MIUNDOMBINU YA ELIMU ZANZIBAR SASA YALINGANA NA MAHITAJI YA KARNE YA 21

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Zanzibar imepiga hatua kubwa katika kuimarisha mazin...

Latest Post

KIKWETE AMWAKILISHA RAIS SAMIA KWENYE MAZISHI YA RAIS WA ZAMANI WA FINLAND

Written By CCMdijitali on Saturday, November 11, 2023 | November 11, 2023


Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan katika hafla ya Mazishi ya Kitaifa ya Rais wa Zamani wa Finland, Hayati Martti Ahtisaari iliyofanyika Helsinki tarehe 10 Novemba 2023. 

 

Wakati wa kutoa salamu za pole, Rais Kikwete alisema kuwa Rais Samia anatoa salamu za rambirambi kwa Rais wa Findland, Mhe. Sauli Niinistö, Familia ya Marehemu na watu wote wa Finland kufuatia kifo cha kiongozi huyo mashuhuri duniani. 

 

Rais Kikwete aliungana na viongozi mbalimbali walioshiriki mazishi hayo wakimwemo Rais wa Kosovo, Mhe. Vyosa Osmani na Rais wa Namibia, Mhe. Hage Geingob na kummwagia sifa Hayati Martti Ahtisaari kwamba alikuwa kiongozi mwenye maono na mpenda amani duniani.

 

Hayati Martti Ahtisaari aliwahi kuwa Balozi wa Finland nchini Tanzania kuanzia mwaka 1973 hadi 1976 na alikuwa Rais wa Finland kuanzia mwaka 1994 hadi 2000. Katika vipindi vyote hivyo, Hayati Martti Ahtisaari aliimarisha uhusiano wa Tanzania na Finland katika nyanja mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufanya ziara ya kitaifa nchini Tanzania mwaka 1997 wakati wa Serikali ya Awamu ya Tatu iliyokuwa inaongozwa na Hayati Benjamin Mkapa.

 
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Kikwete akimpa pole Mjane wa Rais wa Zamani wa Finland, Hayati Martti Ahtisaari

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Kikwete (kulia) akiwa na viongozi na waombolezaji wengine katika hafla ya mazishi ya kitaifa ya Rais wa Zamani wa Finland, Hayati Martti Ahtisaari iliyofanyika Helsinki tarehe 10 Novemba 2023. Rais Kikwete alimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi hayo.

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Kikwete (kulia) akiwa na viongozi na waombolezaji wengine katika hafla ya mazishi ya kitaifa ya Rais wa Zamani wa Finland, Hayati Martti Ahtisaari iliyofanyika Helsinki tarehe 10 Novemba 2023. Rais Kikwete alimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi hayo.

Hafla ya Mazishi ya Kitaifa ya Rais wa Zamani wa Finland, Hayati Martti Ahtisaari ikiendelea Helsinki tarehe 10 Novemba 2023

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Kikwete akiwa katika mazungumzo na Rais wa Finland, Mhe. Sauli Niinistö wakati wa hafla alyoiandaa kwa viongozi na wageni walioshiriki Mazishi ya Kitaifa ya Rais wa zamani wa nchi hyo, Hayati Martti Ahtisaari yaliyofanyika tarehe 10 Novemba 2023.



Balozi Wa Ausralia Nchini Mwenye Makazi Yake Nchini Kenya Aagwa

Written By CCMdijitali on Wednesday, November 8, 2023 | November 08, 2023

Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb.) amemuaga Balozi wa Australia nchini mwenye makazi yake nchini Kenya, Mhe. Luke Williams baada ya kumaliza muda wake wa uwakilishi.



Akizungumza na Mhe. Balozi Williams walipokutana katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam, Waziri Mbarouk amesema Tanzania na Australia zimekuwa na uhusiano mzuri uliowezesha mataifa hayo kuendelea kuimarisha ushirikiano katika sekta za elimu, utalii, madini, nishati, mabadiliko ya tabia nchi, pamoja na biashara na uwekezaji.

Waziri Mbarouk ameongeza kuwa ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Australia ni jambo lililochochewa na kazi nzuri iliyofanywa na Balozi Williams wakati akitekeleza majukumu yake ya kibalozi.
“Katika kipindi chako umeiwakilisha vyema Australia na kuonesha mafanikio makubwa ambayo yamefikiwa kati ya Tanzania na Australia.

