MIUNDOMBINU YA ELIMU ZANZIBAR SASA YALINGANA NA MAHITAJI YA KARNE YA 21

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Zanzibar imepiga hatua kubwa katika kuimarisha mazin...

Latest Post

SERIKALI YAIOMBA ACBF KUJENGEA UWEZO WATAALAMU KWENYE MASUALA MTAMBUKA

Written By CCMdijitali on Friday, February 7, 2025 | February 07, 2025

 SERIKALI YAIOMBA ACBF KUJENGEA UWEZO WATAALAMU KWENYE MASUALA MTAMBUKA


Serikali imeiomba Taasisi ya Kujenga Uwezo Afrika (Africa Capacity Building Foundation – ACBF) kuwajengea uwezo zaidi wataalamu nchini na kuweka kipaumbele kwenye masuala ya ufadhili katika Mabadiliko ya Tabianchi, Nishati safi, Kilimo Biashara, usalama wa Chakula, Biashara, Uwekezaji na Utawala wa kiuchumi na kijamii.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, wakati alipokutana na Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Kujenga Uwezo Afrika (Africa Capacity Building Foundation – ACBF), Bw. Mamadou Biteye, katika ofisi ya Wizara ya Fedha, jijini Dodoma.

Dkt. Mwamba alisema kuwa, vipaumbele hivyo vinalenga kuleta mapinduzi katika kujenga uwezo nchini sambamba na masuala ya sayansi na teknolojia, ubunifu na kidigitali, uchumi wa buluu, na diplomasia ya kiuchumi, kwa kuwa vinawiana kwa ukaribu na Mpango Mkakati wa ACBF wa 2023–2027.

“Tunashukuru kwa fursa ya kushiriki katika mipango ijayo, hasa ile inayolingana na maeneo ya kipaumbele yaliyoainishwa katika Mpango Mkakati wa ACBF wa 2023–2027, kwani maeneo hayo yanahusiana kwa karibu na vipaumbele vyetu vya kitaifa vya kujenga uwezo”

Aidha Dkt. Mwamba alisema kuwa Tanzania imekuwa mnufaika mkubwa wa taasisi hiyo tangu mwaka 1993 ambapo hadi sasa imefanikiwa kupata msaada wa takriban jumla ya milioni 9 zilizoenda katika taasisi mbalimbali ikiwemo Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Ofisi ya Mtakwimu Mkuu Zanzibar, Mtandao wa Kielektroniki wa Jamii wa Tanzania (TANZANET) na REPOA, ambazo zimeimarisha uwezo wetu kama Taifa.

Aliongeza kuwa, katika kukabiliana na changamoto za karne ya 21, umuhimu wa kujenga uwezo hauwezi kuepukwa ili kukabiliana na changamoto hizo ipasavyo zikiwemo Utofauti wa Uchumi, Ukuaji wa Teknolojia, mabadiliko ya tabianchi ili kuhakikisha taasisi zinakua imara imara sambamba na rasilimali watu wenye ujuzi, hivyo jukumu la ACBF linabaki kuwa la umuhimu mkubwa.

“Tunafarijika kuona kwamba nchi yetu ni miongoni mwa nufaika wa mradi mpya wa kuongeza uwezo na kuleta Mabadiliko ya Kimuundo Afrika (Capacity Development for Africa’s Structural Transformation (CADAST) project), ambayo italeta mapinduzi katika kuimarisha usimamizi wa uchumi na fedha, na matumizi bora ya rasilimali za umma” aliongeza Dkt. Mwamba.

Naye kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Kujenga Uwezo Afrika (Africa Capacity Building Foundation – ACBF), Bw. Mamadou Biteye, alisema kuwa Miongoni mwa vitu walivyovibaini kwa kushirikiana na Benki ya Dunia ni kwamba, kiwango cha kutumia fedha zinazotolewa na Mashirika ya kimataifa ni mdogo sana, ambapo kwa upande wa Benki ya Dunia kiwango ni asilimia 30 tu na asilimia 70 ya fedha zinazotolewa hazitumiki.

Amesema kuwa mpango wa Mafunzo kwa nchi za Afrika kuhusu uwezo wa usimamizi wa miradi utasaidia kwa kiwango kikubwa katika kutumia fedha zinazotolewa.

