MIUNDOMBINU YA ELIMU ZANZIBAR SASA YALINGANA NA MAHITAJI YA KARNE YA 21
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Zanzibar imepiga hatua kubwa katika kuimarisha mazin...
MCC CHATANDA ASHIRIKI MAZISHI YA SHEMEJI YAKE MCC RAJABU
Written By CCMdijitali on Monday, February 10, 2025 | February 10, 2025
🗓️ 10 Februari, 2025
📍 Pangani ~ Tanga
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT), Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC) ameshiriki Mazishi ya Shemeji yake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga, Ndg. Rajabu Abdullahman Abdullah (MCC) msiba uliotokea tarehe 09 Februari, 2025, Wilayani Pangani.
Aidha, MCC Chatanda alipata nafasi ya kutoa Salamu za Pole na aliwakumbusha kuwa Tarehe 13 Febuari, 2025 litaanza zoezi la uandikishaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga hivyo watu wote wenye sifa ya kujiandikisha wajitokeze Kwa wingi kujiandikisha.
Msiba huo umehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali na Chama akiwepo Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Batlida Buriani, Mbunge wa Bumbuli Mhe. Januari Makamba(MNEC), Mbunge wa Tanga Mjini Mhe. Ummy Mwalimu, Mbunge wa Handeni Vijijini, Mkuu wa Wilaya ya Pangani, Mhe. Gift Musuya, Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mhe. Zainabu Abdallah na Wengine wengi.
MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR AFUNGUA KONGAMANO,WARSHA NA MKUTANO WA 51 WA CHAMA CHA WAKUTUBII
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema Serikali zote mbili zinatambua mchango mkubwa unaotokana na wanataaluma ya Ukutubi ambayo inachangia kwa kiasi kikubwa maendeleo kwa Taasisi za Serikali na Taasisi binafsi hapa nchini.
Ameyasema hayo kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt Hussein Mwinyi wakati wa ufunguzi wa Kongamano na Warsha inayoenda sambamba na Mkutano Mkuu wa 51 wa Chama cha Wakutubi Tanzania uliofanyika katika Ukumbi wa Hotel ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege jijini Zanzibar.
Amesema kuwa kujifunza kupitia huduma za maktaba za kidijitali itakuwa chachu ya kuwarahisishia wananchi kupata taarifa na habari sahihi kwa wakati sambamba na kujiongezea uwezo wa kukabiliana na changamoto mbali mbali zinazojitokeza kwa mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla.
Makamu wa Pili wa Rais amesema ni wajibu wa wakutubi na watoa huduma za Maktaba kuwekeza katika elimu na ubunifu ili kubaini vyanzo mbali mbali vya taarifa na maarifa vilivyopo kwa ajili ya kuboresha huduma za maktaba katika mfumo wa kidijitali.
Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar amesema Serikali inaendelea na azma yake ya kujenga Mktaba kuu ya kisasa katika eneo la Maisara ambayo itakidhi viwango vya kitaifa na Kimataifa ikiwemo huduma za kidijitali pamoja na kujenga Maktaba kwa kila Wilaya ambazo zitafungamana na utoaji wa huduma za kisasa kwa jamii husika.
Sambamba na hayo MakAmu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewataka wakutubi kusimamia malengo ya Chama chao kwa kuwaunganisha wanataaluma ya ukutubi katika kukuza ushirikiano wa Taasisi wanachama katika utoaji wa huduma za maktaba na kuboresha viwango vya huduma hio kwa Tanzania nzima.
Mhe. Hemed amesema anatambua kuwa Sera ya Taifa ya Maktaba ipo katika hatua za mwisho hivyo amewaagiza Wakuu wa Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania (BOHUMAZA) kushirikiana na vyama wa wakutubi katika kuandaa miongozo mbali mbali ambayo itarahisisha utekelezaji wa Sera hiyo na kuleta mabadiliko chanya kwa tasnia ukutubi, huduma za maktaba na wakutubi wenyewe.
Nae Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Ndugu Khamis Abdulla Said amesema kongamano hilo na warsha kwa wana taaluma ya Ukutubi litaleta mabadiliko makubwa hasa katika upatikanaji wa taarifa za usahihi, na zenye ufanisi na kuwafikia walengwa kwa wakati.
Khamis amesema Serikali kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar imetenga bajeti maalum kwa ajili ya ununuzi wa vitabu vyote muhimu vya kusomea na kufundishia kwa ajili ya kuboresha huduma za maktaba ili kuweza kuakisi mahitaji ya watumiaji.
Amesema Wizara ya Elimu imejipanga kuimarisha Mifumo ya kidijitali katika Maktaba zote za Zanzibar ambao utawezesha kuongeza ufanisi wa huduma za maktaba na kupunguza changamoto ya upotevu wa vitabu pamoja na kuwapatia fursa za mafunzo ndani na nje ya nchi wanataaluma ya ukutubi ili kuendana na mabadiliko ya Teknolojia na ongezeko la mahitaji ya huduma za Maktaba nchini.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania Profesa Ali Mcharazo amesema wakati umefika kwa Wakutubi kuwezeshwa kielimu na kupatiwa vifaa vya kisasa ili kuweza kufanya kazi zao kwa uweledi na ubora wa hali ya juu katika kutoa huduma za Maktaba nchini.