Kazi yako imechochea uboreshaji wa sekta za elimu, utalii, madini, nishati, uchumi wa buluu na kuchangia ukuaji wa sekta ya biashara uwekezaji katika nchi zetu, ni matumaini yangu kuwa utaendelea kuwa Balozi mwema kwa Tanzania nchini Australia na kokote uendako Duniani,” amesema Balozi Mbarouk.

Balozi Mbarouk ameongeza kuwa Australia imekuwa ikitoa fursa za ufadhili wa masomo katika sekta mbalimbali, ila kwa sasa Tanzania inaomba fursa hizo zijikite zaidi katika sekta ya nishati.

Pamoja na mambo mengine, Balozi Mbarouk amemueleza Balozi Williams kuwa kwa sasa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan imeboresha mazingira ya biashara na uwekezaji kwa kiasi kikubwa na kuwaalika wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Australia kuja kuwekeza kwa wingi nchini.

Kwa upande wake Balozi Williams, ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano iliomuonesha wakati wote wa utekelezaji wa majukumu yake ya kibalozi. “Kwa kweli ni ngumu sana kuaga lakini haya ndiyo Maisha ya wanadiplomasia hakuna budi, siku zote nitakumbuka utu na ukarimu wa Watanzania,” amesema Mhe. Williams


Pamoja na mambo mengine, Balozi Williams ameihakikishia Tanzania kuwa Australia itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuhakikisha inaboresha zaidi sekta za elimu, utalii, mabadiliko ya tabianchi, uchumi wa buluu pamoja na biashara na uwekezaji kwa maslahi ya pande zote mbili.
 
Balozi wa Australia nchini mwenye makazi yake Nairobi nchini Kenya, Mhe. Luke Williams akizungumza na Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akimkabidhi zawadi ya picha ya Mlima Kilimanjaro Balozi wa Australia nchini mwenye makazi yake Nairobi nchini Kenya, Mhe. Luke Williams katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.  Balozi Williams amemaliza muda wake wa uwakilishi.

Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akizungumza na Balozi wa Australia nchini mwenye makazi yake Nairobi nchini Kenya, Mhe. Luke Williams katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk na Balozi wa Australia nchini mwenye makazi yake Nairobi nchini Kenya, Mhe. Luke Williams katika picha ya pamoja na watumishi katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk katika picha ya pamoja na Balozi wa Australia nchini mwenye makazi yake Nairobi nchini Kenya, Mhe. Luke Williams katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam



RC MONGELLA AFUNGUA MKUTANO MKUU WA 6 WA (ACFE) MWAKA 2023.

Written By CCMdijitali on Monday, November 6, 2023 | November 06, 2023




Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John V.K. Mongella akifungua Mkutano Mkuu wa 6 mwaka 2023  wa Chama cha  Watalam wa Udhibiti wa Ufisadi, Rushwa na Ubadhilifu (ACFE) Tanzania,  unaofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano Hoteli ya Mount Meru Hoteli jijini Arusha.

Mhe.Mongella amefungua mkutano huo wa siku tano, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Haroon Ali Suleiman.

Mhe. Mongella ametumia fusa hiyo kuwapongeza Waheshimiwa Marais,  Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan  na Rais wa Serikali na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa jitihada na nia thabiti wanayoionesha kwa vitendo katika kupambana na Rushwa, Ubadhirifu pamoja na Ufisadi ambavyo vimekua sumu kubwa inayorudisha nyuma  maendeleo.

Aidha Mada ya kuvutia kwa mkutano wa mwaka huu ni "MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA NA UBADHIRIFU KATIKA KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO NA UTOAJI WA HUDUMA ZA KIJAMII"







@rc_mkoa_arusha @acfetanzania @acfeindonesia.chapter111 @wizaramnn #ccmdijitaliupdates 

RAIS DK.MWINYI AKUTANA NA DK.JUAN PABLO

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amekutana na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Dunia anayeshughulikia masuala ya Afya Dk.Juan Pablo na ujumbe wake Ikulu Zanzibar


Zanzibar,


06 Novemba, 2023

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, ameshukuru ushirikiano wa karibu uliopo baina ya Tanzania hususani Zanzibar, na Benki ya Dunia (WB), Umoja wa Ulaya (EU) na ushirikiano wa diplomasia uliopo baina ya Australia na Tanzania.

Dk. Mwinyi alitoa shukurani hizo Ikulu, Zanzibar alipozungumza na wageni hao walioambatana na ujumbe waliofuatana nao kwa nyakati tofauti.
Alisema, taasisi hizo zinamchango mkubwa wa maendeleo ya Zanzibar hasa kukuza sekta ya Afya nchini, Elimu, Utalii na Uchumi wa Buluu.