“Tutaendelea kuimarisha uwezo wa sekta binafsi kushiriki katika uwekezaji kwenye sekta ya Nishati kwa kuboresha sheria ndani ya nchi za Afrika, lengo ni kuchochea maendeleo ya sekta hiyo itakayoleta matokeo chanya kwa wananchi kwa kuwa Afrika bado ipo nyuma kwenye sekta ya nishati ukilinganisha na maeneo mengine” aliongeza Bw. Biteye






 

WATAALAMU WA UNUNUZI NA UGAVI WAASWA KUZINGATIA MADILI

 Na Mwandishi Wetu, Mwanza

 

Wataalamu wa sekta ya ununuzi wa umma wameaswa kuzingatia maadili ya taaluma ya fani yao katika usimamizi wa miradi ya umma ili kuiwezesha Serikali kupata thamani halisi ya fedha katika miradi yake. 

 

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Said Mtanda katika hotuba yake iliyosomwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Mhe. Hassan Masala wakati wa kufunga mafunzo ya Moduli ya uwasilishaji na ushughulikiaji wa malalamiko na rufaa (Complaint and Appeal Management Module) katika Mfumo wa Ununuzi wa Umma kwa njia ya Kieletroniki (NeST) yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA).

 

Mhe. Mtanda ameongeza kuwa kuzingatia maadili ya taaluma ya fani hiyo katika usimamizi wa miradi ya siyo tu kutaiwezesha Serikali kupata thamani halisi ya fedha bali kutaiheshimisha fani ya ununuzi na ugavi pamoja na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

 

“Kwa kuwa matumizi ya moduli ya moduli ya kuwasilisha malalamiko na rufaa kieletroniki huokoa muda, gharama na kuongeza uwazi na uwajibikaji katika michakato ya zabuni za umma.  Nendeni mkaitumie elimu hii kuwaelimisha na wengine ili waweze kuielewa na kuitumia moduli, naamini ninyi mlioshiriki mafunzo ya awamu hii mtakuwa mabalozi wazuri wa Moduli hii na PPAA kwa ujumla,” amesema Mhe. Mtanda

 

Naye Katibu Mtendaji wa PPAA, Bw. James Sando amesema baada ya Serikali kujenga mfumo wa Ununuzi wa Umma kwa njia ya Kieletroniki (NeST) na kuweka sharti la lazima kufanya ununuzi wa umma katika mfumo huo, PPAA nayo ilishirikiana na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) kujenga moduli ya kuwasilisha na kushughulikia malalamiko na rufaa kieletroniki ili kuwawezesha wadau wa ununuzi wa umma kuwasilisha malalamiko na rufaa zao kieletroniki. 

 

“Katika kipindi cha siku tatu washiriki wameweza kujifunza masuala muhimu kuhusu mfumo wa ununuzi wa umma nchini Tanzania ikiwemo kuitazama kwa ufupi Sheria ya Ununuzi wa Umma ya Mwaka 2023, kufanya mapitio ya Mfumo wa NeST pamoja na namna ya Uwasilishaji wa malalamiko na rufaa kwa kutumia moduli katika hatua mbalimbali,” amesema Bw. Sando.

 

Bw. Sando ameongeza kuwa washiriki wa mafunzo wamejifunza moduli ya uwasilishaji na ushughulikiaji wa malalamiko na rufaa ambayo inajumuisha maeneo ya uwasilishaji wa malalamiko kwa Afisa Masuuli wa taasisi nunuzi iliyotangaza zabuni, uwasilishaji wa Rufaa kwa Mamlaka ya Rufani (PPAA).

 

Maeneo mengine ni jinsi mzabuni anavyoweza kujiunga katika Rufaa iliyofunguliwa, taratibu za uwasilishaji wa maombi mbalimbali ikiwemo ombi la nyongeza ya muda wa kuwasilisha rufaa nje ya muda ulioainishwa katika sheria, ombi la kutengua uamuzi uliotolewa kwa kusikiliza shauri la upande mmoja na ombi la kukazia hukumu.

 

“PPAA imejipanga vyema kuendelea kutoa mafunzo ya matumizi ya Moduli kwa wadau wa ununzi nchini kupitia kanda mbalimbali, hivyo wale ambao hawajafikiwa wajiandae kwani tutawafikia kupitia kanda zao zikiwemo kanda ya Kaskazini, Nyanda za Juu Kusini, Kusini na Kati,” ameongeza Bw. Sando

 

Mafunzo hayo ya siku tatu yaliyojumuisha washiriki zaidi ya 580 yamefanyika mkoani Mwanza kuanzia tarehe 4 – 6 Februari, 2025 yakijumuisha mikoa ya Mwanza, Geita, Mara, Kagera, Simiyu na Shinyanga. 

 

Awamu ya kwanza ya mafunzo ya matumizi ya moduli iliyofanyika Mwezi Mei 2024 kwa mikoa ya kanda ya Pwani iliyojumuisha Dar es Salaam, Pwani, Tanga na Morogoro.

