa ya madeni.

Aidha, Wajumbe wa Kamati hiyo ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Malisili na Utalii wametaka kuwepo mikakati madhubuti itakayowaogopesha wapangaji ili waweze kulipa kodi zao kwa wakati

Vile vile, Kamati hiyo imeonesha kuridhishwa na utendaji kazi wa shirika hilo katika kutekeleza miradi yake ambapo wamelitaka Shirika kuangalia namna ya kujenga nyumba za gharama nafuu kwa kutumia teknolojia rahisi.

‘’Niipongeze NHC pamoja na Wizara ya Ardhi maana kazi za shirika zinaonekana hata kwa macho ila nisisitize muweke jitihada pia katika ukarabati wa nyumba zenu ili wapangaji wakae vizuri’’ alisema mjumbe wa kamati Cecilia Paresso.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza mbele ya Kamati hiyo amesema, kwa sasa upo uhitaji mkubwa wa nyumba na serikali iko katika marekebisho ya sera ili kuwezesha ushiriki wa taasisi na sekta binafsi katika uzalishaji nyumba.

‘’Kama serikali tutahakikisha kasi ya ujenzi wa nyumba inaongezeka maana takwimu za sensa ya watu na makazi zimeonesha uhitaji mkubwa wa nyumba na uzalishaji ukiwa mdogo hivyo msisitizo ni kuzalisha nyumba za gharama nafuu kwa kutumia teknolojia rahisi’’ alisema Dkt Mabula.

----------------------------------MWISHO-------------------

 

 

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula akizungumza mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii wakati wa uwasilishaji taarifa ya shirika la Nyumba la Taifa (NHC) tarehe 25 Agosti 2023.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakiwa katika kikao cha kupokea taarifa ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) tarehe 25 Agosti 2023 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Hamad Abdallah akiwasilisha taarifa ya Shirika lake mbele ya Kamati ya Kudumu ya Ardhi Maliasili na Utalii jijini Dodoma tarehe 25 Agosti 2023.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii Timotheo Mnzava akizungumza wakati Kamati yake ikipokea taarifa ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) tarehe 25 Agosti 2023 jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Lucy Kabyemera akizungumza mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii wakati wa uwasilishaji taarifa ya shirika la Nyumba la Taifa (NHC) tarehe 25 Agosti 2023.
Sehemu ya watendaji wa Wizara wa Wizara ya Ardhi pamoja na wale wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) wakiwa katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii kupokea taarifa ya NHC jijini Dodoma tarehe 25 Agosti 2023. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)



SHUKENI CHINI MKATOE ELIMU YA LISHE-RC MONGELLA.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella amezitaka Kamati za Lishe Mawilayani kuhakikisha zinakwenda Vijijini kufundisha na kuhamasisha masuala ya Lishe kwa Jamii. Amesema hayo aliopokuwa akiongoza Kikao cha Lishe Mkoa wa Arusha kilichofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wakati wakijadili mpango mkakati wa namna ya kukabiliana na changamoto ya Lishe duni katika Jamii hususan kwa siku 1000 za mtoto tangu azaliwe. 

Amesema kuwa suala la Lishe halina mjadala wala mbadala na kuwa Lishe bora ndiyo inayopelekea kupata nguvu kazi iliyobora na Viongozi bora, Viongozi bora huzaa Taifa imara, hivyo kucheza na masuala ya Lishe ni kuhujumu mipango ya maendeleo ya Taifa kitu ambacho ni hatari kwani hupelekea Taifa kuwa na idadi kubwa ya Watu wenye udumavu. 

Katika kuhakikisha suala la Lishe linapewa kipaumbele, Mongella ameziagiza Kamati za Lishe kufanye ziara Vijijini kwaajili ya kwenda kutoa Elimu na hamasa kwa Jamii ili kuwapa uelewa mpana wa faida za Lishe kwa mama mjamzito na Watoto chini ya Miaka 5 kwani kila Halmashauri ilishagizwa kutenga fedha za kuchangia mpango Lishe kwa mtoto mchanga. 

"Nawaombeni Wakuu wa Wilaya mkazisimamie Kamati za Lishe ili ziweze kutoa elimu ya Lishe kwenye Kaya hii itasaidia Jamii kupata uelewa wa umuhimu kwa mama mjamzito na kwa siku 1000 za mtoto toka azaliwe" Alisema Mongella. 