Akizungumza na Balozi wa Australia nchini Tanzania, Mhe. Luke William aliefika kumuaga, Rais Dk. Mwinyi alishukuru ushirikino mkubwa uliopo baina ya Tanzanzia na nchi hiyo na kumueleza juu ya Zanzibar inavyonufaika na sekta ya uvuvi na mwani uliowaneemesha kinamama wengi na vijana kwani asilimia 90 ya wakulima wake ni kina mama.

Pia, Rais Dk. Mwinyi alimueleza balozi huyo azma ya kuendeleza ushirikiano uliopo baina ya Austalia na Zanzibar hasa kwenye masuala ya uwekezaji, biashara na utalii.

Vile vile Rais Dk. Mwinyi alizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa masuala ya Bahari na Uvuvi wa Umoja wa Ulaya (EU), Bi. Charlina Vitcheva alimueleza kuwa Zanzibar ni kisiwa kilichozungukwa na bahari ya Hindi, kinajivunia fursa nyingi zinazotokana na rasilimali bahari kwa kujikita zaidi kwenye uchumi wa Buluu na Utalii.

Alimueleza Mkurugenzi  huyo, Uchumii wa Buluu ni sekta muhimu kwa uchumi wa Zanzibar na kuongeza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, inafanya kila iwezavyo kunufaika na fursa zinazotokana na sekta hiyo kwa ajili ya uchumi na watu wake.

Aidha, alimueleza mgeni huyo kuimarisha zaidi ushirikiano wao kwenye sekta hiyo, ili kujenga uweledi kwani idadi kubwa ya Wazanzibari wamejikita zaidi na masuala ya uvuvi na ajira zinazotona na bahari.

Rais Dk. Mwinyi alisema, Serikali pia inawaungamkono wavuvi na wakulima wa mwani nchini kwani imewawezesha kwa mitaji na vifaa pamoja na kuiungamkono sekta ya Utalii.

Kwa upande wao wageni hao walemueleza Rais Dk. Mwinyi juu ya kuendelea kuiungamkono Zanzibar na Tanzania kwa ujumla hasa kwenye masuala ya kuendeleza ushirikiano wao wa diplomasia na kuona fusra za uwekezaji na uchumi zilizomo Tanzanzia vinanufaisha pande zote na ushirikiano wao.









IDARA YA MAWASILIANO, IKULU ZANZIBAR.


Kinana:CCM INAMPA HEKO DKT. MWINYI

Written By CCMdijitali on Saturday, November 4, 2023 | November 04, 2023



Na Mwandishi Wetu

CHAMA Cha Mapindizi (CCM), kimeridhishwa na uongozi wa Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi.


Hayo yamesemwa leo Novemba 4, 2023, na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana, katika maadhimisho ya miaka mitatu ya uongozi wa Dk. Mwinyi.

Kinana amesema Dk. Mwinyi  amejituma sana na kujikita katika kuleta maendeleo ya wananchi wa Unguja na Pemba huku akiwaunganisha  kuwa kitu kimoja.

Akiyataja mafanikio yaliyopatikana Zanzibar kwa miaka mitatu tangu Rais Dk. Mwinyi alipoingia madarakani, Ndugu Kinana amesema ni pamoja na kuharakisha maendeleo kwa kutekeleza miradi mikubwa ikiwemo ujenzi wa shule, hospitali na miradi ya wananchi ya kiuchumi.

Aidha, amesema amewaunganisha wananchi, hivyo kusahau tofauti za itikadi za kisiasa, na watu wote kuwa wamoja.

Ndugu Kinana amefafanua kwamba,  hatua hiyo inatoa matumaini katika kipindi cha miaka miwili iliyobakia kufikia ukamilikaji wa malengo ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2020-2025.

“Rais Mwinyi tunakushuru sana, katika kipindi cha miaka mitatu umefanya mambo makubwa, ikiwemo kuleta mabadiliko makubwa ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi, pamoja na kuwaunganisha wananchi na kuimarisha amani na utulivu wa kisiasa,” amesema Ndugu Kinana.




‘WATUMISHI WABADHIRIFU SIKU ZAO ZINAHESABIKA’ MCHENGERWA



OR-TAMISEMI

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Mohamed Mchengerwa amewatahadharisha viongozi katika Tawala za Mikoa na Mamlaka ya Serikali za Mitaa ambao ni wazembe, wasio na nidhamu na wabadhilifu kuwa siku zao zinahesabika.