 

Mwisho


Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Mhe. Hassan Masala akifunga mafunzo ya Moduli ya uwasilishaji na ushughulikiaji wa malalamiko na rufaa (Complaint and Appeal Management Module) katika Mfumo wa Ununuzi wa Umma kwa njia ya Kieletroniki (NeST) yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) Jijini Mwanza


Mwenyekiti wa Mamlaka ya Rufani, Jaji Mstaafu Mhe. Sauda Mjsiri akizungumza na washiriki wa mafunzo ya moduli ya kuwasilisha rufaa kieletroniki (hawapo pichani) wakati wa kufunga mafunzo ya Moduli ya uwasilishaji na ushughulikiaji wa malalamiko na rufaa (Complaint and Appeal Management Module) katika Mfumo wa Ununuzi wa Umma kwa njia ya Kieletroniki (NeST) Jijini Mwanza

Katibu Mtendaji wa PPAA, Bw. James Sando akizungumza na washiriki wa mafunzo ya moduli ya kuwasilisha rufaa kieletroniki (hawapo pichani) wakati wa kufunga mafunzo ya Moduli ya uwasilishaji na ushughulikiaji wa malalamiko na rufaa (Complaint and Appeal Management Module) katika Mfumo wa Ununuzi wa Umma kwa njia ya Kieletroniki (NeST) Jijini Mwanza

Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Mhe. Hassan Masala akifunga mafunzo ya Moduli ya uwasilishaji na ushughulikiaji wa malalamiko na rufaa (Complaint and Appeal Management Module) katika Mfumo wa Ununuzi wa Umma kwa njia ya Kieletroniki (NeST) yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) Jijini Mwanza




WANANCHI WATAKIWA KUTUMIA FURSA YA MIRADI KUUNGANISHA UMEME - MHE. KAPINGA

Written By CCMdijitali on Wednesday, February 5, 2025 | February 05, 2025

 WANANCHI WATAKIWA KUTUMIA FURSA YA MIRADI KUUNGANISHA UMEME - MHE. KAPINGA


Naibu Waziri wa Nishati, Mhe Judith Kapinga ametoa rai kwa wananchi kuunganisha huduma ya umeme wakati miradi mbalimbali ya umeme inapotekelezwa ili kuepuka gharama inayoweza kutokea pale miradi inapokuwa imekamilika.


Mhe. Kapinga ameyasema hayo leo Februari 05 2025 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la la Mbunge wa Tanga Mjini Mhe. Ummy Mwalimu aliyetaka kufahamu Serikali ina mkakati gani wa kuwaunganishia umeme wa gharama nafuu kwa Wananchi wa maeneo ya Pembezoni yenye sifa za Vijiji mkoani Tanga.

"Katika kurahisisha upatikanaji wa huduma ya umeme wa bei nafuu kwa maeneo ya pembezoni mwa Jimbo la Tanga Mjini, Serikali kupitia REA inaendelea kutekeleza Mradi wa Peri-Urban III", Amesema Mhe. Kapinga.


Ameongeza kuwa mradi huo unatekelezwa na Mkandarasi OK Electrical kwa kuunganisha wateja kwa baadhi ya mitaa kwa gharama ya shilingi 27,000 ambapo mpaka sasa jumla ya wateja 1,302 wameshaunganishiwa huduma ya umeme. Mhe. Kapinga amesema maeneo ya Tanga Mjini yaliyosalia yapo kwenye mradi wa kupeleka umeme kwenye vitongoji 15 vya kila Mbunge (HEP IIA) ambapo Jimbo la Tanga Mjini litapelekewa umeme kwenye mitaa 15.

Akielezea kuhusu Serikali kuanzisha utaratibu wa kuwaunganishia umeme wananchi kwa mkopo, Mhe. Kapinga amesema Serikali inatekeleza miradi mbalimbali ya umeme ili kuwafikia wananchi kwa gharama nafuu ya shilingi 27,000/-.

Mhe. Kapinga ameongeza kuwa TANESCO ilishawahi kuwaunganishia wananchi kwa kuwakopesha ambapo ilikutana na changamoto ya wananchi kutokuwa na utayari ya kulipa madeni yao.

Akijibu swali Mbunge wa Ilemela, Mhe. Angelina Mabula aliyetaka kufahamu mitaa ya Masenene, Kilabela, Bujingwa, Nyanguku, Butimba na Toronto itapatiwa umeme kutokana na kuondolewa katika mitaa 15 inayotekelezwa na REA kutokana na kuwepo kwa njia kubwa ya umeme.