Profesa Mcharazo amesema wakutubi wana wajibu wa kujiendeleza kitaaluma na kujifunza ubunifu katika kada yao kwa kuzingatia kuwa Elimu bora hutegemea vifaa bora na wataalamu bora wa kuisambaza elimu hio.
Mapema Mkurugenzi wa Bodi ya Huduma za Maktaba Zanzibar Dkt. Ulfat Abdulaziz Ibrahim amesema Bodi ya Huduma za Maktaba Zanzibar imejipanga kufanya Mapinduzi ya Kifikra juu ya maana, matumizi na umuhimu wa Maktaba na wakutubi katika kufikia malengo ya elimu Tanzania.
Dkt. Ulfat amesema kufanyika kwa Kongamano na Warsha kwa Wakutubi wa Tanzania litasaidia kuongeza ujuzi na taaluma kwa watatoa huduma hio kuweza kutoa taaluma bora kwa watumiaji wa Maktaba popote walipo nchini.
Imetolewa na Kitengo cha Habari ( OMPR )Leo tarehe 10. 02. 2025
MKUTANO WA 17 WA BARAZA LA MAWAZIRI LA KISEKTA LA NISHATI, PETROLI NA MADINI LA EAC WAANZA JIJINI ARUSHA
Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Nishati, Petroli na Madini la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) umenza leo tarehe 10 Februari 2025 katika Makao Makuu ya Jumuiya hiyo jijini Arusha.
Mkutano huo wa siku tano kuanzia Februari 10 hadi 14, 2025 utafanyika katika ngazi tatu; ngazi ya Wataalamu tarehe 10 -12 Februari 2025, ngazi ya Makatibu Wakuu tarehe 13 Februari 2024 na kuhitimishwa katika ngazi ya Mawaziri tarehe 14 Februari 2025.
Mkutano huo unatarajiwa kupokea na kujadili taarifa mbalimbali za maendeleo ya sekta ya nishati, petroli na madini katika Jumuiya na kuweka mikakati ya pamoja ya kutatua chagamoto mbalimbali zinazoikabili sekta hiyo ili kuhakikisha nchi wanachama wananufaika kutokana na mchango wa sekta hizo, vilevile kuhakikisha upatikanaji wa nishati ya uhakika, nafuu na endelevu katika Jumuiya.
Ili kufikia adhima hiyo mkutano huo utaangazia agenda mbalimbali ikiwemo; hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa maamuzi ya baraza la hilo la sekta, matumizi ya nishati safi, salama na ufanisi wake, Mkutano na Maonyesho ya 11 ya Petroli ya Afrika Mashariki yanayotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam tarehe 5-7 Machi 2025 na kuhuisha taarifa za utekelezaji wa miradi ya kuunganisha na kusambaza nishati katika Jumuiya.
Akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano huo wa ngazi ya wataalamu Mkurugenzi wa Sekta za Uzalishaji wa Sekretariati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Bw. Jean Baptiste Havugimana ameeleza kuwa licha ya mafanikio yaliyofikiwa katika sekta hiyo bado mchango na weledi wa wataalamu wa sekta hizo muhimu katika kukuza uchumi wa Jumuiya unahitajika ili kutatua changamoto zilizopo na hatimaye kufikia malengo yanayotarajiwa na Jumuiya.
Havugimana ametoa rai kwa watalamu hao kujikita katika kujadili na kuyapatia ufumbuzi wa kudumu masuala muhimu yatakayojili katika mkutano huo kwa manufaa ya Jumuiya.
Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo wa ngazi ya wataalamu unaongozwa na Bw. Abdillah Mataka Mkurugenzi wa Idara ya Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii katika Wizara ya Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Mkutano huo unaotarajiwa hutimishwa tarehe 14 Februari 2025 katika ngazi ya Mawaziri wanaosimamia sekta ya nishati, petroli na madini umehudhiriwa na wajumbe kutoka Nchi zote saba (7) wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
![]() |
| Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Nishati, Petroli na Madini la EAC ukiendelea katika Makao Makuu ya Jumuiya jijini Arusha. |
KAMATI YA ARDHI, MALIASILI NA UTALII YARIDHISHWA NA UJENZI WA MAKTABA CHUO CHA ARIDHI TABORA
Written By CCMdijitali on Sunday, February 9, 2025 | February 09, 2025
Na Eleuteri Mangi, Tabora
Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeridhidhwa na ujenzi wa mradi wa maktaba ya Chuo cha Ardhi Tabora (ARITA) ambao umefikia asilimia 99 na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Februari 2025.
Akizungumza wakati wa majumuisho mara baada ya ziara ya kukagua ujenzi wa maktaba hiyo Februari 8, 2025 mjini Tabora, Mwanyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii Mhe.Timotheo Mzava amesema kamati yake imejionea na kuridhishwa kwa hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa maktaba hiyo pamoja na maendeleo ya chuo hicho.