Akichangia hoja ya taarifa za kamati tatu za Bunge kuhusu ripoti ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali(CAG) Mchengerwa alisema:" wale wote waliotajwa kwenye ripoti naomba kusema maneno yafuatayo; ole wake kiongozi yeyote mzembe, asiye na nidhamu na mbadhilifu  kwenye wizara yangu na nitakayemkuta huko naomba niwaambie siku zao zinahesabika."

Kauli ya Mchengerwa iliamshamshangwe kutoka kwa Wabunge huku wakigonga meza.

Aidha, Mchengerwa alimuelekeza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Adolf Nduguru kuchukua hatua dhidi ya Mkurugenzi wa Igunga ambaye alikua Mkurugenzi Kigoma Manispaa, Athuman Msabila kumsimamisha kazi mara moja kwasababu ya ushiriki wake wa fedha za mifumo akishirikiana na watendaji wa mifumo walioko Ofisi ya Rais Tamisemi waliotajwa.

 "Watu hawa wasimamishwe kazi mara moja."

Aidha, Mchengerwa amesema tayari wizara yake imeanza kutekeleza taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali CAG kwa kuchukua hatua mbalimbali kwa wakurugenzi wa halmashauri zikiwemo za kuwasimamisha kazi, kutengua uteuzi na kuwafikisha mahakamani.

" Serikali ya awamu ya sita inachukia hatua madhubuti za kupambana na wabadhilifu wa fedha za umma kwenye mamlaka za Serikali za Mitaa."

Amesema wamewasimamiasha kazi watumishi walioshiriki kwenye ubadhirifu wa fedha za Serikali katika Halmashauri mbalimbali na kuchukua hatua kwa wakurugenzi wa halmashauri mbalimbali ikiwemo wa Jiji la Mbeya, Mwanza, Dar es Salaam na Arusha.

"Na hata aliyekuwa Mkurugenzi wa Sumbawanga akahamishiwa kwengine tumemrejesha ili akajibu kesi iliyoko mahakamani. Zile taarifa kuwa kuna watu wanahamishwa, katika kipindi hiki cha Serikali ya awamu ya sita ya Dk.Samia Suluhu Hassan mtumishi yeyote popote alipo awe amehamishwa, awe amestaafu, atakayeshiriki kwenye ubadhilifu wa fedha za umma hatutasita kumchukulia hatua.









UWT WAWATAKA WENYE KUUTAMANI URAIS ZANZIBAR 2025 WAMWACHIE DK.MWINYI



Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amewashukuru viongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kwa kuthamini kuandaa mkutano uliojumuisha Wanawake kutoka sehemu mbalimbali nchini ikiwemo  mikoa yote ya Tanzania bara.

Dk.Mwinyi amesema hayo  katika mkutano wa kumpongeza kutimiza miaka mitatu ya uongozi wake ulioandaliwa na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) uliofanyika viwanja vya Maisara Mkoa wa Mjini Magharibi leo tarehe 04 Novemba 2023.

Aidha, Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania bara Abdulrahman Kinana ampongeza Rais Dk.Mwinyi kwa kuimarisha umoja, mshikamano na utulivu wa nchi na kuwaletea maendeleo Wazanzibari.

 Amesema katika miaka miwili iliyobaki utekelezaji wa miradi ya maendeleo utakuwa mkubwa zaidi na Zanzibar baada ya miaka 10 itakuwa ya maendeleo makubwa. 

Naye, Mwenyekiti wa UWT Taifa Mary Chatanda amesema UWT wameridhika na utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020/2025 kwa kuvuka malengo ya utekelezaji ndani ya miaka mitatu kwa miradi mbalimbali ya maendeleo iliyotekelezwa Zanzibar .

Vilevile ameeleza kuwa UWT watamchukulia na kumjazia fomu ya kuomba Urais wa Zanzibar  Dk.Mwinyi pia watafanya hivyohivyo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dk Samia Suluhu Hassan  mwaka 2025.

🗓️04 Novemba 2023

📍Viwanja vya Maisara, Mkoa wa Mjini Magharibi.






















UJERUMANI KUSHIRIKIANA NA TANZANIA KUBORESHA MAKUMBUSHO YA MAJIMAJI

Written By CCMdijitali on Wednesday, November 1, 2023 | November 01, 2023

Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, Mhe. Dkt. Frank-Walter Steinmeier akiweka shada la maua katika kaburi la walilozikwa mashujaa wa Vita vya Maji Maji



Serikali ya Ujerumani imeahidi kushirikiana na Serikali ya Tanzania kuboresha Makumbusho ya Majimaji ili  kuhifadhi kumbukumbu sahihi kwa ajili ya wakati huu na kwa  vizazi vijavyo.