Akijibu swali hilo Mhe. Kapinga amesema miradi ya vitongoji ni ya ujazilizi ambayo inajumuisha ujenzi wa miundombinu ya umeme kwenye maeneo ambayo yamepitiwa na njia kubwa ya umeme ambapo pamoja na mitaa hiyo itanufaika.

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe Judith Kapinga akijibu maswali Bungeni leo Januari 05, 2025




MFUMO WA KITAIFA WA TAARIFA ZA KIJIOGRAFIA KUCHANGIA UCHUMI WA TAIFA

Written By CCMdijitali on Tuesday, February 4, 2025 | February 04, 2025

 Na Munir Shemweta, WANMM

 

Serikali imesema Mfumo wa Kitaifa wa Taarifa za Kijografia (National Spatial Data Infrastructure- NSDI) ni kiungo muhimu cha dira ya kimkakati ya uchumi wa kidigitali wa Tanzania 2024-2034 na kuchangia uchumi imara wa Taifa.

 

Uanzishwaji Mfumo wa Kitaifa wa Taarifa za Kijografia (NSDI) ni jambo la kimkakati kwa maendeleo ya Taifa.

 

Hayo yameelezwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi. Lucy Kabyemera wakati wa uzinduzi wa warsha ya wataalamu ya kuandaa Mpango Kazi wa Uanzishwaji Mfumo wa Kitaifa wa Taarifa za Kijografia (NSDI) jijini Dodoma.

 

‘’Kwa kifupi NSDI ni msingi wa kufanikisha malengo ya maendeleo ya Tanzania ikiwa ni pamoja na Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2050 inayoandaliwa hivi sasa’’ amesema.

 

Kwa mujibu wa Naibu Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Ardhi, mfumo wa NSDI utaiwezesha nchi kujua kwa mapana ufanisi na mipango ya maendeleo, rasilimali zote za nchi na athari za mabadiliko ya tabia nchi, vikwazo vya uchumi na maendeleo ya nchi na kuboresha upatikanaji taarifa muhimu za kuimarisha mifumo ya usalama na uchumi wa nchi.

 

Aidha, Bi Kabyemera amesema, Sera ya Kitaifa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) 2023 inasisitiza umuhimu wa kutumia teknolojia kwa maendeleo ya jamii na kuichumi hivyo mfumo huo unalingana kikamilifu na sera hii kwa kutoa miundombinu ya data ya kijografia inayohitajika Mamlaka ya Serikali Mtandao ikiwa ni kiwezeshi muhimu katika kupanga na kuanzisha NSDI.

 

Akigusia Dira ya kidigitali ya Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 2030, Bi Kabyemera amesema dira hiyo inalenga kuiweka Tanzania kuwa kinara wa mawasiliano ya kidigitali na Mfumo wa Kitaifa wa Taarifa za Kijiografia ni kipengele muhimu cha dira hiyo kwa kuwa itawezeshwa kuunganishwa taarifa za kijiografia katika huduma mbalimbali za kidigitali.

 

‘’Mfumo huo utakaopoanzishwa utawezesha na kuhakikisha matumizi bora ya taarifa za kijografia kwa ajili ya kufanya maamuzi ya kupanga mipango mbalimbali katika sekta zote za maendeleo ya uchumi wan chi yetu’’ amesema Bi Kabyemera.

 

‘’Ni juhudi za pamoja za kuhakikisha kuwa taarifa za kijiografia zinapatkana kwa urahisui na kutumika kwa njia sahihi katika taasisi za serikali, mashirika ya umma, sekta binafsi na taasisi za elimu na utafiti’’ amesema.

 

Mfumo wa Kitaifa wa Taarifa za kijiografia ni rasilimali muhimu kwa ajili ya kufanya maamuzi sahihi katika maeneo mbalimbali kama vile mipangpo miji, usimamizi wa maafa, kilimo na uhifadhi ya mazingira.

 

Uanzishwaji mfumo huo kutaweza kuboresha usahihi na ufanisi wa usimamizi wa ardhi, kusaidia usimamizi endelevu wa rasilimali za asili na ulinzi wa mazingira na kurahisisha mipango na uwekezaji wa msingi katika sekta za uchumi.

 

Warsha hiyo ya uandaaji Mpangokazi wa uanzishwaji Mfumo wa Kitaifa wa Taarifa za Kijografia (National Spatial Data Infrastructure- NSDI) ni ya siku sita kuanzia Februari 3-7, 2025.