Sambamba na hilo, Mongella amesema ni vyema Ofisi za Waganga wa Wakuu wa Wilaya wakateuwa timu ya Maafisa uhamasishaji Lishe waliobobea katika eneo hilo na ambao wanatambua malengo na mikakati ya Taifa kuhusu Lishe kwani kwa kutofanya hivyo zoezi la Lishe litakuwa bure. 

"Tunapofika kwenye suala la uelemishaji nawaomba saana Waganga Wakuu wa Wilaya lazima tupeleke Maafisa Lishe wanajua kusoma vizuri Scorecard ya Lishe ili watusaidie kutoa elimu na kutupa takwimu sahihi za hali ya Lishe kwenye Wilaya zetu" Alisema Mongella. 

Kikao hicho cha Lishe Mkoa kilihudhuriwa na Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi pamoja na Wataalam wa Lishe toka Wilaya zote za Mkoa wa Arusha ambapo kila Wilaya iliwasilisha taarifa zake za utekelezaji na mikakati ya kukabiliana na changamoto za Lishe katika Jamii.

🇹🇿RAIS SAMIA AMEWEKA HISTORIA. MKUTANO WA BRICS+, KWELI MAMA YUKO KAZINI HASWAAA! 🇹🇿


Ukiachana na hotuba ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu katika mkutano wa BRICS nchini Afrika Kusini iliyoangazia masuala ya ushirikiano wa kimataifa, ukuzaji biashara na uwekezaji, utatuzi wa pamoja wa changamoto za kidunia na maboresho ya Umoja wa Mataifa.

Tanzania tumevuna vingi sana katika mkutano huu wa BRICS endapo tutajiunga na muungano huu tutakuwa katika kundi la nchi nufaika. 

Kwa tathimini BRICS+  asilimia 45 ya mafuta yanayozalishwa Duniani au zaidi ya pipa milioni 37 zinazozalishwa kwa siku zinatoka katika Jumuiya hii. 

Asilimia 50 reserve ya Gesi asilia inapatikana katika muunganiko huu wa nchi za BRICS+ 

Asilimia 30 ya GDP Dunia inapatikana katika nchi zinazounda muunganiko wa BRICS+ 

Kwa siku ya Jana Rais Samia alifanya mikutano midogo kando na mkutano wa BRIC+ jambo ambalo liliwavuta viongozi wengi zaidi kutaka kufanya vikao naye pamoja na kutafuta fursa za ushirikiano;

Kwa siku ya Jana pekee Rais Samia alifanya vikao takribani 9 na viongozi mashuhuri wa Dunia.

1. Mazungumzo na Rais wa China Xi jinping kikao cha pamoja. 

2. Alikutana na Rais wa Brazil Lula Da Silva na kufanya naye kikao. 

3. Alikutana na Rais wa Afrika kusini Cyril Ramaphosa na kufanya naye kikao 

4. Alifanya mazungumzo na Rais wa Iran Seyyed Ibrahim Rais. Kikao cha kando 

5. Alifanya kikao na Waziri Mkuu wa Bangladeshi Sheikh Hassina Wazeed. 

6. Alifanya kikao na Rais wa Malawi Lazarus Chakwera 

7. Alifanya kikao na Rais wa Senegal Macky Sall. Pamoja na kukutana na viongozi wengine mashuhuri yote ni katika kukuza diplomasia ya ushirikiano na kutafuta masoko ya pamoja. 

Tunaweza kusema Rais Samia she is always step ahead katika kutazama fursa na kupanga mipango ya mbeleni.

#Mamayukokazini

MAPOKEZI YA NAIBU KATIBU MKUU WA CHAMA CHA   MAPINDUZI TAIFA BARA Mkoani Arusha  Ndugu Christina Mndeme

Written By CCMdijitali on Thursday, August 24, 2023 | August 24, 2023

📸:- MAPOKEZI YA NAIBU KATIBU MKUU WA CHAMA CHA   MAPINDUZI TAIFA BARA Mkoani Arusha  Ndugu Christina Mndeme   06 Oktoba, 2022 kwenye viwanja vya CCM Mkoa wa Arusha. 
Pichani ni Waziri wa Maji Mheshimiwa @jumaa_aweso
Kiongozi muungwana asiyekuwa na makuu, mtoto wa Pangani akifurahi jambo na Cde Jasper Kishumbua akimwambia karibu Arusha Morani !!!!

@jumaa_aweso @ofisiyambungepangani



 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link