Ahadi hiyo imetolewa na Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, Mhe. Dkt. Frank-Walter Steinmeier alipotembelea Makumbusho ya Vita vya Maji Maji  Songea Mkoani Ruvuma.

Mhe., Dkt. Steinmeier amesema Ujerumani ipo tayari kufanya uchambuzi na mchakato wa historia ya vita vya Maji Maji kwakuwa kilichotokea zamani hakipaswi kusauhilka na mtu yoyote.

“Ili kuweka kumbukumbu sawa kwa sasa na kwa wakati ujao, Ujerumani tunaahidi kushirikiana na Tanzania kuboresha makumbusho hii,” alisisitiza Mhe. Rais Steinmeier.

Mhe. Dkt. Steinmeier alisema Ujerumani inatamani kufanya uchambuzi na mchakato wa historia ya ‘Vita vya Maji Maji’ na kuongeza kuwa mchakato huo utahusisha vijana, wanafunzi wa shule na vyuo vikuu, wasomi na wataalamu wa hifadhi na sehemu za kumbukumbu.

“Mwaka 2024, Ujerumani ina mpango wa kufanya maonesho kwa kushirikiana na Makumbusho ya Taifa ya Tanzania, maonesho hayo yatajulikana kwa jina la  “Historia ya Tanzania”, alisema Mheshimiwa Steinmeier.

Awali Waziri wa Sanaa Utamaduni na Michezo, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.) alisema historia ya Tanzania na Ujerumani ina sura mbili tofauti. Alifafanua kuwa sura ya kwanza ni kuhusu vita waliyopigana babu zetu na sura ya pili ni yale mazuri yaliyofanywa na Serikali ya Ujerumani Kama vile kujenga shule, hospitali na kutoa huduma nyingine za kijamii.

“Muhimu zaidi ni kukumbuka na kusahau yaliyopita na kuendelea kudumisha uhusiano mzuri uliopo na kusonga mbele kwa kuleta maendeleo kati ya mataifa yetu mawili, lakini pia katika mji wetu wa Songea ,” alisema Dkt. Ndumbaro

Dkt. Ndumbaro aliongeza kuwa Songea wanatamani kuona makumbusho ya kisasa ya ushirikiano kati ya Ujerumani na Tanzania yakijengwa Songea, “pia tunatamani Ujerumani itusaidie kuboresha chuo cha VETA Songea ili kuwawezesha vijana wetu kupata mafunzo mbalimbali,” alisema Dkt. Ndumbaro.

Waziri Ndumbaro pamoja na mambo mengine, ameiomba Serikali ya Ujerumani kushirikiana na Mji wa Songea kwa kuwawezesha kutembeleana, kushirikiana na kuendeleza utani kati ya Wangoni na Wajerumani.

Mheshimiwa Rais Stenmeier mbali na kutembelea Makumbusho ya Vita vya Maji Maji pia ametembelea Shule ya Msingi ya Majimaji.

Makumbusho ya Vita vya Maji Maji ni makumbusho pekee nchini Tanzania inayoonesha historia kubwa ya Vita vya Maji Maji katika harakati za ukombozi dhidi ya ukoloni wa Wajerumani.

Mheshimiwa Rais Stenmeier amehitimisha ziara yake ya Kikazi ya siku tatu nchini leo tarehe 01 Novemba 2023.

Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, Mhe. Dkt. Frank-Walter Steinmeier akipokelewa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro katika Uwanja wa Ndege wa Songea kutembelea Makumbusho ya Vita vya Maji Maji Wilayani Songea Mkoani Ruvuma

Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, Mhe. Dkt. Frank-Walter Steinmeier akiwa amekaa na wanafunzi wa Shule ya Msingi Maji Maji wakati alipofanya ziara shuleni hapo

Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, Mhe. Dkt. Frank-Walter Steinmeier akiweka ua katika kaburi la Chifu Nduna  
 


Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, Mhe. Dkt. Frank-Walter Steinmeier katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali katika Viwanja vya Makumbusho ya Vita vya Maji Maji, Wilayani Songea, Ruvuma

Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani, Mhe. Dkt. Frank-Walter Steinmeier akizungumza na wananchi wa Songea (hawapo pichani) katika Viwanja vya Makumbusho ya Vita vya Maji Maji, Wilayani Songea, Ruvuma
 




 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link