 

-------------MWISHO----------


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi. Lucy Kabyemera (Katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu wanaoshiriki warsha ya kuandaa Mpangokazi wa uanzishwaji Mfumo wa Kitaifa wa Taarifa za Kijografia (NSDI) jijini Dodoma jana. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)

Mratibu wa Mradi wa Kuimarisha Miundombinu ya Upimaji na Ramani Dkt. Erick Mwaikambo akichangia mada wakati wa warsha ya ya kuandaa Mpangokazi wa uanzishwaji Mfumo wa Kitaifa wa Taarifa za Kijografia (NSDI) inayofanyika jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Hamdouny Mansoor akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku tano kuandaa Mpangokazi wa uanzishwaji Mfumo wa Kitaifa wa Taarifa za Kijografia (NSDI) inayofanyika jijini Dodoma.

Sehemu ya washiriki wa warsha ya kuandaa Mpangokazi wa uanzishwaji Mfumo wa Kitaifa wa Taarifa za Kijografia (NSDI) inayofanyika jijini Dodoma.

Sehemu ya washiriki wa warsha ya kuandaa Mpangokazi wa uanzishwaji Mfumo wa Kitaifa wa Taarifa za Kijografia (NSDI) inayofanyika jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi. Lucy Kabyemera akizungumza wakati akifungua warsha ya siku tano kuhusu Uandaaji Mpangokazi wa uanzishwaji Mfumo wa Kitaifa wa Taarifa za Kijografia (NSDI) jijini Dodoma jana. Kulia ni Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani Wizara ya Ardhi Bw. Hamdouny Mansoor na kushoto ni Prof Elifuraha Mtalo.


WAKILI MKUU WA SERIKALI ATOA WITO WA MATUMIZI YA MIFUMO YA KIDIJITALI

Written By CCMdijitali on Sunday, February 2, 2025 | February 02, 2025

 

WAKILI MKUU WA SERIKALI ATOA WITO WA MATUMIZI YA MIFUMO YA KIDIJITALI KWA AJILI YA UFUATILIAJI WA MIGOGORO NA UIMARISHAJI WA HAKI

Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi ametoa wito kwa taasisi zote za kisheria na wadau wa haki nchini kutumia mifumo ya kidijitali kupata takwimu sahihi zitakazowawezesha kufuatilia migogoro yote waliyoisikiliza ili kuhakikisha inamalizika kwa mafanikio.

Dkt. Possi ametoa wito huo tarehe 01 Februari, 2025 alipotembelea mabanda ya maonesho ya taasisi mbali mbali nchini zinazoshiriki Maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini yanayoendelea kwenye viwanja vya Nyerere Square vilivyopo jijini Dodoma. Dkt. Possi ameeleza kuwa matumizi ya mifumo ya kisasa yatasaidia kuboresha usimamizi wa haki na kuongeza uwajibikaji katika utatuzi wa migogoro ya kisheria kwa kuwa kwa kiasi kikubwa itawezesha kutoa takwimu sahihi na kwa haraka pale taasisi husika itakapohitaji kufahamu mwenendo wa mgogoro husika ulioshughulikiwa.

Akizungumza na watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria, Dkt. Possi  amesisitiza kuwa mifumo ya kidijitali ina uwezo mkubwa wa kuboresha utendaji kazi wa taasisi za kisheria kwa kuwezesha upatikanaji wa taarifa kwa wakati hatua itakayosaidia kuhakikisha migogoro yote inayoshughulikiwa kwenye kliniki za sheria inamalizika ili wananchi waweze kufanya shughuli zao za kukuza uchumi kwa amani. “Kwa kutumia mifumo ya kisasa, tunaweza kufuatilia mwenendo wa migogoro yote kwa urahisi ili kuhakikisha migogoro yote inasimamiwa kwa weledi na kupunguza ucheleweshaji wa haki ili wananchi waendelee na shughuli zao za kujiletea maendeleo wao binafsi na taifa kwa ujumla,” alisema Dkt. Possi.

Alibainisha kuwa matumizi sahihi ya mifumo hiyo yatasaidia kuondoa changamoto zinazoikabili Sekta ya Sheria nchini katika kushughulikia migogoro ikiwa ni pamoja na kupotea kwa nyaraka muhimu ambazo zimechangia ucheleweshaji wa maamuzi huku akisisitiza taasisi zinazohusika na usimamizi wa sheria kushirikiana katika kuunda na kutekeleza mifumo ya ki dijitali inayolenga kuboresha uwajibikaji na uwazi.

Dkt. Possi alieleza kuwa mifumo hii itaiwezesha Serikali kupata takwimu sahihi kuhusu migogoro inayoshughulikiwa, muda wa utatuzi wa migogoro husika na kiwango cha mafanikio ya migogoro inayosimamiwa na kumalizika kwa mafanikio makubwa hatua hii itatimiza azma ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuhakikisha tunajenga jamii imara isiyo na migogoro kwa kuhakikisha wananchi wanaishi kwa amani ili waweze kuendelea na shughuli zao za kujiletea maendeleo.