“Kwa ujumla Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii baada kupitia, kukagua, kupata taarifa na kujionea kwa macho, imeridhishwa na kazi kubwa na nzuri inayofanywa na uongozi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi pamoja Chuo cha Ardhi Tabora katika kukamilisha jengo hili la maktaba” amesema Mhe. Mzava.
Aidha, ameishukuru Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kiasi cha Shilingi milioni 500 Septemba 2024 ambayo ilipitishwa na Bunge katika bajeti ya mwaka 2024/2025 ili kukamilisha ujenzi wa maktaba hiyo na kuleta tija kwa kuwa utasaidia vijana wanaosoma katika chuo hicho.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda ameishukuru kamati hiyo ambayo ndiyo yenye dhana ya kuisimamia, kushauri, kutoa maelekezo mbalimbali na kufuatilia kazi zinazotekelezwa na wizara hiyo.
“Wajumbe wa kamati hii wameridhika na kazi ambayo imefanyika na wanasisitiza jengo hili lianze kufanyakazi mara moja. Sisi wizara tumeiahidi kamati kuanzia tarehe 01 Machi, 2025 wanafunzi wataanza kutumia vyumba hivi kwa ajili ya huduma ya maktaba” amesema Naibu Waziri Pinda.
Akiwakaribisha wajumbe wa Kamati hiyo mkoani Tabora, Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Paul Chacha amesema miradi mingi ya maendeleo inatekelezwa na Serikali katika mkoa huo na kuihakikishia kamati hiyo kuwa Ofisi yake itahakikisha miradi yote inakamilika ukiwamo mradi huo wa ujenzi wa maktaba ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Akitoa taarifa kwa kamati hiyo, Mkuu wa Chuo hicho Bw. Jeremiah Minja amesema maktaba hiyo ilianza kujengwa mwaka 2014 na itakamilika mwezi Februari 2025 ambapo hadi sasa umegharimu kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 2.2 za Kitanzania.
![]() |
| Muonekano wa maktaba ya Chuo cha Ardhi Tabora ambayo inatarajiwa kuanza kutumika Machi 01, 2025. |
![]() |
Wajumbe wa Kamati ya
Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakikagua ujenzi wa mradi wa maktaba ya
Chuo cha Ardhi Tabora (ARITA) Februari 8, 2025 mjini Tabora. |
![]() |
Wajumbe wa Kamati ya
Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakikagua ujenzi wa mradi wa maktaba ya
Chuo cha Ardhi Tabora (ARITA) Februari 8, 2025 mjini Tabora. |
![]() |
Naibu Waziri wa Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda akizungumza na Kamati ya
Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, menejimenti ya wizara Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, pamoja wenyeji timu ya mkoa wa Tabora (hawapo pichani)
wakati wa ziara ya kutembelea na kukagua ujenzi wa mradi wa maktaba ya Chuo cha
Ardhi Tabora (ARITA) Februari 8, 2025 mjini Tabora.
RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKISHIRIKI MKUTANO WA SADC
Written By CCMdijitali on Saturday, February 8, 2025 | February 08, 2025
Mawaziri EAC na SADC wakutana Dar kujadili mzozo DRC
Written By CCMdijitali on Friday, February 7, 2025 | February 07, 2025
Mawaziri wa Mambo ya Nje na Ulinzi wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), na wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC, wamekutana Leo Februari 07, 2025 jijini Dar es Salaam, kujadili mzozo wa Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC), ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kikao cha Marais wa jumuiya hizo, kitakachofanyika Kesho Jumamosi Februari 8, 2025.
“Kinachoendelea DRC inahitaji tuwe wamoja, hali hii inagusa kila mtu, usalama wa DRC ni muhimu sana kwa maendeleo ya jumuiya yetu na ukanda wote kwa ujumla, naamini jitihada zetu hizi zitaleta matunda mazuri" amesema Mhe. Nduva.
“Ni lazima tuchukue maamuzi kurudisha Amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, vita imegharimu maisha ya watu wengi, wanawake na watoto wanataabika, hali hii ikiendelea kutakuwa na madhara makubwa, natoa wito kwa sehemu zinazohusika na mgogoro huokusitisha na kufanya mazungumzo" amesema Mhe. Magosi.
MWENYEKITI WA UWT TAIFA AFANYA KIKAO NA WABUNGE WANAWAKE WA MAJIMBO
MWENYEKI WA UWT TAIFA AFANYA KIKAO NA WABUNGE WANAWAKE WA MAJIMBO
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi, Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC) amefanya kikao maalum na Wabunge Wanawake wanaotokana Chama Cha Mapinduzi kwenye Majimbo Leo tarehe 07 Febuari, 2025 Dodoma.



















.jpeg)
.jpeg)





























.jpeg)