Akizungumzia namna Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali inavyochangia kukuza pato la taifa, Dkt. Possi amesema kuwa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali imehakikisha wakati wote kuwa rasilimali za nchi zinalindwa ikiwemo miradi mikubwa ya maendeleo kama vile bwawa la kufua umeme la Mwalimu Nyerere, mradi wa bomba la mafuta kutoka Hoima Uganda hadi Chongoleani mkoani Tanga, ujenzi wa madaraja makubwa ya Tanzanite na Kigongo Busisi Feri linalojengwa Jijini Mwanza ambayo miradi hii imekuwa chachu ya maendeleo katika kujenga na kukuza uchumi wa nchi.

“Miradi inalindwa kwa kuhakikisha kuwa utekelezaji wake hauathiriwi wala kukwama kutokana na migogoro na pale inapotokea changamoto Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali inasimama kuhakikisha kuwa mradi hausimami,haukwami au kushindwa kutekelezwa kutokana na migogoro na Ofisi yetu imekuwa inashughulika kwa njia moja au nyingine katika uendelezaji wa miradi na kuhakikisha kuwa migogoro haiwi chanzo cha kuzuia utekelezaji wa miradi mbali mbali nchini”, amesisitiza Dkt. Possi.

Ameongeza kuwa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali imeendelea kuzishauri taasisi za Serikali ipasavyo pamoja na kumaliza mashauri nje ya Mahakama hatua ambayo imesaidia kupunguza migogoro na kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi. Naye Afisa Mchunguzi Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria ndugu Laurent Bulilo amesema kuwa wamekuwa na kawaida ya kufuatilia migogoro na mashauri yote kupitia Mfumo wa Mama “Samia Legal Aid Campaign System” hatua ambayo imesaidia kwa kiasi kupunguza migogoro kwenye jamii.

Dkt. Possi ameonyesha jinsi Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali inavyochangia kukuza pato la taifa kupitia usimamizi wa mali za umma, mikataba ya kimataifa na uimarishaji wa mazingira ya biashara. Pia, ameahidi kuendelea kushirikiana na wadau wote wa sheria hasa wadau wa haki madai katika matumizi ya TEHAMA ili kuhakikisha mifumo inasomana ili kuongeza ufanisi katika uendeshaji wa mashauri ya Serikali.


Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi, akiwasili kwenye viwanja vya Nyerere Square alipotembelea mabanda ya wadau mbalimbali wanaoshiriki Maadhimisho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea Jijini Dodoma kwa lengo la kuona namna wadau hao wanavyotekeleza majukumu yao.



 

Msajili wa Mahakama ya Tanzania, Bi. Eva Nkya akimkabidhi cheti cha ushiriki wa Maadhimisho ya Wiki ya Sheria, Wakili wa Serikali wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, ndugu Salehe Manoro wakati wa maadhimisho hayo yanayoendelea Jijini Dodoma.


Msajili wa Mahakama ya Tanzania, Bi. Eva Nkya akimkabidhi cheti cha ushiriki wa Maadhimisho ya Wiki ya Sheria, Wakili wa Serikali wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, ndugu Salehe Manoro wakati wa maadhimisho hayo yanayoendelea Jijini Dodoma.


Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Ally Possi akiwa na watumishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kwenye banda la Ofisi hiyo alipotembelea Maadhimisho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea Jijijni Dodoma.


Wakili Mkuu wa Serikali Dkt. Ally Possi akisaini vitabu vya Taasisi zinazoshiriki Maadhimisho ya Wiki ya Sheria baada ya kutembelea mabanda ya maonesho ya Taasisi hizo kwa lengo la kuona namna Taasisi hizo zinavyotekeleza majukumu yao.


Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi akimsikiliza Afisa Uchunguzi Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Ndugu Laurent Bulilo alipotembelea banda la Wizara hiyo wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea Jijini Dodoma.


Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi akizungumza na Mkurugenzi Msaidizi Usimamizi wa Mashauri wa Mahakama Kuu ya Tanzania alipotembelea Banda la Mahakama ya Tanzania kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea Jijini Dodoma.


Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi akimsikiliza Afisa Uchunguzi Mkuu wa Tume ya Haki za Binadamu Bi. Eugenia Lohay alipotembelea banda la Ofisi hiyo wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea Jijini Dodoma.


Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi, akiwasili kwenye viwanja vya Nyerere Square alipotembelea mabanda ya wadau mbalimbali wanaoshiriki Maadhimisho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea Jijini Dodoma kwa lengo la kuona namna wadau hao wanavyotekeleza majukumu yao.





WATENDAJI ARDHI WATAKIWA KUTOCHELEWESHA HUDUMA KWA MAKUSUDI

Written By CCMdijitali on Saturday, February 1, 2025 | February 01, 2025

  

Na Munir Shemweta, WANMM IRINGA

 

Serikali imewataka watendaji wa sekta ya Ardhi nchini kutochelewesha huduma za sekta ya Ardhi kwa makusudi wakati wanapowahudumia wananchi wanaokwenda kupata huduma katika ofisi zao.

 

Hayo yameelezwa Januari 31, 2025 mkoani Iringa na Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Hamdouny Mansoor wakati wa kikao kazi cha watumishi wa sekta ya Ardhi Mkoa wa Iringa.

 

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Anthony Sanga, Bw. Mansoor amesema kumekuwa na ucheleweshaji huduma kwa makusudi na wakati mwingine watendaji wa sekta ya Ardhi kuwatuma mwananchi wanaokwenda kupata huduma.

 

"Sasa anakuja mwananchi anasema anataka kulipa kodi anaelezwa, aah hiyo kazi ni ya Afisa Ardhi nenda kulee mimi mpima,  si umuelekeze tu, wakati mwingine tunatoa kauli ambazo siyo nzuri kwa wananchi wanaofika kupata huduma za Ardhi kwenye ofisi zetu" amesema.

 

Aidha, Mansoor kupitia kikao hicho kilichoandaliwa na Ofisi ya Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Iringa ametaka kuwekwa utaratibu rasmi katika ofisi zote za Ardhi kuanzia ngazi ya wilaya wa namna ya kupata hati ili wananchi wauelewe na  kuufuata utaratibu huo.

 

"Inasisitizwa ili upate hati ni vitu gani vya msingi vinatakiwa viwepo kwa wananchi kupata hati yake, viainishwe na vibandikwe katika ofisi zetu za ardhi" amesema.

 

Kwa upande wake  Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Iringa Bw. Frank Minzikuntwe ameeleza kuwa, kikao kilichofanyika cha watumishi  kilikuwa na lengo la  kuzungumza na kupeana mikakati pamoja na mipango kazi ya namna ya kushughulikia kero na utoaji huduma za sekta ya ardhi kwa haraka zaidi.

 

"Sisi kama watendaji wa sekta ya Ardhi katika mkoa wa Iringa tunaahidi watumishi wote katika ngazi ya mkoa tutafanya kazi kwa weledi na uaminifu na kuwahudumia wananchi kwa tija ili waweze kupata huduma kwa wakati unaostahili’’. amesema

 

Kikao hicho cha siku moja kimeshirikisha watendaji wa sekta ya ardhi kutoka halmashauri zote za mkoa wa Iringa pamoja na wale wa Ofisi ya Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Iringa.


Sehemu ya watumishi wa sekta ya ardhi mkoa wa Iringa wakifuatilia majadiliano wakati wa kikao kazi cha watumishi wote wa sekta ya ardhi mkoa wa Iringa kilichofanyika jana.

Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Hamdouny Mansoor akizingumza wakati wa kikao kazi cha watumishi wa sekta ya ardhi mkoa wa Iringa kilichofanyika jana mkoani humo.

Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Iringa Bw. Frank Minzikuntwe akizungumza katika kikao kazi cha watumishi wa sekta ya ardhi mkoa wa Iringa jana. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)

Sehemu ya watumishi wa sekta ya ardhi mkoa wa Iringa wakifuatilia majadiliano wakati wa kikao kazi cha watumishi wote wa sekta ya ardhi mkoa wa Iringa kilichofanyika jana.




THBUB YATEMBELEA VYUO VYA MAFUNZO YA AMALI, PEMBA

 THBUB YATEMBELEA VYUO VYA MAFUNZO YA AMALI, PEMBA


TUME ya Haki za Binaadamu na Utawala Bora (THBUB) imefanya ziara ya kuvitembelea vyuo

viwili vya Mafunzo ya Amali vya Vitongoji, Wilaya ya Chake Mkoa wa Kusini Pemba na cha

Daya Mtambwe, Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba, kwa lengo la kutoa elimu na

kujenga uelewa mpana kwa jamii juu ya dhana nzima ya Haki za Binadamu na Misingi ya

Utawala Bora.


Maafisa wa Tume hiyo, Ofisi ya Pemba wakiongozwa na Afisa Uchunguzi Ndg. Ramadhani Slaa

wameifunza jamii juu ya umuhimu wa kutambua Haki za Binaadamu na Utawala Bora pamoja

ushiriki na kuanzisha klabu za Haki za Binaadamu katika vyuo na kuwashauri wanafunzi wa vyuo

hivyo kujiunga na klabu hizo.


Akizungumza kwenye ziara hiyo, ofisi za chuo cha Vitongoji, Bw. Slaa alieleza nia ya ziara yao

chuoni hapo mbali na kutoa elimu ya Haki za Binaadamu na Utawala Bora lakini kushirikiana na

vyuo hivyo kuanzisha Klabu za Haki za Binadamu na Utawala Bora ili kukuza ushirikiano na nguvu

ya pamoja kwa kuongeza uelewa kwa jamii juu dhana ya Haki za Binaadamu na misingi ya Utawala

Bora.


Aidha, Bw. Ramadhan Slaa awasihi wanafunzi vyuoni humo kuendelea kuwa mabalozi wazuri wa

jamii zao katika kueneza dhana halisi ya Haki za Binaadamu na misingi ya Utawala Bora ili kukuza

jamii yenye uelewa mpana kwa maeneo hayo.


Katika hatua nyengine, THBUB ilimshauri, Mkuu wa chuo cha Daya cha Mtambwe, Mwl. Saada Ali

Hamad, kuanzisha Klabu ya Haki za Binadamu na Utawala Bora chuoni hapo ili kuongeza hamasa

na uelewa zaidi kwa jamii.


Naye, Mwalimu dhamana wa Chuo cha Mafunzo ya Amali cha Vitongoji na Mkuu wa Idara ya

Masomo Mtambukwa chuoni hapo, Mwl. Khamis Abdalla Khamis alitoa shukrani kwa THBUB kwa

kuwatembelea chuoni hapo sambamba na kuishauri Tume kuwa karibu na Klabu hizo ili kuzijengea

uimara na ziwe endelevu pamoja na kuahidi kuzisimamia vyema katika kuendeleza shughuli za

kutoa elimu kupitia klabu hizo.


Halikadhalika,kwa nyakati tofauti wanafunzi wa vyuo viwili hivyo, walipata nafasi ya kuuliza maswali

kuhusu dhana na uelewa wa Haki za Binaadamu na Utawala Bora pia kutaka kujua umuhimu na

faida za kujiunga na Klabu za Haki za Binadamu na Utawala Bora vyuoni humo.


Kwaupande mwengine, wanafunzi hao wameiomba THBUB kurudi tena kwenye vyuo vyao na

kujenga utamaduni wa kuwatembelea mara kwa mara ili wajifunze zaidi. Hata hivyo, waliiahidi Tume

kuongeza ushiriki wao mpana katika kusimamia na kuendeleza klabu hizo ndani ya vyuo vyao.


Kiasi cha wanafunzi wasiopungua 600 wakiwemo 400 kutoka Chuo Cha mafunzo ya Amali cha

Vitongoji na 200 kutoka chuo cha Daya, Mtambile kwa nyakati tofauti walihudhuria hafla hiyo

iliyowajenga kitaaluma na kuelezwa juu ya umuhimu wa kushiriki klabu kama hizo na umuhimu wake

wa kuanzishwa kwenye vyuo vyao.

MAOFISA kutoka Tume ya Haki za Binaadamu na Utawala Bora (THBUB) wakiwapa elimu ya uelewa mapana juu ya dhana ya Haki za binaadamu na misingi ya Utawala Bora katika vyuo vya Mafunzo ya Amali vya Vitongoji na Daya, Pemba.



WANAFUNZI wa Chuo Cha Mafunzo ya Amali wa chuo cha Daya, mtambile,Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba wakiwasikiliza Maofisa kutoka Tume ya Haki za Binaadamu na Utawala Bora (THBUB) juu ya uelewa mpana wa dhana ya Haki za binaadamu na misingi ya Utawala Bora.


WANAFUNZI wa Chuo Cha Mafunzo ya Amali wa chuo cha Daya, mtambile,Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba wakiwasikiliza Maofisa kutoka Tume ya Haki za Binaadamu na Utawala Bora (THBUB) juu ya uelewa mpana wa dhana ya Haki za binaadamu na misingi ya Utawala Bora.


MAOFISA kutoka Tume ya Haki za Binaadamu na Utawala Bora (THBUB) wakiwapa elimu ya uelewa mapana juu ya dhana ya Haki za binaadamu na misingi ya Utawala Bora katika vyuo vya Mafunzo ya Amali vya Vitongoji na Daya, Pemba.



MWISHO.

 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link